Thursday, 31 July 2014

Kwani tuzo za Kikwete zina nini na wanigeria?

Habari iliyosambazwa kwa vyombo vya habari ni kwamba rais Jakaya Kikwete amepewa tuzo nyingine ya  The Icon of Democracy. Ajabu pamoja na wahusika kujisifu, ukichunguza sana unagundua kuwa nyuma ya tuzo hii kuna wanigeria. Kulikoni? Je kuna matapeli wanaomzunguka Kikwete na kusuka apewe upuuzi huu ili baadaye wahusika waje kumtoa upepo au kutafuta fursa na kuchukua kwa njia za uwekezaji uchwara kama ilivyokuwa kwenye tuzo nyingine ya kutia shaka ya The Most Impactful Leader of Africa iliyotolewa na Jarida lenye uhusiano na wanigeria? Maana tunaambiwa yupo Mwandishi wa habari ambaye pia ni pastor Elvis Ndubuisi Iruh kwenye tuzo ya sasa sawa na  African Leadership Magazine ambalo makao yake makuu ni 13 Mambilla street,Off Aso Drive, Asokoro.P. O. Box 9824 Garki – Abuja, Nigeria.

16 comments:

  1. Hivi Ulimboka mwakilishi wa wanyonge yupo wapi hivi sasa, hawa watoa zawadi wanatumia utaratibu upi. Natambua kwamba sisi waafrika tunadahraulika kirahisi kwa sababu viongozi wetu wa Afrika na matendo yetu. Na sasa mpaka taasisi pia zinafuata hadithi hizo hizo

    ReplyDelete
  2. Anon hata nami najiuliza wamewezaje kumpa hiyo "tuzo" wakati ana madudu kibao kuanzia Ulimboka, Kibanda, mauaji ya Arusha, mauaji ya polisi mara kwa mara, ufisadi, uchakachuaji kura, wizi wa EPA, uzururaji, wizi wa mali za umma, uzembe, ubabaishaji orodha ni kubwa tu.
    Kweli wanigeria wamempata kibonde wao na tutasikia mengi.

    ReplyDelete
  3. Nadhani tulie kuwa tuna rais bomu na washauri wasio na akili timamu.

    ReplyDelete
  4. Toba Toba hizo tunzo hutolewa na mafidasi kwa mafisadi
    Tujiulize kafanya nini duniani Kila kukicha kapewa tunzo?
    Tumechoka na tunzo za ufisadi

    ReplyDelete
  5. Anon 10:10 na 06:48 mmenena. Ni kweli hatupaswi kushangilia bali kuomboleza kwa jinsi rais wetu anavyochezewa na matapeli wa kinigeria. Alichofanya hadi kupewa tuzo cha mno ni kuwa bogus president who can be duped and fooled easily by con men. Cheap popularity is the calamity behind Kikwete's uselessness.

    ReplyDelete
  6. Nigeria kutoa tunzo Toba ni ya Tatu duniani kuzalisha mafuta lakini masikini hadi Leo
    Lakini sishangai kumpa tunzo kwani wana Lao wanalolitafuta
    Kwani humjui hata mkewe na Obasanjo ni Shangingi la Kigogo Dar jina lake Salma
    Tunzo kwa shemeji hiyo

    ReplyDelete
  7. Wampe na PHD basi tujue moja sijawahi kuona duniani mtu mwenye PHD Kama jakaya
    Mungu ibariki Tanzania na Watanzania

    ReplyDelete
  8. Wampe U professor
    Kwani ni vasco dagama
    Kwa kuzurura ughaibuni kusiikokuwa na tija wala fadhila kwa Tanzania

    ReplyDelete
  9. Mkapa alisema msichague rais kwa uzuri wa sura

    ReplyDelete
  10. Mambo yote London
    Kuna mtu kanunuliwa appt

    ReplyDelete
  11. Upps semeni yote jamani
    Tunataka rais safi 2015
    Na hapa ni mali pake uwazi na ukweli hakuna ulimboka

    ReplyDelete
  12. Anon hapo juu mmenena. Nadhani wahusika wamepata salamu. Kazi kwao kufanyia kazi mawazo yenu.

    ReplyDelete
  13. Katika marais JK umeundoa Hadhi ya urais
    Umeweka wasaidizi vilaza ikulu imekuwa Kama chooni
    Umekuwa mswahili ,kigeugeu
    Kama makarani Mangesani mtaa wa maminyi. Bagamoyo
    Unatukera

    ReplyDelete
  14. Ushauri wa bure
    Washauri wako wengi bomu bomb
    Shule zenyewe za kuunga kuunga
    Unategemea watakupa ushauri gani zaid ya ushirikina na umbeya

    ReplyDelete
  15. Na hizo risala unazosoma unazipitia kabla au unasoma tu
    Toba yarabi zisome kabla nyingi ni mabomu

    ReplyDelete
  16. Tuombe Mungu balaa hili limalize muda wake na kutokomea hata kuangamia, Pia tuombe na kuwa makini tusichague balaa jingine kama hili., Yana mwisho haya japo tumeishaumia.

    ReplyDelete