tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post223920517180504824..comments2024-03-28T12:20:46.812-07:00Comments on Free Thinking: Tishio la jeshi linadhalilisha taifa na jeshiNdugu Nkwazi N Mhangohttp://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comBlogger10125tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-65853124332001458172012-02-18T16:05:23.538-08:002012-02-18T16:05:23.538-08:00vlaganje denarja [url=http://www.vzajemniskladi.in...vlaganje denarja [url=http://www.vzajemniskladi.info]alta skladi[/url]Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-37056039802426645912010-10-05T12:05:26.304-07:002010-10-05T12:05:26.304-07:00Gen Shimbo kachemka kwelikweli.
Wanajeshi wote wa ...Gen Shimbo kachemka kwelikweli.
Wanajeshi wote wa HadHi yake Duniani hukaa kimya kupanga mikakati ya kuchukua nchi kama jeshi pindi mambo yakienda kingelenyuma.
Sasa huyu Habithi wa kijeshi anashabikia chama,anakubali kukaa mkiani ukingoni mwa VENT ya CCM,anakubali kutumiwa kama ya ndani na wanasiasa wenye matumbo yasiyo shiba kaa magari yakusomba taka.CCM watamtumia kuwatia hofu wananchi kisha watamtosa kama chambio.
Kwa Mjeshi kujenga uaminifu wa dhati chini ya chama cha kisiasa ni sawa kabisa na kulala na changu doa kisha asubuhi yake kukurupuka kwamba na kupigia simu wazazi wako kwamba umechumbia na mipango ya koana iko mbioni. Wewe kama ni mjeshi Heshima na Uaminifu wako ni chini ya serikali. Kama huridhiki na serikali unachukua nchi kinguvu wewe mwenyewe.
Acha kijipendekeza kishamba Gen Shimbo.

MADELA WA MADILUAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-61310650603477233632010-10-04T07:48:42.941-07:002010-10-04T07:48:42.941-07:00Asante sana ndugu yangu Mbele kwa michango na chan...Asante sana ndugu yangu Mbele kwa michango na changamoto zako ukiachia mbali kunitembelea. Jana nilikutembelea na kufurahia mandhari ya mji wetu wa Lushoto ukiachia mbali kukumbuka historia yake ya miaka 1950.
Kwa vile hujawahi kuishiwa kufikiri na kuandika, naamini moto utakuwa ule ule wa kuikomboa jamii yetu na kuonekana watu kati ya watu.
Kila la heriNdugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-74351667059620643132010-10-04T07:13:33.586-07:002010-10-04T07:13:33.586-07:00Ndugu Mhango, shukrani kwa changamoto hizo zote. T...Ndugu Mhango, shukrani kwa changamoto hizo zote. Tuendelee kuyatafakari masuala haya ya Taifa letu na dunia kwa ujumla.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-30173517798679369652010-10-04T02:42:30.554-07:002010-10-04T02:42:30.554-07:00Mimi sijui kwanini, kwasababu polisi na jeshi ni s...Mimi sijui kwanini, kwasababu polisi na jeshi ni serikali. Kazi yao ni kukaa pembeni ili kukipokea chama kitakachotawala...je linafanyika hilo?
'Kuna dalili' Je ni nani akemee kama hizo dalili zipo? Ni polisi, au ni nani? Je anayeongea hapo kapata kibali toka kwanani? Au yeye ana `amri hiyo' kusema pale kunapotokea fununu?
Labda tuelimishwe kidogo na wahusikia, isije tukalaumu bure!emu-threehttp://miram3.blogspot.com/noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-39343633964587553972010-10-03T19:31:50.209-07:002010-10-03T19:31:50.209-07:00Hapa nimekupata Bro. Mbele. Huu umekuwa ugomvi wan...Hapa nimekupata Bro. Mbele. Huu umekuwa ugomvi wangu na mfumo wetu wa uombaomba ambapo rais mzima wa nchi anakwenda akijipiga kifua na majisifu kwenda kupiga magoti kwa rais mwenzie kuomba-umatonya.

Kimsingi fikra zako zinahitaji mfumo mpya wa kufikiri ambao hauko pengine bali kufumua na kufuma upya mfumo wetu wa elimu ambao ni muendelezo wa fikra tegemezi.

Sipendi vyama na sina chama zaidi ya kuamini katika freethinking. Tofauti yangu ni kwamba tunaweza kuanza kuzamisha chama nyemelezi kwa kuchagua vingine ili hapo baadaye utokee msuguano wa kuunda mseto kama tulivyoona Kenya. Matokeo ya msuguano huu ni kupatikana kwa katiba mpya itokanayo na wananchi. Kuuzika mfumo mfu wa sasa unaosimamiwa na kulindwa na wezi-nufaika si suala la kufumba na kufumbua. Tunaweza kuanza kutoa adabu kwa kuipiga teke CCM na kuwaambia wanaoingia kuwa huu ni mwanzo wa mambo.

Japo umependekeza mfumo-huru na asilia wa demokrasia ya kiafrika wa kukaa chini ya mti-bunge, je ni wasomi wangapi tulio nao wana mawazo kama haya au kuunga mkono wazo hili na kulifanyia kazi? Tuna madaktari na maprofesa wengi wasio na hadhi hata ya kugusa kiatu cha profesa wa kweli. Huwa nina mfano rahisi. Je marehemu Abeid Karume na Dokta Salmin Amour nani ni msomi hasa ukiangalia walichofanya kama viongozi wa Zanzibar?

Nakubaliana nawe. Leo utamkua profesa kama Ibrahim Lipumba akifungwa na chama kiasi cha kusimamisha ubongo wake na kuanza kukimbiza ruzuku huku akiendeshwa na Maalim Seif.

Wapo madaktari kama Lamwai Masumbuko. Warid Kaboro na wengine walioamua kujigeuza mbwa badala ya mbwamwitu wanaohenyeshwa na zuzu kama Yusuf Makamba, Kinana, Rostam Aziz, Edward Lowassa hata Jakaya Kikwete.

Nimejadili ugonjwa huu kwenye kitabu changu cha SAA YA UKOMBOZI na kuutolea mifano hai kwenye kitabu kingine ambacho kiko mbioni kutoka cha NYUMA YA PAZIA.
Nimefarijika na kunufaika na uoni wako usio upogo wala makengeza bali miali ya ukombozi na utambuzi vinavyolenga kuirejesha heshima ya taifa na jamii yetu.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-33270048131739002132010-10-03T17:39:36.823-07:002010-10-03T17:39:36.823-07:00Hata mimi msimamo wangu ni huo huo ulioufafanua, k...Hata mimi msimamo wangu ni huo huo ulioufafanua, kwamba tuwe na "mfumo wa uongozi uliojikita kwenye utashi na maendeleo ya watu na si kikundi cha wezi wachache..."

Hii ndio maana halisi ya demokrasia. Tatizo ninaloona ni kuwa wa-Tanzania, bila kutafakari historia yao na uhalisi wake, bila kutumia fikra huru, wameiga tu dhana ya chama au vyama.

Mfumo wa chama au vyama ulibuniwa Ulaya, na huenda unalingana na historia na uhalisi wa maisha yao, na kadhalika.

Watanzania hatukufanya tathmini, ya uhalisia wa kule tulikotoka, katika historia au utamaduni wetu, bali tuliiga dhana ya chama au vyama tangu wakati wa ukoloni, na leo tunashinikizwa kwamba lazima tuwe na vyama. Kinachoendelea leo ni ukoloni mambo leo, si matokeo ya fikra huru zetu wenyewe.

Tukirudi kwenye ile tafsiri ya demokrasia uliyotoa hapa juu, na ambayo tunakubaliana, utaona kuwa kitu kinachoitwa chama au vyama haiko pale.

Sasa hapo ndipo ninaposema kuwa wa_Tanzania tutafute mfumo unaoweza kutufanya tuwe na demokrasia au tujenge demokrasia.

Wahenga wetu walikuwa na mfumo wa demokrasia. Lakini hawakuwa na chama au vyama. Je, sisi wa-Tanzania hatuwezi tukawa na fikra huru, bila kuiga mambo ya Ulaya, tukatafuta njia ya kujenga demokrasia ambayo inaendana na uhalisi wa historia, jadi na mila zetu kama wa-Afrika?

Tumepoteza hata uhuru wa kuuliza suali hili na kulitafakari au kujaribu mfumo mwingine. Tukithubutu, waheshimiwa waliotutawala zamani watatuadhibu. Ndio maana nasema tunachoshabikia wa-Tanzania kinaonekana kama mfumo wa kujenga demokrasia nchini kwetu, kumbe ni ukoloni mambo leo.

Mfumo huu wa chama au vyama unatuletea migogoro ya wazi, kama tunavyoona. Mtafaruku unaonekana wazi katika jamii yetu. Ni ushahidi wa yale ninayosema, kwamba kuna haja ya sisi kuwa na fikra huru na kutafuta mfumo unaotufaa, na naamini utakuwa ni mfumo wa demokrasia bila chama au vyama. Ndio maana nasema kuwa vyama viende na maji, naona sawa tu.

Katika kuongelea demokrasia ya wahenga wetu, Mwalimu Nyerere alisema kuwa wazee walikuwa wanakaa chini ya mti na kujadiliana hadi wakubaliane. Ule ni mfumo walioutumia, na haukuwa wa kuigwa au kushinikizwa kama huu mfumo wa chama au vyama.

Haya ni baadhi ya masuali ambayo nimeyauliza kwa undani zaidi katika kitabu changu cha CHANGAMOTO.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-64490254141075301062010-10-03T16:25:00.291-07:002010-10-03T16:25:00.291-07:00Nakushukuru sana Bro. Mbele kwa mchango wako ulios...Nakushukuru sana Bro. Mbele kwa mchango wako uliosogeza wazo langu mbele zaidi. Ingawa sikubaliani na yote uliyosema, kuna haja ya kukubaliana kuwa nchi haiwezi kuishi bila uongozi. Hivyo, ni kweli kuwa vyama vinaweza kupotelea mbali na taifa likabaki. Lazima liwe na mfumo ongozi uliojikita kwenye utashi na maendeleo ya watu na si kikundi cha wezi wachache kama ilivyo nchini kwetu. Kama wasomi na Thinkers, tunapaswa kulisimamia na kulisisitizia hili kwa nguvu zote. Kuna haja ya kuondokana na CCM na kuanza upya kuanzia alipotuacha Mwl. Julius Nyerere.
Na hatuwezi kuanza bila kuanza na kuifurusha CCM ili tujue mwelekeo wetu kama taifa na jamii ya watu wenye akili na utashi wa kuendelea kwa ajili ya vizazi vijavyo.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-68993336223310072902010-10-03T12:40:10.578-07:002010-10-03T12:40:10.578-07:00Nimechungulia kwenye taarifa magazeti, na kama kil...Nimechungulia kwenye taarifa magazeti, na kama kilichoandikwa ndicho kilichosemwa na Afande, sina matatizo na kauli zake.

Ila tu, napenda kukumbushia kwamba CCM ina historia ya kuhujumu amani, kama ilivyotokea Visiwani mwaka 2001. Taarifa ya Human Rights Watch inaonyesha kuwa CCM na polisi ndio chimbuko la matatizo yale.

Kwa hivi, jeshi lijitahidi kuichunga CCM, maana watu wanaogopa yaliyotokea kabla, kama vile kuibiwa kura. Hii hofu ya kuibiwa kura na CCM iko, na niliishuhudia nilipokuwa Tanzania kuanzia mwezi Juni hadi Agosti.

CCM itamke hadharani, na isisitize na kuthibitisha kabisa, kwamba haina mpango wa kuvuruga uchaguzi, wala kuiba kura. Hii ni muhimu katika suala la kuhakikisha kuwepo kwa amani.

Mimi kama raia ambaye si mwanachama wa chama chochote ninasikitishwa na hali iliyopo, ya watu kuogopa kuibiwa kura zao. Na kwenye hizi kampeni, naona jinsi wapinzani wanavyohangaikia suala hili, wakitafuta mbinu za kulinda kura.

Mazingira ya hofu namna hii ndio mazingira yanayokaribisha uvunjikaji wa amani. Hii hofu inatokana na yale yaliyotokea kabla.

Ningetegemea kuwa rais angeweka kipaumbele kwenye kuhakikisha kuwa kuna amani nchini, hata ikibidi kuwakemea CCM ambao kuna taarifa kuwa wamekuwa wakileta vurugu.
Sijamsikia amewakemea hao CCM. Amezama kwenye kampeni kama mgombea wa CCM, badala ya kukumbuka kuwa ana kofia ya urais ambayo inamlazimisha kuweka mbele maslahi ya nchi kwanza, si maslahi ya chama.

Mimi kama m-Tanzania ambaye si mwanachama wa chama chochote naifikiria nchi yangu. Sina undugu na chama chochote, na hata vikisambaratika, nchi itabaki. Nchi ilikuwepo kabla ya vyama, kabla ya CCM, kabla ya TANU. Vyama vyote vikienda na maji, nchi itabaki. Namtegemea rais wa nchi akumbuke jambo hilo na kulizingatia.

Taarifa ya Human Rights Watch,ambayo inaonyesha jinsi kule Visiwani CCM ilivyofanya hujuma na uchokozi, na jinsi polisi ilivyofanya umachinga kwa CCM, ni hii hapa.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-84095399698577831942010-10-03T11:00:05.994-07:002010-10-03T11:00:05.994-07:00Ni kweli jeshi letu limepoteza heshima na maana. K...Ni kweli jeshi letu limepoteza heshima na maana. Kikwete amegeuka mzigo kwa kila mtu na hafai hata jeshi liingelie kati. Hii ya The Hague ni jibu kwa ubabaishaji na vitisho vya jeshi.Anonymousnoreply@blogger.com