tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post249726814053560349..comments2024-03-25T17:42:20.850-07:00Comments on Free Thinking: Je uraia wa nchi mbili ni kwa wageni tu Tanzania?Ndugu Nkwazi N Mhangohttp://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comBlogger4125tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-72792293399220830152016-08-09T16:03:14.556-07:002016-08-09T16:03:14.556-07:00Mwalimu Mhango,
Najuwa fika kabisa kwamba wakati w...Mwalimu Mhango,
Najuwa fika kabisa kwamba wakati wako upo finyo kiasi gani lakini cha kushukuru tu kwamba kuwapa umuhimu na kutowapuuza wasomaji wako pale wanapotoa machango wao wa kimawazo hata ikiwa kwa uchache kiasi gani,hili linatupa moyo na nguvu sisi wasomaji wako kuweza kukufuatilizia na kukusoma.Sisi wengine kutokana na pilika pilika na majukumu ya kimaisha katika ulimwengu wa tatu kama unajvyojua tunakuwa hatuna wasaa wa kutosha wa kuweza kuwa karibu na matandao mara kwa mara,lakini ikitokea tu kupata nafasi tunaitumia nafasi hiyo katika kukusoma na kama kuchangia maoni tunakuwa hatusiti kufanya hivyo,

Tunamuomba tu Mwenyezi Mungu akupe uhai mrefu ukiambatana na afya njema ili uzidi kupandikiza mbegu za mawazo ambayo mimea na miti yake watafaidika nayo kizazi kijacho na kujiuliza kwa nini kizazi cha wakati wako hawakufaidika na mimea hiyo na miti hiyo.kwani kizazi chetu hichi tumekuwa wavivu wa kujisomea na kushiriki katika changamoto za kuchangia mawazo baki salama na kila kheri.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-54548979231127375602016-08-06T10:00:59.568-07:002016-08-06T10:00:59.568-07:00Anon,
Hata kama nimechelewa kujibu kutokana na kut...Anon,
Hata kama nimechelewa kujibu kutokana na kutingwa na majukumu, nakubaliana na nyingi ya hoja zako zenye mashiko. Hata hivyo, kama tutaangalia ukweli wa mambo, ni kwamba taifa letu na Afrika kwa ujumla iko utumwani chini ya ukoloni mamboleo anbapo kujikana kumegeuka fasheni. Siwashangai wanaotumia salamu za kigeni kutokana na ukweli kuwa wanaonyesha wao ni nani. Asiyevuta kamba nasi si mwenzetu. Hawa -hata kama wamesoma -ni waathirika ambao kuwatofautisha na wajinga sipati. Ni bahati mbaya kuwa tumefundishwa kujikana na kujitukana huku tukitetemeka tunaposhauriwa kuasi utumwa huu wa kiakili na kimwili. Walipoleta mila zao wakaziita dini, wakabadili majina yetu na kutupa yao kama mbwa, tulipoteza kila kitu. Hivyo, tunachopaswa kufanya -kwa wale wanaojitambua -ni kuasi na kuendelea kupiga kelele. Huenda kuna wachache tutawaokoa na kuwaongoa.
Kwa ufupi hayo ndiyo mawazo yangu; pia nakushukuru kwa mchango wako adhimu na adimu.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-40673110904688018032016-07-31T08:59:30.101-07:002016-07-31T08:59:30.101-07:00Tunawasamehe na kuwasahau wale ambao waliotuathiri...Tunawasamehe na kuwasahau wale ambao waliotuathiri kwa kutufanya watumwa na hadi hii wanaendelea kutufanyia utumwa mambo leo,tunawasamehe na kuwasahau wale ambao wametukoloni na bado wanaendelea kutukoloni ukoloni mambo leo na hatimae ni sisi wafrika ndio tumeaamua kuwa walinzi wao wa utajiri wetu ambao wananufaika nao kuliko sisi wenyewe waafrika na dio sisi tunaopigania masilahi yao kwa kila njia na ya kila aina likiwemo hili la hata kupewa wao uraia pacha ıli wazidi kuyalinda masilahi yao kwa kadiri iwezekenavyo.

Mwalimu Mhango.endapo hukulelelewa au kujengewa tangu udogo hisia ya kujifaharia taifa lako,uafrika wako.rangi yako.dini yako,na mila desturi zako kamwe hautokuwa mwenye kutambuliwa na kuheshimiwa na watu wengine.Je Mwalimu Mhango.umeiona Tanzania ya leo ya wanasiasa wetu wakiwaamkia wananchi wao katika majukwaa ya kisiasa na ya kıjamii maamkizi ya dini za kigeni Asalaamu Alaykum.Na asifiwe Bwana.Tumsifie Yesu Kristo?Hivi ni kweli tumefelisika kwa kiasi hiki hata yakawa maamkizi ya kidini kuwa ndio maamkizi yetu katika siasa na katika mahafali ya kijamii?Kwa nini maamkizi hayo yasibaki tu misikitini na makanisani?Namalizia kwa kuandika kwamba kuna hizi power za nje zinazofanya kazi nyuma ya pazia zikishirikiana na wengi wa viongozi wetu wa Kiafrika kuhakisha kwamba masilahi ya wageni wa race isiyokuwa ya kiafrika yanatetewa hadi mwisho wa dunia na kama kiongozi wa kiafrika atakwenda kinyume cha hayo atawekewa mibiginyo yote stahiki kwake na watu wake lumumba,ıddı Amını na hatimae Mugabe ni mfano hai. Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-42829085795310974912016-07-31T08:31:51.581-07:002016-07-31T08:31:51.581-07:00Salamu Mwalımu Mhango,
Niweke kando kwanza kuhusu ...Salamu Mwalımu Mhango,
Niweke kando kwanza kuhusu hii kadhia ya uraia pacha pamoja na umuhimu wake ulivyo kwa wananchi wa Tanzania kuweza kupewa haki hiyo kama ni haki ya kitabia baada ya dunia kubadilika na kuwa ni kijiji kimoja.

Tatizo kubwa Mwalimu Mhango,ni sisi waafrika kuwa vıctims kutoka kwa watu wengine wote duniani wasiokuwa waafrika.Mwarika huyu nje ya Afrika ni mwenye kunyanyaswa.kudhalıshwa na kuonekana kwamba astahiki kuwa na sifa za mwanadamu kamili,na hatimae mwafrika huyu kana kwamba ameikubali hiyo na kujıtahidi kwa kadri anavyoweza kuukataa uafrika wake,mila na desturi zake na hata dini yake.

Mwalimu Mhango,Kadhia ni utumwa wa kiakili na utamaduni wa kitumwa na kwetu sisi waafrika wa Bara Mama hali yetu ni mbaya zaidi ya kuukubali utumwa huu wa kiakil na utamaduni huu wa kitumwa kwani sisi waafrika wa Bara Mama tunachopıganıa daima ni kujınasibisha na wale wote waliotusababishia huu utumwa wa kiakili na utamaduni wa kitumwa.Sisi waafrika wa Bara Mama ndio ambao tunaoinua bango la "FORGIVE AND DO NOT FORGET".Swali linalojiuiza hapa kwa nguvu ni hili,kwa nini tu ni sisi waafrika ndio wenye kusamehe na pia ni wenye kusahau?Anonymousnoreply@blogger.com