Ingawa kuna miji inayovutia sana wengi nchini Kanada, nimetokea kupenda mji wa Montreal. Najua wapo watakaoshangaa utapendaje mji ambao hauko kwenye chati ya miji inayovutia kama vile St John's (Mji wangu wa zamani), Guelph, Halifax na mingine mingi. Pamoja na kuipenda Montreal, ninapenda kanisa hili hapa chini lililoko Guelph Ontario.
NNakumbuka kanisa hili la St John's. Ni mojawapo ya vivutio vya mji huu wa kwanza Amerika ya Kaskazini.
Usthaadh karibu tena Montreal. Wenyeji tupo tele kama pishi la mchele.
ReplyDeleteUstaadh nakaribia nikipata nafasi. Nahisi kama mwanafunzi wangu fulani maeneo ya Al Haramain kwa jina la M....ba... Mji wenu mzuri sana. Umenikumbusha mji wangu wa awali St John's kisiwani.
ReplyDeleteTupo njiani kuja kukutembelea...
ReplyDeleteNawakaribisheni ila msije kwenye winter mtaichukia Kanata bure.
ReplyDeleteSwadakta staadh, nipi hapa. Ukiwa tayari basi karibu sana. Dada na wewe unakaribishwa pia.
ReplyDeleteTuombeane dua shehe. Kila la heri
ReplyDelete