tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post7396808859915359969..comments2024-03-25T17:42:20.850-07:00Comments on Free Thinking: Janga la taifa: Vyuo vikuu vinapoeneza ujingaNdugu Nkwazi N Mhangohttp://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comBlogger2125tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-86632011780766574022016-03-15T18:50:38.712-07:002016-03-15T18:50:38.712-07:00Anon swali na shaka yako ni vya muhimu. Jibu la sw...Anon swali na shaka yako ni vya muhimu. Jibu la swali lako unalo hasa unapowaangalia watu kama January Makamba mtoto wa kihiyo na Dk Hussein Mwinyi walivyosomeshwa nje wakaja kurithi nafasi za wazazi wao. Hao ni wachache tunaowaona kwenye medani za kisiasa. Ukienda kwenye mabenki hasa BoT na wizara zenye mishiko na balozi zetu nje unaweza kuzimia kujua kuwa kumbe wakubwa ndiyo walioanzisha kiama hiki. Akina Msekwa watoto wao wamejazana kwenye balozi zetu nje. Nadhani walifanya makusudi ili watoto wao wapate wajinga wa kutawala kama wao. Tofauti ya Magufuli na wao ni kwamba yeye ametokea kwenye kizazi cha kajamba nani. Hivyo, anaelewa matatizo ya wenzake na ndiyo maana anakuwa mkali hivi ili angalau taifa liende mbele kwa pamoja. Tuombe Mungu wasimkolimbe au kumSokoine.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-7492381243837788462016-03-15T15:44:43.845-07:002016-03-15T15:44:43.845-07:00Naam Mwalimu Mhango ni kweli kabisa sera mbovu za ...Naam Mwalimu Mhango ni kweli kabisa sera mbovu za Kiliberali mambo leo za kubinafsisha kila kitu na kile walichokiita soko huria ndio chanzo au mwanzo wa mabalaa yote ya kuzifanya nchi zetu za kiafrika kiujumla na nchi yetu hususa kurudi nyuma kimaendeleo nakumbuka Mwalimu Nyerere alikuwa na hoja ya kuwanyamazisha wakosoaji wake wa siasa yake ya Ujamaa pale alipokuwa akiwauliza "Nionyesheni nchi yoyote ile ya kiafrika inayofuata siasa ya kibepari ambayo inafanya maendeleo kwa siasa hiyo ya kibepari"
Mimi naamini kabisa kwamba shindikizo waliowekewa nchi za kiafrika na nguvu za kibepari na za kabeberu kuukubali mfumo wa uchumi wa kiliberali au soko huria kwa kukidhi mahitaji ya mashiriika yao makubwa ya kibiashara kwa kuendelea kuziibia nchi zetu utajiri wake na rasilimali zake wizi ambao umekuja kwa utaratibu wa matual consent na viongozi wetu waliotudanganya kwamba ndio mwanzo wa maendeleo

Naam Mwalimu Mhango.kwa watanzania baada ya utawala wa Mwalimu Nyerere kulisikika malalamiko kwamba Mwalimu Nyerere amewanyima watanzania elimu na hatimae watanzania waka2a wengi wao wanajihisi upungufu muda wa kudumu tu hawana uw3zo mzuri wa kujieleza katika lugha ya kiingereza kama ilivyokuwa kwa wale waliotawaliwa na mkoloni wa kifaransa kwamba kifaransa ndio kila kitu kwa hiyo ikaambatanishwa kuongea kiingereza au kifaransa ndio elimu au umeelimika kwa mfumo huu wa kufikiri ilipokuja mfumo huu wa kiliberari tunakuta tu wajanja wakaingia sana kuwekeza ktk sekta ya elimu kwa shule binafsi kuanzia chekechea,msingi,sekondari mpaka chuo hatimae ndio hayo yaliyotokea na yanayotokea katika baadhi ya vyuo vikuu yva watu binafsi.

Lakini swali muhimu hapa la kujiuliza au linalojiuliza lenyewe je kama asingekuja rais Magufuli madarakani uhoza huu na ufisadi huu si ungekuwa ukweli wa kuendelea?Na katika ufisadi huu je hakuna uwezekano wa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu kushiriki katika kuwatia wanafunzi wa kitanzania ujinga na wao kufaidika kiuchumi wakati watoto wao wanawasomesha nje ya nchi katika vyuo vyenye majina?Kama ilivyoathirika sekta hii ya kielimu kwa kupitia mfumo mbovu wa kileberali ndivyo hivyo hivyo wajanja hao hao na viongozi hao hao mafisadi walivyoiathiri sekta ya afya katika nchi yetu.

Na tuzidi tu kumuombea na kumpongeza rais wetu Magufuli kwa kutupia macho sekta zote hizo zinazogusa msatakibali wa vijana wetu na nchi yetu pia nakupongeza kwa kushauri ufumbuzi wa ufisadi huo ni matumaini yangu rais Magufuli na serikali yake watauzingatia na kuutekeleza.

Anonymousnoreply@blogger.com