Wednesday, 21 June 2017

Hivi bado Eliakim Maswi ni Mwanaume au Mwanamke kwa sasa?


THE BOTTOM LINE : In voting, fear the politics of the tummy like leprosy

A Kenyan man casts his ballot in a past

        For high-pitched Kenyans, the time to mint and print dosh’s arrived.  Do you want quick dosh? Become an opinion pollster. Thereafter, just analyse and say things with full sangfroid even if you truly know are abracadabra and quackery. It’s super easy. Use tribal science to interview tribesmen and women instead of citizenry. Add a tribal mind; and draw a tribal conclusion in predicting the tribal lord that’ll carry the day in the coming elections.
            The other day I read Gitau Warigi’s piece on how to make dosh in Kenya through forming briefcase political outfits, churches not winning a government tender. Provided that the eating season aka electioneering is close, smart nibblers are now prepared with their knives set to chop and chomp the meat UhuRuto once said it’s devouring while the challengers were drooling.
            Apart from becoming a pollster, there’s another cool way of making a killing at this point and time. Just become a political analyst answering to intimidating titles such as professor muta wa Ngumi even if you’re not but a quack sort of. To nicely mug political jobseekers, just plagiarise some terms such as the tyranny of small decisions which make people forget important things so as to latch on small and an important things. After doing so, you come to the nambers game of making your targets believe. When the tyranny of numbers was propounded to the country of Nyayo, I wondered to hear some enlightened people saying it’s somebody’s invention while it's been in academic circles even before the cheap theorist purporting to coin the words wasn’t even conceived. Even gurus such as Angello, Howard Bowen, Mackintosh and Green and others who used this term in the sixties have never claimed to formulate it.
            In applying the bootleg tyranny of nibblers, ignore all other crimes such as the sabotage of Biometric Voter Registration (BVR) Kits despite sinking taxpayers’  billions of shillings to put in place. Instead of reporting results digitally, you just propose that the IEBC goes back to pre-Adamic era by manually counting the ballots. Why use computers while they don’t lie? Once again, here you can apply the doctrine of tyranny of choice in which Fredrick Schauer argues that there must be a distinction between  rules and standards. Electoral rules must be applies to see to it that the elections and their results meet standards of free, fair, credible and meaningful elections. There should not be any hanky panky or horse trading this time around.
            I don’t want repeat the same bunkum that saw Kenya go up to smokes in 2007. However, this time , there won’t be any room for the tyranny of the numbers. Instead, I’d say; voters who are, in a sense, consumers will, as Fasolo, McClelland and Todd would put it “neglect most product information and yet make good choices, so long as either there is no conflict among the product attributes or the attributes are unequally important.” If Kenyans choose issues in lieu of personalities fighting for eating free, there won’t be any conflict. Shall they cascade to the habits of the past, conflict will surface in that, instead of standing for the interests of their nation, many’ll defend the interests of their tribes. Hence, it is upon voters to choose between the nation and the tribe.
            However, one choice is safe and progressive for Kenya, a nation. Under it, all Kenyans are united as opposed to tribe under which they're sharply divided.
            Voters need to heed this. Of all chicaneries, fear the politics of the tummy like leprosy. For, it is through this sort of politics, corrupt and venal politicians bribe voters with nonsenses such as drinks, meals,  Khangas, small amount of money, T-shirts and whatnots. Instead of buying into this fake generosity, take their stuff and ask them what they’re buying and how they made their dosh. Voter oh voter, it’ll be great.
            By the look of things, personalities seem to outweigh issues. Here’s where the Francis Nyenze thing comes in. many’ll like to see one of theirs been anointed and become a tenant in ikulu. Eish!  What’ll the hoi polloi get by pushing one of theirs to the throne. Do they know that unga and madondo don’t know their alliances,ethnies, parties and horse trading? The lack of sanitation, clean and safe water,  reliable power and dosh in pockets don’t have brains, eyes or tribes.
Voters, these are dangerous times. Beware. What  a lying season that is!
Source: Citizen Wednesday today.

Natamani Tanzania ingekuwa Korea ya Kusini

Image result for photos of park geun-hye in handcuffs
            Hivi karibuni, nchi ya Korea ya Kusini iliingia kwenye historia ya dunia kwa kuwa miongoni mwa nchi zinazopambana na ufisadi mkubwa bila huruma kuonea. Rais wa zamani wa nchi hiyo Park Guen-hye alijikuta akiondolewa madarakani na kusindikizwa gerezani anakongojea kusikilizwa shauri lake la kuruhusu rafiki yake Choi Soon-sil kutumia ofisi ya rais kujitajirisha kinyume cha sheria. Choi ambaye naye yumo gerezani akingojea kusikilizwa kesi yake, alitumia ukaribu wake na rais kuyasumbua makampuni mengi ya kibiashara kuchangia asasi yake isiyo ya kiserikali ambapo kipindi kimoja, alilazimisha kampuni ya Samsung kuchangia dola za kimarekani 69. Wakati akiingizwa gerezani hapo tarehe 31 Machi, 2017 bango moja lilimpokea likisema “hongera kwa kuingia gerezani. Toka ukiwa binadamu baada ya miaka 30.”
Park angekuwa rais wa kiafrika, nani angemgusa.  Asingeondoshwa madarakani kwa aibu na kuishia korokoroni. Angetafutiwa mazingira ya kumlinda hata baada ya kuthibitika kuwa alitenda ufisadi. Lakini kwa wenzetu hilo hakuna. Hakuna aliyeko juu ya sheria; wala anayeruhusiwa kutumia ofisi yake kwa manufaa binafsi kama ilivyo kwa Afrika ambako marafiki, watoto, wake au waume na ndugu wa viongozi nao hujipachika uongozi kwa sababu wazazi au ndugu zao ni marais.
Hakuna ubishi. Kwa sasa, Tanzania inakumbwa na kashfa kubwa tu zinaohusisha hasara za mabilioni zilizosababishwa na baadhi ya watawala wetu na wasaidizi wao ima tokana na uroho, ujinga na ufisadi au roho mbaya kama siyo ulimbukeni. Kashfa hizi si mpya. Kinanchofanyika ni baada ya rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli kuingia madarakani na kufanya ambacho karibia watangulizi wake wote walishindwa kufanya–kuanza kufukua kila aina ya uoza–na kuchukua hatua hata kama si kwa wahusika wote. Zoezi la Magufuli la kupambana na ufisadi nchini limevutia wengi ingawa pia linakosolewa na wengi kutokana na kuhangaika na vidagaa huku mapapa wakisazwa. Wanaomuunga mkono Magufuli wanaona kuwa amethubutu. Wanaopinga harakati zake japo si wengi, wanaona kama hafanyi mambo kisayansi na hayawezi kuwa endelevu hasa kutokana na mfumo wa kikatiba wa kutekeleza haya ukiachia mbali mapungufu kama upendeleo wa baadhi ya watu wa karibu wake kama ilivyotokea kwa mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda anayetuhumiwa kughushi vyeti vya kitaaluma.
Mbali na Makonda, juzi baadhi ya wabunge wa upinzani waliposhinikiza kuwa marais wastaafu walioshiriki uoza na uovu huu washughulikiwe. Vyombo vya habari vilimkariri mbunge Kilombero (Chadema) Peter Lijualikali akisema “Haiwezekani mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe ili wahojiwe.” Baada ya Lijualikali kutoa pendekezo la kuondoa kinga kwa marais, spika wa Bunge Job Ndugai alisikika akiwaonya kwa kusema “Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena” akimaanisha mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye waliohamia kwenye kambi ya upinzani. Hapa unaweza kuona namna kulindana kulivyo tatizo la kimfumo zaidi. Badala ya spika kutumia mamlaka yake kuunga mkono haki ya kutenda haki, anaonekana kutoa vitisho kama ishara ya kuonyesha kuwa wapo wasioguswa. Hata hivyo, spika alisahau kitu kimoja kuwa hao mawaziri anaotishia nao watasombwa hawana kinga kama marais wastaafu ambao kimsingi ndicho chanzo cha ufisadi, uovu na uoza huu uliofanya taifa lenye kujaliwa raslimali lukuki kuwa maskini na ombaomba bila sababu zaidi ya ubinafsi, uchoyo, uroho na roho mbaya za baadhi ya watawala wetu waliogeuza ikulu kuwa chimbo la utajiri badala ya kuwa hekalu la haki la wananchi. Ingekuwa Korea ya Kusini, kauli ya spika ingemgharimu. Kwani, ameonyesha wazi kuunga mkono ufisadi.
Naye mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu wala hakuficha wala kuzungusha. Alitaka rais Jakaya Kikwete ashitakiwe kwa vile ndiye aliingia mkataba wa mgodi wa Bulyankhulu tarehe 5 Agosti, 1994. Na wakati ule hakuwa na kinga yoyote kisheria. Je rais atawashughulikia watagulizi wake na nani yuko tayari kumvisha paka kengele zaidi ya yeye aliyeanzisha na anayesimamia mchakato huu? Maana, ukiangalia ushahidi uliopo, mambo mengine hayahitaji hata uwe mtaalamu wa sheria wala msomi kujua kuwa kinachoenda kufanyika ni kinyume na common sense. Sijui tunatoa taswira gani kwa wananchi wetu na vizazi vijavyo kwa kupendeleana na kulindana hata katika maovu?
Kwa taifa linalotaka kujikomboa tokana na ufisadi lazima tujenge utamaduni wa kuhoji kila mtu bila kujali cheo chake. Wengi walidhani kama wahusika wanasingiziwa, wangejitetea na kuwataka wanaowatuhumu watoe ushahidi; wakishindwa wawajibishwe. Haiwezekani  rais awe mlalamikaji, mwendesha mashitaka, shahidi, haki na polisi. Kufanya hivyo, licha ya kuwa kinyume cha sheria, kunakinzana na ahadi za rais za kuwatendea watanzania haki bila kujali ukubwa wa cheo cha mtu.
Tumalizie kwa kusema kuwa Tanzania inakabiliwa na matatizo yasiyo ya kawaida yanayohitaji majibu yasiyo ya kawaida yatokanayo na busara, ukweli, uwazi na ithibati vya aina yake. Siku zote huwa tunasikia watu wakiambiana wafanye maamuzi magumu. Korea Kusini walichukua maamuzi magumu. Nasi kama taifa, kama kweli hatuwadanganyi watu wetu na kuwageuza hamnazo, tunapaswa kufanya maamuzi magumu kwenye kupambana na ufisadi bila upendeleo wala kutishana. Natamani Tanzania ingekuwa Korea Kusini.
Chanzo; Tanzania Daima Jumatano leo.

Ufisadi: Kijiwe chataka haki sawa kwa wote

Image result for photos of magufuli kikwete and mkapa
            Baada ya kutolewa onyo kali la hovyo kuwa tusiwaguse wakubwa mafisadi, kijiwe kimekaa kama kamati kulidurusu na kutoa angalizo kikizingatia sharti la katiba ya kaya kuwa kila mtu anastahiki haki na wachovu wote ni sawa. Hivyo, bila woga wala upendeleo, kijiwe kitatongoa na kudurusu baadhi ya masuala na kuyatolea majibu.
Msomi Mkatatamaa anaingia akiwa na magazeti mengi tu. Anayaweka mezani na kuamkua na kusema “jamani mmesikia ujinga wa kutaka kutufundisha woga ili tuendelee kupigwa?” Anapiga hafa yakuendelea “katika maisha yangu sikutegemea kuwa wale wanaotuaminisha kuwa wanapigana na ufisadi kwa ajili yetu wangekuwa vigeugeu na woga kiasi cha kuogopa hata mawazo. Nani alitegemea kuwa majizi makubwa yaitwayo maheshimiwa yangekingiwa kifua wakati wanaofanya hivyo walituaminisha kuwa watatenda haki bila kujali itikadi, cheo, dini, kabila, eneo na makandokando mengine?”
Kablaya kuendelea Mheshimiwa Bwege ambaye huwa hana tabia ya kuchomekea, anaamua kumchomekea na kusema “wewe uliamini rongorongo za wanasiasa wakati wakisaka kula ya kura siyo? Hujui kuwa baba na mama yao ni moja! Hata hivyo, kama tutakuwa wakweli, nani amkamate nani wakati wote ni watoto wa nyumba moja? Nani amshughulikie nani wakati wote ni sehemu ya tatizo ukiachia mbali hizi rongorongo za kutafutia umaarufu? Pamoja na ubwege wangu, sikushangaa hasa ikizingatiwa kuwa huku Afrika wateule huwa hawaguswi hata wanapopiga kama ilivyokuwa kwenye madili ya ANBEN, EPA, ESCROW, Richmonduli, IPTL na mengine, mnapaswa kula pini kwa vile jukumu lao ni kuwala na kuwatumia nyinyi.”
Mgoshi Machungi naye anaamua kula mic “hata sisi hatishangai hasa ikizingatiwa kuwa hakuna kesi ya ngedee inaweza kushindwa mbee ya nyani. Mimi najua fika. Wengine sea zao ni za kuindana; na huu ndiyo wakati wa kufanya hivyo hasa ikizingatiwa kuwa tinaendeshwa kifaumefaume bia kujitetea tokana na woga na ujinga tena unaofanywa na wae unaoweza kudhani wamisoma wakati ni bue kabisa. Hamkuona madaktai wakijikombakomba kana kwamba hawakusoma?”
Mpemba naye anakatua mic “yakhe hapa nkuunga nkono. Hata mie nilishangaa sana pale nilioposoma kuwa jarida fulani limefungiwa kwa kuchapisha picha za wateule wenye mazonge na kashfa. Wallahi mie ningependa wabadilishe katiba lau waseme kuwa ufisadi ni halali ya wanene na si wadogo kama hawa tuwaonao wakihangaishwa kwa vile walipiga tena kiduchu ikilinganishwa na hawa walotuuza hadi rahis akajikuta pakanga akishughulikia kashfa tu badala ya mambo mengine muhumi kwa kaya.”
Mipawa anaamua kumpoka Mpemba mic “hapa lazima tukubaliane kuwa ufisadi si kosa  hasa linapotendwa na wakubwa, washirika, watoto hata wake zao kama ilivokuwa kwenye kashfa ya Kiwila na nyinginezo zinazokingiwa kifua wakati hata ndege wanazijua na kutushangaa kwa tunavyodanganyana kuwa twaweza kujenga kaya ya haki na ya maendeleo bila kutenda haki sawa kwa wote.”
Kabla ya kuendelea, Kanji anampoka mic Mipawa na kudema “mimi hapana sangaa. Samaki vote iko na surubu. Hivyo, hapana samaki nasulubu menjake kwa kuwa na surubu. Kama nachunguza yote wizuri, nakuta iko na kashfa kama ile ya kuuja jumbani ya umma kwa vakuba chini ya hii moja nono nalinda sasa na naambia chowu kuwa iko wiwu va kufikiri. Halo halo natoka vachowu natoka Kapa!”
Mijjinga aliyekuwa akibukua magazeti anaamua kutoa ya moyoni “mie naona tuache woga. Tuingie mitaani kudai tuambiwe kaya hii ni ya nani kati yetu na hao wateule wezi. Maana, wamekuwa wakitwambia kuwa kaya hii yetu na wao ni watumishi wetu. Huu ndiyo utumishi au wanatutumia wakimaanisha watumishi? Kwani hizo ofisi ni mali zao au za wachovu? Natamani marehemu Chris Mtikila angekuwa hai. Hapa pangechimbika bila jembe. Hata hivyo, sijui kama akina Tunda Jisu watakubali ghilba na vitisho hivi. Kwa ufupi ni kwamba tulianzishe kwa kuingia mitaani kudai uhuru wetu wa kutendewa haki na kusikika vingenevyo tutajikuta chini ya imla bila sababu zaidi ya woga na kujigongagonga kwa wale wanaobembeleza kitumbua uchwara kama yule daktari uchwara aliyefungia jarida kwa kuchapisha picha za wanene wenye mizogo ya kashfa.”
Sofia Lion aka Kanungaembe anaamua kula mic “kwanza nilishangaa kusikia tishio na onyo kuwa waliopiga wakiwa kwenye ulaji wasiguswe wala kuandikwa kiasi cha kufungia jarida. Je wanasingiziwa; na kama wanasingiziwa kwani mahakama zimeisha kayani? Waende wakalalamike mahakamani badala ya kutumia mabavu bila sababu. Huu ni utumiaji mbaya wa mamlaka kusema ukweli. Hii ni kinyume na viapo vya uadilifu ambavyo mara nyingi wengi wamekuwa wakilishwa na wale wanaoweza kufanya mambo ya wachovu kuwa kama masuala yao binafsi wakichagua nani wa kuadhibu na nani wa kusamehe kama kwamba hii kaya ni falme la mja mmoja. Ni aibu hata ndege wanatucheka kwa kufanya kila jambo kuwa sanaa na sinema.”
Kijiwe kikiwa kinachanganya si ukapita msafara wa Njaa Kaya akitoka zake kuzurura Ukanadani alikokwenda kuwapigia magoti wapiga wa makinikia bila kuwa makini. Acha tuuzomea na kutaka kupopoa kama si ndata kutuzidi nguvu.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano leo.

Monday, 19 June 2017

ESCROW NA HISTORIA NA MTANDAO WAKE


What a powerful message!

Cartoon showing how voters are blatantly robbed- Courtesy of the Daily Nation, Kenya

KUSHITAKIWA WEZI WA ESCROW: Nampongeza Magufuli Japo NI Wajibu Wake


rugemalira.png
Watuhumiwa wakuu wa Escrow Harbinder Singh na James Rugemalira wakiwa mikononi mwa polisi
                   Taarifa tulizo nazo ni kwamba wale watuhumiwa wakuu wa kashfa iliyoliibia taifa mabilioni ya shilingi kupitia mfuko wa ESCROW, James Rugemalira na Harbinder Singh wamefikishwa mahakamani leo. Tunaipongeza serikali kwa kuamua kutoka usingizini na kuanza kufanya kazi. Maana, kashfa hii, licha ya kulitia hasara taifa, ililetea aibu na mateso hasa kwa watumiaji wa umeme.
            Tunampongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuthubutu. Tunamsihi hata kwenye kushughulikia marais wastaafu waliofanya ufisadi kama vile Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa aachane na kuwaramba miguu. Maana kufanya hivyo kutamuonyesha kama mtu msafi na mwenye nia ya kupambanan a ufisadi kwa haki na si kwa upendeleo, woga na unafiki.

Sunday, 18 June 2017

Mpaka Mtu Atoke Kuna Juhudi Nyingi


Bila katiba mpya Magufuli anajipiga mtama


            Kupiga mtama ni neno la mtaani lenye kumaanisha kupiga ngwara. Kwa kishona humaanisha ujuzi au maarifa na maumivu ayapatayo mtu kidoleni hasa unapojikwaa. Leo nitatumia neno ngwara kuonyesha namna Tanzania, kwanza, ilivyohujumiwa kiasi cha rais John Magufuli kuuliza”nani alituroga Tanzania?”
Nitajaribu kudurusu mambo au sababu zinazoikwamisha Tanzania au tuseme uchawi –kwa wale wanaoamini katika kurogwa kiasi cha kutaka kuombewa badala ya kuambiwa ukweli kuwa sisi ni sehemu ya tatizo. Hivyo natoa yafuatayo:
Mosi, urathi wa au mabaki ya ukoloni au colonial carryover. Baada ya kupata uhuru na kurithi mfumo mbovu wa uongozi wa ima kuiga au kudandia, tulijikuta tukijenga matabaka ya watu miongoni mwa raia wetu. Hii unaweza kuiona kwenye sheria zinazoongoza nchi yetu kuhusiana na makosa ya wizi mkubwa na mdogo. Mtu akiiba kuku anafungwa miaka mingi kuliko anayeiba mabilioni. Wakoloni waliweka mfumo huu ili kuwafunga waswahili pale wanapowadokolea huku wakiwalinda mawakala wao ambao walikuwa wakinyanya fedha nyingi jambo ambalo tuliliendeleza hadi leo.
Pili, ni ile hali ya nchi kuendesha na katiba zisizotokana na matakwa wala utashi wa wananchi au superimposed constitution. Katiba ya Tanzania haijawahi kutokana na wananchi. Badala yake ima ilitokana na mkoloni–baada ya majadiliano katika jumba la Lancaster–au chama kimoja–katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 iliyotokana na vyama vya Tanu na ASP. Kihistoria Tanzania imekuwa na katiba tano, yaani Katiba ya Uhuru (1961-62), Katiba ya Madaraka au Jamhuri (1962-64), Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (1964-77) na Katiba ya Jamhuri ya Muungano 1977 ambayo iliundwa baada ya vyama vya ASP na TANU kuunganishwa na kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo imekuwa ikifanyiwa marekebisho na kujaa viraka kiasi cha kujitenga na wakati na matakwa ya watanzania.
Matumizi mabaya ya madaraka ya baadhi ya viongozi wetu. Rais wa Tanzania yupo juu ya katiba. Unategemea nini unapomuweka binadamu juu ya sheria zaidi ya matumizi mabaya ya madaraka. Anayebishia hili arejee historia ya Tanzania aone namna serikali za kuanzia awamu ya pili hadi ya nne zilivyoshiriki na kuhalalisha ufisadi kiasi cha kuzaa kadhia ya ufisadi wa kutisha kama unavyoendelea kuibuliwa na serikali ya awamu ya tano. Tokana na rais kuwa juu ya sheria, karibu awamu zote tajwa zilitegemea utashi wa rais kuendeshwa. Mfano, rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi aliporuhusu kile kilichotafsiriwa kuwa RUKSA, wengi hawakujua madhara yake. Kimsingi, hapa ndipo mizizi mikubwa ya ufisadi ilipojikita nchini. Haina maana kuwa hapa mwanzo hapakuwapo na rushwa. Ilikuwapo; ila mwalimu Julius Nyerere alijitahidi sana kupambana nayo chini ya mfumo wa Kijamaa ambao ulimpa uwezo wa kumwajibisha yeyote aliyeshuku alikuwa fisadi.
Alipoingia Benjamin Mkapa–hasa muhula wake wa mwisho–viwango vya ufisadi vilikua zaidi hasa ilipobainika kuwa kumbe kuna watu waliomtumia yeye au mkewe kujinufaisha kwa kutegemea ukoo au nepotism. Rejea kashfa ya kuuzwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambapo ushahidi ulionyesha kuwa waliokuwa makuwadi wa walioinunua walikuwa washirika wa shemejize rais. Hata huu wizi mkubwa katika sekta ya nishati na madini chanzo chake ni kwenye serikali hizi mbili. Pamoja na kwamba ufisadi ni kizalia cha mfumo wa kipebari usio na huruma, kuna ushahidi mkubwa kuwa mabaki ya ukoloni nayo yamechangia sana hasa nchi zinapokuwa zinaendeshwa na katiba zisizotokana na watawaliwa au hoi polloi.
Tuje kwa Magufuli ambaye ameonyesha ujasiri na uzalendo wa hali ya juu unaoandamana na uchungu wa kuona Tanzania ikichezewa na kuliwa mbele na nyuma. Je atafanikiwa kwenye mapambano yake bila kuwa na katiba wezeshi na wananchi? Jibu analo Magufuli ingawa hataki kulikubali na kulitumia. Hapo tarehe 12 Juni, 2017, akipokea taarifa ya pili ya makinikia, alikaririwa akisema “ndugu zangu watanzania nimewambia nafanya hivi kwa ajili yenu…kazi [urais] ni ngumu sana… ndiyo maana tunaomba mtuombee…mimi muda wangu utapita.” Magufuli anakiri kuwa atapita na mfumo anaousimamia hauwezi kujiendesha. Kinachoshangaza ni namna anavyosuasua  au kuahirisha katiba mpya wa wananchi ambao licha ya kutumia fedha zao nyingi na muda, ilishafikia pazuri; na ilishapata maoni yao. Kwa wanaojua mchakato huu ulivyotekwa, kuvurugwa na kuchakachuliwa wanajua fika waliofanya hivyo hawakutaka iwatupe korokoroni tokana na ufisadi uliasisiwa na kusimamiwa na awamu zao. Sijui Magufuli anahofia nini wakati alishalionyesha taifa uzalendo wake? Pia, kama rais anajua kuwa atapita, sasa anashindwa au kuchelea nini kurejesha mchakato usiochakachuliwa wa katiba iliyopendekezwa na watanzania kwa maslahi yao na vizazi vijavyo; siyo kama kujipiga mtama? Wakoloni kwa kujua walichowatendea wengine, waliamua kuachana na katiba za kizamani na kutunga katiba ambazo zinaendesha nchi zao bila kutegemea utashi wa rais au awamu kama ilivyo Tanzania na nchi nyingi za kiafrika.
Tumalizie kwa kumtaka Magufuli atumie ujasiri, usongo na uzalendo alioonyesha kwenye kupambana na ufisadi, kurejesha katiba ya wananchi ili isaidie si kupambana na ufisadi bali kuuondoa kutokana na kuwa na vifungu vinavyoshughulikia ufisadi na maadili ya viongozi kivitendo na kisheria. Bila katiba mpya ya wananchi, Magufuli atashindwa na anajipiga mtama kama wasemavyo watoto wa mjini.
Chanzo: Tanzania Daima Jumapili leo.

Friday, 16 June 2017

Kashfa ya IpTL: Barua ya wazi kwa EWuuRA

        Baaada ya kuchacha kiasi cha kukosa njuluku ya kupatia ulabu, niliamua kujisomea magazeti lau nijue umbea wa mjini; na nikakutana na kiroja cha mwaka! Guess what. Eti vilaza wetu wa mamlaka ya ulaji angani, nchi kavu na majini walioruhusu ujambazi wa IpTL wanatutaka tutoe maoni juu ya kuendelea kuhalalisha ujambazi huu. Mnakumbuka shuka asubuhi siyo? Mbona mlipoingia huu ujambazi hamkutaka maoni yetu; au mnataka mpate kisingizio cha kusema kuwa tulishirikishwa kubariki ujambazi huu? Mshindwe na kulegea. Kwanini kutangaza kwenye magazeti binafsi na si govt gazette?
            Kwa vile mmejivua nguo wenyewe, acha niwape ya moyoni kama ifuatavyo:
Kwanza, IpTL si kampuni sawa na makampuni mengine. Hivyo, haipaswi kufikiriwa wala kufaidi haki sawa na makampuni mengine yasiyotupiga kama wao. Hivyo, kama mnatafuta sababu ya kutushirikisha kwenye uchafu wenu, mkome.
Pili, kabla ya kutaka maoni yetu, mnapaswa kutueleza ni kwanini mliingia ujambazi huu; na nani walihalalisha hii jinai; walipata nini na kiasi gani kwa sheria ipi? Kwanini sasa; na si huko nyuma mliponyea na kuivuja sheria kiasi cha kuigeuza kaya kichwa cha mwendawazimu aka shamba la chizi?
Tatu, muweke wazi mikataba yenu na majambazi haya ili tujue kuna nini; na tunaongelea na kuchangia nini badala ya kutuuzia nguruwe kwenye gunia. Kumbaff.
Nne, mtupe uhakikisho kuwa hamna nia mbaya nasi na kaya yetu kama ambavyo mmekuwa mikifanya ili kujipatia njuluku za haraka wakati mkiendelea kutupandishia bei ya umeme. Mnadhani hatujui kinachoendelea?
Tano, muwachukulie hatua wote walioshiriki kuingiza kaya kwenye balaa hili la kiuchumi. Kama hamuwajui, ngoja niwatajie makuwadi wao. Yupo Jimmy Rugemalayer ambaye anasifika kuwahonga walafi kuanzia mawaziri, wabunge, viongozi wa kiroho wenye uroho hata majaji. Pili, yupo gabacholi Singasinga anayeishi Kenya ambaye aliibuliwa na majambazi wetu wa ndani ili kuficha uchafu wao.
Sita, mtwambia chanzo cha upendo na uwazi huu ambavyo havikuwapo hapo mwanzo mlipofunga ndoa hii haramu ya kuangamiza kaya na walevi wake.
Saba, mtuhakikishie kuwa walioingia mikataba hii hatari hamtawaita makaburi na kushindwa kuwafukua kwa kuhofia kushindwa kuwafukia kama alivyowahi kusema dingi ambaye ameonyesha wazi kuwagwaya hawa jamaa kana kwamba ana faida nao. Haiwezekani mkaendelea kutugeuza hamnazo huku mkitusanifu kuwa mnataka maoni yetu wakati mlipoingia kitandani kufanya ufuska huu wa kiuchumi tulipiga kelele mkatupuuza. Tutaamini vipi kama hamtatupuuza wakati huu. Kimsingi, kama mnataka mawazo nenda kwa akina Bashite wanaosikika na kusifika. Huenda watapata fursa hii kuanzisha sinema nyingine ili kuendelea kuwa madarakani wakati wana vyeti feki na wanatumia majina feki.
Tukiachia mbali hawa vidagaa tuliowatajia hapo juu, je mko tayari kuweka wazi majina ya marais na mawaziri walioshiriki kusuka dili hili hadi likazaa jingine liitwalo EPA ambalo lilisababisha hasara ya mabilioni kwa kaya? Je mko tayari kuwaumbua waliotumia njuluku za EPA kuukwaa ulaji huku wakituache tuendelee kuliwa mbele na nyuma? Je hapa mnataka kumsanifu nani; na kwanini mnaendelea kututia madole machoni?
Guess what. Nimeamua kugusia kashfa hizi ili kuwaumbua Eula kuonyesha mnavyotaka kuendelea kuula wakati sisi tukiliwa. Mbona hamuongelei njuluku ya rada ambayo wakoloni kwa kiingereza walitaka kuwarejeshea mkakataa? Mbona  hamkumbushii kukataa kwenda Uswizini kupewa njuluku nyingi tu ambazo majambazi wetu wakubwa, mibaka na mipapa imeficha kule? Mbona hamuongelei kubadili sheria kuhusiana na kashfa kama ya IpTL?
Kwa uzembe wenu mmekatiwa kitu kidogo na kikubwa mkalegea na kuachia kila kitu; halafu mnaanza kujishaua kuwa mnatafuta maoni. Nenda mkamuulize Kafulia aliyeibua na kuvalia njuga sakata hili hadi mkamtosa mjengoni. Kwani hatujui? Katika kufanya utafiti wangu juu ya kashfa hii niligundua kuwa kumbe IpTL inaweza kuwa Independent Protectorated Tanzia Ltd ambayo inalindwa na sirikali kama siyo sirikali ndani ya sirikali tena inayofanywa kuwa siri kali.
Nimalizie kwa kutoa maoni yangu na ya walevi ninaowangoza kama ifuatavyo:
Mosi, wanyonge wote walioguswa na kashfa hii bila kujali vyeo wala sura zao au ubashite wao.
Pili, taifisheni mitambo ya IpTL kutokana na ukweli kuwa ni mali ya walevi ambayo imekuwa ikitumiwa kuwalangua umeme na kuwaibia.
Tatu, taifa mimali ya wale wote waliohusika kwenye ufuska huu wa kiuchumi ndipo mje tuongee; na tuwafundishe jinsi ya kusimamia mali za umma. Itoshe kusema; walevi wamechoka kutiwa vidole na kugeuzwa samaki ambaye hukaangwa kwa kugeuzwa geuzwa kwa vile yu mfu.
Leo hii tosha. Ngoja nikapige kanywaji tayari kuwatolea uvivu zaidi pale itakapobidi. Kwanini msiunde tume huru kama ya makanikia yatokanayo na ukosefu wa umakini?
Chanzo: Nipashe Jumamosi kesho.

Adui Magufuli si Magazeti bali Yeye MwenyeweKufungiwa kwa gazeti la Mawio ni ushahidi kuwa rais John Magufuli hapendi kukosolewa wala hana nia ya kupambana na ufisadi kama anavyojitapa. Gazeti hili lilifungiwa baada ya kuripoti habari toka bungeni ambapo baadhi ya wabunge toka upinzani walipendekeza marais wastaafu Jakaya Kikwete na Benjamin Mkapa ambao wanajulikana dhahiri kwa kuingiza Tanzania kwenye matatizo ya kiuchumi tokana na tamaa zao. Wanaojua historia ya ufisadi Tanzania, wanajua kuwa na Magufuli ni sehemu ya mfumo wa kifisadi ambao alitaka kuukabili. Hata hivyo, kwa hali ilivyo, ni kwmba Magufuli punde tu atarudi kwenye mfumo na kuwa mmojawapo kama alivyokuwa. Vinginevyo, asingepoteza muda kuwalinda wahalifu wanaojulikana hata kama wana madaraka makubwa tu. Nadhani hapa tatizo ni kwa Magufuli kuamua kuwatumikia wateule badala ya watawaliwa. Je anahofia yake naye yasifumliwe hasa ikizingatiwa kuwa si msafi kama anavyoonekana? Rejea utwaliwaji wa nyumba za umma wakati akiwa waziri husika ukiachia mbali kashfa ya hivi karibuni ya mabilioni yaliyopotea kwenye wizara yake ya mwisho.

Wednesday, 14 June 2017

Ewura should stop taking Tanzanians for a ride

Image result for photos of iptl tanzania james rugemalira
        Joking aside, I was shocked when I read somewhere that the Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA) is seeking public input on how to go about Independent Power Tanzania Ltd (IPTL) mega holdup. EWURA’s acting director for legal services, Edwin Kadifu was quoted by this paper (June 9th, 2017) as saying “we call on public to exercise their right, and send us their views on whether to extend IPTL’s licence, or not instead of using the media platforms to complain about the procedure which is legally based.” To show how this is goofy and devoid of any momentousness, Kadifu didn’t provide the address to which to send the said views. So, too, the EWURA decided to use private media but not government gazette. Ironically, Kadifu seems to abhor the tendency of using media to complain while he ironically did the same.
Due to this travesty, I’d like to ask the following questions to the EWURA:
First, did the EWURA write to any stakeholders such as Human rights organisation, Non-Governmental Organisation and others firms dealing with public advocacy to see to it that it gets what it wants?
Secondly, why didn’t the EWURA apply the same rationale–namely seeking public inputs–before, especially at the time it entered such spurious agreement that saw our country being turned into El Dorado; and since when did the powers that be seek public views on anything?
Thirdly, why’s the EWURA advertised its appeal on public media but not government gazette; if, indeed, it’s serious so as to be taken seriously?
Fourth, is the EWURA ready to make public the contracts our homemade criminals entered with the IPTL first so that we can see what’s in there in order to be well versed with the goings-on? Who’s fooling whom so as to take him or her for a ride easily?
Fifth, is the EWURA ready to divulge the names of the culprits who entered the agreements; and those who benefitted from the deal therefrom?
            Sixth, how far sure are we that our inputs will be accommodated; not to mention being used to the letter?
Seventh, is the EWURA ready to sponsor the motion of amending the laws governing contracts so that the hoi polloi can put their inputs?
Eighth, what’s government’s position in this vis-à-vis punishing the culprits of who many are still in public services illegally thanks to being connected or bashited?
 Ninth, is the EWURA ready to prosecute the culprits so that we can evidence justice being delivered? Under which law’s the EWURA seeking hoi polloi’s inputs?
 Tenth, is the EWURA seeking to involve the general public in this criminality; and why now not then when the deal was done and dusted by a few criminals who have since gone Scott free? Will the general public allow itself to be hoodwinked; and being taken for a ride for its obvious peril?
Demonstrably, there’s something fishy in this new and impromptu mercy that the EWURA seeks to display. I’d candidly say that before seeking our inputs, the EWURA must do the following:
            First, look the culprits in the face–be they small or big–and thereby duly punish them so as to convince the hoi polloi that such delinquency won’t be replicated apart from sending a clear and strong signal to those still at large contemplating to replicate the same.
            Second, amend the laws governing the current contract before issuing such a gobbledygook appeal so that we can efficiently tackle the problems.
            Thirdly, prosecute the culprits so that they can receive their rewards according to the law and logic.
            Lastly, retrieve all spoils such as monies, cars, houses, land, and other property made out of the scam.
Source: The Citizen Wednesday today.

Tuesday, 13 June 2017

IPTL Serikali Ikiri Kushindwa

Image result for photos of iptl tanzania
            Hivi karibuni, serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ilitoa mpya ya mwaka katika harakati zake za kuendelea kubariki na kuhalalisha haramu ya wazi. EWURA iliwataka watanzania kutoa maoni yao juu ya ima kampuni kidhabi la independent Power Tanzania Ltd (IPTL) lipewe leseni ya kuendesha hujuma yake au la. Bila kujali wala kukumbuka kuwa watanzania wanajua kuwa IPTL ni serikali ndani ya serikali tena iliyoendelea kujitanua nchini bila ya hata kuchaguliwa. Imekuwa madarakani kwa vipindi vitatu bila kuchaguliwa tangu ilivyoingizwa nchini kimezengwe mwaka 1995 chini ya awamu ya tatu ikiwagusa moja kwa moja marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete.
            Meneja wa Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo alikaririwa akisema “Ewura tunapokea maoni ya wananchi kwa maandishi, kwa hiyo litakuwa jambo la kizalendo kwa wananchi kujitokeza kutoa maoni yao ama kupinga IPTL au kuunga mkono ili itusaidie nasi kufanya maamuzi.” Kwanza, huyu Kaguo sijui kama ni mtanzania; na anajua maada ya uzalendo. Kwanini EWURA wawatake wananchi kutoa maoni sasa na si wakati wakiiingiza balaa hili nchini? Nini kimebadilika hadi wananchi kuwa na maana wakati walishaibiwa miaka nenda rudi ukiachia mbali kulalamika bila kusikilizwa kwa muda mrefu? Ni bahati mbaya kuwa EWURA imetoa maelezo kidogo kiasi cha kuacha maswali mengi bila majibu. Mfano, wanatumia sheria gani kutaka maoni ya wananchi; na wananchi watakuwa na hakikisho lipi kuwa maoni yao hayatachakachuliwa au kutumika kuhalalisha jinai hii ya muda mrefu?
            Kwa wanaojua ukubwa wa hujuma iliyofanywa na IPTL na makuwadi wake wa nchini, wanashangaa upendo, uwazi, ushirika, ushirikishwaji, ushikaji hata ushidau na udau vimeanza lini na kwa nini?     Wapo wanaodhani kuwa hii ni janja ya walaji wenye madaraka walioshirikiana na kampuni hii kwa muda wote ambao imekuwa ikiliibia taifa kuwaingiza mkenge mwingine watanzania kwa kuwashirikisha kwenye jinai hii ambayo imewatesa watanzania kwa muda mrefu. Rejea kuendelea kuhujumiwa na kudhoofishwa kwa Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO) ambalo wezi walioko nyuma ya jinai hii wamekuwa wakiikamua fedha kiasi cha kuilazimisha kuwatwisha mzigo wateja wake bila huruma.
            Je watanzania watakubali ghilba hii ya kutaka kuwafanya sehemu ya jinai hii ya kikatili? Je hata wakitoa maoni yao yataheshimika? Nani anamdanganya nani na nani anataka kumtumia nani katika dhambi hii ya kuhujumu taifa? Je EWURA wana nguvu gani kisheria kuanzisha mchakato huu wa mashaka? Je ni kwanini serikali inajitoa kiasi cha kuachia taasisi ndogo kama EWURA wakati ina mamlaka ya kuingilia kama ilivyofanya kwenye sekta ya madini? Je hii ni namna ya serikali kuficha sura au dalili za kukiri kuwa IPTL haigusiki kiasi cha kuwa kama serikali ndani ya serikali? Kwanini serikali isiunde tume maalum ya wataalamu ya kuchunguza jinai hii ya muda mrefu? Mbona makampuni mengine ya kigeni hayapitii mchakato kama huu wenye kuhitaja maoni ya watanzania?
            Kwa vile rais John Magufuli ameonyesha kuwa na uzalendo na uchungu na raslimali za taifa, tunashauri aingilie kati kuondoa upuuzi huu wa kutaka maoni ya wananchi wakati hayana nguvu kisheria. Magufuli amekuwa mwepesi kushughulikia kadhia mbali mbali kama vile ujenzi holela, wizi bandarini, vyeti feki na ajira hewa, madini na mengine; ingawa anaonyesha kusuasua au kukaa kimya kwenye sakata la IPTL ambalo lina maslahi makubwa kwa taifa hasa ikizingatiwa hujuma ambayo IPTL imekuwa ikifanya nchini kwa muda mrefu. Je Magufuli anachukulia kashfa hii kama kaburi kwa vile walioiasisi na kuitumia ni baadhi ya watangulizi wake ambao aliwaahidi ulinzi dhidi ya kashfa mbali mbali zinazowakabili? Hadi sasa hakuna anayeweza kueleza ni kwanini Magufuli anasitasita kukaa kimya kuhusiana na kashfa hii yenye madhara makubwa kwa maisha ya watanzania.
            Wengi wanahoji: kwanini EWURA wanataka maoni ya watanzania wakati hawajui kilichoko kwenye mikataba yao na IPTL? Je EWURA wako tayari kuweka wazi mikataba hiyo kwa kuipeleka bungeni ili wawakilishi wa wananchi waione na kuridhia au kupinga kilichopo kabla ya kutaka maoni ya jumla yanayolenga kuhaendelea kuhalalisha uwepo wa IPTL nchini ikifanya hujuma ile ile ambayo ni hatari kwa usalama wa taifa? Kwanini EWURA wasiitake serikali kupeleka mswaada wa sheria bungeni kuangalia namna ya kuondokana na donda ndugu na jinamizi hili liitwalo IPTL?
            Tumalizie kwa kuwataka EWURA waache kutuhadaa kwa kutaka kulinda maslahi ya wezi wachache wenye mamalaka. Huu umchakato wa kutaka maoni unapaswa kulaaniwa na kusimamishwa ili kuangalia namna bora ya kushughulikia jinai ya IPTL kwa kuwakamata wote waliohusika na hujuma hii, kuwafilisi na kuwafikisha mahakamani huku mitambo ya IPTL ima ikikamatwa au kutoipa kampuni hii leseni nyingine ya kuendelea kuwaibia wananchi wasio na hatia. Rais Magufuli, tafadhali, simamisha ghilba hii na utumbue IPTL na wote walioko nyuma yake. Haiwezekani Tanzania iendelee kugeuzwa kichwa na mwendawazimu na matapeli wa ndani na nje kwa kisingizio cha uwekezaji ambao kimsingi, ni uchukuaji na ujambazi wa mchana kweupe.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

Kijiwe Kupeleka Maazimio Yake Ewuuura


Baada ya kuzinyaka kuwa kuna zengwe la kutaka kuwashirikisha wachovu kwenye wizi mwingine chini ya ujambazi wa IpTL, kijiwe kimekaa kama kamati ya uokozi ili kutoa mwelekeo wa namna ya kuzuia na kukomesha wizi huu donda ndugu.
Msomi Mkatatamaa analiamsha dude kwa kufichua kile alichodurusu kwenye gazeti fulani ambalo leo hatutaji jina. Anasema “wasomi wanakijiwe, nimeinyaka kuwa mamlaka ya ulaji wa angani, ardhini na majini ina mpango mchafu wa kutaka kutuhusisha kwenye jinai yake ya kuendelea kubariki wizi wa IpTL.” Anatoa gazeti na kuliweka mezani na kuendelea “hebu angalieni wanavyodai tutoe maoni yetu kabla hawajaruhusu wizi huu kuendelea kama njia ya collective consent au uhusika wa umma katika kuhalalisha haramu hii donda ndugu. Sijui hawa wezi wanataka kutumia sheria gani wakati kila kitu kiko wazi kuwa IpTL ni jipu ambalo rais Kanywaji anapaswa kulitumbua haraka. Hata sijui kwanini amekuwa mwepesi wa kutumbua majipu mengine kuanzia Bandarini, Uwanja wa ndege, Madini na kwingineko lakini anaigwaya IpTL utadhani nayo ni Bashite!”
“Kweli hapa kazi tu na ipo kazi kweli kweli! Yaani baada ya kulala kitanda kimoja miaka yote hii wakifanya ufuska wao wametuchoka kiasi hiki hadi kutaka tubariki haramu hii! Wallahi mie simo na kama nimo basi nitatibua dili zima. Nadhani hapa dokta Kanywaji anatanivumilia kusema kuwa hili ni jipu lake analopaswa kulitumbua. Kama akishindwa ajue amejitibulia vibaya sana. Maana alisema hataogopa wala kumuonea mtu. Je inakuwaje anaendelea kufumbia macho ujambazi huu wa wazi?” anachomekea Kapende huku akitafuna meno na kusonya kwa hasira.
Kabla ya kuendelea kudema Mpemba anampoka mic “yakhe nami nkubaliana nawe. Yanini walete hii kitu leo wakati wamekuwa wakitutafuna pamoja bila kujali? Je haya mapenzi yantoka wapi au wantakaendelea tuchafua na kutuibia kama kwamba sie ni hamnazo kama wao waliojilegeza na kuachia kula kitu utadhani vyangu au hamnaazo? Kula mmeisha kula eti mnataka tutoe mawazo wakati mnaosha vyombo; ile iweje?”
Mipawa hajivungi. Anakwanyua mic “kwanini sasa na si nyuma na mbona huko nyuma hawakuwa hivi? Kwanini wametangaza upuuzi huu kwenye gazeti binafsi kana kwamba government gazette haipo? Hapa lazima kuna namna na si ndogo wallahi. Napendekeza, tusipinge tu. Mnaonaje tukaamua kwenda huko huko Ewuuura tukawape maazimio ambayo shurti leo tuyafikie na kupanga siku ya kuwapelekea?”
“Wazo lako la mbolea sana. Kama wanataka kutugeuza rubber stamp, acha tuwaendee huko huko. Tukifika tunahakikisha tunaandamana na waandishi wa habari ili warushe tendo hili takatifu na la ukombozi wa kaya. Tukishatoka huko, tunapeleka nakala ya maazimio yetu kwa rahis ili naye ajue tunavyopanga kuikomboa kaya yetu toka kwenye mikoni michafu ya majambazi wa kiuchumi wanaotaka kututumia kubariki ufuska wao; au vipi?” anachangia Mijjinga huku akibofya kisimu chake cha Sumsung 10.
Kanji anakwapua mic “veve dugu yangu asema jambo juri sana. Mimi iko nyuma yako na takwenda bele kama naamua kwenda toa hii azimio kwa wuura. Tena nakubali ile nasema kuva hii sasa natia vidole sisi. Kama nataka tenda haki kwanini nagoja muda refu sana? Kwanini napandisa bei ya umeme kila muaka nasi vachowu natobolewa kila siku?”
“Kanji hemu eeza vizuri tikueeewe. Natoboewa wapi na nani na kwanini? Na kwanini uwe nyuma yake ii ufanye nini? Nadhani hapa kia kitu chapaswa kuwa mbee kwa mbee.” Anajibu Mgoshi huku akimpa kikombe muuza kahawa ammwagie kahawa.
Kanji anacheka na kumtazama Mgoshi na kujibu “sasa kwanini tukana mimi. Kama veve hapana elewa ile nasema vatu vote kwanini nataka changia nini?”
Baada ya kuona utani unaanza kupoteza mada, Sofia Lion aka Kanungaembe anakatua mic “jamani acheni utani kwenye mambo nyeti. Nadhani alichomaanisha Kanji ni kuwa kaya yetu imekuwa ikichezewa na hawa wezi kiasi cha kugeuka shamba la bibi kama siyo kichwa cha chizi. Ni simpo hivi.”
Mheshimiwa Bwege aliyekuwa kimya muda mrefu anaamua kula mic “nataka niwe mkweli. Ninachoona hapa ni ukweli kuwa hawa jamaa kuwa wanaliwa kwa muda mrefu kwa kupewa vijisenti kidogo, wanataka na wananchi waingizwe kwenye ulaji huu wa kipuuzi. Nakubaliana na wanaohoji ni kwanini rahis Kanywaji ameshikwa na kigugumizi kuhusiana na kadhia hii ambayo iko wapi kuwa tunapigwa kiasi cha wachovu kulanguliwa umeme na kufanya maisha yawe aghali bila sababu tokana na ujambazi huu wa IpTL. Suluhu ya tatizo hili ni simpo. Kamata akina Rugemalayer, gabacholi Singasinga na akina Njaa Kaya na Ben Makapi walioingiza ujambazi huu wa nchana au vipi? Taifisha mali zote walizopata na kuwanyonga ili kupumzisha mzimu wa hujuma hii kwa kaya. Simpo.”
Kijiwe kikiwa ndiyo kinachanganya si lakapita shangingi la Rugemalayer! Kwa vile tulikuwa na usongo, tulinkamata na kumfanyia kitu mbaya ambacho si vizuri kutaja hapa tokana na kuheshimu maadili. Hata hivyo, “mimba” yake karibuni itazaliwa ili kuwa mwanzo wa mwisho wa kashfa ya ufuska wa IpTL.
Chanzo: Tanzania Daima Jumatano kesho.

Sunday, 11 June 2017

Gaddafi's Dirty Linens and Racism against Blacks Exposed

Although we do not concur with or support how former Libyan strongman Muammar Gaddafi was pulled down, so too, we condemn his blatant racism against black people he pretended to love and call brothers while he actually, like any arab, hated and discriminated against. In this clip, everything is put on the agora for eyes to see and judge. What do you call the situation whereby a person is living in his or  her own country as second class citizen simply because he or she is black? Again, ironically, such a racist used to go to African Countries South of Sahara preaching islam and brotherhood as it he was serious.Gaddafi knew the art of deception. A hypocrite of the highest order Gaddafi was able to contribute immensely in dismantling apartheid in South Africa while at home he replicated and lived the same. Now Gaddafi is long gone. Libya needs a leader who will never labour under xenophobic lenses but who will uphold and promote humanity, equity, justice and human rights.


Wahamiaji Haramu: Kuna siku Tanzania itatawaliwa na mgeniBaptista Marco raia wa Burundi aliyekamatwa nchini hivi karibuni akifanya kazi kama mwanasheria wa TBS kinyume cha sheria.
                Matukio ya wageni kukamatwa wakifanya kazi nchini–tena nyingine nyeti–kinyume cha sheria yanazidi kuongezeka kiasi cha kuanza kujenga shaka juu ya usalama wa taifa na wananchi kwa ujumla. Hapa lazima tujiulize tatizo liko wapi; na nini kifanyike kuondoa hatari hii ambayo inaweza kutugharimu kama taifa. Wahenga walinena: usipoziba ufa, utajenga ukuta; jambo ambalo ni gharama baada ya nyumba kubomoka.
            Kuna matukio ambapo wakimbizi wa kiuchumi wa kigeni wamemeajiriwa nchini na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kustukiwa. Je vyombo vyetu wa usalama vinafanya kazi gani na kama vinafanya kazi je vinaifanya vizuri? Mtu anaajiriwa kwa ngazi ya juu. Je anapataje kazi kama hakuna rushwa? Je wako wangapi wahalifu wa namna hii? Je wako peke yao au wana mitandao ya watanzania wanaowasaidia kutekeleza jinai hii? Je mamlaka zinachukua hatua gani dhidi ya mitandao hii ambayo bila shaka itakuwa inajulikana?
            Japo mimi ni muumini wa umoja na ushirikiano vya kweli kwa Afrika, si mpenzi wa ushirikiano wenye kuvunja sheria ambapo baadhi ya wahalifu hujipenyeza kwenye nchi nyingine kinyume cha sheria na kujipatia kazi na elimu wakati wananchi wakikosa vitu hivi. Si mpenzi wa uchoyo wa baadhi ya mataifa hata watu kupenda kwenda kuchuma kwa wenzao bila kujali madhara wanayosababisha au bila kuruhusu watu kutoka huko wanakohujumu kwenda kupata kazi au kuishi kwenye nchi husika. Uumini wangu wa Afrika ni kwa nchi zote kuunganishwa na kurejea kuwa moja kama Afrika ilivyokuwa kabla ya kugawanwa na wakoloni kwenye mkutano wa Berlin 1884-85.
Kwa taifa kuondokana na kadhia hii, kuna haja ya kutunga sheria kali zinazowapa adhabu ya vifungo virefu sana hawa wakimbizi wa kigeni waliojipenyeza na kupata kazi au elimu nchini kinyume cha sheria ili wasifaidi vitu hivyo nchini na nje ya nchi ama makwao. Pia wahalifu hawa wanapogundulika, wasipewe dhamana ili wasitoroke. Hapa ndipo umuhimu wa kubadili sheria ili kuondoa dhamana unajitokeza kama kweli taifa lina nia ya kuondokana na kadhia hii.  Maana uzoefu unaonyesha kuwa wengine hupewa dhamana na kutoroshwa na washitiri wao ili wasiumbuke kama ilivyotokea kwenye kashfa ya kutorosha wanyama hai kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikimhusisha mhalifu wa kipakistani ambaye alitoroshwa nchini.
Pia kuna haja ya mamlaka kujua; kwa sasa Tanzania inao raia wengi wa kigeni wanaoishi na kufanya kazi nchini kinyume cha sheria tokana na mfumo wetu mbovu na ile hali ya wananchi kutoelimishwa vya kutosha ili kusaidia kuwabaini wote wanaofanya hivi.  Haiwezekani watu wetu wakose ajira wageni wapate. Hapa lazima kutakuwa na tatizo kubwa mojawapo ikiwa ni ukosefu wa uzalendo na umakini katika kulinda mipaka na maslahi ya taifa letu. Nchi nyingine ukiingia tu, kila mtu anajua; na taarifa zako zinaifikia serikali mara moja. Tuachane na mambo ya kizamani. Kwani wakimbizi hawa wa kiuchumi wanadhoofisha uchumi wa taifa letu kiasi cha kufanya serikali ishindwe kutoa huduma bora kwa wananchi wake.
            Jingine, wote watakaobainika kutenda jinai wafilisiwe mali walizochuma nchini kwa kutumia elimu na fursa ya ajira nchini ili liwe somo kwa wengine wanaopanga kutenda jinai kama hii. Twende mbali; sambamba, tuwafunge waliowawezesha, kwa kuwahifadhi hata kuwatoza rushwa na kuwapatia ajira kinyume cha sheria.  Hapa lazima tuwe wakali na kuhakikisha kuwa yeyote anayeshirikiana nao , bila kujali cheo chake au uraia wake, anaadhibiwa vilivyo ili kuondoa uwezekano na vishawishi vinavyoshamirisha jinai hii nchini. Maana, tukiendelea na uhovyo na ulegelege huu, kuna siku Tanzania itatawaliwa na raia wa kigeni bila kujua; jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa letu.
Kuondokana na kadhia hii, tuwabane marais wetu waunganishe nchi zetu ziwe nchi moja ili kuondoa kadhia kama hizi zinazoweza kuvuruga uhusiano wa mataifa.
            Tumalizie kwa kuitaka serikali hasa rais John Magufuli ambaye anasifika kwa juhudi zake za kuanzisha vita dhidi ya kughushi sifa na vyeti vya kitaaluma, apanue wigo hadi kuwashughulikia matapeli hawa wanaojipenyeza nchini na kupata elimu na kazi nchini bila stahiki yoyote kiutu na kisheria. Inatosha kusema kuwa wakati wa kuigeuza Tanzania shamba la baba inabidi ufikie mwisho. Hili litawezekana tu pale wananchi wetu watakapoelimishwa juu ya madhara yanayosababishwa na wakimbizi wa kiuchumi ambao wengi wao wanapata usaidizi toka kwa watanzania wenyewe wasijue wanajikomoa na kujichelewesha. Haiwezekani nchi yenye kila aina ya vyombo vya usalama iendelee kuhujumiwa kirahisi hivi huku vyombo husika vikipoteza muda kuwachunguza wapingaji, wapinzani na mambo mengine madogo badala ya kutoa kipaumbele kwa usalama wa taifa kwa maana ya usalama wa taifa badala ya kuwa usalama wa chama kama ilivyo kwa sasa ambapo vyombo vyetu vya usalama vinatumika vibaya.
Chanzo; Tanzania Daima Jumapili leo.

Saturday, 10 June 2017

Taasisi ya kuzuia rushua inaponuka rushua!

     Image result for photos of dr hoseah     Juzi tulibigwa na butwaa tukalewa bila kunywa. Si baada ya kigogo wa Taasisi ya Kukuza, sorry, Kuzuia na Kupamba, sorry, Kupambana na Rushua kukutwa na mimali ya mabilioni tofauti na stahiki yake. Leo sitaongelea mambo yaliyoko kwa pilato. Nitadurusu kilevi yanayowachanganya walevi kiasi cha kutaka tugawane kaya kila mmoja ajue njia yake kama mambo yenyewe ni hivi. Natamani tugawane kaya ili nipige zangu majuu lau nitanue kama wao watanuao wakutumia kodi za walevi. Nadhani Njaa Kaya na walevi wenzake ambao kitaalamu huitwa globetrotting parasites the boozers feed as they feed on them tunaelewana hapa.
            Nikirejea, huyu parasite mwingine, pamoja na kunaswa ntegoni, wapo wengi. Utawaona wakitukoga mitaani utadhani ukwasi wao halali. Ajabu nasi ni wa kulaumiwa. Tunapataje jeuri kuchoma vibaka tunagwaya kuwachoma mibaka iliyotamalaki kayani?
            Leo acha niwachomee kwa kutumia utafiti nilioufanya kayani kwa muda mrefu. Haya ndiyo matokeo yatokanayo na samples kidogo toka maeneo mbali mbali ya ofisi za umma. Katika utafiti wangu niligundua kuwa pale Bandarini wapo wengi tu. Wapo vijana wadogo–tena wenye elimu kiduchu–hasa wa vitengo vya makontena na mafuta wanavyomilki midude ya kutisha kuanzia akaunti nono, mahekalu, migari ya bei mbaya na mali nyingine fichi. Nenda TrA uone wezi hawa wanavyolipwa kodi ambayo ilipaswa kwenda sirikalini; viwanja vya ndege maarufu hutumika kupitisha bwimbwi. Wapeleleze wafanyakazi wa maeneo yale, utashangaa ukwasi waliokwishapunyua kwa walevi. Huwa nashangaa Usalama wa kaya kuacha kupambana na mipapa hii hadi wanageuka Uhasama wa Kaya (UK).
            Pekueni mikataba ya kijambazi inayoangamiza kaya kiasi cha kutufanya kushindwa kukata kanywaji. Nenda kwenye wizara ya viwanda muone madudu yanayoendelea kule ambapo viwanda vilibinafsishwa na kuishia kung’olewa mashine au kugeuzwa mabohari yakufichia wakimbizi wa kiuchumi toka ugabacholini na kwingineko. Nendeni uhamiaji ambapo pasi za kaya zinauzwa kwa magabacholi, wanigeria hata wasomali kama njugu. Nenda gesi la polish muone vijana wadogo wanavyomilki mimali haramu ya kutisha. Nenda mbuga za wanyama na kwenye wizara ya utalii uone wahalifu wanavyouza mali zetu kwa wachukuaji kuanzia wanyama hadi vitalu. Hivi ile kesi ya kutorosha wanyama hai iliishia wapi; au ndiyo huko kuendelea kuliwa tusistuke wala kulalamika? Nenda kwenye mahakama zetu zinazosifika kuuza haki japo wanaojihusisha si wote; mahospitali yetu uone midawa inavyouzwa; machimbo uone walivyofurika wageni walionunua vibali. Nenda mikoa ya mipakani uone wahamiaji haramu wanavyotanua. Nenda kila mahali, kama akili yako ni timamu, utalia sana kwa namna unavyoliwa mbele na nyuma.
            Leo ni mwendo mdundo. Nenda Masaki, Msasani, Oyster Bay, Mikocheni,Msasani, na maeneo mengine wanakokaa wazito muone mijengo iliyoporomoshwa bila maelezo. Ama kweli kaya yetu ishauzwa. Kwa walevi wasio na chochote wanapaswa kulia au kuamua kufanya kweli kuhakikisha wanawatokea wanaoibia kaya na kuwaponda na michupa yao. Nenda mipakani muone mipaka ya kaya ilivyogeuzwa maduka ya hawa wadukuzi wa njuluku zetu.
            Mie si bingwa wa kulalamika; nashauri yafuatayo:
            Mosi, tungeni sheria ya kumtaka kila mlevi kutangaza utajiri au umaskini wake na namna alivyoupata; akishindwa ukwasi utaifishwe huku akifikishwa lupango kutubia udokozi wake.
            Pili, taasisi ya UK isipoteze muda kuchunguza wanasiasa na wakosoaji; iwapeleleze wakwasi wezi. Hii ndiyo ilifanya mzee Mchonga kufanikiwa kwenye utawala wake kabla ya kuhujumiwa na wakoloni.
            Tatu, itungwe sheria ya kuhakikisha kila mlevi anajaza taarifa za mapato yake kila mwaka ili kujua kilichoongezeka na kilichopungua.
            Nne, tunga sheria za kufilisi na kunyonga wote watakaobainika wanaibia kaya. Tujifunze toka Uchina ambako ukipatikana umeibia kaya wanakufanyia kitu alichofanyiwa Saddam Hussein baada ya kuvunja ndoa yake na Wamarekani.
            Mwisho, uwepo utaratibu wa walevi kuwaripoti wenzao wanaojua wanapunyua njuluku zao. Lazima kila mmoja awe askari wa mwenzake bila kujali cheo, rangi wala ubashite, kujuana na upuuzi mwingine. Ngoja niende kupata kanywaji ili nichaji bongo tayari kuendeleza utafiti.
Chanzo: Nipashe Jumamosi leo.

Thursday, 8 June 2017

Huu ni Ubinafsi, Ulimbukeni, Upofu au Utukufu?

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, akichoma
Watawala wetu mara nyingi hutuaminisha kuwa tuko sawa na wao. Hutuaminisha kuwa wanatutumikia sisi siyo kututumia. Wanahubiri usawa na kutenda ubaguzi. Picha hiyo hapo juu anaonekana makamu wa rais Samia Suluhu Hassan akichoma nyavu haramu. Hilo ni jambo jema. Ukiangalia walioshuhudia wote hawajafunikwa pua zao. Aliyefunikwa ni makamu wa rais. Je yeye na hao wanaoshuhudia wako sawa? Je ana aleji? Je wanaomshauri Makamu wa rais wamempa ushauri juu ya madhara ya kujionyesha kama binadamu zaidi ya wenzake. Sijui kama bosi wake rais Magufuli angefanya hivyo.