tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post4454008252947773244..comments2024-03-25T17:42:20.850-07:00Comments on Free Thinking: Lowassa angejisaidia na kuusaidia upinzani kamaNdugu Nkwazi N Mhangohttp://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comBlogger3125tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-75245397652533781072015-08-09T20:33:13.245-07:002015-08-09T20:33:13.245-07:00Ndugu Mhango
Hii mijadala, na uchambuzi wa kila s...Ndugu Mhango

Hii mijadala, na uchambuzi wa kila suala la kipengele ni muhimu. Inatoa mwanga kwa kila anayeshiriki au anayefuatilia. Siku na saa na dakika itakuja ya kupiga kura, kuamua kunyoa au kusuka. Ningekuwa mpiga kura, kwa hali ilivyo sasa, na kama hakutakuwa na mabadiliko yasiyotarajiwa, kura yangu ningempa Lowassa.

Ni uamuzi wa kusuka au kunyoa. Hatuna malaika kati ya wagombea. Hilo ni wazi. Kila mpiga kura atajijua mwenyewe.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-3482110242950811522015-08-09T14:33:27.584-07:002015-08-09T14:33:27.584-07:00Kaka Mbele shukrani kwa mchango wako japo sikubali...Kaka Mbele shukrani kwa mchango wako japo sikubaliani na jinsi ulivyorahisha mambo. Nadhani tunapaswa kuangalia upande wa pili wa shilingi--kama CCM haitadondoka nini kitafuatia? Je UKAWA wanaootea kuiondoa CCM kwa kumeguka? Umenifurahisha na kunichekesha kusema eti maslahi ya Lowassa ni sawa na UKAWA. Naweza kukubaliana nawe kama ungesema lengo lao lakini si maslahi. Pia naweza kukubaliana nawe ukisema ni maslahi binafsi na si ya taifa. Ila kusema wanataka kuing'oa CCM kwa maslahi ya watanzania kidogo inatia shaka. Najaribu kumtathmini Lowassa kwa upande mwingine, mfano kama angepitishwa na CCM unadhani angekuwa mpole na MKAWA kama unavyomuona? Nadhani UKAWA wamethibitisha kitu kimoja au viwili. Kwanza, wanaweza kuchukua risk jambo ambalo ni zuri na hatari kisiasa. Pili, wamekuwa wakweli kuwa miaka yote walikuwa wanapiga siasa na kubangaiza. Maana haiwezekani mtu mmoja awe na nguvu kuliko vyama vinne na hivi vyama vikwa na maana kama tutakuwa wakweli.
Naona niachie hapa nisiandike makala ndani ya makala.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-47629299324641374912015-08-09T13:00:16.097-07:002015-08-09T13:00:16.097-07:00Ni muhimu kuzingatia pia kwamba UKAWA walimtaka na...Ni muhimu kuzingatia pia kwamba UKAWA walimtaka na wanamtaka Lowassa, na walitaka awe mgombea wao wa urais. Hili si suala la upande moja. UKAWA wanatambua nguvu ya Lowassa, na walitaka, na wameridhia kuwa yeye awe mgombea wao wa urais. Wanatambua kuwa kwa yeye kuwa mgombea urais, kuna uwezekano mkubwa wa kuing'oa CCM madarakani.

CCM yenyewe inatambua tishio hilo, na ndio maana inafadhaika sana. Baada ya Lowassa kuhamia UKAWA, upepo wa kisiasa unazidi kuvuma kuelekea UKAWA. Kila kukicha tunasikia wazito wa CCM na wanachama wa CCM wanakimbilia UKAWA. Hili si suala la kubuniwa, ni hali halisi inayoonekana siku hadi siku.

Lowassa hayuko UKAWA kwa ajenda yake binafsi. Atakuwa anasimamia maazimio na matakwa ya UKAWA. Ila tu ni kwamba ajenda na matakwa ya UKAWA na yale ya Lowassa ni yale yale kwa kiasi kikubwa. Ndivyo walivyoanza. Huko mbele ya safari, katika kufanya kazi pamoja, katika kufahamiana zaidi, katika kuelimishana, na katika kurekebishana, wanaweza wakaondoa tofauti zao, kama ziko, wakawa kitu kimoja thabiti.Mbelehttps://www.blogger.com/profile/16077261126944002622noreply@blogger.com