tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post743396597407432580..comments2024-03-28T12:20:46.812-07:00Comments on Free Thinking: Wasanii ni wakereketwa au njaa na upogo?Ndugu Nkwazi N Mhangohttp://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comBlogger7125tag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-91862018867610973072015-10-22T15:36:36.751-07:002015-10-22T15:36:36.751-07:00Anon21 October 2015 at 01:13 nakushukuru sana kwa ...Anon21 October 2015 at 01:13 nakushukuru sana kwa kumfikishia ujumbe Anon mwenzako ambaye hajui maisha yalivyo huku ukilinganisha na Bongo ambako wengi wangetamani lau watoke wakapumzike kwa muda kutokana na machungu kama mgao wa umeme, misongamano, ukosefu wa usalama, msongamano, chuki, ufisadi, umaskini, dhuluma, ubabaishaji, na mengine mengi. Ni bahati mbaya mimi sina connection wala nia ya kujiingiza kwenye siasa za kilafi zinazoendelea huko. Hivyo, kuja huko ni sawa na kujitia kitanzi. Hata ningeamua kuja kwenye sabbatical najua sitafaa kutokana na mifumo na miundombinu mibovu mashuleni na vyuoni. Pia naamini ninayoweza kufundisha yanaweza kuwakwaza hata watawala. Hivyo, heri niendelee hapa kuchapa kazi na kufanya mambo mengine. Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-2701839381551655872015-10-22T15:32:57.117-07:002015-10-22T15:32:57.117-07:00Anon umenifumbua macho kuwa "njaa upogo na uk...Anon umenifumbua macho kuwa "njaa upogo na ukereketwa" vimewamotisha wasanii kuiunga mkono CCM ukiachia mbali kuhadaiwa kuwa Kikwete aliwapenda wakati aliwatumia. Kwa vile wasanii wengi wamo kwenye fani kutafuta tonge, sitashangaa tena. Hili la Kikwete kujitia kimbelembele kutafuta umaarufu umeniacha hoi na swali lako kuwa kama kweli Kikwete amewakomboa au kuwatumia nalo limenifikirisha. Mimi niliandika kama kuwaonya waangalie nafasi yao kijamii kama wasanii. Sijaona models kwenye sanaa zaidi ya wengi kupwakia siasa baada ya kuona Mr II ameukwaa ubunge wasijue alijiandaa muda mrefu. Nangoja kuona wasanii wangapi wataukwaa kama mwenzao au kuishia kubwagwa kama mmojawapo aliyetaka kupitia ubunge wa dezo akabwagwa na kuendelea kujikomba akidhani huenda atateuliwa. Kwa nimjuavyo Magufuli, sijui kama ana nafasi ya usanii zaidi ya kufanya kweli. Nasema Magufuli kwa vile amegombea na kiza hivyo lazima ashinde.
Nakukaribisha na kukushukuru kwa michango yako yenye mashiko siku zote. Karibu tena.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-22814811517217171432015-10-21T19:17:03.842-07:002015-10-21T19:17:03.842-07:00Mwalimu Mhanhgo,hapa kuna haja ya kujiuliza kwa ni...
Mwalimu Mhanhgo,hapa kuna haja ya kujiuliza kwa nini mapenzi haya ya wasanii yawe makubwa kwa chama cha CCM?kwa kujibu swali hili kama utakumbuka Mwalimu Mhango uliandika makala yako ya "Nitakavyomkubuka Kikwete"na kuoredhesha yale ambayo utakayomkubuka katika utawala wake,kuna hili kwa maoni yangu ambalo ndio sababu ya wasanii kuikumbatia CCM kama chama chao nalo ni kwamba Kikwete anazingatiwa kama Rais ambaye amewaiinua na kuwasapoti wasanii wa Tanzania,na wasanii karibu wote wanakubaliana kwa hilo na utawasikia wakimsifia kwa hilo.Mimi kwa muono wangu nimekuwa nikijiuliza kwa lipi alilowasapoti?kana kwamba usanii umeanza katika utawala wa Kikwete?Je ni kutokana na kuhudhuria mazishi ya wasanii?Au je kuwaita wasanii watumia madawa ya kulevya Ikulu?Au je kupiga nao picha za hadarani na wasanii hao?au hata kuwaalika wasanii wa Kimarekani na kukutana nao Ikulu?Je hiyo ndio sapoti kwao na ndio kuwainua kisanii?

Na ikumbukwe tu kwamba Kikwete ni mwanasiasa kama mwanasiasa yoyote yule anaekuja kwa zama zake,na zama zake ni zama za kuabudiwa mashujaa wa kila aina kuanzia wanamichezo wasanii na hata waonyesha mavazi (models) hata kama mashujaa hao wana ufisadi wote wa kijamii na hata kukosa kuwa kiigizo bora kwajamii,Kikwete alilijua na aliliona hilo kama mwanasiasa na kuona kwamba litamsaidia katika umashuhuri rahisi katika utawala wake kwa hiyo akajiweka kimbelembele mpaka kufikia kuchafua haiba yake kama Rais wa nchi.Sasa kwa wasanii wa Tanzania wamemuona hivyo na wamemshukuru kwa hilo na ili kumfadhili ndio wakamfanyia tafrija ya kumuaga na kuamua kukikumbatia chama chake kwa kuamini kwamba uwenda atakeyekuja madarkani kupitia chama chake atakuwa ni kama msanii mwenzi wao Kikwete.Na hata tumemsikia mgombea wa CCM akiwaahidi kwamba atawafanya matajiri kama wasanii wa kimarekani,kwa viigizo gani?mimi sijui.

Mwalimu Mhango UKEREKETWA,NJAA NA UPOGO ndio sababu za kimsingi ya mapenzi hayo ya chama tawala.Ingekuwa vyema wasanii hao wangewajibika kila wanapokodishwa na kualikwa katika burudani zingine za kijamii kuliko kujiiadhirisha mbele ya jamii kwa njaa yao upogo wao na ukereketwa wao kwa kujifichia mwamvuli wa kisiasa cha kuhuzunisha zaidi ni kwamba wale wasanii ambao wanayaona maovu ya wanasiasa kwa kuidhalilisha nchi na wananchi na wakayakemea hayo ndio kwanza wanapigwa vita na kupigwa marufuku kwa nyimbo zao kusikika maridioni au hata kutosikika kabisa!Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-57828585057483715182015-10-21T19:15:50.314-07:002015-10-21T19:15:50.314-07:00
Salamu Mwalimu Mhango,
Sababu zote tatu ulizozita...
Salamu Mwalimu Mhango,
Sababu zote tatu ulizozitaja katika kichwa cha habari cha hawa wasanii za kuibuka na mapenzi kwa chama tawala zote ni sahii na zinafiti kutokana na wao walivyo.Mwalimu Mhango swala la siasa ni swala ambalo linalomgusa na linalomuhusu mwananchi wa kawaida mwenyewe moja kwa moja na kwa vile kuna vyama vinavyowawakilisha wananchi hao katika kuyaweka masilahi ya wananchi mbele kuliko masilahi yao binafsi na kwa bahati mbaya chama cha siasa cha CCM hatukuliona hilo tangu utawala wa awamu ya pili hadi hii ya nne.Na kwa kusema hivyo basi,wanasiasa wetu hususa wa chama cha CCM wamekuja na mbinu ya kuwatumia wasanii katika kampeni zao za kisiasa kana kwamba wasanii hao ni wanachama wa chama chao cha CCM,na hapa ndipo swali la kujiuliza,je ni kweli kwamba wasanii hao wote waliokodiwa na kutumiwa na CCM ni wananchama wa CCM?Kama jibu likiwa kwamba ni wananchama wa CCM mimi hapa naona hakuna haja ya mjadala kwani watakuwa wanatekeleza haki yao ya kupigania kukufikisha chama chao katika madaraka kama atavyokuwa mwananchi yoyote yule mwachama wa CCM amabaye sio msanii.Lakini sidhani na nina uhakika kwamba sio wasanii wote waliokodiwa na CCM ni wanachama wa CCM,bali kuna baadhi yao sio wananchama wa chama hicho na wala hawatokuwa tayari kuwapa kura zao CCM lakini kwa vile ni wasanii na kwa sababu ya njaa yao na upogo wao kwa sababu zote ulizozifafanua tunakuta kwamba wamepoteza maadili na sifa sahii za jukumu la usanii hapa tukiwaondoa wale wasanii wakereketwa ambao watakuwa wanajulikana katika chama chao na hata kuelekwa mbele ya wananchi kwamba ni wanachama wa CCM kwa hawa sio kesi yetu.
Lakini kwa wasanii wenye njaa na wenye upogo kweli inakuwa ni usaliti kwa mashabiki wao na usaliti kwa wananchi na usaliti kwa usanii wenyewe ambao una maadili yake na una dhamana kubwa mbele ya jamii ambao wanatakiwa wawe dira na muongozo na watibabu wa maradhi ya kijamii,na kwa maoni yangu walitakiwa wawe kama viongozi wa dini ambao hawatakiwi kujihusisha kabisa na siasa isipokuwa pale tu kweli watakapoona wanajiamini na wanastahiki kujiunga katika siasa kama wanasiasa kwa vile wana kadhia ya kuipigania kwamasilahi ya wananchi na ya nchi na sio kama alivyojiingiza msanii mmoja katika siasa kwa kuwawakilisha wananchi(ubunge) akiwa na kadhia ya kuwapigania wasanii bungeni kana kwamba wananchi anaowawakilisha wa jimbo lake ni wasanii wenzie!!!
Inaendelea........Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-59869230356073560602015-10-21T01:13:51.492-07:002015-10-21T01:13:51.492-07:00Mwalimu Mhango,
huyo Anon anaganzi ya akili hivy...Mwalimu Mhango,

huyo Anon anaganzi ya akili hivyo ni ngumu kwake kufahamu nje ya Tanzania kuna nini haswa kinachoendelea wakati wa kupatia mkate wako kila siku mwalimu.

Sisi baadhi yetu tulionja kidogo hayo maisha halafu tukarejeshwa huku Motoni pasipo hiyari yetu sasa tunaelewa vizuri matatizo yetu yanasababishwa na uwezo wetu duni wa kufikiri.Na hata unaweza kuona sasa wasanii wanafikiri tatizo lao ni pesa pekee na kujaribu kutofautisha na uzalendo eti wamekodishwa kupiga kampeni za siasa.

Kwani wao wapo sayari tofauti. Hivi wanafahamu madhara ya kumpata mmbovu yatawagusa wao pia miaka mitano ijayo na kwa uharibifu utakafanyika wakati uongozi huo mbovu inaweza kuwa uharibifu utakaodumu kwa vizazi na vizazi vijavyo pasipokuwa rahisi kurekebisha huo uharibifu.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-62388647694493684842015-10-20T16:32:05.527-07:002015-10-20T16:32:05.527-07:00Anon Asante sana sema si kwamba huku nakula dezo. ...Anon Asante sana sema si kwamba huku nakula dezo. Natumia vipawa na nguvu zangu kula na kukuza vitegemezi vyetu. Nitakuja wakati ukifika ingawa kwa sasa hakuna cha mno cha kupotezea mamilioni ya shilingi.Ndugu Nkwazi N Mhangohttps://www.blogger.com/profile/11640087613265490788noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-8636874348650313883.post-14472577849809986282015-10-20T02:45:06.273-07:002015-10-20T02:45:06.273-07:00Well come to tanzania mwalimu wacha kula dezo huko...Well come to tanzania mwalimu wacha kula dezo huko
Anonymousnoreply@blogger.com