The Chant of Savant

Friday 31 October 2014

Bye bye Compaore as you wait to be brought to book


Honore Traore, centre, 31 Oct

The reports we have are that former Burkina Faso strong man Blaise Compaore has resigned. If anything, this is good news for peace lovers. Compaore found himself in the hot soup after  conspiring with the parliament to amend the constitution to enable him to run for yet another term in office after ruling for 27 years. As MPs met, demonstrators  stormed the parliament, set it on fire and the MPs escaped. This was the beginning of the end of Compaore. Given that many African countries such as Uganda, Tanzania, Eritrea, Togo, Gabon, Equatorial Guinea, DRC, Mozambique, Morocco, Mauritania, Gambia, Lesotho, Swaziland and Zimbabwe face the same problem, will the citizenry stand up and pull down long time dictators in their countries? Is it time for new breath to be realized and experienced in Africa South of Sahara. Will the fire that gutted Compaore down be doused? Will it spread even further south? Who knows. At least africa is happy to have buried one dictator. Importantly, Burkina  people should not celebrate the ouster of their dictator. Instead they must stick to their guns to see that Compaore and his cronies are brought to book.So, too, they should not allow what transpired in Egypt after the fall of Hosni Mubarak whereby the army hijacked the revolution. For more info please CLICK HITHER.

Thursday 30 October 2014

Je araobaini ya Blaise Compaore imefika?




Palais Kosyam the state house of Burkinabe

Jenerali Honere Troure aliyetangaza kusimamia serikali ya mpito

Hali ilivyo ni kwamba Blaise Compaore imla wa taifa maskini la Bukinabe amefikia arobaini yake. Compaore alichukua madaraka mwaka 1987 baada ya kumpindua na kumuua rafiki yake rais Thomas Sankara aliyependwa na kusifika kwa usafi na uzalendo wake. Wengi walishangaa na kulaani kitendo hiki cha kinyama na hovyo kufanywa kwa rafiki. Hivyo, wengi wangependa na wanangoja kwa hamu kuona mwisho wa muuaji na fisadi huyu anayetuhumiwa kutumia viungo vya mazeruzeru kutambikia ili aendelee kukaa madarakani. Je jeshi la nchi hiyo litaungana na wananchi kuangusha imla wao? Je jeshi litatumia fursa hiyo kutwaa madaraka kama ilivyotokea Misri au kukaa kati kama ilivyotokea Tunisia? Je Compaore atafanikiwa kuzima nguvu ya umma? Je Burkinabe itafufua matumaini kuwa Afrika Kusini mwa Sahara (SSA) bado inaweza kufanya kile walichofanya wenzao wa Maghreb? Je kikinuka Burkina, nani atafuata, Chad, Sudan au Uganda? Natamani na Danganyika waamke na kuiondoa CCM kwa staili hii. Je kuna haya ya kukata tamaa? Lolote lawezekana? Tuzidi kuomba. Long live Burkina, Long live Thomas Sankara's spirit working in the people of Burkina. Kwa kinachoendelea, BONYEZA HAPA.

Wednesday 29 October 2014

Jana nilipokea kitabu cha Dk Sengondo Mvungi

Japa nilipokea nakala ya kitabu juu ya marehemu Dk Sengondo Mvungi Breathing the Constitution toka Tanzania. Kilitumwa na Kituo cha Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Centre-LHRC). Kwa namna ya pekee nawashukuru LHRC kwa kunitumia nakala ya kitabu hichi ukiachia mbali kutumia moja ya makala zangu kwenye kitabu husika  uk. 86. Namshukuru Dk Elen Kijo-Bisimba aliyehakikisha natumiwa nakala hii. Pia nimepata fursa ya kushiriki kwenye kueleza maisha ya nguli huyu wa sheria na haki za binadamu aliyeuawa kwenye mazingira ya kutatanisha kipindi alipohitajika kutoa mchango wake kwenye upatikanaji wa katiba safi ya wananchi ambayo hata hivyo imechakachuliwa na mafisadi ili kulinda uoza wao. Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya Dk Sengondo Mvungi. AAAMIN.

Tuesday 28 October 2014

Kikwete urais si kazi ngumu


WAKATI mwingine baadhi ya wanasiasa huongea vitu visivyoingia akilini kana kwamba wanaowasikiliza hawana akili za kutosha au wenye kufikiri sawasawa. Hivi karibuni, akiwa nchini China, Rais Jakaya Kikwete alitoa mpya pale alipokaririwa akisema, “Pili, kazi hii ya urais ni ngumu sana. Kwa hakika nawaonea gere sana wenye nguvu na ubavu wa kutaka kubakia kwenye kazi hii kwa miaka mingi. Pengine wana nguvu zaidi kuliko mimi.”
Hii si kweli. Kwanza, tupinge, kurekebisha na kusahishia kauli ya Rais Kikwete. Urais si kazi bali cheo cha kisiasa ambacho kinaweza kukaliwa na yoyote awe na elimu, ujuzi au hata asiwe navyo.
Ndiyo maana wahuni na majambazi kama Joseph Mobutu, Idd Amin, Sani Abacha na wengine waliweza kuupata na kuutumia tena kwa muda mrefu na wengine kuung’ang’ania hadi wakaondolewa ama kwa mapinduzi au mitutu ya bunduki.
 Je, Kikwete aliongea kwa mafumbo akimaanisha kinyume cha ugumu? Marais kama Yoweri Museveni, Robert Mugabe, Theodoro Obiang, Denis Sassou-Ngwesso au Blaise Compaore wangemsikia wangemcheka na kuthibitisha kuwa anayosema hayana ukweli bali kutaka kujipa sifa tu.  
Tangu kupata uhuru, urais umekuwa ni ufalme uliojificha kwenye koti la demokrasia. Hata Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, pamoja na usafi wake, alithibitisha hili pale alipoanzisha utawala wa chama kimoja huku akigombea na kivuli ili asiuachie huu ulaji wenye kila aina ya raha na ulinzi kisheria.
Hata hivyo, si mara ya kwanza kusikia uongo huu toka kwenye kinywa cha Rais wa Tanzania kwani hata Benjamin Mkapa alipoulizwa alipomaliza kipindi cha kwanza alisema hivyo. Ajabu aliwazuia wengine chamani kwake kumpinga ili aendelee na “kazi hii ngumu.”
Urais, hasa kwenye nchi zilizokataa na kuzika uwajibikaji na maadili ya utumishi wa umma, ni ufalme na fursa ya mwenye kuwa nao kujitajirisha yeye na watu wake wa karibu.
Ni nafasi ya kutengeneza utajiri, japo uwe haramu, wa haraka sana. Urais hasa wa Tanzania anaoongelea Kikwete ni rahisi hasa baada ya kubariki ufisadi na umangimeza. Tumpe mfano mdogo Kikwete. Urais ungekuwa mgumu na wenye changamoto za kiuwajibikaji angeweza kweli kuficha hata majina ya watu anaoandamana nao kwenye ziara zake za mara kwa mara ughaibuni?
Kweli Kikwete angeweza kuwa bingwa wa kuizunguka dunia kwa kuunguza fedha za umma ambao umepiga kelele kumtaka aache tabia hii ya ufujaji wa fedha za umma hadi ukachoka naye akaendelea kutumia mamlaka yake kusafiri nje?
Hapa nani anataka kumdanganya kiasi cha kumgeuza hamnazo akubali kuwa urais ni kazi ngumu wakati ni ulaji wa dezo hata bila kufanya kazi yoyote?
Hata kama tukikubali kuwa urais ni kazi ngumu kama Kikwete anavyotaka kutuaminsha, kuna maswali ambayo yakiulizwa ukweli unakuwa tofauti.  Kama kweli mbona kila mmoja anautaka? Ilikuwaje hata baadhi ya marais wakafikia hata kuiba fedha benki kuu kuupata.
Nani mara hii amesahau mchafuano ambapo vyombo vya habari vilitumika kuwachafua baadhi ya wagombea mwaka 2005? Nani amesahau baadhi ya waandishi wa habari nguli waliogeuzwa nepi za wagombea waliowachafua wenzao wakaupata urais na kuwalipa nyemelezi hawa fadhila hata kwa kuwateua kuwa wasemaji wao na wengine wakuu wa wilaya? Akina Salva Rweyemamu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu na Mihingo Rweyemamu wanaweza kuthibitisha hili.
Kama tutakuwa wakweli, urais si kazi ngumu hasa kwenye nchi ambapo rais yuko juu ya sheria akijifanyia atakavyo kama mfalme wa tawala za kiarabu. Urais utakuwaje mgumu wakati rais hawajibishwi kiasi cha kutumia nafasi hii na watu wake kula watakavyo? Ungekuwa mgumu kama kubeba zege nchi ingejiendea bila rais.
Hebu tujaribu kuthibitisha kuwa urais ni kazi rahisi ambayo kila mwenye kutaka kuukata haraka anautaka kwa udi na uvumba hata kwa kuvunja sheria au kuhujumu nchi yake.
Mosi, ukiwa Rais, mkeo watoto, wako hata waramba viatu wao wanakuwa marais kwa namna yao. Wanatumia nafasi yao nao kutengeneza utajiri wa haraka kwa njia mbali mbali.
Pili, unasafiri nje na kuizunguka dunia utakavyo kila unapotaka na hakuna anayekuuliza wala hulipii matanuzi yako.
Tatu, unapewa shahada hata bila kuingia darasani wakati watu wanasotea miaka hadi wengine kughushi wasipate.
Nne, unalindwa utadhani utaibiwa wakati hakuna mtu mwenye hamu hata ya kukuiba.
 Tano, mkeo na mashoga zake wanaanzisha kampuni ziitwazo NGO na kukata kutajirika haraka na wanapata wafadhili kirahisi kutokana na cheo chako cha rais.
Sita, mwanao, marafiki zake hata watoto wa marafiki na marafiki zako, wanatumia nafasi yako kugombea vyeo mbalimbali vya kisaisa kama vile ubunge na vinginevyo na wanavipata kutokana na kuwa watu wako. Waulize akina Ridhiwan, Dk Hussein Mwinyi, January Makamba, Stephen Masele na wengine watakupa ukweli.
Tumalizie kwa kuongeza msisitizo kuwa urais wa Tanzania si kazi bali cheo wala si ngumu kama anavyotaka kutuaminisha Kikwete. Matendo yake na waliomtangulia yanaonyesha hili bila kupingwa.
Hivyo, tusihadaike na maneno ya wanasiasa kuamini kuwa urais ni kazi na ni kazi ngumu. Hakuna, Kikwete aliponiacha hoi kama kusema eti angetamani akachunge mbuzi na ng’ombe na kulima mananasi. Ngoja amalize. Utamuona jijini sawa na watangulizi wake. Wakati huo muulize ahadi yake imeishia wapi. Hutopata jibu!
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 28, 2014.

Kijiwe chalaani upogo wa vigogo

LEO Mgosi Machungi anaonekana ana usongo na jambo. Alivyoingia mwenye mawazo, si bure. Baada ya kujiridhisha kuwa ni wakati muafaka kusema linalomsimbu, anaangalia huku na kule kujihakikisha kuwa wote tuko naye na kusema, “Mwenzenu leo sina furaha.”
Kabla ya kuendelea, Mbwamwitu anauliza, “Kunani Mgosi hadi ukose furaha?
Anajibu, “Si huyu mgosi Yusufu anayeendeea kutitia aibu wasambaa wote kwa kutiambia kuwa sisi siyo dijitai utadhani yeye ni hiyo dijitai yake. Anadhani sisi sote ni mataahia?”
Mipawa anauliza, “Mgosi mbona unalalamika na kutuacha Solemba? Kwani tatizo ni nini?”
Mgosi Machungi anajibu, “Ina maana hamisomi magazeti? Hamkusikia kuwa Jose Makamba anataka kumsimika mwanae Jan kuwa rais wa kaya hii wakati hana sifa zaidi ya jina kubwa?”
“Alaa! Kumbe unaongelea hii ya vigogo kutaka kuwarithisha ulaji vitegemezi wao utadhani ni kaya ya kifalme siyo? Huyu anapoteza muda wake. Maana ukimuangalia huyo kitegemezi chake anayesema amesoma hajaifanyia kaya chochote zaidi ya kuitumia kufika hapo alipo.” Anapayuka Mijjinga huku akikunja mikono ya shati lake utadhani anataka kumfundisha adabu Makambale.
Msomi Mkatatamaa hangoji. Anatia guu, “Huu uroho na roho mbaya sasa vimezidi. Umiss watoto wa vigogo. Ubunge watoto wa vigogo.Kughushi vigogo.Epa vigogo.Escrow vigogo.Kazi ubalozini watoto wa vigogo.Shule nzuri watoto wa vigogo.Scholarship watoto wa vigogo.Je hii kaya ni ya vigogo na vitegemezi vyao au wachovu?”
Kijiwe kinamshangilia kwa kupiga makofi na vigeregere kwa jinsi alivyounga mistari utadhani anarapu!
Mgosi anakula mic baada ya vigeregere na hoihoi kutulia, “Umenikumbusha huyu Januai aivokimbia shule ngumu hapa akikimbilia kwa Joji Kichaka. Kama baba yake ni mzalendo kwanini alimkimbizia mtoto wake nje?”
“Nadhani aliogopa kufeli tena. Nasikia kwa Joji Kichaka hata ukimpeleka kilaza wa mwisho hapa kayani atapeta tu kutokana na kuangalia fedha zaidi ya uwezo. Huoni madaktari feki walioghushi vyeti nje wanayotesa kwenye lisirikali?” Anaongezea Kapende aliyekuwa akijiweka vizuri kwenye benchi.
Msomi anarejea tena, “Wameharibu elimu. Wanakimbizia vitegemezi vyao nje. Wameharibu mahospitali wanakwenda kujiangalia afya zao nje. Kimsingi, watu wa namna hii hawapaswi hata kupewa kura ya kuongoza hata mbuzi. Hawafai hawafai hawafai hata kidogo.”
“Jamaa mie kaniacha hoi hasa pale aliposema eti huyo kitegemezi wake digitali. Digitali gani wakati kompyuta yenyewe kaanza kuitumia alipotoshewa huko kwa Joji Kichaka?” Anakamua Mpemba.
Mzee Maneno hajivungi. Anakatua mic, “Nadhani usomi wa kitegemezi cha Yusufu haunipi taabu. Wenye kaya tunataka mtu anayetokana nasi na anayefanana nasi. Mtu ambaye anajua na kuyashiriki matatizo yetu na aliye na uwezo wa kuyatatua na si kuyatumia kuzidi kutuibia. Tunataka mtu atakayeondoa huu uoza uliwawezesha hata wacheza ngoma za kienyeji kuwa vigogo bila hiyo elimu.”
Sofia Lion aka Kanungaembe hakubaliani na wasemaji waliotangulia. “Jamani acheni roho mbaya na wivu. Mbona kijana kasoma tena nje na elimu ya nje ndiyo inayoabudiwa hapa kayani? Halo halo mna dola nyie?”
Kanji anamchomekea Sofia hata kabla hajamaliza, “Ile toto iko soma sana hadi Amerika. Mimi ona faa sana kuwa rahisi ya kaya. Kama nagombea mimi pigia yeye kura.”
Mijjinga hamkawizi. Anakula mic, “Kanji unataka kumdanganya nani? Mbona kwenu mmechagua jitu zee tena lisilo na mke wala mtoto? Nadhani unamshabikia mtoto wa rafiki yenu aliyekuwa akitumiwa na Yusufuuu Maaaaanji kuibia kaya kwani hatujui?”
Kapende anapoka mic, “Hawa wanaounga mkono watoto wa vigogo ni wale wanaofaidika nao. Nani anataka rahisi atakayekuwa kama Joyce Wowowo huku baba yake akiongoza toka nyuma ya pazia kama Joji Kichaka na dingi wake?”
Mheshimiwa Bwege aliyekuwa ndiyo anamaliza kumkabidhi gazeti Mchunguliaji anakula mic, “Inaonekana kuna kitu hamjui hapa. Hamkumsikia Njaa Kaya akisema kuwa rahisi lazima awe kijana kama yeye alipoukwaa utadhani alikuwa kijana. Kama ujana ndiyo sifa ya pekee basi nendeni kwenye shule za sekondari mkatafute wagombea.”
Msomi hajivungi. Anakwanyua mic tena, “Mheshimiwa bwege usemacho ni kweli ingawa huyu Jan anachofanya ni kujijengea sifa ya kuwa kingmaker kwa yule atakayeingia madarakani kumkumbuka kama Ben alivyofanya kwa Njaa Kaya. Janja yake kipindi hiki haitafanikiwa. Nadhani kama ni wasomi tupo tena tulioiva. Hivi unaweza kumlinganisha huyu kitegemezi anayebebwa na jina la baba yake namia ua Dokta Silaha au Prof Ibra Lipu-mba?”
Kabla ya kuendelea, Mbwamwitu anachomekea, “Thubutu. Utamlinganishaje kicheche na tembo?”
Mpemba anaamua kuwavunja watu mbavu, “Nyie wallahi mwanikumbusha yalotokea kwetu pale walipomsimika mtoto wa Karumekenge wakati bomu. Sasa yu ahangaika ataka eti shemeji yake naye awe rahisi utadhani kaya ya kifalme. Tuwakataeni hawa waroho wa madaraka wallahi.”
Kapende anarejea, “Nadhani hatuna haja ya kupoteza muda na wabangaizaji na wasaka tonge. Huyo Joseph mwenyewe anayesema eti atamnadi kitegemezi chake kaya nzima afya yake ugogoro.”
Kijiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi la Jan. acha tumzomee hadi atoke mkuku akimuachia dereva kwa kuhogia huenda tungemfanyia kitu mbaya!
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 28, 2014.

Monday 27 October 2014

Hebu angalieni ubaguzi wa wahindi kwa waafrika


MISS UMEME 2014 SCANDAL UNFOLDS!


             The organisers of Miss Umeme Tanzania, Dar-based event promoters VIP (Latrines) Ltd, have strongly denied that corruption was involved in this year’s competition. Tanzanian social media are full of claims that Ms Paulina Fatma Pinduzi, popularly known as ‘Pap’, who won last month’s competition, forged her Tanzanian passport in order to qualify. In fact, it appears that she was born in Nairobi, Kenya. In a press conference held in VIP (Latrines) Dar es Salaam office yesterday, spokesman and long-time Miss Umeme organiser Mr J B Rungumalaya strongly denied any wrongdoing: “There is no truth whatsoever in the rumour that Ms PAP does not deserve the Miss Umeme crown,” he claimed, looking agitated. When asked by journalists to comment on Ms Pap’s Kenyan passport, a copy of which was posted on BongoForum’s website last week, Rungumalaya claimed: “This document is a forgery concocted by my enemies to rob me of the Ms Umeme franchise, which I have enjoyed for the last 20 years. Ms Pinduzi is Tanzanian born and bred. And by the way, I have incurred debts of USD 75 million to put on this very successful show, which is not vigisenti”, he fumed, claiming that most of the money had already been spent in promoting the event.
A finger of suspicion also points at the judges of the Miss Umeme 2014 competition, consisting of Dr Bono Nduluti, Chairman of the Federal Bank of the Middle East (FBME), Dr Saltpetre Mwongo, Minister of Regular Power Shortages (MRPS) and Dr Hanna Tabia Choka, Minister of Land Grabbing and Human Resettlement (MLGHR).  Why, critics claim, did the judges not check Ms PAP’s credentials, which had been rumoured suspect months before the contest took place. None was available for comment by the time of going to press. Dr Choka has already expressed her support for VIP (Latrines) promoter Rugumalaya, pooh-poohing the idea that corruption was involved in the Ms Umeme competition.
If stripped of her Ms Umeme crown, Ms Pap will be barred from representing Tanzania in the forthcoming Miss Umeme Universe competition. She may also have to repay the TShs 200 billion she received in prize money from the competition’s sponsors and may have to return the 100 MW genset generously donated by MeckMark (East Africa) Ltd.  Other sponsors of the competition include Tanzanian Taxpayers Ltd (TTL, an NGO), Standard Charitable Banking (HK) Ltd (SCB-HK), the International Independent Budget Support Group (IIBSG) Ltd., and Bold Wank Ltd (BW), a consortium of investors promoting Public-Private Partnerships (PPP) in the African beauty contest industry. (SCB-HK have already denounced the contest as a hoax and are demanding that the pageant’s organisers return their money). 
Contacted by this newspaper, a spokesperson for the Miss Umeme Universe organisers, the International Consortium for the Selection of Interesting Dollybirds (ICSID) said: “We are watching events in Tanzania closely: without a rapid resolution to this affair  it is unlikely that Ms Umeme Tanzania will be eligible to participate in the global event for an extended period.”

The Tanzanian parliament is expected to discuss the Miss Umeme crisis in the forthcoming parliamentary session.  Opposition Member of Parliament Kobe Mzito has been at the forefront in condemning Pap’s victory in the Miss Umeme Competition, claiming a conspiracy involving VIP (Latrines) Ltd and Ms PAP’s backers. “If this is a harbinger of how the Ms Umeme beauty pageants are going to be managed in future, then the beauty pageant industry will bring this country to its knees,” he said in an exclusive interview.  “If VIP/PAP can get away with this fraudulent contest, then we can expect more of the same going forward.”
Source: Guest Boozer

Why’s Mr Head mum on IPTL?


          President Jake Kiquette’s house’s on fire. The source of fire’s nothing but Independent perfidy and Thuggery Limited aka Interdependent papa and Tumbili Limited (IpTL). Donors have recently said it expressly that they’re not going to keep on pumping dosh to sinkhole aka the powers that be that don’t have any fiscal discipline. This is imperative by all standards. Again, boozers are shocked to see that the head of the same powers that be have kept mum as if this doesn’t concern him. Such silence can create a precariously wrong assumption that there’s a way he benefits from this sacrilege.
          Again, shall good donors stick to their guns, how’ll Mr Head run the hunk whose lifeline is but donors’ dosh? If I were him, I’d not cow or keep mum. Instead, I’d have already ditched those pals of mine despite what. At such a moment, survival tactics are important. If this happens, it won’t be the first or the last time Mr Biggie to have ditched his pals. Refer to what happened to his consigliore, Eddie Luwasha and Roasttamu la Aziz who wanted to cling unto political powers to no avail after Richmonduli f/o Dowans and Kagodamn s/o EPA became a thorny stuff for Mr Biggie. Mr Man, just do it again with rote, at least, to save your face despite the assumption, wrong as it might seem, that you’re part and parcel of all these ogres exploiting boozers.
          When I look at the cost of Escrew’s dosh of which swindlers screwed boozer, I smelly something fishy. Why’ve the powers that be kept mum? Is it because they’re among chief suspects of the crime? Refer to all those implicated as were unveiled by David Kafulia. The good MP named names such as Freddie We-rema, Saada Mkuyati, A Liar Kim Maswie, prof Beni Ndururu,  prof Sossie Muongo and Fleecing Muramba. Again, are these sacred cows better than all boozers whose hunk they rape wantonly and pointlessly? Where is Mr Biggie who always tells boozers that he loves them dearly?
          Let’s face it. IPTL, if is going on unabated as it is currently, it is going to throw our hunk in a Catch-22.  Boozers know that the thing was formed dubiously and illegally. They know that its capital was just 50 dollars though it illicitly claimed to have millions which it later scooped from our banks in conjunction with leechlike biggies. Donors know this too well.  We all know this, even birds do. Now what are the powers that be trying to hide if everything is but an open secret? Who wants to see his or her hunk been crucified simply because a few hard-headed creatures don’t want to carry their crosses? Is it fair for boozers to keep mum just like their head? Given that all lies and intrigues behind the creation and legalization of IPTL are out in the open, those responsible should be dealt with in order to avert the looming menace this thing might cause to our hunk. Arrest them and deliver them to Ukonga or Segerea to do their time.
          Importantly, while boozers need to bay for the blood of those bloodsuckers, they must avoid being tempted with ludicrous offers such as IPTL’s ploy of donating some dirty dosh to various organization as it was recently evidenced whereby Harbinger Set’s seen offering dosh to some dubious churches and some cops’ stations in Bongo. Such a suspect pretends to be an anthropologist. Why now after being implicated in a mega scam robbing boozers billions of dosh? Where was he before? This is unacceptable. Instead of accepting this grubby dosh, those receiving it’d ask the guy where he got it.
          If boozers keep mum or become inert, like Roasttamu la Aziz, the punk will run for a political office and get it. Once he snatches it, take it from me. He’ll become even more unbeatable just like other leeches we've in many political offices especially Mjengoni. Don’t you know the guys who are MPs not just because they've anything to offer except protecting their or their fathers’ biz? How does one mix politics and biz without facing conflict of interest?
          Now given that boozers are sick and tired of waiting to hear what their  head’s to say, and do, vis a vis IPTL, it is time to remind him that the ball’s squarely in his court. Thus, he’s to do the needful to avert the imbroglio boozers are facing. He’d declare his interest and offer leadership at this very time donors want to cleanse his house. We need to know if IPTL is the powers that be within the other.  And they’d tell us why if so? Are their some bigwigs behind this ogre? Who knows especially in Bongo where what’s done before the curtain’s totally different from what’s done behind it? Please Mr President utter at least one word boozers’ hearts will recover from the gloomy shock and malady of graft and wrong doings.
Source: Guardian Sunday.

Sunday 26 October 2014

Mlevi kuanzisha IpTL yake


          Baada ya kugundua wadanganyika wanavyodanganyika na kuibiwa kirahisi kwa kusalitiwa na wakubwa zao, nami nasukuti kuanzisha Independent perfidy Thuggery Limited aka Interdependent papa andTumbili Limited (IpTL) ambapo nitakuwa nawakamua walevi njuluku kwa kudai kuwa nitawauzia bangi na gongo kwa bei mchekea na wakati mwingine kuwapa dezo wakati ni mkenge. Najua nitashinda hasa ikizingatiwa kuwa mimi sitaiba njuluku ya wafadhili kama wao bali ya walevi. Hivyo, sina hofu ya wafadhili kusimamisha misaada yao ili kunikomoa. Kwanza, walevi si ombaomba na hawategemei misaada ya wafadhili. Nani anaweza kuwafadhili fyatu wasioogopa mtu? Laiti kaya nzima ingekuwa na akili na tabia kama zetu huenda haya manyang’au yangeishaGaddafiwa kama si kuMabutuiwa.
Naamini walevi watauingia mkenge kirahisi. Kwani najua hawatajali hasa ikizingatiwa kuwa kwao bangi na ulabu vinaruhusiwa kama haki za walevi tofauti huku kinachoruhusiwa ni ulevi wa madaraka na si wa gongo wala bangi. Hivi wavuta bangi na walevi na wezi wakubwa kama hawa wa IPtL nani wabaya kama tutakuwa wakweli? Hivi walevi wa bangi na gongo wanamwibia au kumuumiza nani zaidi ya wao wenyewe na saa nyingine na bi wakubwa zao? Je hawa wa madaraka wanaumiza na kuaibisha wangapi? Hivi kweli si aibu kwa kaya iliyojaliwa kila aina ya raslimali na aslimali kuombaomba utadhani tuliumbiwa jangwani! Hata jamaa zangu wamanga wa jangwani hawaombi. Wanajua jinsi ya kutumia wese lao. Nasikia siri kubwa ya mafanikio ya wamanga ni kutotoa uraia wao kama njugu kama ilivyo Danganyika ambayo wageni hasa matapeli wameigeuza danguro na shamba la bibi.
Hebu jiulize tunatoa uraia kwa magabacholi wangapi kwa mwaka? Hivi unaweza kwenda kwao ukapewa uraia? Je tumejaza wakimbizi wa kiuchumi wangapi? Mitaa ya Sinza mnanipata ambapo najua kuna matapeli kibao wa Kinigeria waliowaingiza mjini mabinti wa kibongo kwa ushamba wao wa kushobokea wageni wasijue ni apeche alolo kuliko wao. Je tunao wakenya wangapi ambao wanakimbia njaa na dhiki kwao wanaokuja kuchukua ajira za wadaganyika kwa kisingizio cha kujua ung’eng’e wakati hawajui kitu? Wangeujua wangesomesha vitegemezi vyao kwa M7? Hayo tuyaache.
           Kama nitafanikiwa kuanzisha IpTL basi mchongo wangu wa kwanza nitauita Escrew yaani Endelea kuwa-screw walevi hadi wakome. Nitakula bila kunawa tena kwa miguu na mikono baada ya kuangukia hii njuluku ya walevi.  Chini ya mchongo wa Esrew lazima nitawashirikisha mwanasheria mkuu wa walevi, waziri wao wa njuluku,  na wengine wanaoonyesha kushabikia ulaji wa kilafi wa mikono na miguu bila kunawa.
          Najua nikianzisha zali hili bei ya bangi na ulabu itapanda kiasi cha maisha ya walevi kuwa mabaya kama ilivyo nishati kwa wachovu ambao hata hivyo wameendelea kuliwa wakijiona wasifurukute. Hata hivyo, kuna haja ya kujali katika ulimwengu wa kulana kama samaki? Kwa vile nina jamaa yangu bonge la tapeli aitwaye Jimmy RugeSingasinga, lazima nimpe kibarua ya cha kuwaingiza walevi mkenge mchana kweupe. Ila kwa walevi walivyo fyatu kama sitafanikisha dili hili bila kuacha nyayo kama wale wapumbavu na waroho wakigundua watanichoma moto kama kibaka. Maana wanavyochukia mibaka bila shaka wanaweza hata kugawana nyama yangu na kuwapa mbwa kama siyo fisi.
          Kwa vile siku hizi bangi na ulabu vinaonekana kupungua, nitawafunga kamba kwamba nina mpango wa kufungua kiwanda cha kisasa cha kutengeneza ulabu na kile cha kusindika bangi na kugawa bure. Kwa vile walevi wanapenda sana vya dezo, watauingia mkenge wangu. Nitaita ahadi hii Maisha Safi kwa Walevi (MASAWA) ambayo kimsingi si maisha bora chochote bali kuwekana sawa ili walevi waliwe tu.
          Kwa vile nimesoma mchoro mzima wa IPtL kama ilivyoanzishwa akina Horse Kolimbaye,Kig-oma Milima, Saymon Mhaville, Ali Sahani ya Mwinyi, Ben Makapu Endelea Chenga, Abdi Kigodae, Dan son of Jonah, na majambawazi wengine wakubwa na wadogo waliowaingiza wadanganyika kwenye zali za IPtL inayozidi kuwanyonya na kuharibu maisha yao, nami nitafuata mbinu zote waliozotumia. Hata hivyo, nina shaka. Maana walevi pamoja na ulevi wao si mataahira kama wadanganyika wanaodanganywa na hata mafala na mataahira kama ilivyo. Ukiliangalia jitu kama Jimmy RugeSingasinga na jisura na akili yake mbaya unashangaa liliwezaje kuwaingiza mkenge? Ngoja niachane na sura za akina handsome and beautiful. Maana mtu anaweza akawa handsome lakini akaishia kuwa bogus upstairs na mwingine akawa ugly kuanzia roho akili hadi sura kama Dugong aka Dangerman Makapu. Hayo tuyaache.
          Tofauti na wadanganyika, mie sitaiba njuluku zaidi za walevi kwa kumtumia ponjoro wala gabacholi kama walivyofanya kwa kumtumia jambazi kibaraka wa akina Daniel arap Mwehu wa kule kaya ya manyang’au ambaye jamaa yangu hivi karibuni alinilalamikia kuwa wanajipenyeza Danganyika wakijifanya akina Mura wakati si kweli. Hawa jamaa kwa ulafi uchoyo na roho mbaya sina mfano. Nasikia baadhi ya vyombo vya umbea vinawalipa mshiko mkubwa huku wakiwa vihiyo na kuwapunja wadanganyika.Wachome wakitoe wakafakamie makande kwao. Hayo tuyaache.
          Nikishaanzisha IpTL naamini nitachanga njuluku kiasi cha kupata njuluku nyingi kuliko hata zile za EpA na Escrew ambazo nitazitumia kugombea urahisi na ulaji wa dezo ili kutanua ughaibuni na bi mkubwa na washirika zetu. Kwa vile walevi wamelewa sana kiasi cha kutojitambua, naamini watauingia mkenge sawa na huu wanaokaribia kubamizwa na akina Sam Sixx na Njaa Kaya.
          Nami nitashirikiana na walevi walio chini yangu ili kuhakikishia likibumburuka tunalindana kama wanavyofanya wao ambapo kila mwizi anajifanya hajui kitu wakati nyuma ya pazia unakuta kuwa wote ni kambale, wana sharubu au tuseme ni vyangu kwa vile wote wana magamba. Nani alidhani kuwa wale walevi wanaowakimbilia kushitakia uoza wao wameushiriki na saa nyingine wameoza kuliko hata hao tunaowaona mbele ya pazia?
          Kwa ufupi ni kwamba baada ya kugundua kuwa usaliti hasa wa kuwaibia wale waliokuamini unalipa nimeamua nijitajirishe kwa kutumia njuluku za walevi.
CHANZO: NIPASHE

Friday 24 October 2014

Hii nayo imekaaje?

 Ina maana kuna akina Rweyemamu wengine ambao hawajatosheka siyo? Kila mtu anataka kulipwa fadhila. Sasa wangoje jamaa aende kuchunga mbuzi huenda watafadhiliana huko kwa kupewa japo mananasi kama si ahadi ya maisha bora baada ya Ikulu.

DICTATORSHIP? GO TELL THAT TO THE BIRDS, MISTER MAKAMBA!

THE Tanzania deputy minister for Science&Tech, January Makamba, left many in stitches. He's quoted as espousing dictatorship as the only means to eradicate endemic graft...  That Tanzanians need a dictator to end corruption! 
One way to end graft is visible heavy punishment, he said. That's why dictators execute people in public, to show that those who try to overthrow them will face a firing squad. The aim is to induce fear,  Makamba argued. 
Wow! My foot...! Who wants a tyrant in these times of democracy, accountability and pursuit of human rights?
Makamba needs help to understand the dynamics of top leadership. 
However, there's no need to be shocked by such remarks from a guy who prides himself as an elite youth. Methinks Makamba's suffering from 'Chronic Political Monopoly Syndrome (CPMS), having been born and bred under tactful dictatorship whereby his political party has bulldozed the led for generations! 
Lets face it. Without his fathers name, Yusuf, what does January have to deserve being where he's today? 
Does he think weve forgotten that his father once said that his son would be appointed a Govt. minister? Lo and behold: he was so-appointed! Is this the style he wants us to accept to our peril? No, Sir; go tell it the birds! 
Who wants a dictator in multi-party politics? The likes of January are pulling us back to tyranny with the miseries currently evidenced! We need 'clean' leaders with vision and love of their country, not dictators. We need a 'clean' Constitution stipulating how to deal with venal leaders. 
Why doesnt January underscore the fact that, under Bennys dictatorship, Tanzania was wantonly turned into a private estate to benefit him, his family and friends? Why doesnt January appreciate the fact that Benny got away with it all because  another dictator protected him? 
The time for dictatorship is long gone and whoever seeks to  rejuvenate same must be feared like Ebola, HIV and leprosy, so to speak! 
We need leaders who uphold democracy, human rights, accountability; who have what it takes to deliver our people from poverty and tyranny, instead of using them to mint money for themselves! 
Ironically, January attacked his government that seeks to to enact a corrupt Constitution aimed at entrenching the status quo which unduly benefits those in power. 
However, the man's entitled to his views. Indeed, we need to do away with graft. But, we cant do this by installing self-seeking dictators as advocated by him. We need leaders who can apply law equitably and judiciously, not dictators whose personal dictates become law! 
We need leaders who'll use the Constitution to lead judiciously, not rulers who abuse it. We need leaders who abhor graft; who act sanely and responsibly; leaders who arent in cahoots with corrupt elements; who condone and protect criminals. 
We need leaders whom criminals' will fear and respect, not ones they can use wantonly... 
I'm aware that January undertook Conflict Resolution studies,
an academic field seeking to alleviate – and, possibly, put a stop to -- conflicts whose 'good' source is poor leadership, dictatorship! 
January accuses the extant system of embedding leaders obtained through corruption. If he seriously means what he says, shouldn't he be first to resign from that system? 
Suffice it to say that Tanzanians must beware of his likes, some of whom have plundered our resources and positions. 
In a nutshell, January is politically bankrupt, daydreaming of sending us back to the old dark days of tin-pot dictators...
Source: Business Times Oct., 23, 2014

Muziki wa wiki ni kwa wana ndoa


Hii nayo imekaa vipi?


Thursday 23 October 2014

Uprofesa wa Kikwete je ni aina mpya ya rushwa?

Rais Kikwete akipewa uprofesa wa heshima
Ukiwa na kasoro wengi wanaitumia kukugeuza kinyago hata mwanasesere. Wanakuchezesha kama kile kinyago cha Joyce Wowowo. Hivi Kikwete na uprofesa tena wa kilimo wapi na wapi? Je hawa kuna kitu wanachotaka kama vile kupewa ardhi wakalime chakula cha kulisha watu wetu. Je hii nayo si aina mpya ya rushwa? Kama hii si rushwa, mbona huo udaktari na uprofesa wa heshima hawapewi viongozi wa mataifa makubwa? Sijawahi kusika Obama kazawadiwa uprofesa wala Putin udaktari. Kuna haja ya kuwa na katiba inayozuia viongozi malimbukeni kuhongwa upuuzi kama huu. Kama unataka uprofesa au udaktari kasome.

Katiba feki imepita au imepitishwa?


          Vyombo vya habari viliripoti tukio la kupitishwa rasimu iliyochakachuliwa ya katiba mpya. Vilionyesha Chama Cha Mapinduzi, na vyama nyemelezi washirika wakie wakishangilia kufanikiwa kupora na hatimaye kupitisha katiba yao wanayoiita ya wananchi. Walishangilia hujuma na si huduma. Si jambo la kushangila kwa vile ni maafa kwa taifa na wao wakiwamo tokana na upogo na ulafi wao. Kwa upande mmoja ilikuwa furaha. Kwa upande wa pili wa Umoja wa Katiba ya Wananchi, (UKAWA) na wananchi wapenda mabadiliko, haki na uwajibikaji ilikuwa ni kilio.
          Pamoja na CCM kufanikisha hujuma hii kwa umma na vizazi vijavyo, kuna masomo mawili matatu tuliyopata kama jamii ya kitanzania.
          Kwanza, CCM imethibitisha wazi kuwa iko madarakani si kwa ridhaa na maslahi ya wananchi bali ya kikundi kidogo cha walaji kilichopania kuendelea kula hata kama ni kwa kuvunja sheria. Hili linapaswa kuwa onyo na kumbusho kwa umma wa watanzania kutafuta jibu ya jinsi ya kupata serikali na katiba vinavyowafaa. Maana hii rasimu iliyopita na serikali iliyopo haviwafai tena. Vingewafaa visingedharau mawazo na maoni yao. Visingewapuuzia na kuchakachua katiba yao waliyodhamiria kuandika.
          Pili, tumejifunza kuwa CCM na washirika zake hawana nia nzuri na taifa hili. Maana kwa walivyopoteza muda na fedha za umma ni ushahidi mwingine kuwa mambo si sawa. Hivyo, watanzania, kwa mara nyingine, wanapaswa kufikiri sawa sawa namna ya kujikomboa na kuondokana na ufisadi na uhujumu vilivyotamalaki kiasi cha kujipatia uhalali japo kwa njia haramu ya uchakachuaji wa rasimu na matumizi mabaya ya fedha za umma.
          Tatu, CCM wameonyesha wazi kuwa hawana huruma na wala hawaujali wala kuuheshimu umma uliowaweka madarakani. Wangeujali na kuuheshimu umma, wasingefanya madudu waliyofanya.
          Nne, tumejifunza kuwa watanzania bado wana safari ndefu ya kufikia ukombozi kamili hasa kutokana na tabia yao ya kuacha suala la katiba ambayo ni mkataba baina ya watawala na watawaliwa kupokwa na watu wachache wanaolinda madhambi na maslahi yao. Haiwezekani rasimu ichakachuliwe kwa kuondoa mambo ya msingi kama vile kupunguza mamlaka yanayotumiwa vibaya ya rais nao wakawa mashahidi kusiwe na tatizo tena kubwa. Haiwezekani mambo mazuri kama vile kupambana na ufisadi yaondolewa na watanzania wasifanye kitu kusiwe na tatizo kitaifa na kijamii. Je tatizo ni woga, ujinga au kutojua haki na wajibu wao kama jamii. Maana inashangaza kuona kikundi kidogo cha watu tena wenye kutia kila shaka kikajifanyia mambo kama kitakavyo kana kwamba taifa limeishiwa watu wanaofikiri sawa sawa.
          Tano, tumejifunza kuwa wengi wa wanasiasa wetu wamo madarakani kutumikia matumbo yao na si wananchi kama wanavyodai. Hivi, kwa mfano mbunge aliyeonyesha wazi kupinga rasimu iliyochakachuliwa akapiga kura kuiunga mkono kama hakuna namna ya hongo au kutetea maslahi binafsi. Kwa wanaomkumbuka mbunge huyu kidhabi, alinusurika kupigwa na wajumbe toka Visiwani baada ya kudai kuwa wanalalamikalalamika hovyo. Ajabu, ili kumaliza hasira zake binafsi na hao waliotaka kumtia adabu, ameramba matapishi yake kwa kuwa wa kwanza kuiunga mkono rasimu aliyoipinga. Imam mbunge huyu aliunga mkono baada ya kuahidiwa kitu au kulipiza kisasi kama siyo kwa kipindi kile alichopinga kutafuta gea ya kulipwa posho ya kila siku ya laki tatu.  Pia yupo mbunge wa Chama Cha Wananchi (CUF) aliyeenguliwa chamani na kusimikwa na mahakama aliyejitapa kuwa ndiye aliwezesha kupata kura mbili zilizopitisha jinai hii ikiwa ni njia ya kuikomoa CUF asijue suala la katiba si la chama wala mtu binafsi bali taifa na vizazi vijavyo. Huyu hakupaswa kuwa mbunge. Heri angeuza nyanya kuwa mganga wa kienyeji kama si mchezesha kamari.
          Sita, tumejifunza kuwa baadhi ya watu wetu bado wana tamaa na ubinafsi wa kutisha hasa ikizingatiwa kuwa wengi waliendelea ana Bunge Maalumu la Katiba (BMK) hata baada ya kuishiwa uhalali kisheria ili walipwe posho ya kila siku. Walitanguliza matumbo yao na kuuweka nyuma umma uliowaamini kufanya kazi hii adhimu iliyodhulumiwa.
          Saba, tumejifunza kuwa ufisadi Tanzania hautaisha hasa kama hujuma hii itapita. Na bila shaka, kama imevuka kizingiti cha kwanza, itapita kwa njia zile zile chafu na haramu, uchakachuaji hata wa kura ya kuipitisha.
          Hivi karibuni mwenyekiti wa Kamati bandia ya uandishi wa katiba bandia, Andrew Chenge alikaririwa akisema, “Bunge hili limeboresha Rasimu ya Katiba vizuri sana. Rasimu hii imebeba asilimia 75 ya maudhui ya Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba (Joseph) na nyie wajumbe mmeboresha kwa asilimia 25 tu.” Limboresha au limeboesha (bore)? Ajabu Chenge hakutaja ubovu wa hiyo aslimia 25 ukiachia mbali walipopata mamlaka ya kufanya hivyo na kwa misingi na sababu gani zaidi ya kulinda mafisadi wanaoogopa kuburuzwa mahakamani kama ingepita kama ilivyopendekezwa na wananchi.  Huwezi kuondoa vipengele, mfano, vinavyotaka viongozi kupeleka serikalini zawadi wanazopewa ukasema umeboresha. Huwezi kuondoa kipengele cha kuwawajibisha viongozi wanapofanya madudu hasa wabunge ukasema umeboresha. Kama kuboresha ni huku basi hakuna maana zaidi ya kukingia kifua ukale na ufisadi vilivyotamalaki ambapo uongozi umegeuka biashara ya kutengeneza fedha chafu na haramu kwa haraka kwa kuwaibia umma. Nadhani kwa sasa wezi wa EPA na Escrow wanachekelea. Wameshindaa. Wale waharifu wote waliofanya ufisadi madarakani waliostaafu sasa wanaashangilia. Mafisadi wanaopanga kuendelea na business as usual ya kuuibia umma lazima waangushe party.
Je katiba imepita au imepitishwa tena kwa mbinu, njia na nia chafu za kuendelea kuwashika mateka watanzania? Je huu ni mwisho au mwanzo wa mwisho wa kuiangusha katiba hii isiyojali wananchi?
Chanzo : Dira ya Mtanzania 

Tuesday 21 October 2014

Makamba anapomchimba Kikwete

NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, mtoto wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba aliyemtabiri angeteuliwa kuwa waziri, aliwaacha Watanzania hoi kwa kuonesha utoto na uhovyo wake.
Alikaririwa akisema, “Kiongozi anayetumia fedha kununua uongozi hawezi kupambana na rushwa hawezi kuleta mabadiliko ya aina yoyote katika nchi hii”. Je, Makamba anamlenga nani zaidi ya Jakaya Kikwete, japo hajawahi kukiri au kukanusha, ila ndiye aliyetuhumiwa kuingia madarakani kwa kununua wapiga kura kwa fedha ya EPA iliyoibwa toka Benki kuu?
Je ni kwanini Makamba ameliona hili au ni kwa vile hana fedha za kutosha kuhonga katika mbio zake za urais? Japo kiongozi aliyepatikana kwa rushwa na kuibia umma hafai, hata hawa wanaoona hili kama tatizo kwa sasa wakati walikuwa na nafasi ya kuliongelea zamani hawafai pia.
Je, Makamba ameishiwa hoja? Maana gia yake kubwa ilikuwa ni ujana bila kujali kama mhusika ni fisadi wala nini.
Makamba hakuishia kwa mtu binafsi bali hata mfumo mzima unaoelea uoza ingawa naye ni tunda na matokeo ya mfumo huo huo anaoushambulia kwa sasa kama janja ya kutaka aonekane mwana mapinduzi wakati siye.
Alisema, “Kama mfumo wa uchaguzi unaingiza viongozi kwa rushwa au viongozi waliowahi kula rushwa, tusahau kabisa nchi hii kuondokana na rushwa. Hapo ni pa kupafanyia kazi sana.” Je, aliyebariki jinai hii zaidi ya chama chake ni nani?
Hivi kweli anaweza kutoka mtu yoyote ndani ya CCM akafanya tofauti na mazoea yaliyoiweka madarakani miaka yote tena kinyume na utashi wa wapiga kura na wananchi? Rejea ambavyo imekuwa ikichakachua kila uchaguzi tangu kuingia mfumo wa vyama vingi.
Je, Makamba ameyasema hayo ndani ya chama akapuuziwa akaamua kumwaga mtama au ni ile hali ya kutaka kujipatia umaarufu kwa kujionyesha kama mtu anayepiga vita rushwa wakati yeye ni matokeo ya mfumo ule ule?
Je, Makamba ameanza kuunda mtandao wake unaojifanya kuwa tofauti na chama kama alivyojaribu Samuel Sitta akaangukia pua? Sijui kama konokono anaweza kukana gamba lake akaishi.
Makamba ni tunda na kizalia cha mfumo huu anaoushambulia. Anaweza kuukana. Ila bado hataukimbia kwa vile uko kwenye damu yake. Angekuwa anataka kueleweka, basi angejitoa CCM kwanza.
Je, January angeweza kuyasema haya wakati baba yake akiwa madarakani akimuandalia nafasi ambayo aliipata kama baba yake alivyotabiri wakati akijivuna kuwa amezaa watoto wenye akili?
Makamba alizidi kuonyesha kuwa anayajua mengi ingawa wengi wanaona kama amechelewa kiasi cha kuuliza: Kwanini anayesema sasa na si siku za nyuma kama kweli ana nia njema.
Alisema, “Kuna wizi na ubadhilifu mkubwa siyo tu kwa viongozi wa kisiasa, hasa kwa watendaji na watumishi wa kada za kati na chini. Watu wanawatizama wabunge na waziri pekee wakati wapo wahasibu wa wizara na halmashauri.” Zaidi ya chama chake, nani anawalinda wabadhirifu hawa?
Nani amesahau kashfa ya uuzaji wa madawa feki inayomkabili  mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es Salaam Ramadhani Madabida, anayeendelea kukaa ofisini pamoja na tuhuma nzito kama hizi?
Makamba aliongelea sifa za anayepaswa kuwa rais ajaye. Alisema,“Awe na uwezo wa kuwaunganisha Watanzania kwa sababu kama mnavyoona chembechembe za mgawanyiko zimeanza, mgawanyiko kati ya Tanzania bara na Tanzania Visiwani, mgawanyiko wa kidini na kikanda.”
Inashangaza Makamba kuongelea mgawanyiko wakati chama chake kimeuridhia kwa kuchakachua rasimu ya wananchi. Je, ina maana kuwa Rais Kikwete ameshindwa kuwaunganisha watanzania kiasi cha waziri wake kulalamika?
Kauli ya Makamba inaonyesha hata mgawanyiko ndani ya serikali ambapo waziri anaweza kumnanga bosi wake wakati ana uwezo wa kukutana naye akaeleza maoni yake au hiyo nafasi hawapewi?
Je, Makamba anataka nani abebeshwe mzigo wa hizi tuhuma zote ambazo zinaonyesha wazi kuwa mambo si sawa zaidi ya Kikwete? Je, Makamba anaanza kujitofautisha na Kikwete baada ya kugundua kuwa muda wake wa urais umekwisha?  Kwanini alingoja saa ya lala salama kama kweli ni mtu makini na wa kupaswa kuaminiwa?
Kwa wanaojua madudu yaliyofanyika chini ya utawala wa Kikwete, hawashangai madai ya Makamba zaidi ya anayemlenga. Bila shaka hapa anayelengwa si mwingine bali Rais Kikwete.
Je, Kikwete atayachukuliaje madai haya ya waziri wake ambaye alipaswa kuyatoa kwenye vikao vya chama? Je, wakati wa kila mtu kufa kivyake umefika ambapo marafiki watakanana na kuumbuana kama alivyoanzisha Makamba?
Kweli ulaji tena wa dezo mtamu kweli! Nani alitegemea watu kama Makamba waugeuke mfumo uliwaumba na kuwafikisha pale walipo. Je, wanadhani kuwa watanzania wamesahau historia zao na matendo yao? Je, watanzania ni wepesi wa kusahau hivi?
Ni raha namna gani Makamba anapomchimba Kikwete akitegemea kumrithi. Je, Kikwete atamsamehe kwa kosa hili? Yetu macho. Muhimu ni kuwaasa watanzania wasihadaike na maneno mazuri. Wakumbuke kuwa hata nyoka husifika kwa kuimba nyimbo nzuri kuwavutia wadudu ambao hatima yao ni kugeuzwa kitoweo.
Chanzo: Tanzania Daima Oktoba 22, 2014.

Kijiwe kutoshiriki kura feki

WIKI iliyopita Kijiwe kilimkumbuka nguli mwalimu Julius Mchonga. Japo wale waliowatengeneza, kuwatengenezea na kuwaachia ulaji walimtosa baada ya kuwa wakimsanifu kila mwaka, sisi tulimkumbuka kwa dhati na kweli. Kwa kuendeleza mapambano ya kuleta haki na usawa aliyoanzisha mzee Mchonga, Kijiwe kimepanga kutoshiriki kwenye uchakachuaji wa kupitisha katiba feki iliyoacha maswali mengi kuliko majibu.Kama wamechakachua Idodomya watashindwa nini kuendelea na ujambazi huu?
Leo Msomi amewahi kijiweni kuliko wote. Inaonekana ana jambo linalomkera. Maana hata usoni hana bashasha kama kawaida.
Baada ya kujiridhisha kuwa ni wakati muafaka wa kuanza mada, anajiweka vizuri kwenye benchi na kusema, “Mwenzenu usiku sikulala vizuri. Maana nilikuwa nawaza jinsi ya kuepusha kaya yetu kuingizwa mifukoni mwa mafisadi hasa kwa kuwapa kibali cha kuendelea kutugeuza mabunga na kitoweo chao kupitia kushiriki kinachoitwa kura ya kupitisha katiba mpya ambayo si mpya chochote bali kiini macho na maigizo ya kitoto na kishenzi. Sijui wenzangu mnasemaje?”
Mijjinga anakuwa wa kwanza kula mic, “Msomi una hoja na umefanya vizuri kuweka jambo hili hapa mezani. Nadhani kabla ya kuamua kushiriki hiki kiini macho, tungepewa kwanza maelezo ya escrow na namna watakavyoziba pengo la fedha waliyogomea wafadhili.”
Anapiga chafya na kuendelea, “Unaona hata chafya inakataa! Hata wafadhili wamegoma kugeuzwa shamba la bibi kwa kutoa njuluku zinazoishia kuliwa huku wanaofanya hivyo wakiendelea kujitia hamnazo, wakiomba waongezewe waibe zaidi.”
Kapende anakwea mic, “Nangoja kumsikia yule kihiyo Masele akiwabwatukia kama alivyosema kwenye skandali ya Escrew. Pia nangoja kusika kauli ya mjivuni Mura Werema kuhusiana na kuumbuliwa huku. Nakumbuka alivyomtishia balozi wa Uswazi kuhusu njuluku zilizofichwa kule. Sijui nazo zimeishia wapi. Ajabu hata Njaa Kaya anajifanya kutosikia joto ya jiwe!”
Msomi anadakia, “Asisikie joto ya jiwe yeye nani? Nadhani anachofanya ni kungoja mambo yapoe aende kuwaramba miguu wamsamehe japo amalize ngwe yake. Tena kabla sijasahau, mmesikia skandali yake ya kuhongwa saa ya Rolex na tapeli aliyempa ubalozi wa heshima wakati si chochote wala lolote bali mwizi wa kawaida?”
Mgosi Machungi anajibu, “Tangu jamaa ahongwe suti tilimzalau. Usishangae kashfa hii ikafutikwa chini ya busati kwa kuleta sanaa nyingine. Wako wapi waiokwepa njuuku Uswazi? Nani anajai?”
Mipawa ameng’ang’ania rasimu ya Waryuba. Anakula mic, “ Kukata mzizi wa fitina lazima turejeshewe rasimu orijino ya jaji Waryuba vinginevyo kushiriki huu upuuzi ni sawa na kujitia kitanzi kwa hiari ya kura zetu ambazo bila shaka zitachakachuliwa na kudharauliwa kama ilivyotokea Idodomya walikododomya demokrasia na rasimu orijino ya wadanganyika.”
Mgosi Machungi anapoka mic, “Waioihujumu na kuhaibu fedha yetu wafungwe maisha. Hatiwezi kupoteza mabiioni ya kuwapa hao waliokutana kutuibia na kudharau na kuchakachua mawazo na haki yetu haafu watu wakaendelea kuturingia mitaani baada ya kuwapa kura zetu. Mimi sishiriki hata kama ni kwa kutiwa kitanzi.”
Mpemba anakwanyua mic, “Waliohusika wote wasiruhusiwe kushiriki na wajiuzulu ili watu safi wachukue nafasi zao. Maana twachezewa mahepe nchana kweupe. Tukataeni jamani.”
Kapende anakwanyua mic, “Hawa wajivuni na mafisadi wanaodhani yamekwisha wajue ndiyo yanaanza. Tusishiriki zoezi la kuhalalisha haramu yao huku tukiweka saini hati ya kifo cha kaya yetu na vizazi vijavyo. Tunataka katiba kweli lakini iwe mpya na itokanayo na utashi wetu na si nguvu na hila za mafisadi na wezi wa mchana. Katiba lazima iongelee ufisadi kwanza maana haya mambo ya kuhongana kila upuuzi na kuuza kaya hayavumiliki.”
Mbwamwitu anakula mic na kusema, “Acha nikuongezee. Katiba lazima itangaze kuwa na kaya moja na si vipande vipande kama ilivyo.  Hivi kusingekuwa na kipande cha zenj huu ujambazi wa kura ungefanikiwa vipi?”
Mpemba anaguna na kusema, “Wallahi heri kila mtu aende kivyake ati kama mwataka tuwe kaya moja.”
Bi Sofia Lion aka Kanungaembe kapata upenyo! Anazoza, “Nanyi mkienda kivyenu mtasambaratika. Hapa najua ami anataka Pembe iende kivyake na Zenj hivyo hivyo.”
Kanji anakamua, “Kama vunja ungano tapata tabu sana. Mimi iko ona India na Pakistan. Ilipovunja ungano lianza gombania witu howo howo. Hiwo mimi sema hapana tengana. Kama nataka amani basi fanya kaya moja yote iwe sawa.”
Mpemba haridhiki, “Wafahamu? Hata hawa mahabithi walochakachua rasimu walitaka epuka hili wasijue ndo walipa nguvu. Kama tungekuwa na sirikali tatu maana yake kila upande ungepata nguvu na uchaguzi wa kuendelea au la. Sie twataka sirikali tatu ili kila mmoja aheshimu mwenzie ati.”
Mheshimiwa Bwege alikuwa kimya kitambo. Anaamua kutia timu, “Mie naona wote hamjakosea. Kinachopaswa kufanyika ni maridhiano na makubaliano. Kama wachovu wangetaka hata sirikali mia nyie yawahusu nini. Ajabu eti wale wanaowaibia wanawadanganya kuwa sirikali tatu zitaongeza gharama. Mbona wanapochora michoro kama EPA, Escrew na mingine hawaoni huu uchungu kama siyo urongo na woga wa kawaida? Warejeshe rasimu ya Waryuba ndipo kieleweke vinginevyo kuna kila sababu ya kugomea hiki kiini macho kama alivyokiita Msomi. Tukatae katakata kushiriki jinai hii kwetu na vizazi vijavyo.”
Kijiwe kikiwa ndiyo kinanoga si lakipita shangingi la Sam Sixx. Wacha tumtoe mkuku ili kumfanyia kitu mbaya. Bahati yake. Kama si ndata kurusha mibomu ya michozi angepatikana!
Chanzo: Tanzannia Daima Oktoba 22, 2014.

Sunday 19 October 2014

Huwa napenda sana Makossa orijinali toka kwenyewe!


IPTL, donors stick to your guns please

          No joke. Independent Power Tanzia Limited is fleecing boozers. Since its inception under Ruksa regime, this thing has become an ogre to boozers. Since it came into being, instead of solving power problems that’s used as a pretext of its creation, it has worsened everything especially after becoming a good conduit of robbing boozers. I recently received a dossier showing the history of this weak-willed creature dating back to 1994. Many big names feature high in this thuggery to the hunk.
          When you read this please do so inaudibly so that nobody hears you. The dossier says that the late Kig-oma Milima, Horrie Kolimba and Bill Shija were the honchos of the whole make-believe. It goes on touching on names such as Mzee Ruksa, Ben Makapa, Jake Kiquette who was then minister responsible for energy and other matters, Abdie Kigo-da, Endru Chenga, Kamazima, Jimmy Ngasongwa, Saymon Mhavile, Raph Mollel, Eddie Maoki Majogoo, Merry Ndosi, Dan son of Jonah, and many more big filches who received their cuts and vended the hunk to international and local conmen. So you can see from the list how thugs in this open sesame are well connected. Actually, they’re not only connected but they also are the powers that be.
           I recently felt relieved when one boozer informed me that donors have decided to step in to save boozers who seem to be at home with this long-time economic slayer. After our hunk suffered from chronic power cut and power hiking, donors wrongly thought that boozers would wake up from the slumber and take actions.  Sadly though, boozers are always on deck for eaters. They don’t bother with anything except their booze and other nonsensical things such as fiestas, get-togethers and merrymakings.
          After IPTL discovered that boozers are unreasonable and mad, it decided to scoop even more dosh. After metamorphosing in something next to a devil itself, it went to the Bank of Thieves and scooped over 200 grand million. For the first time this hit home so as to cause brouhahas even in mjengoni where we evidenced the govt’s chief counsel, Mura Freddie We-rema threatening to behead an MP after calling him a mandrill. Reasonable and probable people wondered how a govt chief counsel can play devil’s advocate if there wasn’t something fishy.
          After the powers that be found that the cat was out of the bag, they tried to find other flicks in order to deflect the attention of boozers. New Constitution aka constipation epic movie showcased by Sam Sixx was brought in to easy down the attention. One, Davie Kafulia, stood his ground. IPTL went to the court to seek protection against being dressed down even more. The court granted its will wee knowingly that donors were watching. Now we’re told that the hunk is likely to miss a trillion schilling simply because of protecting IPTL which seems to be a govt within another thanks to the names of its current and former bigwigs mentioned in the scandal.
          Reliable sources quoted the Permanent Secretary Ministry of Dosh, Dr Sevacius Likwe as saying, “And this comes as a result of donors demands that issues related to IPTL to be resolved first…this IPTL issue was never in our agreements.” I suppose. Yeah it was not an issue given that some bigwigs wanted to get away with murder. To boozers this is a big issue that should be addressed before being given more dosh to swindle.
          Again, looking at what donors say, the matter’s an issue. Finnish emissary Sinikka Antila had this to say, “Budget support development partners in Tanzania take the emerging IPTL case with the utmost seriousness and are carefully monitoring its development as the case involves large amounts of public funds.” Antila is dead right. How can donors keep on pumping dosh to a venal govt while this dosh is the taxes of their diligent and hardworking earthlings? Who wants to keep and feed a leech or Jennie? If boozers can donors can’t.
          If donors want Bongo forge ahead, this IPTL thing must be slayed once and for all. For, it has sucked boozers to the extent that it wants now to swallow them.  Just imagine. The thing apart from offering poor services, it contaminates and pollutes our environment. Yet it is paid millions of bucks simply because it is connected to biggies. This hunk is for boozers not their venal biggies. So donor, please stick to your guns to see to it that this monster is slayed and felled. Please donors show these goons how rash and parochial they’re. Insofar as they think they’re smart while they actually are automatons, please never make a U-turn as far as IPTL is concerned. Never allow the ape to preside over the case of the rascal. They are all the same cabal.
Source: Guardian Oct., 19, 2014.

Saturday 18 October 2014

Draft Constitution: Will CcM get away with murder?


          Looking at the look of things, it is obvious. Chama cha Maulaji (CcM) is wantonly hell-bent to superimpose its will on Tanzanians. Refer to the recent sideshows whereby CcM was able to “pass” the so-called new constitution that’s nothing new but only old stuff. How can the said document be referred to as the constitution of the people whereas the same people were sidelined, and their views being snubbed?  Who are these people in the first place? Do people mean a gang of self-seekers who doctored the document to foster and protect their hidden interests? When they started voting to pass the thing we’re told that CcM fell shy of required votes. All of the sudden, manoeuvers were employed and the said numbers balanced after the fate of the constitution hanged in balance.
          Elations, self-flattery and whatnot were evidence as the dying horse managed to legalize its hocus-pocus. Caught between a rock and a hard place, CcM applied every trick in the book to see to it that its project succeeds even if it meant rigging aka chakachua. Will CcM get away with murder?  Will Tanzanians swallow this bitter pills aimed at allowing a kit and caboodle of swindlers to fleece them wantonly?
          Now we’re told that the thing is waiting for presidential assent, which it will surely get, ready to be rolled over to the voters. Will the voters offer their consent to the thing they know is the product of deceit and self-preservation for people grappling with allegations of corruption? Will hoi polloi stay side and look as we witnessed them during the haggling of passing the doctored document while, in the end, they are the ones to get a raw deal? Will they rebel and say enough is enough this time around? Verily, time will tell.
          For those who bothered to follow what was going in Dodoma under Bunge Maalum la Kuula (BMK), will agree with us that everything was but a sham. After Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) staged a good fight, CcM had all signs of losing the battle had it not for the eleventh hour that allowed them to doctor and pass the document.
          It is on record that 25% of the original document was either/or tampered with. Andrew Chenge, the chair of fake committee that was tasked with writing the draft was quoted as saying that they better 25% of the document. Ironically, Chenge didn't show the weakness of the document something that’d warrant the betterment of the same. Did they better it or batter it? The major questions are: Why was it doctored whereas some articles were removed or changed? Who authorized such a crime? Who empowered self-style BMK that lost legality after UKAWA boycotted the proceedings?
          Although CcM may go on with this pipedream believing that the battle has been won, my foot, the battle is yet to commence.  We heard some bigwigs championed by Judge Joseph Warioba and UKAWA vowing to continue with the fight to see to it that the thing doesn't go anywhere. Again, looking at how the thing was arrogantly passed, we’d urge them not to allow people to participate in the process they know won’t be free and fair. The same “tricks of the jungle” that were employed in this monkey business in Dodoma will be deployed to see to it CcM gets off the hook. This being the case, what should wananchi do? Simple, boycott the potpourri of deceits and scam so that those plotting to hoodwink them get the lesson that they’re not the boobs they think they’re.
          In sum, if CcM thinks it can get away with murder, it’d think again. Given that our people wanted a new constitution, they’d get it but not this gobbledygook known as new constitution without anything new but dupery, trickery and jiggery-pockery. Again, will CcM get away with murder? Will wananchi allow it to hoodwink them once more? Time will tell surely.
Source: Business Times Oct., 17, 2014.