The Chant of Savant

Tuesday 28 February 2017

Tanzania imefikia kupewa ardhi yake na walioiibia!

Image result for photos of makonda kigamboni
            Kampuni ya Azimio Housing Estate, iliyotuhumiwa kujihusisha na ufisadi kwenye mradi mzima wa Dege Eco Village ilitoa mpya kwa eti ilijifanya kuwa na huruma na kuwajali watanzania kwa  kutoa hekari 1,500 bure kwa mkoa wa Dar Es Salaam ili kujenga viwanda vidogo vidogo. Wema mara nyingi ni kitu chema japo kinaweza kuwahadaa wengine hasa unapotendwa na mtu mwenye kutia kila aina ya shaka. Sina ugomvi na wema kupitia kutoa misaada inayohitajiwa na jamii. hata hivyo, nina ugomvi na sifa na dhima ya kutoa misaada husika hasa mtoaji anapokuwa na mawaa au tuseme tuhuma za kuwahujumu wale wale anaolenga kuwahadaa kwa kujifanya anawajili kiasi cha kujinyima na kuwasaidia leo wakati aliwaibia jana.  Ieleweke; sina haja ya kuwa hakimu katika kashfa hii ambayo kesi yake bado iko mahakamani. Ninachojitahidi kufanya hapa ni kuonyesha utata na shaka vinavyoweza kujengwa na msaada wa namna hii na wakati unapotelewa ukiachia mbali mazingira ya kuupata ambayo hayajabainishwa. Kwanini sasa ambapo mtoaji na mpokeaji wanaandamwa na kashfa kibao zote zikijikita kwenye upatikanaji na ulimbikizaji haramu wa mali?
            Ukiachia kuhoji muda na watoaji na wapokeaji misaada, napata taabu sana. Je tunahitaji kupwakia misaada kama jamii bila kujua nani anatoa na kama ana sifa hasa pale tunapojua kuwa mhusika ni mtuhumiwa katika kashfa ya wizi mkubwa kwa taifa ukiachia mbali lengo la kufanya hivyo? Je tumegeuka wa hovyo kiasi cha kupewa vitu vidogo vidogo ili tusiulize vikubwa vikubwa vimeliwa na nani?
            Je Mkuu wa Mkoa aliyepokea ardhi kwa niaba ya rais alijiuliza namna nchi ambayo sheria inatamka wazi kuwa serikali yake ndiyo yenye dhamana ya kusimamia ardhi kwa watanzania ilikuwaje maskini wa ardhi hadi kupewa ardhi na watu binafsi? Je huyu mkurungenzi wa Azimio Housing Estate, Mohamed Ikbar, alipataje na lini ardhi hii anayogawa? Je nani atamrejeshea fedha aliyotumia kununua ardhi husika kama kweli aliinunua? Je anategemea kupata nini au anajenga mazingira gani? Kinachoshangaza sana na kuhuzunisha, utakuta baadhi ya wale wale waliohujumu taifa letu na kufanya vijana wawe maskini ndiyo hao hao wanaojifanya kuwajali kwa kuwapa udohoudoho huku wao wakikalia makubwa. Kuna ushahidi wa wazi kuwa kuna watendaji wetu wanaopwakia kila kitu bila hata kufikiri wala kuhoji. Mfano mzuri ni mbunge Mbunge wa Mkuranga (CCM), Abdallah Ulega alikrarirwa akibariki upogo huu akisema “papai si haramu, ila kinachotokana na papai ndicho haramu ambayo ni pombe ya gongo. Sasa kama mtu katoa ardhi yake bure tupambane kupata viwanda maana ajira hakuna. Tupate Sido kubwa na siyo kuwaza mtu aliyetoa ardhi hiyo,”
            Kama jamii na taifa, je tutaendelea na upofu, uroho na upogo huu hadi lini? Yaani tumegeuka samaki kutegwa kwa utumbo wetu wenyewe? Samaki ni hayawani. Je sisi tumeridhika na uhayawani huu tena wa kujitakia? Nani ameturoga.
Tunashauri yafanyike yafuatayo:
            Kwanza, kabla ya Azimio Housing Estate kutoa ardhi, ima ichunguzwe ilivyoipata huku serikali ikiulizwa ilikuwa wapi hadi inakuwa maskini wa ardhi wakati ndiyo yenye dhamana ya kusimamia ardhi nchi nzima?
            Pili, hili dili la Makonda na Ikbar lizuiliwe ili kujua ukweli wa ardhi iliyotolewa na namna ilivyopatikana? Waingereza wana usemi kuwa amlipaye mpiga filimbi ndiyo huchagua nyimbo. Je tunahitaji msaada wa watu ambao wametumia mianya ya ufisadi na upumbavu kwenye mfumo wetu hadi wanatupa kilicho chetu wakati ni chetu tena wakiondoka wakijiona wametutendea hisani wakati siyo?
            Wasiojua chanzo cha maswali haya, warejee ukweli kuwa mwaka 2015 Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa fedha  aligundua ufisadi wa kutisha ambapo inadaiwa kuwa NSSF imenunua ekari hizo kutoka kwa mbia mwenzake Azimio Housing Estate Limited kwa zaidi ya Sh800 milioni kwa ekari, wakati shirika hilo linamiliki viwanja vingine maeneo hayo vyenye thamani ya Sh4.5 milioni kwa ekari. Kwanini Azimio Housing Estate wasimalize kashfa hii ambapo hata hizi hekari 1500 ni sehemu ya kashfa. Huu ni ukarimu au kugeuzana majuha. Vijana wasitumiwe kuhalalisha ufisadi tena uliofanywa dhidi yao. Kwanini serikali isitaife hii ardhi kama watuhumiwa watashindwa kutoa maelezo yanayoingia kichwani? Je hawa siyo wale ambao waziri mmoja waliyetaka kumhonga kama alivyodai aligwaya kuwataja majina? Ilikuwaje akaficha majina yao?  Kuna haja ya watendaji wetu kujifunza kujenga shaka na kila anayetaka kuwafadhili kwani si wote wanaowafadhili ni wasafi au wanafanya hivyo kwa nia njema zaidi ya kuficha uovu wao. Haiwezekani maafisa walioshiriki kwenye kashfa ya Dege eco village wawe gerezani wakati washirika wao wakitoa sadaka kwa serikali ili wasamehewa madhambi yao. Kwanini waswahili hatupendi kujifunza? Kila kashfa nyuma yake kuna hawa hawa na wanawaacha washirika zao solemba huku wakiendela kusuka madili mengine tokana na ukosefu wa kushukiana na kupenda vya dezo. Huu msaada wa Makonda si wa dezo na wala wa nia nzuri.
            Tumalizie kwa kuwashauri watanzania wasikubali kugeuzwa samaki kutegwa kwa nyama yao wenyewe. Badala ya kupwakia ofay ardhi inayodhaniwa ni ya ubwete, tuhoji upatikanaji wake na sifa binafsi za wahusika tusije kuingizwa mkenge kwa kuhalalisha harama na mauti yetu kama jamii na taifa.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.

Kijiwe chataka rahis aunde tume ya Escrew na Lingumi

Image result for lugumi enterprises photos

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema
                Baada ya kushuhudia sekeseke, hata kama ni kisiasa, la kupambana na bwimbwi, kuna somo tumejifunza. Tumejifunza kuwa tukiamua tunaweza. Tunaweza lolote lile ilmradi tuwe na utashi kisiasa na kijamii. Hivyo, leo Kijiwe kinatumia somo hili kupanua wigo lau tuweze kuwa na kaya safi, salama na yenye mafanikio ambapo kila mchovu anapata riziki yake na utajiri kihalali badala ya mazoea ya kuibiana na kuumizana. Katika kuondokana na mkwamo uliokuwa umeanza kuzoeleka na kuhalalishwa, tunashauri baadhi ya hatua mujarabu ili kukabiliana na matatizo na kadhia nyingine tena ambazo ni sugu na hatari kuliko hata bwimbwi.
            Mgoshi Machungi analianzisha “jamani hivi kashfa za Ungumi na Eskoo zimeishia wapi; mbona sisikii daktai wa kutumbua majibu akizitumbua au tumeingizwa mkenge tena? Mimi sieewi kusema ukwei.”
            Kapende anachomekea “unashangaa kitu ambacho ni cha kawaida! Haya ndiyo matokeo ya uvivu wa kufikiri ambapo yule aliyetutukana kuwa tu wavivu wa kufikiri alituuza na akajiuza mwenyewe huku akiendelea kukingiwa kifua na wavivu wenzie. Nani anaongelea Escrew na Lungumi wakati sinema imehamia kwenye bwimbwi?”
            “Yakhe hapa umepiga kwenyewe wallahi. Mie sidhani kama tutaamua kukumbushia hizi kadhia kama zinaweza kuzikwa tukiamua. Kama waathirika wa wizi huu wa kutisha, lazima tupaaze sauti zetu lau haki itendeke. Au vipi?” Kapende anajibu.
            Mipawa anakula mic “Ni kweli. Hakuna haja ya kushangaa. Nani asiyejua kuwa nyuma ya kashfa hizi wapo wazito wanaotumia madaraka yao kuendelea kutuzingua kwa kuanzisha hili na lile ilhali matatizo makubwa kama haya yakisukumwa chini ya busati? Tunapaswa kulikumbusha lisirikali kuwa lilituaminisha kuwa litapambana na uovu na uoza zikiwamo kashfa za Esrew, Lungumi, IptL, uDA na nyingine nyingi. Kama wameweza kuanzisha sekeseke la bwimbwi, wanashindwa nini kushughulikia mazimwi haya kama hawana namna wanavyonufaika nayo?”
            Mheshimiwa Bwege leo anaamua kutia guu wakati mada ikiwa mbichi. Anakula mic “mie napendekeza Kijiwe hiki kitukufu kiunde tume maalum kupambana na balaa la escrew ambapo matapeli wa ndani na nje hushirikiana kuwaibia wadanganyika tena kwa kushirikiana na wanene uchwara na mafisi katika kaya. Rejea kilichotokea ambapo jikampuni la IpTL lilivyopunyua mabilioni toka kwenye fuko la Escrow kwa njia ya esrew ambayo hadi sasa inaonekana kumtisha Dokta Kalaji ambaye ameonyesha umwamba kwenye kushughulika ugonjwa wa majipu huku akishihdwa ugonjwa hatari wa escrew ambao dalili zake na waathirika wake viko wazi..”
            Anapiga chafya nakuendelea “huwezi kupambana na gonjwa la escrew bila kuondoa viini vyake yaani IpTL yaani Immoral putrefaction Transmitted legacy.  Hivyo, tunashauri rahis aunde tume maalumu ya kushughulikia gonjwa hili.”
            Msomi Mkatatamaa anakwanyua mic “kaka kuna tatizo jingine liitwalo Lingumi. Baada ya kusikika kwenye vyombo vya habari kipindi fulani, inaonekana sasa hivi kashfa hii imefishwa kama siyo kufichwa au tuseme kusukumwa chini ya busati na wakubwa walioshiriki kuliasisi na kulianzisha. Kwa wasiojua Lingumi ni nini, ni kashfa ambapo mdudu mmoja aitwaye Lingumese intestiopsis norbitalis gluttonic and uncaring man especially and seemingly endangered. Yuko wapi mtuhumiwa mkuu wa ujambazi huu? Kuna source yangu iliyonitonya kuwa jamaa huyu kaishavushwa na yuko majuu akifaidi kuku huku sisi tukipigika. Tunapaswa kuondoa woga na kumtaka rahis ashughulikie Lungumi na Escrew kwa uzito aliouweka kwenye bwimbwi kama kweli anaanisha kuisafisha kaya.”
            Sofia Lion aka Kanungaembe anakula mic “kaka usinikumbushe kashfa hii. Yuko wapi yule gabacholi toka kaya jirani aliyeletwa akidai yeye ndiyo mmilki halali wa IpTL wakati ni tapeli na kinyago kilichotumiwa na wakubwa kutufunga kamba? Yuko wapi Jimmy Rugemalayer mbwahe mwingine aliyetumiwa katika ujambazi huu uliofanyika chini ya Bingwa wa uvivi wa kufikiri aka Denjaman Makapi? Ina maana dokta Kanywaji hajui yote haya au ni yale yale ya mtu aliye hai kuogopa makaburi tena yaliyojaa uoza?”
            Kanji naye anaamua kukwanyua mic “mimi ikosangaa sana dugu zangu. Mizi nakuja naiba naondoka na juluku yote. Nini kazi ya sirikali jamani? Mimi unga kono na guu vote nasema sirikali ikamatate vote naiba juluku yetu kama nakamata ile vote nauza bimbi.”
            Mchunguliaji anamkosoa Kanji “Kanji sema bwimbwi siyo bibi au bimbi.”
            Mijjinga aliyekuwa bize akisoma gazeti moja la kimataifa lichapishwalo Lushoto anakula mic “naona tunapoteza kuwalaumu akina Lingumi, esrew na IptL wakati wenyewe tunawaacha. Kwani hatuwajui waliosuka dili hili? Ukitaka kuwajua, jiulize madili yote haya yote yalifanyika lini na chini ya uongozi wa nani. Nashauri tuandamane kwenda kwenye ofisi zao na kuzitia nari ili wanaojifanya hawasikii wala kuona wapate salamu kuwa nasi tunaweza kuchukua hatua katika kupambana na maovu kwenye kaya yetu. Huu si wakati wa kugeuzana mabwege, kuburuzana na kuibiana huku tukiendelea kuteseka. Tumeshindwa hata uDA ambayo ni saizi yetu jamani! Tunadanganywa na nkwingwa Kisenena ambaye namjua tangu nyumbani kuwa hana chochote wala lolote bali ni con artist tu wa kawaida.”
            Wakati kijiwe kikinoga si likapita shumbwengu la IptL. Wacha tumkamate na kumfanyia kitu mbaya na kutawanyika!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo

JE TANZANIA INAHITAJ MAOMBI AU KUUELEKEA UKWELI? JIBU ANALO ANONYMOUS HAPA CHINI

           Pongezi zangu nyingi sana kwako kwa kuligongomea sanduku la maiti MSUMARI WA MWISHO kuhusu hawa Matapeli wa kidini.Tukumbushe tu kihistoria kwamba tangu jamii za kiduni(Primitive society) waliposhindwa kuelewa jinsi gani tabia(nature) inavyofanya kazi kwa uchanga wao wa kiakili zao kufikiri kisayansi wakaja na fikira kwamba kila tabia(nuture)ambayo wameshindwa kuielewa jinsi inavyofanya kazi na ikawa inawaletea madhara na kushindwa kujitetea na madhara hayo kwa kufikiri kisayansi,wakaja na ufumbuzi wa kwamba kila tabia(nature)inayowadhuru au kuwanufaisha kuuimbia miungu mbali mbali na kuiabudu na hatimae kuifanyia madhabahu ya kuwafurahisha na kuwaridhisha miungu hiyo pale tu wanapogundua kwamba miungu hiyo imekasirika kwa madhara wanayoyapata kwa kuwatoa wanadamu kafara katika madhabahu yao au kuwafikishia mazao yao na wanyama wao kama ni sadaka pale tu wanapoona wamefanikiwa katika maisha yao.Na zilipokuja dini za mbinguni zikaondoa kafara ya wanadamu na kuwatoa wanyama kama ni sadaka au kafara katika madhabahu hayo.Na tunakuta tu kwamba MAKUHANI,WACHAWI NA WATAWALA WALIKUWA NI KITU KIMOJA KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA UTARATIBU HUO UNAENDELEA KWA KUUFANYA KAMA NI DINI NA KUNUFAIKA NA WANANCHI WAO KWA KUWANYONYA KWA KILA NJIA YA HADI HII LEO UTARATIBU HUO UNAENDELEA NA DINI KUWA NI TATIZO KATIKA JAMII BADALA YA KUWA UFUMBUZI NA UFUMBUZI WA DINI NI KWAMBA NCHI NI YA WOTE NA DINI NI YA MUUMINI NA ANACHOKIAMINI NA KUKIABUDU NA BILA YA KULAZIMISHANA,KUUANA,KUCHUKIANA NA KUIINGIZA KATIKA SIASAWA.
        Watu wa ulaya walipofanikiwa kuzitenganisha taasisi za kidini na kiserikali katika zama za kufikiri kisayansi na baada wanadamu kujua ni jinsi gani tabia(nuture)inavyofanya kazi kwa kupitia nyanja zote za kisayansi.Makuhani wamepoteza nafasi zao au haiba zao za kuombea jamii au kuliombea taifa na kufikisha kafara na sadaka mbele ya madhabahu.Na katika makala yako ya hivi karibuni uligusia kwa kusema kwamba jamii ambayo watu wake ni wajinga na washirikina matapeli wa kidini wataendelea na utapeli wao huu wa kidini.Kwa hiyo Muda wa kudumu jamii yetu bado ina mihimili yote ya jamii duni(primitive society) na hatuna utaratibu wa kufikiri kisayansi ndio upuuzi huu na ujinga huu utaendelea kubaki daima na milele.Swali ambalo linalojiuliza hapa je hivi watawala wetu nao hawashiriki katika kuundeleza ujinga,ushirikina na upuuzi huu?Je ni kweli tumefeli kiasi hiki kwa kushindwa kuwaandaa watu wetu wawe na uwezo wa kufikiri kisayansi tangu mashuleni na sio kuwapa elimu na shahada za kupatia riziki?


Nakumbuka vyema tu kwamba katika kinyang'anyiro cha mashindano ya kombe la dunia la mpira wa miguu ya mwaka 1982 yaliyofanyika Uhispania ambapo nchi ya Poland iliyashiriki,viongozi wa timu hiyo na wachezaji wake waliamua kwenda kumuona Pope John Paul 11,Mpoland mwenziwao ili awaombee kwa Mwenyezi Mungu ili waweze ushindi wa kulitwaa kombe hilo la dunia katika mashindano hayo.Lakini Pope John Paul 11 aliwajibu kwamba "Katika mpira wa miguu Mwenyezi Mungu apendelei timu yoyote".Kwa msemo huo wa Pope ni kuwaambia viongozi na wachezi wa timu hiyo kwamba ni maandalizi yenu na majuhudi yenu ndio yatakayo waletea ushindi.Kwa mfano huo hai kinyume chake ni kwamba timu za mpira wa miguu zilikuwa klabu binafsi au timu ya taifa utakuta makuhani wa kidini,waganga na wachawi wanaziombea,kuzirogea na kuzichawia timu hizo ili zitoke na ushindi.Sasa tunategemea nini katika jamii kama hizi?Kwa hiyo makuhani hawa wa kidini kusema kwamba wanaliombea taifa ili iweje na je ikiwa makuhani wa kila taifa watamuomba Mwenyezi Mungu kuhusu taifa lao je hapa hatuoni kwamba Mwenyezi Mungu atakuwa na aina moja au nyingine ya ubaguzi kwa kuwapa taifa moja na kulinyima taifa lingine ambayo hii sio sifa yake Mwenyezi Mungu?Katika kitabu cha Waisilamu kuna aya inayosema"Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao"
Hapa hata Mwenyezi Mungu anawakumbusha waumini wa dini kwamba hakuna mabadiliko yoyote yale katika jamii au nchi yatakayopatikana kwa MAOMBI TU mpaka waumini hao wabadilike wao wenyewe kwa kuyabadilisha yale yote ambayo yanayo wakwamisha kijamii au katika Taifa na hapo ndipo Mwenyezi Mungu atawapa sapoti yote kwa kubadilika kwao huko.
      Ninachoelewa mimi katika historia ni kwamba ni taifa moja tu kama linastahiki kuitwa taifa ni lile taifa la watoto wa Israel alipopewa Mtume wao Moses na Mwenyezi Mungu Jukumu la kuwatoa watu hao kutoka Misri na kuwafikisha katika Ardhi walio ahidiwa.Na ni Mwenyewe Mungu mwenyewe ndie aliekuwa mstari wa mbele kuwaongoza na kuingilia kati katika maisha yao, kuwaadhibu wanapomkosea na kuwapa faraja wanapomtii na hata kupigana vita kwa niaba yao dhidi ya mataifa mengine.Lakini mwisho wa siku watoto hao wa Israel au taifa hilo lilimkana Mwenyezi Mungu wao na wakaamua kujitawala wenyewe kama wanadamu na kumuweka Mwenyezi Mungu wao pembeni na kufuata sababu na visababisha vyote vya kujiendeleza kama wanadamu bila ya kuhitaji MSAADA WA MWENYEZI MUNGU.
Mwalimu Mhango.Msumari wa mwisha umesha ugongomelea kwa nguvu zako zote,je kuna sikio litakalo sikia?kuna akili itakayofahamu na kufanyia kazi maelezo yako haya?Au ndio matapeli wa kidini wataendelea kupeta tu na kutanua katika jamii ya wajinga na washirikina?

Why Have South Africans Easily Forgotten Africa's Contribution to their Independence?

Photo for the courtesy of the Daily Nation Kenya today.

Saturday 25 February 2017

Tanzania aihitaji kuombewa bali kuambiwa

          Ninapoandika kuna kundi la matapeli wa majoho wanaoandaa tamasha eti la kuombea taifa! Hivi Tanzania inahitaji kuombewa au kuambiwa ukweli mchungu hasa kupambana na vikwazo vinavyoifanya iwe shamba la bibi na ombaomba duniani? Kwanini kuomba badala ya kuyakabili matatizo ya kweli yaani ujinga, umaskini, rushwa, ufisadi, usanii, ukondoo, ukijiko, ukuku na adha nyingine?
            Ni matapeli wengapi wamejificha kwenye uganganjaa kama kutenda miujiza wanaowaibia watanzania maskini na wajinga mchana hadi kugeuka matajiri wa kuktupwa kwa muda mfupi? Si tunawaona kila siku wakijipachika vyeo kuanzia uchungaji, uaskofu hadi udaktari? Nani aliwawekea mikono zaidi ya utapeli na njaa zao?
            Juzi wamejitokeza wengine eti wanabariki mafuta huku wakijifanya kumpenda rais John Pombe Magufuli ambaye huweka picha yake mbele kwa kisingizio cha kumuombea. Japo kuomba siyo jambo baya, kwani lazima mtangaze na kuitisha makongamano kama siyo kutaka kujiweka karibu na rais?  Kama tutaendekeza kuomba, kazi tutafanya lini? Hivi hawa wanaojifanya kuipenda Tanzania kiasi cha kuandaa matamasha na makongamano ya kuiombea, hawawezi kufanya maombi yao majumbani au makanisani mwao bila kutangaza kama siyo kutafuta kuwa karibu na rais?
            Sikumbiki Yesu kuandaa mkesha wa kuombea chochote zaidi ya kufanya kila alichoweza bila kutafuta sifa tena akiwaambiwa walionufaika na huduma yake wasimwambie mtu. Yesu hakutaka sifa wala makuu. Ndiyo maana hakuwa tajiri wala hakuwa na vyeo vya kujipachika na vya kughushi kama vile daktari zaidi ya kuitwa Mwalimu na wanafunzi wake.
            Kama tutakuwa wakweli kwa nafsi zetu, kweli Tanzania inahitaji maombi kama majibu ya matatizo yake? Mbona hatusikii nchi jirani zikiwekeza katika kuomba. Tunapaswa kufanya mambo kisayansi na kwa kuangalia ukweli na uwezekano badala ya ndoto na visingizio kama maombi. Kwanza, maombi hayatuhakikishii majibu ya tatizo kwa muda tunaotaka. Pili, maombi si njia yenye kuaminika ya kupambana na matatizo. Na tatu, tunaweza kuomba lakini kufanyike baada ya kazi na si kwa matangazo na kutafuta sifa kirahisi kwa baadhi ya walioko nyuma ya mradi huu wa sala ambao kimsingi, hauna uhakika.  Kuomba hakuna haja ya kugeuka kazi ya kundi fulani au watu fulani au dini fulani.  Kwa watu wanaoipenda nchi yao, bila shaka watakuwa wakiiombea kila siku kwenye maombi na sala zao iwe ni misikitini, makanisani hata majumbani. Hivyo, hawa wanaokuja na gea ya kuliombea taifa, wanapaswa kujua kuwa walichelewa kujua wajibu wao kama watanzania. Leo tutaanza kuombea taifa. Kesho  tutasikia kuliimbia. Na kesho kutwa tutasikia kulitoa sadaka. Dawa ya matatizo ya taifa letu si maombi bali kuambiana ukweli kuwa kuna wenzetu hawafanyi kazi na wengine wanawaibia watanzania  kwa kushiriki vitendo viovu kama vile ufisadi, biashara haramu ya mihadarati, ubabaishaji, utapeli na maovu mengine mengi ambayo yametamalaki. Kama kuna kitu taifa letu linahitaji, nadhani si kuomba bali kuambiwa ukweli kuwa tusipolipenda na kuchapa kazi, hata tuombe uchi au bila kukoma tutazidi kuumia. Hivi wanaoajiri wageni kinyume cha sheria nao wanahitaji maombi? Mateja nayo yanahitaji maombi? Wauza unga wanahitaji maombi? Polisi na maafisa forodha wanaowezesha wauza unga kupitisha mizigo yao hatari nao wanahitaji maombi kweli? Wanaotumia madaraka vibaya na wababaishaji wa kisiasa nao kweli wanahitaji maombi? Wanaotumia vyeo kuwaumiza, kuwakomoa na kuwachafua wapinzani wao nao kweli wanahitaji maombi? Wanaotukana viongozi wetu kweli nao wanahitaji maombi? Wanaofuja fedha na mali ya umma kweli wanahitaji maombi au kuambiana kuwa tupambane nao kwa udi na uvumba?
            Kuna njia zinazoingia akilini za kushughulikia matatizo yetu kama watu na jamii. Kwa mfano, tunapopambana na ukame, dawa si kuomba mvua tu bali kubuni namna ya kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji. Tunaposhindwa kuelewana, njia si kuomba bali kutafuta namna ya kuelewana. Tunapokumbwa na umaskini dawa si kuombeana tena kuombewa na wale wanaotufanya maskini ima kwa kula bila kufanya kazi au kuwaibia maskini bali kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa. Kutofanya kazi lakini baadhi yetu wakatakea kuwa matajiri bila maelezo ni dalili za ufisadi ambao kimsingi, ndicho kikwazo kikubwa kwa taifa letu.
            Hakuna taifa lililopata maendeleo kwa njia ya kuomba iwe ni misaada au maombi zaidi ya uchapa kazi. Kwa vile sera ya rais Magufuli ni ‘Hapa Kazi Tu’ namshauri awaulize hawa wanaopoteza muda na fedha nyingi wakiandaa makongamano na matamasha ya kuombea taifa, wafanya kazi kwanza; maombi baadaye. Anachoweza kufanya rais kulisaidia taifa ni kuwachunguza wote waliojipachika vyeo vya kidini na vinginevyo wenye utajiri wa kutisha ili watumbuliwe.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.

Hapa sijui nani anachanganya dini na siasa

Hakuna ubishi kuwa ndoa ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na baadhi ya madhehebu ya dini inogile kiasi cha kutoonekana bughudha ya kuchanganya dini na siasa. Sijui nani anamtumia nani hapa na nani anamdanganya nani. Haya anayefanyiwa huyu dogo wangefanyiwa upinzani ungesikia kuwa ni mwiko kuchanganya dini na siasa Tanzania. Je huu ni usanii, woga au unafiki? Je nani atatoa nini na nani atapata nini? Je hapa kuna uwezekano wa kuambiana ukweli au kufurahishana ilmradi kila mtu apate chake? Ama kweli bembeleza kafiri upate mradi na isitoshe baniani mbaya kiatu chake dawa. Kama zilivyo ndoa za namna hii zenye kutia kila aina ya shaka, siku itakapobuma mtasema alisema. Sisi yetu macho na masikio.

Friday 24 February 2017

Barua ya wazi kwa FreePerson MboHwe

Image result for photos of mbowe and magufuli
            Bwana Freebinadam
 Salaam; na pole kwa yaliyokusibu hivi karibuni kuanzia kuhamishwa kwenye nyumba ya msajili, kubomolewa Bilcanas, na kubwa katika yote, kutuhumiwa kwa biashara ya madawa ya kulevya. Hata hivyo, kutuhumiwa si jambo la ajabu hasa ikizingatiwa kuwa yeyote anaweza kutuhumiwa ukiachia mbali kuwa kutuhumiwa si kuhukumiwa kisheria; ingawa kilevi ni vinginevyo. Wengi wamesikitishwa na kushangazwa sana hasa na utaratibu uliotumika kufikia hitimisho la kukutuhumu. Tangu lini watuhumiwa wakaitwa kwa vyombo vya habari badala ya summons au kutumiwa ndata kuwadaka na kuwapeleka lupango tayari kwenda kwa pilato? Hapa kilichofanyika ni kutaka kutumia njia chafu kufanya jambo safi. Mwisho wa siku matokeo huwa ni uchafu unaomeza usafi.
            Pili nakupongeza kwa msimamo wako dhidi ya kile ambacho kilevi huita Kangaroo Court ambayo wajivuni wachache tuliodhani wangejua hata sheria za msingi kutaka kuitumia kuadhibu ima wabaya wao au kuitumia kutafutia maulaji. Tangu lini dingi wa mkoa akawa ndata, hakimu, mpelelezi na upuuzi mwingine? Nakushukuru kwa kuwastua.kwani, baada ya kugundua walivyoingia choo cha kike, siku hizi hawataji kiasi cha kushangaza kwanini wengine watajwe na wengine wasitajwe? Hapa dogo Po ameula wa chuya. Kama si kulindana, kibarua chake kilipaswa kiote mbawa. Hata hivyo, huu waweza kuwa mwanzo wa mwisho; hasa ikizingatiwa kuwa mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi. Msimamo wako wa kukataa kuripoti kwa mamlaka haramu umenifurahisha na kunikumbusha mlevi mwingine wa kanywaji kaitwako justice almarhum Chris Mtikisa, ambaye bila shaka, angekuwa hai ashafungua kesi mia kidogo dhidi ya wasaka ulaji na wabangaizaji hawa.
            Tatu, nakushukuru kwa kuonyesha mfano na uongozi dhidi ya ubabaishaji na utaka sifa vinavyoanza kugeuzwa sera na baadhi ya wajivuni na waroho wa madaraka waliojisahau.  Mungu si Mlevi mie. Si juzi nikasoma sehemu kuwa waliotoa taarifa zilizosababisha utuhumiwe kumbe zilikuwa zimeelekezwa kwa Bilcanas kama sehemu ya matanuzi lakini si kwako binafsi. Hili liko wazi. Ila kwa vile wahusika walikuwa na lengo la kupata sifa, na si kupambana na mabwimbwi, waliamua kupinda mambo ili kukukomoa sijui ili iweje? Hapa naanza kuamini kuwa mazonge mengi yanayokuandama kumbe ni ya kisiasa zaidi ya kisheria. Nani, kwa mfano, hajui kuwa magabacholi wengi wanaishi dezo kwenye nyumba za Asajile Mwaijumba na bado familia na biashara zao havijaguswa?
            Bwana Freebinadam, hata nilipoangalia makaratasi uliyosema yameandikwa kwa mwandiko wa darasa la pili, sikuona jina lako zaidi ya Philemon jambo ambalo linaonyesha umaamuma na ukihiyo wa wahusika. Sijua hawa jamaa walipitaje kwenye vyuo wanavyodai kuvipitia wakati walishindwa jambo dogo kama hili; au ni yale yale ya Gus Lyatongolwa wakati wa mzee Ruksa ambapo kila upuuzi ulipewa nafasi katika kusaka sifa zilizogeuka chanzo cha mauti ya mhusika kisiasa?
            Walevi wanaunga mkono mapambano dhidi ya bwimbwi kama hata nawe ulivyobainisha kuwa huna ugomvi na vita hii zaidi ya namna inavyopiganwa kiuonevu, kibabaishaji, kisiasa na si kisayansi. Pia walevi wanakubaliana nawe kuwa vita ipigiganwe kweli kweli lakini si kwa kukomoana, kuzushiana, kuchafuana, kulindana na upuuzi mwingine ambavyo vilijitokeza nje nje kwenye awamu ya kwanza ya vita hii. Walevi wanamshukuru dokta Kanywaji kwa kuingilia na kumteua dingi wa vita hii huku akionyesha wasiwasi juu ya wale walioianzisha japo aliwasifia kinamna ili wasikate tamaa.
            Hata hivyo, kuna mambo ya kujikumbusha. Mithali 16:18 inasema “kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.” Kwa vile wanaokukamia wanajidai kuamini katika Mungu, tunatoa mstari huu lau uwasaidie hata kama unatoka kwa mlevi. Hakuna kitu kibaya kama kiburi na ulevi wa madaraka. Kiburi na majivuno mara nyingi ni silaha za juha hasa ikizingatiwa kuwa madaraka ni kama koti kwenye mabega ya mvaaji tena la kuazima. Tuliwaona wengi. Wako wapi akina Lyatongolwa? Wako wapi akina Ditto waliofikia hata kupiga walevi risasi na walevi wa maulaji wenzao wakawakingia kifua? Hawa ni vidagaa. Wako wapi akina bwana majivuno aliyewaita walevi wavivu wa kufikiri akaishia kuwa bingwa wa uvivu huo kwa kuwauza na kaya yao? Wako wapi akina Nebukadnezza na wengine wengi waliokuwa miamba na mabingwa wa fitna? Wako wapi akina Richard Nixon? Wako wapi akina Slobodan Milosevic, Nicolae CeauÈ™escu na wengine wengi waliohaiwa na madaraka? Wako wapi akina Saddam Hussein na watoto wao waliokuwa juu ya sheria wakaishia kufa vifo vya aibu? Kuna haja ya kutumia historia kufanya mambo badala ya kufanya mambo kutafuta nafasi katika historia tena nyingine chafu. Je nani hawajui wauzaji bwimbwi ambao wanahengwa hengwa? Nashauri tupambane na biashara ya bwimbwi kisayansi na kwa haki na si kisiasa na kwa kubambikiana na kupakaziana mambo kama ilivyoanza.
Chanzo: Nipashe Jumamosi kesho.

Tuesday 21 February 2017

When Eco-terrorism is called Tourism

In the following clip you will see how the so-called tourists are decimating African animals under the  pretext of tourism as Africans laughs. Is this tourism or terrorism? ironically, the victims are joining their assailants to celebrate their future demise.  Is there any difference between joy hunting and  Poaching? To such tourism is either legalised eco-terrorism or poaching. Who bewitched Africa to swallow any garbage in the name of business? 

Makonda: Tume ya maadili na Magufuli wanamdanganya nani?

Image result for photos of makonda and magufuli
        Pamoja na kwamba katiba yetu inasema wazi kuwa Tanzania itaongozwa kwa misingi ya usawa; bila ubaguzi, uonevu na upendeleo, kinachoendelea kuhusiana na baadhi ya watu ni kinyume kabisa na maagizo ya katiba. Katiba yetu imekuwa ikivunjwa kirahisirahisi na baadhi ya watawala kiasi cha kugeuka kama kitabu cha hadithi tofauti na inavyopaswa kuwa. Mfano wa hivi karibuni ni pale baadhi ya waheshimiwa, tena wakiwa mbele ya bunge, walimtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Paul Makonda kwa kujilimbikizia mali nyingi na kufuja fedha kama kusafiri ughaibuni tofauti na katazo la rais tena kwa muda mfupi aliokuwa madarakani. Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini alikaririwa akiliambia bunge akisema“Makonda amenunua apartment pale Viva Towers kwa shilingi milioni 600, Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedez Benz lenye thamani ya  Dola 250 za Marekani (shilingi milioni 550) kama zawadi ya birthday.” Hizi tuhuma si ndogo; na wala si za kupuuzia. Je rais Magufuli au washauri na wasaidizi wake hawasomi magazeti kiasi cha kutojua tuhuma hizi nzito?  Je Magufuli, kama mamlaka iliyomteua Makonda amechukua hatua gani ukiachia mbali kutotoa maelezo yoyote?
            Kwa upande wake, Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma imeonyesha wazi uhovyo kwa kujitenga na kile kilichopaswa kuinyima usingizi kama kweli ipo kwa misingi ya kulinda uwajibikaji na kupambana na ufisadi na wizi wa fedha za umma.  Je Tume hii imepigwa ganzi kama anavyosema Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Rushaku (Msukuma) ambaye alikaririwa akihoji “utawala bora, Mambo ya Ndani na Waziri wa Sheria…kwanini mmepigwa ganzi?”
Msukuma aliongeza kumwaga mtama akisema “anatumia (Makonda) Lexus ya petroli ya Sh milioni 400, lakini imekarabatiwa ofisi (yake) ya RC Dar es Salaam kwa zaidi ya Sh milioni 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi wa Serikali. Ana ma-V8 na Mwanza amejenga jengo la ghorofa…ni kina nani wanaotakiwa kujadiliwa na kufanyiwa uchunguzi? Na hawa mawaziri tulionao humu kwanini wamepigwa ganzi?”
            Kwa wanaojua uchungu na kasi ya Magufuli vya kupambana na uoza, walidhani kuwa angechukua hatua mara moja bila kukaa kimya kama ilivyo. Je ina maana ni kweli kuwa rais na taasisi nyingine kama vile polisi, Tume ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wamepigwa ganzi kiasi cha kufumbia macho uoza na tuhuma hizi? Je hii inajenga picha gani kwa watanzania wa kawaida? Je kwanini Makonda, kama yanayosema ni uongo, amekaa kimya bila kutoa maelezo wala kwenda mahakamani kusafisha jina lake?
            Kwa wanaojua matatizo ya kiutawala ya taifa letu watakumbuka kuwa, ukimuondoa marehemu baba wa taifa Mwl. Julius Nyerere, karibia waliomfuata wote walikuwa na mizigo yaani kukingia kifua watu wao wa karibu kiasi cha kujengeka dhana kuwa walikuwa wakiwatumia kuliibia taifa. Mifano ni mingi. Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi alikuwa naye marehemu Kighoma Malima. Hakutaka aguswe; na ilipotokea akaguswa, Mwinyi alijifanya haoni wala hasikii. Benjamin Mkapa alikuwa nao akina Basil Mramba na Daniel Yona wakati Jakaya Kikwete alikuwa na akina Shukuru Kawambwa na Hawa Ghasia na wengine. Sasa rais Magufuli ameanza kujenga picha kuwa anaye Makonda. Hii ni tofauti na alivyomshughulikia rafiki na waziri wake wa zamani Charles Kitwanga kwa ulevi. Ajabu ya maajabu, Magufuli alipomtimua kazi Kitwanga hakuchelewa wala kueleza kama tuhuma zake za ulevi zilithibitishwa na mkemia mkuu. Kwanini anasitasita kwa Makonda’ na kunani? Sitaki niamini kuwa Magufuli hajui tuhuma za mkuu wake wa mkoa wala kukerwa na tuhuma hizi kiasi cha kuzinyamazia. Je rais anafanya uchuguzi ili achukue hatua au ana-buy time ili mambo yapowe na ulaji uendelee? Je Makonda atanusirika na tuhuma hizi ambazo zinakolezwa moto na ukimya wake pamoja na ule wa rais ukiachia vyombo husika kuonekana kumgwaya? Je huku si kuvunja na kudharau katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ameapa kuilinda na kuitetea kama sheria mama inayompa madaraka aliyo nayo?
            Kwa vile tuhuma dhidi ya Makonda ni nzito na zimetolewa wazi na watu wazito, itakuwa jambo la aibu na ajabu kama wahusika wataendelea kulinyamazia au kutafuta visingizio kama ilivyoonyesha Tume husika. Inashangaza kuona Tume husika ikijificha nyuma ya sheria wakati kila kitu kiko wazi. Sasa nini maana ya sheria kumtaka kila mtanzania atakayeshuhudia au kujua kuwa kosa la jinai limetendekea alipoti polisi au kwenye mamlaka zinazohusika? Je TAKUKURU nao wanangoja wapelekewe maombi? Kwanini watuhumiwa wa biashara haramu ya mihadarati hawakupewa fursa hii; na badala yake walikamatwa na wengine kuwekwa ndani baada ya kupokea tuhuma? Je hapa polisi, TAKUKURU, Tume na Magufuli wanataka kumdanganya nani; na ili iweje? Je Makonda ni nani katika Tanzania? Mbona Mwl. Nyerere alipotuhumiwa na marehemu Oscar Kambona alitoa maelezo na utetezi haraka bila kujali nafasi yake tena ambayo kwa mfumo wa chama kimoja uliokuwepo, angejinyamazia na mambo kuisha?
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

Kijiwe chataka wasiojua lugha ya taifa wasipewe uongozi

            Baada ya Kijiwe kujikita kwenye kadhia ya biashara hatari na haramu ya bwimbwi, leo kinakuja na inshu moja kali na nyeti kwa kaya. Msomi ambaye hana kawaida ya kuanzisha mada, leo anavunja mwiko wake. Anaamukua na kuanza, “mwenzenu juzi nilinusurika kuvunja TV yangu tena Hi Def.” kabla ya kuendelea Mbwamwitu anamchomekea, “kwani ilikutukana hadi uivuje au ni kutokana na usanii wa kupambana na bwimbwi kijinga?”
Msomi anajibu “hakuna kitu kilitibua siku yangu kama kuona clip mmoja ambapo muishiwa mmoja gabacholi akimtukana rahis tena kimzahamzaha huku waishiwa wenzake wakimshangilia utadhani alichokua akitenda si jina na machukizo kwa kaya yetu. Bila aibu wala woga gabacholi huyu baniani aliamua kumtukana rahisi kwa kujifanya kakosea majina yote ya rahis. Alimwita Mapombe Makufuli. Kituko zaidi ni kwamba matusi na kejeli hizi vilifanyika mjengoni huku vyombo vya habari na kamera zake vikirekodi.” Anatulia kidogo na kuendelea “Gabacholi huyu alishangiliwa sana kiasi cha kupata mori wa kuendelea kubomoa lugha ya taifa letu na viongozi wetu. Ajabu ya maajabu waishiwa waliangua vicheko badala ya kuomba mwongozo ili mhusika afute upotoshaji na kusanifu huku kwa majina ya mkuu wa kaya kiasi cha kuwafanya wote wawe washiriki katika jinai hii.”
Kabla ya kuendelea Kapende anakula mic na kusema “hata nami niliona jamaa akiongea Kiswahili kibovu kiasi cha kunifanya nijiulize: Inakuwaje watu wasiojua au wanaojifanya kutojua Kiswahili ambacho ni lugha ya kaya wanapewa dhamana wakati kwenye kaya zote duniani, huwezi kupewa dhamana kama hujui lugha ya taifa. Kwa mfano, huwezi kuwa mbunge wa India kama hujui mojawapo ya lugha za india.”
            Mijjinga naye anapoka mic na kuronga “ukiachia baadhi ya jamii kujifanya kutojua lugha ya kaya au kudharau kujifunza, zinasifika kwa ubaguzi dhidi ya watu weusi. Je hapa lawama ni kwa nani?
Tunahitaji kubadili mfumo huu wa kikokolo ambapo kila ajaye anapewa fursa ya kupewa dhamana ya umma bila kuangalia yeye ni nani na ana mchango gani.”
            Mipawa anachomekea “wapo waliokataa kutangamana nasi kama vile kuoleana, na kuwa karibu. Hawa hawafai kupewa dhamana za uongozi kwenye kaya yetu ili kuwakilisha wabaguzi wenzao kwa mgongo wa wajinga wetu wanaowapa kura ya kutula. Je wanapataje dhamana hii? Je hapa tatizo ni rushwa, ujinga au kupinda sheria kama siyo kujibagua binafsi kama watu weusi tunaobaguliwa karibu na kila jamii hata nyingine za kiafrika ima kwa rangi au nywele?”
Mpemba anakatua mic “mie wallahi sishangai hata kidogo. Kwani hawa wamejitenga wengine kiasi cha kuwa na shule, dini na kila kitu chao. Nasi kwa ujinga na kujibagua, tumeruhusu ubaguzi huu kuwa sehemu ya mfumo wetu. Kuna haja ya kuwa wakweli kwa nafsi zetu na kuambiana ukweli. Kwani kuna baadhi ya jamii miongoni mwetu kama vile magabacholi, wamanga na hata baadhi ya waswahili wenzetu wa kialshabaab ambao wanajiona bora kuliko sisi kiasi cha ima kuchanganyikana nasi kwa kutuolewa au kutoruhusu ndoa kabisa ukiachia mbali kujiweka mbali na sisi. Nenda mikoa ya pwani kwa mfano. Wamanga na mazalia yao huwa na fursa ya kuoa waswahili lakini si waswahili kuwaolea wao. Inapokuja kwa magabacholi na maalshabaab, hakuna cha kuchanganyikana. Je hii itaendelea hadi lini?”
Kanji kwa aibu ya wazi anakula mic “dugu zanguni, hapa hukumu vatu vote kama moja nafanya kosa. Mimi kama napata bibi Swahili naona kesho.”
Kabla ya kuendelea Mgoshi Machungi anampoka mic na kusema “hei Kanji ungejinyamazia. Tinajua janja yenu yote. Tangu mkooni mwingeeza awabwage hapa hamjawahi kutaka kuchanganyikana nasi. Tinabaguiwa wazi wazi na mamuaka zinanyamaza. Sasa titaona kama wakubwa watamiadhibu hii baniani uchwaa. Ajabu kama huyu mwishiwa angekuwa wa upingaji, tingesikia makeee ya kuomba mwongozo na kumtaka afute kaui zake za kishenzi. Lakini kwa vie huyu ni gabachoi, hakuna kiichofanyika kiasi cha kutionyesha kama majuha yanayojitukana yenyewe.”
Bi Sofia Lion aka Kunungaembe anaamua kukatua mic “kusema ukweli hata mimi kashfa hii imenikera. Ajabu waandishi wa utani wakibadilisha majina ya rahis wanaambiwa wanamtukana kiasi cha kuonywa mara kwa mara. Hapa kinachojitokeza wazi ni kwamba hawa jamaa, licha ya kutubagua, wanatudharaua na kutuona kama hamnazo. Naungana na Mgoshi kusema wazi kuwa kama wahusika hawatafanya lolote, watakuwa wamethibitisha madai yetu kuwa wanawagwaya magabacholi. Leo wanamwita Mapombe Makufuli. Kesho watamwita bwimbwi, gongo na matusi mengine ya ajabu ajabu. Kama mtu hana la kuchangia basi anyamaze. Mie hakuna kilichonichefua kama naibu kipaza sauti bi Asiye Tulia kuchekelea na kusifu matusi haya pamoja na PhD yake tena ya sharia.”
Kijjiwe kikiwa kinanoga si likapita shangingi la baniani! Acha tulitoe mkuku tukitaka fanyia yeye kitu bay asana. Matusi yalisikika kila aina huku wazomeaji wengine wakisema “ponjoro nenda kwenu katukane hao magabacholi wenzako lakini si viongozi wetu. Mapombe baba yako na makufuli maza wako, unabwia bwimbwi nini, mbona huna adabu wala aibu?”
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

When Azerbaijan goes Obiang and Museveni


Azerbaijan's President Ilham Aliyev (R) leaves a voting booth next to his wife Mehriban at a polling station during parliamentary elections in Baku, November 7, 2010. REUTERS/Vugar Amrullaev
Azerbaijan dictator Ilham Aliyev has appointed his wife his vice president. This was only heard of in Africa whereby Equatorial despot and Ugandan one, Theodoro Obiang and Yoweri Museveni respectively appointed his son to be his vice president and wife a minister. Now that Azerbaijan has followed suit. Who follows next? For more info, Please CLICK HERE.

Saturday 18 February 2017

Serikali izuie bendera madhabahuni na vyeo bandia

  Image result for tanzanian flag
 
              Kwa walioangalia mahubiri ya Josephat Gwajima baada ya kuachiwa toka Central police station, watakubaliana nami kuwa ana bendera ya taifa na ya Israel kwenye jukwaa lake. Siku zote tunaonywa kuchanganya dini na siasa. Je huyu anayetumia bendera kwenye mambo ya kidini wakati hana stahiki ya kuwa na bendera anadhamiria nini? Je kama makanisa na misikiti yote watafanya hivyo, tofauti ya dini na siasa ambayo Tanzania imeitengeneza itakuwapo?
            Hata ukisikiliza mengi ya mahubiri ya Gwajima ni ya kisiasa. Cha mno anajaribu kujipigia debe ili kuwa karibu na rais John Pombe Magufuli ambaye hata hivyo anaonyesha msimamo wa kutotaka kuchezewa. Ni ajabu kuwa Gwajima amekuwa mwepesi wa kusahau kuwa ni jana tu alikuwa shirika la Edward Lowassa dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sasa baada ya mtu wake kushindwa, Gwajima anajitahidi kwa kila hali kujifanya anampenda na kumuunga mkono Magufuli kwenye wakati wa kuvuna wakati alimpiga kiatu kwenye kulima (uchaguzi). Je Gwajima anadhani kuwa Magufuli naye ni msahaulifu au msanii kama yeye?
            Ukiangalia ujio wa Gwajima na wenzake kama yeye waliojivisha vyeo vikubwa vya kidini, unagundua mambo mengi mojawapo likiwa ni kutojiamini. Wakati umefika wa kuondokana na viongozi wa kidini wa kujipachia madaraka ili kuepusha watu wetu kuzidi kuibiwa na kutapeliwa tokana na ujinga na shida zao. Kimsingi, kinachoendelea nchini licha ya kuwa ushirikina, ni ufisadi wa kiroho ambao madhara yake ni makubwa sana. Mtu asiye na shahada hata ya kwanza anaamka na kujiita daktari na lecturer na mamlaka zinamvumilia. Hili haliwezekani. Serikali zilizopita tokana na kuongozwa na watu wasioelimika na kusoma vilivyo, ziliwavumilia wasanii hawa kiasi cha kutosha. Magufuli daktari wa falsafa anajua uchungu wa elimu. Hivyo, tunamshauri atumbue ufisadi huu. Kwanini kwa mtu kujiita mheshimiwa Mbunge lazima achaguliwe au ateuliwe lakini si kwa askofu na vyeo vingine vya kiroho? Tunajenga taifa la namna gani kwa kuruhusu udhalilishaji wa taaluma? Je hatutoi motisha kwa watu kudharau elimu na kutafuta vyeo na stahiki za kisomi hata kwa njia ya kughushi ambalo ni tatizo kitaifa linalowahusisha wanasiasa wengi; na sasa viongozi waroho wa kiroho wa kujipachika? Kwanini wanaojifanya madaktari wa kutibu watu wanakamatwa na kufunguliwa mashtaka wakati matapeli wanaojiita au kupeana udaktari uchwara wanaachiwa? Nadhani waziri wa Elimu anapaswa kuliangalia hili kwa makini hasa ikizingatiwa kuwa naye ni msomi wa kumenyekea na si wa kupewa.
            Japo ni kielelezo cha ujinga wa aina yake kwa mtu asiyesomea shahada yoyote kujipachika shahada husika, kwa wajinga na vihiyo hili si tatizo. Kuwasaidia ni kuhakikisha hakuna mtu anaruhusiwa kutumia cheo cha heshima wala kujipachika au kughushi. Kwanini wachungaji kama hawa wa kujipachika hawakuwapo wakati wa utawala wa Mwl Julius Nyerere? Jibu ni rahisi kuwa Nyerere hakuruhusu ujinga na ufisadi kama huu wakati wake kwa vile alikuwa ameelimika na kusoma vya kutosha.
            Tukirejea kwenye suala la kutundika bendera, bendera ina stahiki na namna za matumizi yake. Wapo maafisa wa serikali walioruhusiwa kutumia bendera ya taifa kama alama kuu ya utaifa wetu. Sasa hawa wachunaji wamepewa na nani mamlaka na kwa sheria gani kutumia bendera yetu kwenye shughuli zinazotia kila aina ya shaka ukiachia mbali kuwa si wote wanaoamini kwenye maigizo yao? Kuna taasisi zinazoruhusiwa kupeperusha bendera ya taifa kama vile ofisi za serikali, taasisi za umma kama vile shule na nyinginezo lakini si makanisa wala misikiti; kwa vile taifa letu halina dini japo linaundwa na watu wenye dini tofauti na kinzani. Hatuwezi kuruhusu wafanya biashara ziwe za bidhaa au kiroho watumie bendera yetu. Kufanya hivyo, licha ya kuidhalilisha ni kubariki biashara hizo hata kama nyingine ni haramu. Siku hizi dini umegeuka uchochoro wa kila tapeli kupatia mkate wake. Tutaishi kwa mahubiri kweli? Nashauri serikali itenge mahubiri kuwa ni jumapili na ijumaa. Zaidi ya hapo wahusika lazima walazimishwe kufanya kazi nyigine. Wale waliojipachika wasimamishwe haraka ili kuepuka utapeli huu kuendelea kuumiza watu wetu wengi wajinga na washirikina. Ni ajabu katika karne ya 21 bado kuna watu wanaaminishwa kuwa kuna anayeweza kutenda miujiza wakati miujiza yenyewe ni kuwaibia na kuwageuza majuha wa kawaida tu kama si mabuzi ya kuchunwa. Huwa nasema kila mara kuwa Yesu licha ya kuwa maskini, alisema tajiri hawezi kuuona ufalme wa mbinguni. Rejea kisa cha Zakayo. Ajabu ya maajabu leo wachunaji wengi ndiyo wakwasi wa kutupa. Je wataweza kuwatumikia mabwana wawili yaani mali na Mungu kweli wakati Yesu wanayejidai kumhubiri alishaweka mambo sawa? Je nani anamdanganya nani hapa?
            Tumalizie kwa kuishauri serikali imalize kadhia hii ambayo wachunaji wengi wameitumia kujipatia utajiri wa haraka ama kwa kufaidi misamaha ya kodi au kuwaibia watanzania wajinga na maskini wenye matatizo wasiojiamini. Hali imekuwa mbaya hadi matapeli wanaosifika toka kwenye mataifa kama Nigeria wamejipenyeza kwenye nchi yetu chini ya kivuli cha kuhubiri. Enough is enough.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili kesho.

Habari njema



JANA rafiki yetu na kijana wetu Sirili Akko Mionntini alliuacha ukapela. Tunafurahi kuwatangazia marafiki na wasomaji wetu kuwa tumepata mwanachama mpya.
Japo hatukuweza kufika Hanang kuhudhuria mnuso, tulisindikiza kitu hii na hii ngoma hapa chini kutokana ukweli kuwa kijana wetu ni mbobezi katika mambo ya utalii.

Friday 17 February 2017

Siuzi bwimbwi nimeokoka

Image result for photos of makonda and gwajima
Baada ya dogo Po kuwatibuliwa wanene, wasanii na ndata kwa kuwatuhumu baadhi yao kuwa wanasepa na mibwimbwi nimesikia walevi wengine wakilalamika kuwa walishukiwa kuuza bwimbwi; na hivyo kuchafuliwa majina yao na kuvunjiwa heshima katika dugudwa hili. Tangu lini kumshuku mlevi ikawa kumvunjia heshia?  Kwani kaya ya walevi imegeuka ya malaika? Huwa sielewi madai ya namna hii hasa ikizingatiwa kuwa chini ya sheria ya kaya wanakaya wote ni sawa isipokuwa mtukufu rahis ambaye yuko juu ya sharia. Ajabu ya maajabu, wale wanaolalamika kuwa wamedhalilishwa walidhalilika zamani kutokana na shughuli zao za kutia kila aina ya shaka katika jamii. Hivi jitu linalokurupuka na kutangaza kuwa linatenda miujiza wakati ni uongo mtupu halijadhalilika? Nani anaweza kutenda miujiza usawa huu? Kama kweli mnatenda miujiza, basi itendeni sasa mnapokabiliwa na shutuma za kuuza bwimbwi.
Tuache utani jamani na kuchunguza dafina za mioyo yetu. Hivi mwanakaya kapuku ambaye hata kazi zake hazieleweki kulala maskini na kuamka tajiri si alama na ushahidi kuwa kuna tatizo hasa njia haramu za kupata utajiri? Wanagapi wanakula haramu itokanayo na kuwaibia au kuwarubuni walevi waliokwama kimaisha na kuukata huku waathirika wao wakiendelea kuhangaika? Mnajipachika vyeo na kufanya mambo ya hovyo halafu tuwaache siyo? Huwezi kuwa tajiri bila maelezo na ukakubalika katika jamii. Kama mlizoea utawala wa kijambazi sasa mtakoma na kukomaa.  Ni wangapi wanamilki mindinga mikali hata mapipa wakati hawana kazi yoyote ya maana zaidi ya kuwapigia kelele walevi kwa kisingizio cha dini? Nani anahitaji dini usawa huu ambapo kila mlevi anajua anachopaswa kufanya kama kiumbe wa Mwenyewe aliye juu? Unafiki na ubabaishaji mtupu. Baadhi ya walevi wanajipachika vyeo vikubwa na vitukufu huku wakifanya usanii wazi wazi na kijinga kama kuponya wagonjwa na kutenda miujiza ya uongo na ukweli. Narudia tena. Fanyeni hiyo miujiza yenu ili tuhuma za kuuza bwimbwi ziwatoke badala ya kulalamika. Kwani hatuwaoni wala kuwajua? Juzi juzi mtuhumiwa wa bwimbwi mmojawapo alijifanya kuwa amepooza na kujiombea na kupona.  Ukimwambia nenda Muhimbili ukawaponye wenye ulemavu anaanza stori za kuwa hadi uponywe lazima uwe na imani. Ni mgonjwa gani asiye na imani wakati ana shida ya kupona? Tumegeuza kaya kuwa ya washirikina na wababaishaji tokana na ujinga wa kimfumo. Hapa lazima rais Kanywaji afanye kweli kuhakikisha kaya inaondokana na upuuzi na ujinga huu wa ajabu. Napendekeza akamate mali zote za wale walioukata bila maelezo ili tuanze kuheshimiana na kufanya kazi badala ya kupiga politiki na kuhubiri ujinga. Tangu lini mganga akajiganga kama si ujinga na upuuzi? Mlizoea mfumo wa hovyo wa kukwapua. Sasa mtakoma na mkomae. Tunataka kila mlevi aeleze alivyochuma ukwasi wake kwa wale wenye ukwasi wa ghafla bin vu tena wa kutia shaka.
Inakuwa shaka zaidi kwa wale wanaodai wameokoka kuwa matajiri wakati yule wanayedai kumhubiri alikuwa kapuku wa kutupwa hadi kushindwa hata senti tano ya kulipa kodi hadi alipomkopa samaki. Wapo waliosema kuwa walipaswa kupigiwa simu. Sheria gani hii iwapo kila mwanakaya anaweza kutuhumiwa? Mbona Yesu alipotakiwa kwa Pilato hakupigiwa simu? Wao ni nani zaidi ya kutapatapa? Kama huuzi bwimbwi si uende ueleze na kuwasuta waliokutuhumu badala ya kutupigia mikelele?
Nadhani baadhi ya wana kaya walisahau kuwa mfumo wa kijambazi uliokuwa umeanzishwa na tawala uchwara zilizopita ambapo kila mhalifu alikuwa akijihudumia ungefikia mwisho. Well, kila kilicho na mwanzo shurti kiwe na mwisho ndugu zanguni. Kubalini mmefulia; na imekula kwenu usawa huu wa dokta mtumbua majipu ambaye hana mchezo na mtu. Kwanini hamkubali kuwa hakuna kasma wala bajeti ya kuwapigia simu watuhumiwa? Kama hutaki kuchafuliwa au kushukiwa basi fanya mambo yanayoeleweka kama mimi ambaye nimeokoka kweli kweli na hivyo situhumiwi kwa vile maisha yangu ni mambo hadharani?
Juzi jamaa yangu anayejidai kaokoka katoa mpya pale tulipokuwa tukikamata kanywaji pale uwanja wa Hyena. Baada ya kumpa pole kwa kutuhumiwa na kusema ni kwanini yeye na si wengine si alijibu “hata kama nauza bwimbwi wewe yakuhusu nini wakati nimeishakwambia kuwa nimeokoka? Nikishasema nimeokoka kila kitu kinasamehewa. Hivyo, hakuna anayepaswa kufuatilia misele na mishemishe zangu isipokuwa bwana mwenyewe aliyeniokoa.” Upuuzi kiasi gani? Yaani kila mmoja akisema ameokoka wakati anahitaji kuokolewa tumwamini?  Lalamikeni pale mnaponyimwa nafasi ya kujitetea; kutuhumiwa si kosa wala uonevu bali utaratibu wa kisheria.
Nimalizie kwa kusema wazi; mie siuzi wala kubwia bwimbwi. Hivyo, nikituhumiwa sitalalamika bali kwenda kumwaga nondo za kuthibitisha kuwa tuhuma zangu si za kweli badala ya kujificha kwenye kuokoka. Simpo.
Chanzo: Nipashe Jumamosi kesho.

Tuesday 14 February 2017

Makonda akae kando kupisha uchunguzi

        Waswahili wana msemo kuwa muosha naye huosha. Pia husema kuwa ukijua huu wenzio wanajua ule. Baada ya mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuwatuhumu wenzake kuwa walikuwa wakipokea rushwa kwenye sakata la  shisha jijini Dar, sasa amegeuziwa kibao na wabunge wanaotaka achunguzwe ili kubaini ukweli wa mambo yake hasa umilki wa mali zenye thamani ya mamilioni na kuweza kwenda nje kutanua.
            Mbunge wa Kawe, mheshimiwa Halima Mdee alisikika bungeni akihoji waliomfadhili Makonda kwenda kutanua ughaibuni kwa muda mrefu tofauti na kipato chake. Tokana na shutuma hizi, wengi tunajiuliza; je ni wakuu wangapi wa mikoa wamekwenda nje kutanua kama Makonda? Yeye ana nini cha mno? Mdee alikwenda mbele na kudai kuwa huenda Makonda alifadhiliwa na wauza unga kwenye safari yake ya ughaibuni hivi karibuni.  Je ni kweli alikwenda ughaibuni kutanua tena kwa kufadhiliwa na fedha chafu? Je alijilipia mwenyewe? Wabunge walitaka kujua kama mshahara wake, kwa muda mfupi aliokuwa ofisini, ungemewezesha kufanya hayo.
            Mbali na Mdee, Mbunge wa Geita Vijijini, mhesimiwa Joseph Msukuma (CCM), aliongoza mashambulizi alipokaririwa akisema “RC wa Dar es Salaam anamiliki ma-V8 na Mwanza amejenga maghorofa ndani ya mwaka mmoja. Je, ni akina nani hao wanaomfadhili kupata mali hizo?”  Kama haitoshi, Msukuma alionekana kuungana na Mdee kuhusiana na safari ya Makonda ughaibuni na nani walimfadhili akisema “wauza dawa za kulevya wanajulikana na hata walio mstari wa mbele kukamata wenzao wanashinda nao na kuwasafirisha nchi mbalimbali kama Marekani.” Makonda hakwenda Marekani tu. Msukuma anasema “kwanini vyombo vya ulinzi na usalama visimchunguze Makonda maana anasafiri sana Ulaya, Ufaransa na Dubai, hivi anasafiri kwa mshahara upi alionao?”  Msukuma anaonekana kujua mengi kuhusiana na Makonda. Kwani aliongeza kusema kuwa “kama Rais Magufuli amesema kama mkewe Mama Janet anahusika na dawa za kulevya akamatwe, kwanini Makonda naye asihojiwe kwa sababu amewapangisha watu nyumba wakati wanajihusisha na dawa za kulevya?”
            Tuhuma hizi, licha ya kuwa nzito, zimetolewa na watu wazito wanaowakilisha watanzania wengi tokana na nafasi zao. Hivyo, haziwezi kuchukuliwa kivyepesi. Zinapaswa kupewa uzito na kuchunguzwa na matokeo ya uchunguzi wake kuwekwa hadharani. Kwa namna hiyo, Makonda anapaswa kuwekwa kando kupisha uchunguzi ili aweze kusafishwa au kukutwa na hatia. Huu ndiyo uongozi bora; na hakuna anayepeswa kuwa juu ya sheria.
            Tunaomba yafayike yafuatayo haraka:
Mosi, mamlaka husika kuchunguza madai dhidi ya Makonda yawe ni ya kushirikiana na au kunufaika toka kwa wauza unga au kumilki mali nyingi tofauti na uwezo wake kisheria. Tungependa haki itendeke kwa kumhoji na kushughulikia mhusika kama alivyosema rais John Magufuli kuwa hata kama akiwa ni mkewe akamatwe.  Hata hivyo, uzoefu unaonyesha, kama alivyodai Mdee, kuna baadhi ya watendaji wa serikali wanasikilizwa zaidi ya wengine kiasi cha kuaminiwa bila sababu ya msingi au kutoshughulikiwa wanapotuhumiwa. Mfano rahisi ni pale Makonda alipowatuhumu Makamanda wa polisi Simon Sirro na Suzana Kaganda kupokea rushwa toka kwa wauza shisha. Hakuitwa na vyombo husika kumhoji wala kutoa taarifa ya matokeo ya mahojiano na uchunguzi wa sakata husika. Hii ni tofauti na ni kinyume na dhana nzima ya utawala bora na wa sheria. Na rais Magufuli asipoangalia, hili litamkwamisha na kuweza hata kumchafulia. Kwani amekuwa akiunga mkono kila anachofanya Makonda kiasi cha kujengeka dhana kuwa yeye ndiye anayemtuma. Je anamtuma kweli? Sidhani kama Magufuli anahitaji kujificha nyuma ya Makonda hasa ikizingatiwa kuwa si mwoga. Je Makonda anapata wapi au kinga hii dhidi ya madai anayotoa? Jibu au majibu yatapatikana kutokana na namna serikali itakavyoshughulikia tuhuma hizi zilizotokewa na wabunge tena nyingi zikitolewa na wabunge wa CCM. Hakika, huu ni mtihani mwingine kwa Magufuli.
Pili, kama Makonda yu safi na tuhuma zinazoelekezwa kwake ima ni za uongo au zinalenga kumkatisha tamaa na kumwamisha, atafurahia ushauri huu na kuwa wa kwanza, kupisha uchunguzi na kutaka achunguzwe ili ukweli ujulikane ili aendelee na vita hii aliyoanzisha ambayo imewashinda wengi. Maana, kwenye shughuli za umma hakuna cha kuaminiana ukiachia mbali kuwa tetesi mara nyingi huelekea kwenye ukweli. Tusimhukumu Makonda kabla ya kufanyika uchunguzi hasa ikizingatiwa kuwa mitandao ya wauza mihadarati inajuana na kupigana vita.
            Je mwanzo wa mwisho wa Makonda ndiyo unaanza? Je yanayosema juu ya Makonda ni kweli au siasa? Je ni yale ya ivumayo haidumu? Je Makonda ataendelea kuwa kitendawili au mamlaka zitazinduka toka usingizini na kumtendea sawa na watuhumiwa wengine?
            Tumalizie kwa kumtaka Makonda na serikali kuanza uchunguzi mara moja ili mbivu na mbichi zilijulikana na kuendelea na mapambano yetu dhidi ya janga hili la kitaifa.  Pamoja na mapungufu yatakayojikeza, tuseme wazi; Makonda angalau amethubutu na kujaribu pale wengi waliposhindwa. Atusaidia katika hili ili kukata mizizi ya fitina. Naomba kutoa hoja.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.

Kijiwe Chajadili Bwimbwi

Mpemba anaingia akiwa na bashasha.  Lazima ana jambo la kutujuza lau tulidurusu na kutongoa huku tukitoa mapendekezo ya nini kifanyike kama suluhu ya tatizo liwe la kibinafsi au kitaifa.
Baada ya kuamkua, Mpemba anamwaga pwenti “jamani mmesikia kilivoumana kuhusiana na biashara haramu ya bwimbwi? Maana naona pachimbika bila jembe ati. Kila ntu asamaka Makonda hadi watuchanganya. Iweje leo ndiyo waamue kuanika siri za Makonda au nao wameguswa pabaya? Huko nyuma mbona hawakuwa hivyo. Au wote ni wale wale?”
Kapende anampoka mic na kuronga “wewe unaamini kuwa vita hii dhidi ya wauza bwimbwi inaweza kufanikiwa wakati inaonekana kufanyika kienyeji na kisiasa?”
Mpemba anajibu “wamaanishani kusema eti vita yapiganwa kisiasa na kienyeji?”
Kapende anajibu “uliona wapi watuhumiwa wanaitwa kwa ndata na kuachiwa wakati siku zote wezi wa kuku wanapotuhumiwa huozea lupango; sijui nani anataka kumdanganya nani katika sanaa hizi?”
Mipawa anakwanyua mic “hata mimi nilidhani ni usanii hasa pale walipokamatwa dagaa huku mipapa ikipeta. Lakini baada ya kuona na watukufu wakiitwa kwenda kujieleza, nilianza kujenga imani ingawa bado nina shaka na utaratibu mzima unaotumika wa kishikaji.”
Msomi Mkatatamaa anaamua kutia daluga. Anakohoa kidogo na kudema “ yote yanawezekana hasa ikizingatiwa kuwa huu ni mwanzo. Nadhani wengi mnashuku zoezi hili tokana na udogo wa aliyetanga na wale waliokamatwa mwanzo na namna walivyoshughulikiwa. Mie nafurahi kuwa angalau wanene wameamua kusema kitu hata kama si jibu. Maana ilifikia mahali bwimbwi na ufisadi vilihalalishwa. Napenda nitoe ushauri kuwa lisirikali linapaswa kuangalia mfumo mzima ulioweza kumotisha na kuruhusu baadhi ya wahalifu kumaliza vijana wetu kwa bwimbwi. Hivyo ningependa yafanyike yafuatayo: kila mwanakaya aeleze alivyochuma ukwasi wake huku wale watakaoshindwa kutoa maelezo mali zao zikamatwe na watupwe lupango.”
Kabla ya kuendelea Mgosi Machungi anakula mic “hapa Msomi umenena. Tingependa wae wote tinaowajua kuwa wana ukwasi wa haamu lazimu tiwataje na washikwe kwanza haafu mengine yafuate.hapa bia shaka wanapaswa kutieeza waivotengeneza ukwasi huu kama hakuna kitu nyuma ya pazia.”
Msomi anaendelea, “ukiachia mbali kukamata mali haramu, nashauri lisirikali lipige marufuku mianya yote ya uchumaji utajiri haramu kama vile baadhi ya wenzetu kujipachika vyeo vikubwa vikubwa vya kidini huku wakivitumia kuwaibia wachovu wetu kwa vile wana matatizo na ni wajinga. Hamjaona uchunaji ulivyogeuka uchochoro wa kutengeneza njuluku haraka? Nijuavyo, Yesu alikuwa kapuku. Sasa inakuwaje mtu anahubiri tu na kugeuka milionea hata bilionea ghafla bin vu wakati kazi anayofanya haina kipato kikubwa kama hakuna namna?”
Kanji anamchomekea “Somi mimi kubali veve sana dugu yangu. Iko vatu tajiri sana. Kama nauliza veve iko fanya kazi gani, hapana jibu zuri. Kama piga kelele naingiza juluku haraka sana mimi iko anza hubiri ili nipate juluku haraka.”
Mijjinga anakatua mic “mimi ni mchumi. Huwa sielewi namna ambavyo jamii inaweza kuruhusu jinai hii halafu isikumbwe na hatari kama hii ya kuuza bwimbwi na ujambazi mwingine bila kusahau ufisadi. Anayeiba sadaka au kuwatoza wachovu njuluku ili awahudumie hana tofauti na mwizi. Kwanza hawa wezi hawalipi kodi. Nashauri watozwe kodi na kuwekewa mfumo wa kuhakikisha wanaonyesha vyeti vya taaluma ya hayo wanayosema wanaweza kufanya kama vile kutenda miujiza na ujambazi mwingine ulioanza kuhalalalishwa kwa mlango wa nyuma tokana na kuwa na tawala uchwara zilizopita ambazo ziliruhusu kila mmoja ajiibie wakati wakubwa nao wakihomola na kufuja.”
Da Sofia Lion aka Kanungaembe anabusu mic “mie naunga mkono mapambano dhidi ya bwimbwi. Kwani hapa tunapoongea kaka yangu ni teja. Alikuwa amesoma vizuri na kazi nzuri lakini ameharibiwa na mibwimbwi kiasi cha kugeuka mzigo kwa familia. Hapa lazima kila mmoja wetu ashiriki vita hii kwa kutaja anaowajua ilmradi asiseme uongo wala kuonea mtu. Nafurahi kuwa wamethubutu hata kama ni kwa njia za kutia shaka.”
Mheshimiwa Bwege anakwanyua mic. Ansema “da Sofia tafadhali niruhusu nikuchomekee kidogo hapa. Nakubaliana nawe ingawa napingana na baadhi ya mawazo yako. Napendekeza kuwepo na utaratibu wa kisheria unaoeleweka ili kuepuka uwezekano wa baadhi ya wanene kuwamaliza maadui zao kisiasa au kuwaachia washirika wao kwenye balaa hili. Hii vita ni kubwa kuliko tunavyodhania. Hivyo, ningeshauri rahis mwenyewe awe taskforce yake ya kushughulikia balaa hili kwa mujibu wa sheria na kwa haki na usawa bila kujali cheo au jina la mhusika.”
“Hakuna kilichoniacha hoi kama waheshimiwa wa njengoni. Wanashangaa kwanini Makonda asafiri na kwenda kutanua ughaibuni na nkewe tena kwenye business class wakati Dk Kanywaji alipiga marufuku kwenda kutanua nje? Je ni wakubwa wangapi wa mikoa wamekwishakufanya hivyo? Hapa napo kuna so washikaji. Wengine wanasema jamaa ana ukwasi kama Bill Gates. Sijui hapa muongo na mkweli ni nani na kwanini sasa?” anakula mic Mijjinga.
Kijiwe kikiwa kinanoga si likapia Humvee la Makonda. Acha tulikate shingo kwa mshangao namna jamaa alivyochanganya njuluku haraka!
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.