Tatu, wapo niliowafyatua hasa wanene wanaotamani nishuke kwenye pipa na pingu nao wanifyatue kuelekea lupango. Hafyatuliwi fyatu vinginevyo nitake. Kwanza, siishi kwa Joji Kichaka mbali na kuwa, hata nikipewa green card, nitaichana. Nani aishi kwenye kaya inayofyatuliwa na kichaa mbaguzi japo ana pwenti?
The Curse for Salvation
Wednesday, 19 February 2025
Barua kwa waliofyatuliwa na Tarampu
Tatu, wapo niliowafyatua hasa wanene wanaotamani nishuke kwenye pipa na pingu nao wanifyatue kuelekea lupango. Hafyatuliwi fyatu vinginevyo nitake. Kwanza, siishi kwa Joji Kichaka mbali na kuwa, hata nikipewa green card, nitaichana. Nani aishi kwenye kaya inayofyatuliwa na kichaa mbaguzi japo ana pwenti?
Monday, 17 February 2025
Ndoa yako imejengwa kwa nguzo ngapi?
Ndoa inaweza kuwa nzuri au mbaya. Pia, ndoa inaweza kujengwa au kubomolewa. Wajenzi na wabomozi wa ndoa ni wanandoa. Ndoa, kama taasisi yoyote ina changamoto zake. Kuna kufanya makosa kwa sababu, kama binadamu wowote, wanafanya makosa. Pia, yanapofanyika makosa lazima kuwepo na suluhu na namna ya kufikia suluhu. Leo tutaongelea ulazima na umuhimu wa wanandoa kkuwa kama daraja au uwili usiotenganishwa wala kuyumbishwa. Daraja, huwa ima na nguzo mbili ingawa kutokana na kukua kwa teknolojia, kuna madaraja yana nguzo moja. Pamoja na kuwa na nguzo moja, madaraja yote huwa na sehemu kuu mbili yaani sehemu ya kuingilia na kutokea.
Katika kufanya daraja kufaa, kuwa na nguvu, kuhimili mikiki, na kutumika, lazima nguzo mbili zisimame pamoja na kutegemeana ili kufanikisha umuhimu wa kuwapo daraja. Mfano, upande mmoja wa daraja lazima ujue na kukubaliana au kujenga mazingira wezeshi kwa upande wa pili na wa pili kadhalika kwa upande wa kwanza. Mfano, kama upande wa kuingilia utaruhusu magari au wavukaji wengi, upande wapili utashindwa na daraja litayumba au kushindwa kufanya kazi yake ya kuvusha watu na vitu.
Udaraja katika ndoa unajengwa kwa njia mbalimbali zikiwemo:
Mosi, kukubaliana. Kila kinachoingia au kutoka lazima kipitie sehemu mbili na kubebwa na nguzo mbili au nguzo moja ambayo katika ndoa ni ushirika na wawili. Hapa lazima tukazie. Tunaongelea ndoa ya mke na mume mmoja. Kwa ndoa za mitala, udaraja unawezekana japo kwa taabu. Huko hatutaenda.
Katika dhana ya kulindana, lazima wawili wawe kama nyuki au siafu wanapojilinda au kulinda mzinga au shimo lau. Ukiangalia uhohehahe na utepetevu wa wadudu tajwa, utagundua kuwa bila kushirikiana na kuhamiana, si chochote si lolote. Na wanandoa kadhalika. Mkshikamana, kulilindana, na kuhamiana, wengine watawaogopa. Mkibomoana inakuwa rahisi maadui ambao ni wengi kumalizia. Katika kulindana, lazima kuwa kulihali. Mpendane, mheshimiane, mshirikiane, mhifadhiane, na kuaminiana. Mfano, mkianza kuitana viatu na majina mengine mabaya, wengine watawaita hata makanyagio. Kila kitu mnacho na mna uwezo kubomoa au kujenga, kusuka au kunyoa. Tutatoa visa viwili vinavyotuhusu. Cha kwanza, Nkwazi alitembelea rafiki yake mmoja aishie Kanada. Siku ya kwanza kufika tu, baba alimkaribisha Nkwazi kwa shangwe. Kitu kimoja kilitibua kila kitu. Jamaa alikuwa akimfokea mkewe mbele ya mgeni kama mtoto mtoto mdogo. Hata mtoto mdogo huwezi kumfokea na kumdhalilisha hivyo. Jambo hili lilimuudhi Nkwazi kiasi cha kumwambia mwenyeji wake kuwa asingerudi katika nyumba yake. Mwenyeji alishangaa na kustuka na kuuliza “kwanini.” Nkwazi alimjibu kuwa hakupenda anavyomdhalilisha mkewe hata mbele ya mgeni kitu ambacho kwa Waswahili ni dharau hata kwa mgeni. Jamaa aliahidi kujirekebisha na mambo yakaisha.
Cha pili, kabla ya Nesaa kuja Kanada, marafiki zake Nkwazi walizoea kuuliza ana mke wa aina gani. Aliwajibu kuwa madam huwa ni mtu wa kupenda amani. Ajabu ya maajabu, marafiki zake karibu wote, walianza kumuita Nesaa Madam jina ambalo lilimkaa hadi tunahama mkoa ule tulikofikia. Hata kwenye mapokezi yake uwanja wa ndege, marafiki walionyesha wazi heshima na aina fulani ya woga kulingana na Nkwazi alivyokuwa amemjenga Nesaa ambaye kiumri alikuwa mdogo kuliko marafiki wa Nkwazi.
Mafunzo
Kwanini rafiki wa Nkwazi aliyemkaripia mkewe mbele ya mgeni aliamua kuachana na tabia hiyo? Jibu ni rahisi kuwa mwenzake alimfundisha tabia ya kumjali na kumheshimu mkewe.
Kwanini marafiki wa Nkwazi, kwa pamoja, walimuita Nesaa Madam kama ishara ya heshima? Ni kwa sababu Nkwazi alimjenga badala ya kumbomoa. Somo kubwa hapa ni kwamba mwanandoa anao uwezo wa kumjenga, kumbomoa, kumheshimisha au kumdharaulisha mwenzake.
Mwisho, kila mwanandoa anao uwezo huu. Hivyo, ili mheshimike, lazima mjiheshimu na kuheshimiana. Kufanya hivyo, lazima kuwa na tabia za haki, usawa, upendo kulindana, kuhamiana, na kutegemeana. Akitukanwa au kudharauliwa mwenzio, nawe kadhalika unatukanwa au kudharauliwa. Kadhalika, akiheshimiwa mwenzio nawe kadhalika unaheshimika. Hapa kuna faida bila hasara. Hivyo, wanandoa, wajue ni daraja lililojengwa na nguzo mbili yaani mke na mume.
Chanzo: Mwananchi Jpili jana.
Sunday, 9 February 2025
Ndoa na vibabu, vibibi vya kizungu vijana muwe macho
Tunaona bibi wa kizungu na kijana MwAfrika uwanja wa ndege–––hatuutaji–––wakibusiana. Tumeamua kuandika haya juu utumwa kimapenzi ambamo waafrika ndiyo wahanga. Utumwa huu umejikita kwenye mapenzi bandia ambapo mmoja wa ‘wapendanao’ humtumia mwenzake kulingana malengo na hadhi na rangi yake. Htuzushi. Utaona vibabu/bibi vya kizungu vikifunga ndoa na wavulana/wasichana wa kiafrika mtawalia. Bila kupoteza muda–––hapa kuna tamaa, ujinga, na umaskini–––kama vyanzo vya ukoloni na utumwa huu wa kimapenzi.
Katika mila za kiafrika, mwanaume hutegemewa kuoa mtu ima wa umri wake au anayemzidi umri japo si kwa mbali sana. Inapotokea mwanaume akaoa mwanamke sawa ua zaidi ya mama yake au binti akaolewa na kibabu sawa na babu yake, jamii hustuka, kuhuzunika, kushangaa, kuchukuia, hata kulaani. Hakuna kitu muhimu katika ndoa kama tegemeo la kuzaa watoto ambao ndiyo malipo kwa jamii na wazazi. Ndoa bila mtoto, kwa muafrika, ni janga. Tujiulize. Inakuwaje wahusika wanaweka kando hitajio hili muhimu? Kuna cha mno? Inakuwaje kijana wa kiafrika kufunga ndoa na zee lisiloweza kumzalia au kumzalisha au kumuachia ujane? Je ni tamaa, ujinga, au umaskini ukiachia mbali kuabudia rangi ambapo mweupe, hasa mzungu, anaonekana mali japo si mali kitu?
Katika ndoa hizi, kama kweli ni ndoa, wazungu hutumia waAfrika. Hatujawahi kuona MuAfrika mzee akioa msichana mzungu au kijana mzungu akioa bibi muAfrika. Kuna tatizo. Si rahisi kupata majibu sahihi bila kudurusu. Kwa akili ya kawaida, hili si jambo la kawaida, hasa kwa waswahili. Kimsingi, katika ndoa hizi, mweupe ana mamlaka na mswahili hana. Si vibaya kusema kuwa mswahili anaolewa katika mahusiano haya.
Kiafrika, mwanaume huoa na mwanamke huolewa. Ila katika uhusiano tunaojadili, mwanamke/mwanaume wa kiAfrika huolewa na mzungu ambaye humuoa bila kujali jinsia. Hata katika utumwa huu, mswahili hutegemea akiolewa na mzungu ataukata kwenda majuu na kuchuma madola. Hapa thamani ya maisha ya binadamu ambayo ni kubwa kuliko chochote, huwekwa kwenye vitu vya hovyo tokana na ujinga au umaskini kama masalia ya ukoloni wa kimila ambapo mtu mweupe ni mkombozi wa mtu mweusi ni mkombolewa–––hata kama dhana hii ni hovyo na ushahidi wa utumwa wa kiakili, kimaadili, na kimila.
Tuweni wakweli. Hivi kuna mapenzi ya kweli kati ya kizee cha miaka–––tuseme miaka 60, 70 au zaidi kuoa kijana wa miaka 30, 35 hata 40 au babu kuoa kigoli umri wa mjukuuwe? Hapa tunapata dhana ya ubaguzi wa kujitakia ambapo muathirika hujiona dhaifu mbele ya mkoloni wake bila kujali jinsia. Je kuolewa na mzungu ni kuukata au kupatikana licha ya kudhihirisha ujinga, umaskini, na tamaa ya wahusika? Tumeisha Ulaya kitambo si haba. Kuna kitu wanacho yaani ubinafsi/umimi (individualism) ambapo mtu kujiona kama huru na asiyejali wengine isipokuwa yeye. Hapa ndipo chanzo cha kwanza cha balaa hili kilipo mbali na ukoloni ambapo waafrika wameaminishwa na wakaamini–––iwe ni kwa kupitia dini au siasa–––kuwa wazungu ni wakombozi wakati ni waangamizaji. Utamuona Yesu mweupe wakati hakuwa mzungu. Mitume wote siyo waafrika. Maandiko matakatifu yote ni ya kigeni na lugha zinazotumika kuyaeneza. Huu ndiyo mzizi wa kila kitu. Waligundua, kutengeneza, na kueneza ‘weupe’ kuwa ukombozi na wengine wenye dhambi. Unashawishikaji kuwa kila mtu anazaliwa na dhambi wakati mtoto mdogo ni malaika?
Utumwa kwa waafrika ulianza tulipohujumiwa na kurubuniwa kuacha mila zetu tukakumbatia mila hatari za kigeni ziitwazo dini na ustaarabu japo si chochote wala lolote bali maafa kwetu. Mzazi unajisikiaje kijana wako wa kike/kiume anapoolewa na bi kizee kuliko hata baba au mama yake kwa kisingizio cha ‘mapenzi hayana macho.’ Mapenzi yana macho. Ndiyo maana, hayaishi bila kuwa na uhuru na utashi wa kuchagua, ambao katika balaa hili jipya haupo. Binadamu anapotumia njaa, tamaa, ujinga na umaskini kama nyenzo za kufikiri, anaweza kufanya jambo ambalo hata mnyama hawezi kufanya.
Tumalize kwa kuwashauri vijana wa kiafrika kuacha kuuza utu wao eti kwa tamaa na ujinga wa kwenda majuu. Wakishafikishwa ‘majuu’, huumizwa na kuwa watumwa zaidi wakaishia kujuta kama mmoja niliyekutana naye kwenye mji jirani aliyenyofolewa Arusha na kuishia kwenye utumwa.
Chanzo: Mwananchi leo.
Wednesday, 5 February 2025
I Cry fo Ambazonia and Darfur–––My baby
I Cry for Ambazonia and Darfur
ISBN 9789956554935
Pages 150
Dimensions 203x127 mm
Published 2025
Publisher Langaa RPCIG, Cameroon
Format Paperback
ISBN | 9789956554935 |
Pages | 150 |
Dimensions | 203x127 mm |
Published | 2025 |
Publisher | Langaa RPCIG, Cameroon |
Format | Paperback |
I CRY FOR AMBAZONIA AND DARFUR
by Nkwazi Nkuzi Mhango
The world remains tragically silent on the suffering of the people in Ambazonia, Cameroon, and Darfur, Sudan. Since these conflicts began, the international community has failed to adequately address or arrest the violence and protect innocent lives. Countless people have been killed, displaced, and robbed of their hope. This book serves as both a condemnation and a plea to the international community, urging it to acknowledge its failures in these regions. Nkwazi Mhango argues that this inaction constitutes a form of discrimination against the people of Ambazonia and Darfur, highlighting the stark contrast between the global rhetoric on human rights and the grim reality faced by the victims. “The Cry for Ambazonia and Darfur” is a powerful call for humanity to awaken to its responsibilities. It demands more than just empty gestures; it urges critical self-reflection and a genuine commitment to resolving these conflicts. Mhango implores us to recognize our shared humanity and act with the compassion and justice we would expect for ourselves.
ABOUT THE AUTHOR
Mhango is the author of Saa ya Ukombozi, Nyuma ya Pazia, Souls on Sale, Born with Voice, Africa Reunite or Perish, Psalm of the Oppressed, Perpetual Search, Africa’s Best and Worst President: How Neocolonialism and Imperialism Maintained Venal Rules in Africa and ‘Is It Global War on Terrorism’ or Global War over Terra Africana?: The Ruse Imperial Powers Use to Occupy Africa Militarily for Economic Gains, How Africa Developed Europe: Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth and What Ought to Be Done and Known, Africa’s Dependency Syndrome: Can Africa Still Turn Things around for the Better?, Our Heritage, Family Friend of Animal and Matembezi Mbugani (Children’s book co-authored with his wife Nesaa).
Woga, ukale, kujifyatulisha na kufyatuliwa
Sambamba na Kenya, siku chache kabla ya kutolewa taarifa hii, sirkal iliangaza mikakati ya kupata njuluku za diaspora wetu bila kustahiki wala kujenga mazingira mazuri. Kwani, inakataa uraia pacha huku ikishobokea wawekezaji ambao wengi ni wachukuaji tu. Jikumbushe tulivyofyatuliwa na matapeli toka India waliojifanya kuwekeza kwenye Shirika la Reli wakaishia kutufyatua njuluku hata mabehewa. Kabla ya hapo, walikuja ABSA wakafyatua banki yetu ya Biashara na kusepa. Walifuatia BAE Systems, Barriki dhahabu, CHAVDA, EPA, ESCREW, IpTelo, Mabilioni ya Njaa Kaya, Meremetuka, na nyingine nyingi ambapo tulipigwa njuluku ndefu tu. Kama haitoshi, jikumbushe Richmonduli-Dowan, Kagoda, mwanakaya gold na mazabe mengine yaliyofyatua na kufilisi kaya yetu. Tatizo ni nini?
Wakati wachukuaji wanakuja kufyatua njuluku iliyokwisha tengenezwa, tunakosa njuluku wanayotengeneza wanadiaspora wetu! Akili au matope? Tunazidiwa na vijiinchi kama Gambia chenye watu milioni 2.4 na ukubwa wa 11, 300 km2 kinachozidiwa na mkoa mdogo kama Kilimanjaro wenye ukuwa wa13,250 km2 kilichoingiza dolari 775.6 ikilinganishwa na Bongolalaland iliyoingiza dolari 570 huku uwekezaji ukiwa wa thamani ya dolari milioni 931.60. Fedha ya diaspora haina masharti na shaka kama uwekezaji uliogeuka upigaji.
Tunahitaji uongozi unaojiamini, wenye ubunifu, wa kisasa, na usiotaka kuvuna usipopanda kama ilivyo. Unataka wabongo wa diaspora watume njuluku wakati huwatambui wala kuwamotisha? Inaingia akilini kweli? Hata unapotaka kuwafyatua kuwapa hadhi maalumu, unawazingua na kuvuta miguu. Ajabu, uraia huu huu unaoonekana mali wakati si mali kitu wanajizolea hata wacheza kandanda! Tunamkomoa na kumfyatua nani? Wawekezaji wanakuja na kujizolea njuluku kwenye shamba la bibi hadi mapipa yetu yanakamatwa ughaibuni na kushitakiwa na kufyatuliwa mamilioni ya dolari. Rejea mamilioni ambayo yeshalipwa au yatalipwa tokana na uzwazwa na woga wa kimfumo.
Mfano, mnataka wanadiaspora walete njuluku home wakati hawana haki za kumilki mali? Mnawapa hadhi maalumu. Nani aliwapa mamlaka haya wakati Sir God aliwaumbia Bongo? Tunamkomoa na kumfyatua nani zaidi ya kujikwamisha, kujikomoa na kujifyatulisha? Ukiangalia sababu kubwa ya kuogopa uraia pacha si nyingine zaidi ya woga wa siasa za majitaka. Kwani, hizo kaya zilizotoa uraia pacha zimepungukiwa nini? Je mafisi na mafisadi wote ni wana uraia pacha?
Rafiki yangu Prof Mutua, mwenye uraia wa Kenya na Marekani aliwahi kugombea ujaji mkuu akanyimwa tokana na kuwa mwanafunzi wa jaji mkuu aliyekuwa anamaliza muda wake. Hapakuwa na tatizo na uraia. Ukiachia huyo, Baba wa taifa la Senegal Leopord Sedar Senghor alikuwa na uraia pacha na bado alikuwa rais aliyeleta uhuru na kufanya mambo makubwa kwa Afrika. Inakuwaje sirkal yenye kuogopa na kukataa uraia pacha inaendeshwa na njuluku toka majuu mbali na chaguzi zake kugharimiwa na fedha hiyohiyo? Kunani hapa? Tuambiane ukweli bila kuogopana.
Kuna kipindi nilimsikia fyatu mmoja mnene mwoga na zwazwa akisema eti tukiruhusu uraia pacha, wageni watachukua ardhi yetu. Ajabu. Mbona wageni wengi walikwishakujitwalia ardhi? Hiyo ardhi tunaifanyia nini zaidi ya kuitelekeza tukitegemea kuagiza majanki toka nje? Nani anaweza kuamini kuwa kaya yenye uwezo wa kuzalisha mchele hata kulisha eneo zima la Afrika Mashariki ingeagiza mchele wenye thamani ya dolari milioni 27.49 toka Thailand mwaka 2023? Yaani tunalishwa na nchi yenye ukubwa takriban nusu yetu wa 513,120 km2 na idadi ya watu 64,785,90? Tukifyatuka na kusema tumerogwa, mtasema tunatukana kweli?
Miaka michache iliyopita, bi mkubwa wangu alikwenda uhamiaji kutafuta passports yake na za wanetu wakati akijiandaa kuja huku. Aliulizwa maswali ya kipuuzi mfano, unakwenda kule kufanya nini? Unamuulizaje fyatu mzima tena mjanja anakwenda majuu kufanya nini? Wewe inakuhusu nini? Mbona mnapotaka tulete njuluku home hamuulizi kaipataje?
Juzi nilikuwa napitia tovuti ya sirkal inayosuasua juu ya vibali vya kusafiria nje. Hapa Kanada hakuna kitu kama hicho. Kwanini kumsumbua mtu akwambie anakwenda kufanya nini ughaibuni utadhani taahira? Wapo wanaosema eti wanafanya hivyo kuepuka mafyatu kwenda kufanya uhalifu huko. Kwani hakuna sheria? Je hawa wanaopewa hawafanyi uhalifu hasa uuzaji bwimbwi? Kama fyatu anataka kwenda ughaibuni, mpe pasi asepe. Mengine atajijua. Kwanza, hata balozi zetu ughaibuni hazina mpango wala utaratibu wa kuwasaidia wabongo walioko nje vinginevyo iwe ni kwenye kuunga juhudi na mambo mengine ya kisiasa za majitaka.
Tufikie mahali tukue na kukomaa na kuacha uzamani na woga. Vinatuchelewesha na kutufyatua na kutufyatulisha. Hivi samaki ana miguu mingapi?
Sunday, 2 February 2025
Mpumbavu aliyevunja ndoa akiamini anaihami
Baada ya kuishi na mumewe kwa mwaka mmoja na kulazimisha kubeba mimba bila ya makubaliano, jambo ambalo lililomstua muwe, Gilo aliamini mumewe bwege asiyeweza kustuka wala kushuku. Hivyo, mazabe yake yasingefumka. Taratibu, mambo yalianza kutifuka na kufumka. Mumewe alianza kumshuku kwa kila jambo. Mfano, kuna wanaume waliokuwa wakiwatembelea aliowatambulisha kama ndugu zake. Bahati mbaya, mmojawapo alikuwa akifahamika kwa rafiki wa mumewe waliyekutana JKT. Siku moja, Gilo akiwa ametembelewa na huyu ndugu yake ambaye pia alikuwa mshikaji wake jeshini, alifika rafiki wa mumewe aliyewajua wawili hawa.
Mume aliporejea na kuwakuta wageni hawa, alimtambulisha ndugu mshikaji wa mkewe kama shemeji yake aliyekuwa amempa mtaji kuanzisha biashara. Rafiki yake alishangaa na kuchukia tokana na aliyojua. Hivyo, alishindwa kuvumilia. Wakati wakiagana, alimuomba rafiki yake awe na kifua amwambie jambo. Jamaa alipasua mbarika na kuweka kila kitu wazi. Baada ya kupita miezi kadhaa, jamaa mshikaji wa Gilo alirejea akitaka fedha zaidi toka kwa mumewe ambaye alimkatalia zamu hii. Baada ya mwizi wake kuondoka, alimbana mkewe aliyekiri kuwa na udugu na uhusiano wa kingono. Tangu siku hiyo, mapenzi yalitoweka.
Kuona kitumbua kinaingia mchanga, Gilo alianza harakati za kuhami ndoa yake. Alikwenda kwa wachungaji kuomba ushauri na kuombewa. Mambo yalizidi kuwa mabaya. Mwishowe, aliamua kwenda kwa mganga wa kienyeji aliyemwambia kuwa alikuwa na nuksi na alikuwa amerogwa via vya uzazi na shangazi yake. Hivyo, alipaswa kutumia dawa kuingiza ukeni ili kutibu nuksi. Sharti kubwa alilopewa ni kutafuta mwanaume ambaye si mumewe ajipake dawa na kumuingilia mara moja tu. Kwa kutapatapa na upumbavu, Gilo alikubaliana na sharti. Tatizo, ni nani angempata ajipake hiyo ‘dawa?’
Jibu lilikuwa rahisi. Alimwambia mganga wa kienyeji kuwa hana mtu. Mganga alimwambia kuwa kama angempa fedha, angefanya kazi hiyo. Walikubaliana na Gilo wakajifungia ndani wakafanya ngono. Baada ya kumaliza, mganga wa kienyeji aliongeza sharti jingine kuwa lazima wafanye ngono kwa wiki nzima kila jioni. Gilo alistuka lakini alikuwa ameishaingia mkenge. Alikataa katakata. Mganga kuona hivyo, aliamua kumtishia angemwambia mumewe. Gilo ilibidi akubali. Wakaendelea kufanya mapenzi. Kabla ya wiki kupita, mume alistuka na kuamua kumfuata mkewe pindipo alipoaga jioni anakwenda kwenye maombi. Kimyakimya alimfuata hadi akiingia nyumba ya kulala wageni na mganga. Alifanya harakaharaka akawafuma na kumuacha hapohapo bila hata kurusha ngumi wala tusi.
Katika kushuhudia na baadaye kudurusu sababu za kuvunjika kwa ndoa hii, tuligundua vitu kadhaa. Mosi, ndoa hailazimishwi. Pili, maisha ya kabla ya ndoa yanaaweza kuimarisha, kuyumbisha hata kuvunja ndoa. Tatu, kutokujiamini, ubabaishaji, kutafuta ushauri bila kufikiri na kutahadhari, na kuamini kila ushauri vinaweza kuvunja ndoa. Nne, kutafuta tatizo kwa kutapatapa ni hatari kwa ndoa. Wanadoa wanapaswa kuendana. Kwani, wawili hawa hwakuendana kwa sura na tabia. Japo hili si tatizo, licha ya kulazimisha ndoa, Gilo aligeuka ‘chuma ulete.’ Kwanza, baada ya kuhamia kwa kulazimisha ndoa, Gilo aliwasomba ndugu zake ukiachia kukmtoa fedha mumewe ili kuwatumia wazazi wake kwao. Pili, Gilo, licha ya kumficha mumewe ukweli kuhusiana na maisha yake yaliyosababisha alazimishe ndoa kwa, hakuwa muwazi juu ya maisha yake ya awali.
Je unajifunza nini hapa? Mosi, ndoa inataka uaminifu na ukweli. Pili, siyo kila ushauri unafaa. Tatu, ndoa haina daktari wala mchungaji isipokuwa wanandoa wenyewe. Nne, hakuna siri ya milele. Tano, usiamini kila mtu na kila kitu. Sita, ndoa inataka kujiamini. Saba, waganga wa kienyeji na wachungaji matapeli ni maadui wakubwa wa ndoa. Nane, katika ndoa, wanawake wana maadui wengi kuliko wanaume. Tisa, mchawi au mlinzi wa ndoa yako ni wewe mwenyewe. Kumi, unapopta tatizo, tumia njia sahihi ukiwa umetulia kufikiri na kufanya utatifiti ukiepuka kufanya maamuzi kwa msongo wa mawazo na hofu.
Saturday, 25 January 2025
KATIKA NDOA, USIHUKUMU KABLA YA KUJIHUKUMU
Siku moja alidamka, kama kawaida yake akijiandaa kwenda kwenye kituo cha daladala ili aende zake mjini kuchakalika. Kwa bahati mbaya, siku ile hakuwa hata na nauli. Hivyo, alimuomba mkewe nauli. Badala ya mama kumpa nauli, alimjibu “mwanamme mzima unaomba nauli kwa mkeo! Mwanaume gani suruali.” Kwa busara na upendo, yule bwana hakukasirika wala kujibu zaidi ya kuumia ndani na kufunika kombe mwanaharamu apite.
Kwa vile tabia ile ilituudhi, tulimwita jamaa kando na kumpa nauli bila hata kumpa pole kwa kuhofia tungeamsha uchungu hata kumwaga mafuta kwenye moto. Pamoja na kumhifadhi ndugu yetu huyu, kile kitendo kilituudhi na kutufedhehesha. Cha mno, kile kitendo kilitupa somo kuwa, katika ndoa, kuna wanandoa wengine wanabomoa ndoa zao kwa mikono yao.
Hapa kuna mambo kadhaa ya kujifunza.
Pili, kuna haja ya kuvumiliana hasa wanandoa wanapopata mitihani ya kimaisha ambayo ni mambo ya kawaida yanayoweza kuwajenga au kuwabomoa.
Tatu, kupata si ujanja na kukosa siyo uzembe au ujinga. Kwanin watu wa namna hii hawahoji ni kwanini watu wengine wanaishi kwa muda mrefu wakati wengine wanaishi kwa muda mfupi?
Nne, upendo baina ya wanandoa unapaswa kuvuka vitu vidogo kama vile kipato, elimu, na mengine kama haya. Kwani, kila mmoja anaweza kuwa nayo au asiwe nayo.
Ukiunganisha kisa cha ‘mume suruali’ na cha ‘wewe hukusoma’ unagundua mambo mengi ambayo ni hatarishi na sumu katika ndoa. Mfano, mwanandoa aliyemwambia mwenzie ni mume suruali, naye alikuwa katokea kwenye familia maskini. Je kwanini hakujiuliza kuwa hata baba yake alikuwa mume suruali na hata mama yake mke gauni?
Kama mmejaliwa au mmoja wenu kajaliwa talanta fulani, zitumieni kwa upendo na usawa bila kudhalilishana, kunyanyasana, kutukanana, na kuvunjiana heshima. Leo, unaweza kumuona mwenzio hafai wakati nawe hufai na kesho mkaachana ukajikuta umemkimbia mjuzi na kumkumbatia mamba. Hivyo, kabla ya kuhukumu au kutuhumu, fanya hivyo kwako mwenyewe kwanza. Hiyo ndiyo busara ya leo.
Wednesday, 15 January 2025
Hamisheni mafisi, mafisadi au waanimo na si akina Yero
Nizame kwenye sekeseke na sheshe la akina Yero wa kule Nrongonrongo. Kwanza, mpaka sasa, hatujupewa sababu kuntu za kuwahamisha. Je hii ndiyo njia pekee iliyopo? Je tumechemsha bongo na kushindwa au kuishiwa majibu? Je tumejaribu njia nyingine zikashindikana na kwanini? Je kuna namna?
Turejee kwa akina Yero. Yaani unamtoa morani mbugani na kumpeleka pwani! Huku siyo kumdhalilisha na kutaka kumnyotoa roho taratibu mbali na kuua na kuzima utamanduni na mila zake? Mayero huwa hawali samaki kwa sababu hawawatofautishi na nyoka. Leo, mwawapeleka kwa akina waja leo waondoka leo ili iweje? Kwanini hamkuwapeleka Manyara lau wawe karibu na mazingira yao badala ya huko mlikowatupa ili waangamie taratibu? Mnafanya hivi kwa faida ya nani?
Kama imeshindikana basi waombe majirani zetu wa Kenya wawapokee huko Kajiado na Oloitokot ambako, kama siyo wakoloni kuligawa bara la Afrika, ndiko ilipo nchi yao ya asili? Akina Yeor siyo kama akina shakaza wanaoweza kushamiri mahali popote tena bila kula cha mtu maana wao ni kama mbegha. Huwa hawali cha mtu na ndima zose wanagoshoa bila kinyongo wala mbwai. Tate nane tate nane. Naanza kulikoroga! Anyways, nini kifanyike? Simpo. Hamisheni waanimo. Sababu zifuatazo zinaniaminsha wanene watakubaliana nami kutowahamisha akina Yero kupisha wachukuaji:
Kwanza, ni mafyatu si wanyama na wanyama si mafyatu wala hawana hata uhusiano.
Pili, ni wanakaya. Waanimo hawana uraia wowote. Leo, wako bongo. Kesho wako Kenya. Hawana fungamano wala uwezo wa kujua au kuamua wapi wasimamie. Wao wanafuata mlo.
Tatu, ni wamiliki wa waanimo ambao lisrikal liliwakuta nao likawanyang’anya na kuwawekea masharti namna ya kuishi nao badala ya kujifunza toka kwao. Sasa, limenogewa. Linataka kuwang’oa kabisa tena si kwa faida yake bali wachukuaji waliopewa jina zuri la wawekezaji.
Nne, wanalipa kodi japo waanimo nao wanaingiza madolari mengi tu. Hata hivyo, waanimo hawanunui wala kuuza. Hivyo, mchango wao ni mdogo ikilinganishwa na wahyuman.
Tano, hawana udugu na waanimo japo wana uhusiano wa mamilioni ya miaka wakiishi pamoja kwa amani na furaha.
Sita, walipigania uhuru na kukataa ukoloni wakati waanimo hawawezi kutofautisha kitu.
Kumi, tuage kiYero, Olesere Yero.
Uhuru na usiri ni siri za mafanikio ya ndoa
Binadamu tumeumbwa na kujipenda na kujipendelea kuliko wengine hata kama kufanya hivyo kunaweza kuwaudhi au kuwaumiza wengine. Hivyo, unapaswa kujua kuwa mafanikio yako ni yako siyo ya kuwasimulia wenzako. Kitanda usicholalia, hupaswi kujua kunguni wake. Kama ilivyo kwenye siri ya mtungi, muachie kata pekee ajue siri za mtungi. Unawambia wenzio habari na siri za mwenzi wako ili iweje? Unategemea nini? Je wakikuumiza utamlaumu mwenzio au mwenyewe? Japo mfano wa hapo juu mwenzi wa mmbea aliyewapa siri za mwenzi wake ana makosa, na mumewe pia ana makosa. Ukilinganisha makosa ya wawili, utagundua kuwa mama ana makosa makubwa kuliko mumewe ingawa wote wana makosa.
Japo kuna kipindi mambo huzidi kiasi cha waliotanzwa kutafuta msaada. Katika ndoa, linapotokea tatizo, ni muhimu likashughulikiwa na wahusika peke yao tena kwa usiri. Ndiyo mana tunasema siri za ndani ziishie chumbani. Zisivushwe hata kuchungulia sebuleni. Kama ikizidi sana, basi wahusishe wazazi wenuwa pande zote. Wao, wana uzoefu na uchungu na ndoa na mafanikio yenu kama wazazi. Na hata mkiwahusisha, mpime michango na ushauri wao. Maana, wao hawajui thamani na umuhimu wa ndoa yenu kama nyinyi wenyewe. Ajuaye thamani ya mkonga ni tembo aliyeubeba. Na ndoa ni mkonga wenu. Wengine wanaweza kuukata wakauuza mkauawa au kuumia.
Wakati mkikumbana na mitihani katika ndoa na kutaka msaada au ushauri, mnapaswa kujua kuwa hao mnaowafuata nao wana changamoto, kasoro, na matatizo yao. Kama ikizidi sana, turudie na kusisitiza wahusisheni wazazi wa pande mbili japo nalo hili linataka utafiti na umakini vya hali ya juu. Hata hivyo, kuna angalizo. Kuna baadhi yetu wamezaliwa kwenye ndoa za mitala au zilizoharibika. Hivyo, unapowahusisha wazazi, pia uzingatie ithibati, ubora, au udhaifu wa ndoa yao mbali na uwezo wao wa kujadili matatizo na kuyatafutia suluhu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa ndoa yako ni yako na si yao kama ambavyo ndoa yao si yako bali yao. Mnapozoea kuwapelekea watu matatizo yenu, mnayazidisha na kuyafanya yawe magumu zaidi kuliko mkiyashughulikia wenyewe. Hii ni kutokana na namna mnavyoyaeleza kwao na namna wanavyoyaelewa au hata kutoyaelewa.
Hivyo, ndoa inapaswa kuwa taasisi huru ambapo uhuru huu ulindwa kwa wivu na tahadhari kubwa. Tunaposema uhuru, tunamaanisha uhuru wa kutoingiliwa na yeyote. Hakuna apaswaye kuwa na uwezo wa kuamua lolote kwenye ndoa isipokuwa wanandoa wenyewe. Tutoe mfano. Mwanandoa mmoja mzembe na hatari kwa ndoa yake alizoea kuwapa marafiki zake siri za mwenzi wake. Moja ya siri alizotoa ilikuwa ni ukubwa wa maumbile yake na namna alivyojua shughuli. Katika hao marafiki, walikuwamo wakware waliokuwa wakimmezea mate mwenzi wake. Hivyo, kutotunza na kulinda siri za ndoa yake kuligeuka angamizi la ndoa yenyewe hasa wahusika walipokula njama kumuandamana mhusika na wakampata kirahisi.
Wednesday, 8 January 2025
Mliomba, mnaomba, mtaomba mjue si jibu
Kamchezo/kagonjwa kengine ni kuamini aukutemea miujiza feki na uchwara. Juzi nilisikia fyatu aliyekuwa amekwama kituo cha ngwarangwara kule Kawee akisema eti alitoka mikoani kwenda kwa mchunaji, sorry, mchungaji, habithi, sorry, nabii Dar aombewe amalize mgogoro wa kiwanja! Hii ni akili au utaahira?
Tokana na kuazoeleka kamchezo ka kuombaomba na kuamini miujiza feki na uchwara, kuna wanjanja wachache wanaotaka kuwa karibu na wanene wa kisiasa ili wawafyatue mafyatu wanaokuja na gea ya kuombea kaya. Mfano, wanaomba mvua wakati wanaharibu mazingira wasijue suluhu ni kutunza mazingira.
Majizi manene yanafyatua njuluku ndefu. Yakifa tunaomba yaingie peponi. Mengine yanapiga soga makazini badala ya kuchapa kazi. kuna uzururaji na matumizi mabaya ya raslimali za kaya yanayofanywa na baadhi ya mafyatu wapaswao kuwafyatua wasifyatuliwe. Halafu eti mnategemea kaya itajirike. Vipi?
Waliobukua historia wanajua. Walipokuja watasha na vitabu vyao vya kuomba, walituambia tufumbe macho tuombe. Tulipoyafumbua, tulijikuta wametufyatua kwa kutupa vitabu wakafyatua ardhi na mali zetu. Hawa wanaotufundisha kuomba kwa kila kitu, kwao hawaombi. Walituletea ukoloni na utumwa hivi hivi tokana na ujinga na uzwazwa wetu. Mnadhani akina Mkwawa, Mirambo, Nyungu ya Mawe, na Mchonga wangeomba, mngekuwa huru leo?
Hata kama kuomba kunalipa, si kwa wale wanaoombewa bali wanawaombea. Hamjaona biashara ya neno na miujiza vilivyogeuka dili? Badala ya kujihangaisha na kuchapa kazi, waombaji wanawaibia mazwazwa waliokata tamaa wanaoamini miujiza uchwara. Japo wanaiba kihalali, wizi ni wizi tatizo ni kuufumbia macho na kuubariki tokana na ugonjwa wa kuomba na ushirikina.
Kwa waliosoma historia na kuielewa wanajua namna wamisionari walifyotufyatua. Walitwambia tutubu dhambi halafu wakajua udhaifu wetu na kuwapa taarifa mataifa ya kikoloni yaliyowatuma ikawa rahisi kututawala. Mbali na hili, ukiangalia namna makanisa hasa ya Kirumi yalivyo na ardhi chekwa, unagundua kuwa hakuna kitu walifanya kama kunyakua ardhi.
Tumalizie. Mliomba, mnaomba, mtaomba ila mjue mnakwepa tatizo kwa kutafuta suluhu ya tatizo lisolokuwapo. Mtaomba hata uchi. Matatizo yenu yatabaki palepale na sanasana yataongezeka. Kwa wanaoipenda kaya na wenye kutaka kuisaidia, waiambie ukweli badala ya kupoteza muda na kuomba. Hakuna kaya iliyowahi kujengwa kwa maombi.
Chanzo: Mwananchi leo J'tano.
Tuesday, 7 January 2025
Udhaifu katika ndoa ni sehemu ya ndoa
Kwanza, kila binadamu ana ubora na udhaifu hata awe mzuri au mbaya kiasi gani. Hivyo, wanandoa wanaposhughulikia ubora au udhaifu wao, wanapaswa kukumbuka kuwa wote ni binadamu wenye mapungufu. Unaweza kuwa msomi mkubwa tu, tajiri, mwelewa si kawaida, mkarimu hata katili vipi, bado una ubora na udhaifu wako. Hivyo, tukubali na tujue haya yanatuhusu wote. Hivyo, kuwa au kuonyesha udhaifu katika ndoa, sawa na maisha, ni jambo la kawaida. Kisicho cha kawaida ni namna ya kuukubali, kuurekebisha, au kuupunguza udhaifu huku wahusika wakijitahidi kuujua, kuutumia ubora wao huku wakijitahidi wawezavyo, kuishi na madhaifu yao.
Kila mnapoongea au kusemezana, mwishoni, ulizaneni kama mmesikilizana na kuelewana. Maana, kuna kusikiliza ilimradi kumridhisha mwenzako wakati ukweli ni kwamba unajua unafanya hivyo kumlidhisha wala si kumsikiliza. Kuna kusikiliza bila kuelewa ukutoa michango isiyotegemewa wala kuleta maana. Hivyo, hatua ya kwanza ni kuujua udhaifu. Hatua ya pili ni kuukubali na kuutafutia suluhu. Hatua ya tatu ni kufanya mazoezi ya kutatua tatizo. Na mwisho, ni kutathmiana kwa kuulizana na kutathminiana pasina kuridhishana au kudanganyana.
Baada ya kuomba maelezo, mhusika awe tayari kusikiliza maelezo, utetezi, au welewa wa mwenzake. Mruhusu aseme bila kuingilia ili apate fursa ya kujieleza eleweke nawe umewelewe. Kama bado kuna kutoelewa/kueleweka au hofu ya kutoeleweka, si vibaya kuuliza upya ili kupata maelezo ya kina ili muweze kuelewa tatizo na kulisuluhusha. Hapa, kuna ubora au udhaifu kimawasiliano. Katika maisha, mawasiliano ni muhimu na hayaepukiki. Si kila mawasiliano ni mawasiliano. Hapa, tunamaanisha mawasiliano chanya si hasi. Mfano, mkisikilizana, kuheshimiana, hata kudharauliana, mnakuwa mnawasiliana ingawa matokeo yake yanaweza kukinzana hata kutofautiana.