Free Thinking

I Fear Nothing But Fear Itself

Tuesday, 2 October 2012

CCM inapogeuzwa kuwa mali ya familia ya Kikwete


  1. Angalau baadhi ya magazeti ya Tanzania yameanza kuona mwanga kuhusu uroho wa madaraka ambao umeanza kuwa ndiyo mtindo wa maisha nchini.  Hili la rais Jakaya Kikwete na familia yake kuanza kujipenyeza kwenye nafasi za juu chamani kiasi cha kugeuka kama mali ya familia lingeandikwa na blog hii huenda lingeonekana kama kumchukia. Taratibu ukweli unaanza kuvuka mipaka. Je nini kitafuatia baada ya wakubwa kuvimilkisha vyama vyao kwa wana familia na marafiki zao bila kusahau waramba viatu wao kama inavyofanya CCM?
    Leo utasikia majina ya ndugu kwenye safu za juu chamani hata wake na waume kwenye ubunge wa kuteuliwa hata kuchaguliwa kama ilivyo kwa familia ya Samuel Sitta, Shellukindo kabla ya mume kupigwa chini, Kawawa, Lissu, Nchimbi na wengine wengi.
Ndugu Nkwazi N Mhango at 14:48

1 comment:

  1. Anonymous2 October 2012 at 18:05

    Huyu kilaza wetu umemuonea kutaka afikiri wakati kazi yake ni kutanua. Natamani itokee iliyotokea Libya nimshuhudie akilia na kusaga meno.

    ReplyDelete
    Replies
      Reply
Add comment
Load more...

‹
›
Home
View web version

About Me

My photo
View my complete profile
Powered by Blogger.