The Chant of Savant

Thursday 29 September 2011

Mbunge Lusinde anavuta bangi?

mbunge wa Mtera livingstone Lusinde akimtambulisha mgombea ubunge wa CCM Igunga Dk Dalaly Kafumu huku Lugubu Itumba Igunga Tabora

UHUNI ni kutenda tofauti na ulivyotegemewa kutenda. Kwa mfano, mtu mzima akifanya mambo ya kitoto huitwa mhuni. Je, mbunge anapotenda kama mvuta bangi wa kawaida tumuiteje? Inachanganya hasa kwa msikilizaji au msomaji anaposhindwa kutofautisha maneno ya mheshimiwa mbunge na mpiga debe wa daladala pale Mwenge.

Kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora zimezua mambo. Ukiachia mbali Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuja na mpya ya kuhonga wapiga kura ubwabwa, huku kukiwa na fumanizi la mwaka linalodaiwa kumhusisha kigogo wake wa fedha, Mwigulu Mchemba, vituko vingi vimejitokeza. Hii ni aibu kwa chama kinachojiita mhimili wa usawa, haki na maendeleo ya taifa.

Kituko kitakachojadiliwa hapa ni maneno ya Mbunge wa Mtela, Livingstone Lusinde. Wahenga wanasema mchezo mbaya ni kazi mbi. Na mzoea vya kunyonga, vya kuchinja haviwezi.

Lusinde anasifika kwa kumng’oa madarakani kigogo wa siku nyingi wa CCM, John Malecela, ambaye amewahi kushika nyadhifa nyingi kuliko mwana-CCM yeyote aliye hai.

Hata hivyo ushindi wa Lusinde haukuja kirahisi na kistaarabu ukiachia mbali mizengwe na vita ya kimakundi. Lusinde anakumbukwa jinsi alivyokuwa akitumia maneno ya kihuni dhidi ya mkongwe Malecela, jambo ambalo linaonekana kuwa kasumba kiasi cha kumtukana Dk. Willibrod Slaa.

Kinachoshangaza ni ile hali ya Lusinde kuendeleza matusi hata baada ya CCM kuushutumu upinzani kufanya hivyo. Kinachoshangaza zaidi ni ukweli kwamba Lusinde huyuhuyu alithaminiwa na CCM baada ya kuisaliti CHADEMA chama kilichomfikisha hapo alipo.

Ajabu ya maajabu ni pale CCM ilipodai wapinzani wanaendesha kampeni chafu wakati kiongozi wa kampeni chafu ni CCM yenyewe.

Hivi kuwahonga wananchi ubwabwa ni matusi ya nguoni kiasi gani?

Twende kwa Lusinde anayeitwa mheshimiwa mbunge, ingawa hana hiyo heshima wala kuistahili kama atasikilizwa na kuchunguzwa vilivyo. Hebu soma nukuu hii: “Hapa nimewaona waandishi wa gazeti la Mbowe (Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA); nataka mkaandike kwa namna ambavyo tumezunguka, CCM tukishindwa nakunywa sumu,” alisema.

Je, huyu anayeitwa mheshimiwa hajui kuwa kujiua ni kosa la jinai? Je, anatoa funzo na picha gani kwa Watanzania? Je, asipotimiza hili afanywe nini? Je, ana vigezo gani kuwa CCM itashinda? Je, kuna mbinu ya kuchakachua ambayo Lusinde anaijua kiasi cha kujipa uhakika wa mia kwa mia kuwa watashinda pamoja na kuvuruga kampeni kwa kufumaniwa na kushindwa kutangaza sera zao? Je, CHADEMA hili wamelichukuliaje? Je, wananchi hasa wapiga kura wanalichukuliaje hili? Ajabu CCM imeshindwa hata kumkemea!

Lusinde hakuishia pale kuonyesha uhuni wake. Alikaririwa akisema, “Nataka tuwaambie, tutawapiga bao la mbali kabisa na huyo Dk. Slaa sisi tunammudu ndiyo maana tukamwambia mzee Kikwete, endelea kuongoza nchi atuache vijana tumkabe koo maana yule mzee ni mnafiki mkubwa.”

Hivi huyu Lusinde hajui kuwa kumuita mtu mnafiki ni kumkashifu waziwazi? Sijui kiwango cha elimu cha kiumbe huyu. Ila kwa aliyokaririwa akibwabwaja, kuna uwezekano hana elimu ya kutosha na kama amefika hata chuo basi ni wale wanaobebwa au kuingia kwa namna kama siyo kughushi kama mawaziri waliotamalaki kwenye baraza la sasa la mawaziri waliotuhumiwa na Keinerugaba Msemakweli.

Hebu tuendelee kumchambua Lusinde. Ukiachia nukuu mbili hapo juu, Lusinde alikaririwa akikazia kinachoweza kuonekana kama uhuni kwa kusema: “Kale kazee kagonjwa kale, ndiyo maana nimekuja kuwaambia inawezekana viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi, zile bangi zile, haiwezekani unatembea nchi nzima unahamasisha vurugu, unatangaza vita.”

Ajabu Lusinde, mjumbe wa NEC wa CCM, Je, Lusinde anaweza kuthibitisha madai kuwa viongozi wa CHADEMA wanavuta bangi na amejuaje wanavuta bangi kama yeye havuti? Je, ni viongozi wangapi wa CCM wavuta bangi? Tunauliza swali hili kutokana na Lusinde kuonyesha kipaji cha kuwajua wanasiasa wavuta bangi.

Je ikibainika kuwa viongozi wa CHADEMA si wavuta bangi, Lusinde ataweka wapi uso wake ukiachia mbali kuchukuliwa hatua za kisheria? Je, hizi ndizo sera za vijana wa CCM ambao kutokana na maneno ya Lusinde wanaonesha uhuni na umalaya kutokana na fumanizi la Mchemba?

Leo hatutaandika mengi zaidi ya kuhitimisha kwa kusema kuwa: kwa maneno yake Lusinde, Mbunge wa Mtera, amethibitisha yametuchanganya kushindwa kumuweka kwenye kundi la wahuni na washamba wa siasa wanaopaswa kupelekwa jando au unyago wa kisiasa haraka sana ili kuona mwanga.
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 28, 2011.

Bastola ya Rage angeonekana nayo Lema…


KITENDO cha hivi karibuni cha mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, cha kupanda jukwaani na bastola kiunoni, si cha uungwana hata kidogo na hakiwezi kupita bila kujadiliwa.

Jaribu kufikiri. Kitendo hiki cha kihuni kingetendwa na mwanachama au mbunge yeyote wa upinzani kama Godbless Lema, Zitto Kabwe, Halima Mdee (CHADEMA) au David Kafulila wa NCCR Mageuzi, polisi wangehaha vipi kumweka ndani? Majibu mnayo.

Nije kwenye hoja yangu. Kumiliki au kutomiliki bunduki kwa Mtanzania ni haki ya kila mmoja kulingana na masharti na vigezo vilivyowekwa ili kuwezesha mtu kumiliki silaha.

Kitendo cha Rage kupanda jukwaani na bastola kuomba kura kwa ajili ya chama chake kilikuwa na lengo ama kuwadharau au kutishia usalama wapiga kura. Bastola kwenye mkutano wa hadhara wenye ulinzi wa polisi ya nini? Jamani Igunga si Mogadishu.

Bahati mbaya Rage na wenzake wanaona fahari kuwa na silaha viunoni. Na hii imejionesha hata kwa wabunge wenzake, Aeshi Hilal (CCM) Sumbawanga na Ester Bulaya (CCM) Viti Maalumu ambao ama kwa ulimbukeni au kwa uzuzu wa kumiliki bastola, waliripotiwa kufyatuliwa risasi hewani usiku wa manane.

Ingawa kujilinda ni haki ya binadamu, bunduki zinapotumika kutishia amani zinapoteza maana ya kujilinda na kwenda kwenye kuhatarisha usalama.

Tanzania siyo Somalia ambapo usalama wa mtu uhakikiwa na mitutu iliyomzunguka. Kitendo cha Rage kugeuza bastola kuwa kivutio na kitu cha mzaha kinapaswa kuziamsha mamlaka na kumfutia leseni ya kumiliki silaha hiyo.

Maana kwa tabia aliyoonesha ni wazi kuwa hana sifa za kuruhusiwa kumiliki silaha.

Kwa wanaojua umuhimu wa bastola, imetengenezwa kwenye umbo dogo ili kuweza kufichwa kirahisi kiasi cha kutomstua adui au watu wengine mwenye kuwa nayo anapokuwa nao. Mkutano wa hadhara hauna tofauti na baa. Unapoingia na silaha bila kuwa na mamlaka kisheria ya kufanya hivyo, unatishia amani.

Hii ni hatari kwako na wale waliokuzunguka. Hili ni kosa linalotosha kumsababishia mwenye kumiliki silaha kunyang’anywa haki ya kuwa nayo ukiachia mbali kufunguliwa mashitaka mengine yaendanayo na kutumia vibaya silaha na kutishia amani.


Kimsingi, kumilki silaha si haki kwa maana ya ‘right’ bali ‘privilege’, yaani haki ambayo haiwezi kudaiwa mahakamani.

Sasa tujiulize. Rage alikuwa anawahofia maadui wapi iwapo watu aliolenga kuongea na kuwa nao walikuwa ni wapiga kura? Je, Rage aliamua kwa maksudi kupanda jukwaani na silaha ili kuwatisha wapiga kura? Hizi ndizo mbinu za CCM za ushindi?

Je, Rage alipopewa silaha hakufundishwa masharti ya kumiliki zana hii hatari? Je, kwa mazingira ya mkutano wa kisiasa, kweli kulikuwa na tishio au ulazima wa kuingia kwenye eneo la mkutano na kupanda jukwaani na silaha? Tunaipeleka wapi Tanzania?

Je, kitendo cha Rage hakiwezi kuiathiri CCM, kama itashinda uchaguzi, kwa kigezo kuwa wapiga kura walitishwa?

Uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki wakati kuna watu tena wapiga kampeni wanaingia kwenye mikutano na kupanda majukwaani na silaha viunoni. Maana kiakili ni kwamba mkutano wa kampeni ni sehemu ya amani ambapo wanaoruhusiwa kubeba silaha kwenye eneo hilo ni polisi tu na si vinginevyo.

Kwanini Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, ameamuru uchunguzi badala ya kumweka ndani kwanza huyu mvunja sheria? Hili halihitaji tafsiri za wanasheria. Kuingia kwenye ‘public gathering’ na silaha ni kuvunja sheria. Ni kosa la jinai ambalo mwenye kulitenda hupaswa kukamatwa na polisi na kuchukua maelezo yake na kumfungulia mashitaka. Je, kwanini polisi hawakumkamata na kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa kisheria hadi bosi wao achukue hatua?

Je, polisi wa namna hii wasiojua hata wajibu wao au kama wanaujua na kuwagwaya mabosi wao wanaweza kuaminika kusimamia uchaguzi bila kuibeba CCM? Maana kwa kitendo cha kumfumbia macho Rage ni ushahidi tosha kwa polisi kuwa wanalalia upande wa CCM?

Kwa tabia waliyonesha polisi, imewaondolea heshima na imani kiasi cha kuonekana wahuni kama kina Rage na wenzao wanaodhani silaha ni mwanasesere kwa watu wazima wenye akili za kitoto kuchezea mbele ya kadamnasi kama ilivyotokea Igunga.

Binafsi nalaani kitendo hiki cha kihuni na kigaidi. Tanzania tunapaswa kujiepusha na siasa za kijinga za Somalia, Afghanistan, Pakistan na kwingineko kwenye vurugu kutokana na ujinga wa wachache kukabidhiwa silaha. Rage awe fundisho kwa wengine wenye agenda za siri za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kijambazi.

Ni hatari kwa kitendo cha kihuni kama hiki kutendwa na mtu anayeitwa mheshimiwa mbunge wakati hana wala hastahili. Utastahilije heshima wakati umeshindwa kujiheshimu?

Kuna haja ya kuibana wizara ya mambo ya ndani ili itoe maelezo yanayoingia akilini badala ya kuunda tume za ujanja na ukweli wakati kosa lililotendeka halihitaji tume bali kumweka ndani mhusika na kumfikisha mahakamani.


Chanzo: Tanzania Daima Septemba 28, 2011.

Ukitaka utajiri saidia ukwepaji kodi TRA

NIMEANZISHA Kampuni ya Twalakodi kwa Raha Account au Taint Revenue Ashaming (TRA) baada ya kugundua kuwa kumbe kusaidia watu kukwepa kodi ni utajiri wa haraka kwa baadhi ya waroho na wezi.

Mpayukaji nimeanzisha kampuni ya TRA ili kusaidia serikali ya Bongolalaland kukusanya kodi vilivyo kwa njia ya kuruhusu watu binafsi kuweka kodi mifukoni mwao kwa niaba ya serikali.

Kwanza nikuonye. Ili kufanya hii biashara ya kula kodi ama uwe kigogo serikalini au unajuana na kigogo. Maana rafiki, mke, mtoto au mramba viatu wa kigogo naye ni kigogo. Upo hapo? Ukiona dogo watoto wa wakubwa nao wanakuwa wakubwa, usianze kutafuta mchawi au miujiza kwa matapeli wa Jangwani, Mwenge, Mikocheni na kwingineko.

Hayo ya makando kando ya vigogo tuachane nayo na kuzama kwenye kampuni yangu mpya.

Kampuni yangu itakuwa ikifanya upelelezi na kuuliza maswali. Kwa kuanzia, tuko tunafanya uchunguzi kutokana na ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na waziri mkubwa mwenye Mizengwe ya Kupinda pinda ni kwanini makampuni kwa mfano ya madini yanalipa kodi kidogo kuliko hata yale ya pombe za kienyeji kama Chibuku? Hili ni swali muhimu la kuuliza na kujiuliza.

Je, nyuma ya pazia kuna wezi wenye ushawishi wanaolipwa kodi kwenye akaunti zao za siri kule Jersey na Island of Man? Je, maofisa wetu wadogowadogo nao wanapata kitu chochote kuwasaidia hawa wachukuaji wanaoitwa wawekezaji kuchukua chao kilicho chetu kinachoitwa chao na makahaba wao wenye ulaji?

Kuna uwezekano na hili likawa ni ukweli kutokana na uchunguzi uliofanywa na Dk. Msomi Mkatatamaa (si daktari wa kughushi kama wale washenzi wenye ulaji) na kugundua kuwa kumbe maofisa wengi wa Twalakodi kwa Raha Account pamoja na udogo wa nyadhifa zao ni matajiri wa kutupwa. Kama si mchezo huu, utajiri na ukwasi huu wanaupata wapi?

Tumegundua kuwa wafanyakazi wa TRA hata wawe wadogo kiasi gani ni walaji wazuri wa kodi ya wabongolalaland ya Danganyika. Wana mimali kama hawana akili nzuri. Wengine hawajui hata jinsi ya kutumia hiyo pesa wanayoipata kirahisi. Wengine hata ukisikiliza maongezi yao ni rushwa tupu. Anayebishia hili aende kwenye kampuni za simu na kuchukua nakala za maongezi ya viumbe hawa wenye akili ndogo lakini wanaofanya kazi kwenye ofisi yenye jeuri ya mshiko.

Hatutaishia kuhoji utajiri wa vijizi vidogovidogo vya TRA. Tutahoji hata wakubwa zao. Je, wao hawaoni mchezo huu? Kama wanauona na kuupuuzia wanafanya nini kwenye ofisi za umma? Je, wananufaika vipi na mchezo huu? Jibu lililoibuliwa na uchunguzi wa kisomi wa Mkatatamaa ni kwamba wengi wa waajiriwa wa TRA ni watoto au ndugu wa wazito waliomo sirikalini. Anayebishia hili aende mwenyewe kwenye ofisi za ulaji kama vile TRA, benki kubwa, mipakani, mita za kusoma mafuta, uhamiaji ambayo kwa sasa ni uhamishaji, atajionea mwenyewe.

Watajwa hapo juu kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi nilioamuru na kuwa chini ya mwenyekiti Msomi Mkatatamaa au Kamati Maalumu ya Kijiwe ya Mkatatamaa (KMKM), imebainisha kuwa wafanyakazi wenyewe wa TRA wanamiliki mali nyingi kama vile mahekalu, magari ya kifahari, mashamba na akaunti zilizoshiba kuliko walevi wengine.

Swali ambalo liliisumbua kamati ni kwanini sirikali haiwachunguzi hata kuwastukia? Jibu lilijitokeza kuwa katika nchi ya majizi, watoto na marafiki au jamaa za wakubwa huwa hawachunguzwi wala kushughulikiwa hata kama wanajulikana. Wapo wanaouza bwimbwi achia mbali kukwepa kodi. Wapo wanaokula kodi bila kujali wanaoilipa. Wapo wanaofanya vitu kama vichaa wasijue balaa wanalotengeneza.

Kijiwe kimeamua kuchunguza ili kuwasaidia pia kuusaidia umma kuepusha machafuko huko tuendako. Hivyo basi, wahusika wasidhani tunafanya hivi kuwachukia au kuwatibulia. Tunafanya hivyo kuepusha kaya na maafa yatokanayo na watu kukata tamaa baada ya kuibiwa na kunyonywa sana. Niliyashuhudia kule Masri, Libya na Tunisia. Hivyo, kinachofanyika ni uzalendo uliotukuka.

KMKM ilishangaa kukuta vijana wadogo walioingia kazini chini ya miaka kumi kuwa na mimali ya kutisha huku sirikali ikisema hakuna fedha. Fedha za kufanyia mambo ya maana kama kuwatoa walevi kwenye umaskini hakuna. Ila pesa ya wezi wachache kutumbua ipo tena kwa sana. Tazama yale madini na wanyama vinavyovushwa kila siku huku walevi wakiendelea kusota.

Tazama ajira zinazokwenda kwa wabangaizaji wenye uhusiano na wakubwa. Tazama uchukuaji unaoitwa uwekezaji. Tangu lini mtu akawekeza kwa kuchukua au kujenga kwa kubomoa? Kama wao ni vipofu na matahaira kiasi hiki, kiasi cha kutoona balaa hili, kijiwe kimeliona.

Pamoja na kamati kuchunguza ukwepaji wa kodi, nimeiamuru iwachunguze wafanyabiashara hasara ya siasa na biashara. Ingawa mkuu aliwahi kusema kuwa wahusika wachague moja, kumbe ulikuwa usanii. Tangu aseme hivyo amefanya nini kulikomesha hili wakati tunaona wafanyabiashara wengi tena wa bwimbwi wakizidi kuvamia siasa? Kuna siku nitaamuru yeye na familia yake wachunguzwe. Sitajali kuwa tarumbeta lake, Rweyependekeza atatutukana kuwa tu wambea na wenye husuda. Ikifika siku ya siku nitamchunguza potelea mbali liwalo na liwe.

Leo sichongi sana. You know what? Nawahi aepoti ya uwanja wa ndege kwenda kutanua Nuyoko na shosti wangu. Ukitaka kujua miujiza nenda TRA.

Chanzo: Tanzania Daima Septemba 28, 2011.

Tuesday 27 September 2011

Mwanamke ahukumiwa kwa kuendesha gari!

Je mwanamke akivaa hijab anaruhusiwa kuacha mikono yake wazi hadi tuone bangili na saa? Je hijab ni ushungi au kile kinachomstiri kiwiliwili chote?
Je huyu naye kavaa hijab au ninja, mbona kabla ya mapinduzi ya Iran hatukuwahi kuona maninja kama hawa?

Je hao wawili hapo wamevaa hijab au mavazi ya makabila fulani?


Mahakama moja nchini Saudi Arabia imemhukumu mwanamke mmoja kuchapwa bakora kumi kwa kosa la kuendesha gari.Kituko hiki cha aina yake kilitokea wakati nchini Tanzania kuna fukuto la baadhi ya viongozi wa kiislamu kujiingiza kwenye kumtetea mkuu wa wilaya ya Igunga kwa kuvuliwa mtandio ambao wao wameutafsiri kama hijab! Viongozi hawa wa kujipachika wamesikika wakikitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwaomba msamaha utadhani wao ndiyo waliovuliwa hiyo hijab! Je hii inasababishwa na kukosa kazi, elimu ya kutosha au ajenda ya siri? Kwanini hawa "mashehe" wasivue majoho na kuvaa magwanda ya kisiasa kwa kuanzisha chama chao badala ya kujificha nyuma ya uislam? Je hawa hawautukanishi uislam kama wenzao wa Saudia?

Wakati huku kwetu uislam ukitumika kumtetea mwanasiasa ambaye hata dini yake haswa haijulikani kutokana na aina ya maisha anayoishi, waislam wenyewe wanamdhalilisha mwanamke kwa kumwadhibu kwa kufanya kitu ambacho ni halali na haki yake!
Kweli dunia ina vituko. Je hapa tatizo ni uislam,wahusika kutoujua uislam, siasa au unafiki? Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

Sunday 25 September 2011

HAPPY BIRTHDAY NKUZI



Jana tarehe 25 Septemba kijana wetu Nkuzi Mhango aka Kapayukaji alitimiza mwaka mmoja. Kweli siku hazigandi. Kwani ni kama jana. Jamaa na marafiki walikusanyika kuanzia wenye umri wa miaka miwili hadi 87. Marafiki waliovunja rekodi ni Riadh Salih Hassan toka Darfur ambaye aliwakilisha wazee kwani ana miaka mwili. Naye kijana George Enns toka Kanada aliwakilisha vijana kwenye umri wa miaka 87. Sherehe zilifanyika Altona MB Kanada nyumbani kwao. Habari ndiyo hiyo.

Thursday 22 September 2011

CCM ijifunze toka Zambia



Hayawi hayawi huwa! Rais aliyeko madarakani nchini Zambia Rupia Banda amebwagwa vibaya na kiongozi wa upinzani Michael Sata baada ya jaji mkuu wa Zambia,Ernest Sakala kumtangaza mshindi . Ingawa watawala wa kale na wapya wa Afrika hawatabiriki, huu ni ushindi kwa upinzani barani Afrika.

Kushinda kwa Sata ni somo jingine kuwa hata kama Afrika imeshindwa kuwapindua maimla wake kama walivyofanya waarabu wa Afrika, inaweza kutumia sanduku la kura. Wengi wa watawala wezi na wababaishaji wamekuwa wakiwekeza kwenye hongo na wizi wa kura kusalia madarakani kama ilivyotokea Tanzania, mambo yanazidi kubadilika.
Kuna jambo moja la kuwapongeza Zambia kwalo. Wazambia siku zote wamekuwa mbele kwenye kuleta mageuzi huku na watawala wao wakiwa wakweli ikilinganishwa na wezi wenzao kwenye nchi nyingine.

Rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda mnamo mwaka 1991 aliahidi uchaguzi huru na wa haki na akatimiza ahadi yake kwa kushindwa na kukubali kushindwa. Historia ina tabia ya kujirudia. Rais anayeondoka madarakani Banda amerudia alichofanya Kaunda. Tunawapongeza wazambia huku tukiwaomba watanzania kujifunza toka Zambia. Kwa watawala mafisadi wa Tanzania, ni wakati wa kutia maji pale mwenzao anaponyolewa. Hongera Satta na Hongera Zambia. Muhimu tusingetegemea uoza wa Fredrick Chiluba kujirudia. Tusingetegemea aibu ya Bakili Muluzi, Bingu wa Mutharika au Abdulaye Wade kutokea. Kila la heri Zambia. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA

CCM inapoendekeza njaa na hongo


Kitendo cha kuwahonga wapiga kura wali ni cha kulaaniwa. Huu ni ushahidi wa rushwa, ufisadi na kufilisika kisiasa. Aliyebuni na kutenda jinai hii ni hatari kwa usalama na mstakabali wa taifa kuliko hata Ukimwi. Hatuwatukani. Wananchi wetu wamegeuzwa wadudu na hayawani wapwakizi wa kila upuuzi kiasi cha kufikiri kwa matumbo badala ya vichwa. Jinai hii ingetendwa na wapinzani ingekuwa nongwa. Ni kuwadharau wapiga kura kiasi gani kiasi cha kuwapa ubwabwa ili watoe haki yao ya miaka mitano? Kama hali halitoshi, mkuu wa fedha wa CCM Mwigulu Machemba amenogewa kiasi cha kufumaniwa na mke wa mtu. Haya ndiyo matokeo ya siasa za kifisi na kipanya ambapo kila mtu huangalia atakula nini badala ya atapata nini kisera. Kuna haja ya kuishinikiza CCM kuacha mchezo huu mchafu wa kila fisi kujaribu mbinu zake za porini. Ni mawazo mgando kiasi gani kupata kura kwa gharama ya chakula? Utawasikia CCM wakijisifu: tumeweka, tumechukua waaa! Upuuzi mtupu! Hii ni kuua na kudhalilisha dhana nzima ya demokrasia ya vyama vingi. Kuna kila sababu ya kupambana na jinai hii kama kweli tunalenga kulikomboa taifa.

Wednesday 21 September 2011

Richmond, recycling, kujuana na uteuzi wa Kikwete

HAKUNA ubishi kuwa uteuzi wa wakuu wa mikoa na upanuzi wa ukubwa wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete umewashangaza wengi. Na hii si mara ya kwanza kwa Kikwete kuonyesha anavyotenda tofauti na ahadi zake.

Kwa wanaokumbuka, Rais Kikwete wakati wa kampeni za kuwania urais mwaka 2005, aliahidi kuunda serikali ndogo ili kuokoa kodi za wananchi. Lakini punde tu baada ya kuingia madarakani, alijipiga mtama na kuunda serikali kubwa huku akiunda wizara zisizo na ulazima nyingi tu. Kikwete hakuishia hapo.

Alinogewa na mchezo huu uliompa sifa kwa baadhi ya watu bila kujali madhara kwenye uchumi wa nchi. Aliongeza idadi ya mikoa na wilaya bila kuja hata ahadi zake za awali. Hili la kutojali hali ya uchumi wa taifa na ulaghai yamekwisha kuzoeleka.

Katika uteuzi wake wa juzi, Kikwete kwa mara nyingine aliandamwa na jinamizi la kashfa ya Richmond iliyomng’oa rafiki yake, Edward Lowassa, waziri mkuu wa zamani aliyegeuka hasidi wake mkuu. Baada ya kuondoka Lowassa na baadhi ya mawaziri waliotuhumiwa kuwa nyuma ya kashfa kubwa, Kikwete ‘alisuka’ baraza la mawaziri upya. Katika kufanya hivyo, aliwalipa fadhila wakombozi wake wawili, yaani Spika wa zamani, Samuel Sitta na mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kuchunguza Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe.

Kikwete alisuka baraza la mawaziri upya baada ya kupoteza mawaziri wa zamani waliokuwa ima wamepoteza udhu au kuhusishwa na kashfa mbalimbali, wakiwamo Basil Mramba, Ibrahim Msabaha, Nazir Karamagi, Kingunge Ngombale - Mwiru, Juma Ngasongwa, Anthony Diallo, Joseph Mungai, Zakhia Meghji na Andrew Chenge.

Hawa wawili walipewa uwaziri kutokana na kutimiza majukumu mawili kwa Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Jukumu la kwanza ilikuwa ni kumtwisha Lowassa zigo lote la kashfa ya Richmond kiasi cha baadaye Dk. Mwakyembe kusikika akisema kuwa kama wasingeficha baadhi ya mambo serikali nzima ingeporomoka badala ya ‘bangusilo’ Lowassa.

Jukumu la pili ilikuwa ni kwa Sitta na Mwakyembe kuvuruga mipango ya kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii. Ingawa hatuwezi kueleza kuwa walikubaliana, bila shaka mazingira yanaonyesha hivyo, hasa baada ya wale waliodhaniwa kuwa wapambanaji dhidi ya ufisadi ghafla kupewa vyeo na kuufyata. Hii ndiyo awamu ya kwanza ya Richmond kwenye uteuzi wa Kikwete.

Jukumu la tatu lililotokana na kuteuliwa Sitta na Mwakyembe ni kuanza kuonekana uhasama wa wazi baina ya kambi ya Kikwete na ya Lowassa. Wengine huita kambi hizi mitandao.

Awamu ya pili ya jinamizi la Richmond ilijitokeza hivi majuzi wakati wa uteuzi wa wakuu wapya wa mikoa, ambapo mjumbe machachari wa kamati ya Mwakyembe Injinia Stella Manyanya aliteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Ukiachia mbali uteuzi wa jinamizi la Richmond, kuna kile tunachoweza kuita ‘recycling’ na kurithishana ulaji. Hivi haishangazi kuona kuna Nchimbi waziri na Nchimbi mkuu wa mkoa? Hapa kuna nini kama si kujuana?

Katika ‘recycling’ tunamaanisha uteuzi wa watu walioshindwa kwenye ubunge kama vile Mwantumu Mahiza, Joel Bendera na Ludovick Mwananzila. Hili lilithibitika zaidi pale baadhi ya wakuu wa mikoa waliostaafu kusemekana eti watapangiwa kazi nyingine, ambao ni Bibi Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela aliyekuwa Dodoma; Abeid Mwinyimusa aliyekuwa Tabora na Daniel ole Njoolay aliyekuwa Rukwa. Kazi gani baada ya kustaafu kama si kulea kundi la political Jay-walkers (sina Kiswahili chake).

Ukiachia mbali ku-recycle, kuna kuzidi kuendeleza mfumo wa zamani wa kiujima wa kuteua wanajeshi kwenye ukuu wa mkoa na wilaya.

Hapa hatujaangalia wengine wanaotia kila aina ya shaka jinsi walivyofika hapo. Si ajabu siku moja tukaambiwa wengine walikuwa mashoga wa mke wa rais hata marafiki zake wa utotoni na mambo mengine kama hayo.

Kutokana na tabia hii ya ajabu ya rais, baadhi ya watu wamefikia mahali kutabiri kuwa hata mawaziri walioshindwa kwenye uchaguzi kama Lawrence Masha tusishangae wakapewa ubalozi hata ukuu wa mkoa.

Hapa hujaongelea wengine wasio na mbele wala nyuma kisiasa, watakaoteuliwa kuwa wakuu wa wilaya, kulipwa fadhila kutokana na kutoa baadhi ya huduma halali na haramu. Hayo tuyaache.

Leo tumeangalia jinsi jinamizi la Richmond linavyoandama uteuzi wa Kikwete. Akifanya uteuzi wa wakuu wa mikoa iliyobakia na wilaya, tutakuja na uchambuzi kuangalia msukumo wa kufanya vile hasa kujuana. Pamoja na yote, wengi wanajiuliza, Kikwete atajifunza lini na atakumbukwa kwa lipi la maana zaidi ya kuwa muhimili wa ufisadi na kila aina ya madudu?

Chanzo: Tanzania Daima Septemba 21, 2011.

Mpayukaji ateua wakuu wa mikoa wa kijiwe!

MWENZENU jana niliota ndoto ya maana sana. Niliota nikiwa mkuu wa kaya. Niliota mie na bi mkubwa tuko Ikulu tukitanua na kuhudumiwa kama wafalme. Pia niliota bi mkubwa ameanzisha NGO na kila wafanyabiashara na wenye fweza walikuwa wakiichangia kama hawana akili nzuri. Niliota bi mkubwa wangu amechana na kujitona midhahabu kama hana akili nzuri.

Yawezekana niliota ndoto hii kutokana na jana ya usiku wa ndoto yenyewe kusimamia kikao cha kijiwe kujadili uteuzi wa ulaji wa wakuu wa mikoa uliofanywa na mkuu. Tulikuwa tukijadili jina moja baada ya jingine kuanzia wale wanaolipwa fadhila za mazabemazabe ya Richmonduli, waliochuja na kupachikwa viraka, watoto wa wakubwa wa zamani, mashoga wa bi mkubwa, nyumba nonihino za zamani za jamaa, ndata na vinara wa mitandao. Hivyo basi yawezekana kichwa kilirudia ngoa yangu juu ya jinai hii ya kupeana ulaji.

Nakumbuka. Baada ya kutangazwa idadi ya wakubwa wa mikoa, Msomi Mkatatamaa alitoa sentensi moja ya Kiingereza: “The same mess and blunders.” Hakufafanua ingawa sisi wajuzi wa ung’eng’e tulijua alichomaanisha kuhusiana na mkuu. Hayo tuyaache.

Leo nataka nisimulie ndoto niliyoota nikiwa kwenye maulaji kama mkuu ingawa asubuhi yake nilijikuta peupe nikikimbizana na ngwala ngwala kama kawa kuelekea mission town downtown kusaka uchache wa kununulia kauzi na sembe. Katika ndoto ile niliota nikiwa mkuu kweli kweli tena baada ya kushinda uchaguzi kwa kishindo.

Niliota eti baada ya kumalizika uchaguzi na baadhi ya washirika zangu kubwagwa, niliamua kuwapa ukuu wa kijiwe kwa ngazi ya mikoa. Pia katika ndoto hii wapo niliowapa ulaji kutokana na kuuokoa utawala wangu wakati ulipotaka kuangushwa na tume ya Mwakiwembe ambaye naye nilimpa ulaji kama shukrani.

Nadhani wasomaji bado mnaikumbuka kamati ya kijiwe ya Mwakiwembe iliyochunguza upoteaji wa kashata na mkaa ambapo waziri mkubwa kijiwe bwana Ewassa alitimuliwa ili kunioka mimi. Basi mwenzenu ndoto ya ukuu ilichanganyikana na yale yaliyotokea wakati wa kamati ya Mwakiwembe wakati ule Microphone wa kijiwe akiwa Sam Sixx ambaye naye ilibidi nimpe ulaji ili atulize kiherehere chake cha kutaka ukuu wa kijiwe. Six asiwazuge, naye nimempa ulaji baada ya kukubaliana asijiunge na Chama Cha Jeuri (CCJ) ambacho hapa kijiweni ni kundi la wanakijiwe wakongwe.

Katika ndoto hii niliota nikitoa ukuu wa mkoa wa kijwe kwa sister Stella Artois Matomatoes kutokana na kushirikiana na Mwakiwembe kuficha siri za kijiwe ambazo zilimaanisha kuangusha utawala mzima wa kijiwe na kuzihamishia kwa Ewassa.

Katika ndoto hii pia nimemteua Mwanatunu Baki Shemahiza na Joe Flag ili kuhakikisha wanakuwa kwenye ulaji wasije wakamwaga siri zetu. Niliota eti katika kuteua niliwapendelea washirika zangu hasa Ndata. Mnahabari mimi ni ndata kitaaluma. Nimepiga kwata sana kule Munduli na kupewa cheo cha Luteni Kano?

Niliota eti kuwa washikaji kama Fatie Mawasa na wengine ambao siwataji niliwapa ulaji ili nikitembelea vijiwe vya huko basi wanilinde.

Kuna kitu kilinikera na kunifedhehesha katika ndoto yangu. Nilifedheheka nilipogundua kumbe nilifanya makosa kuwateua watoto wa marafiki zangu na kuonyesha mfano mbaya wa kurithishana ulaji. Niliposoma majina kama Rehemia Nchimvi dada yake Emmy Nchimvi, Leo Gamaa na wengine wenye majina na koo kubwa nilijiona kama jinga vile. Lakini ningefanyaje iwapo nilikuwa nimeishapitisha?

Na kweli. Walevi watakuja kunistukia na kuniadhiri. Ukiangalia majina kama Mape Ninaye, Hoseni Muinyi, Jan Makambale na vitegemezi vingine ambavyo tumevipa ulaji sirikalini na chamani, unaweza kukubaliana nami kuwa kujisuta kwangu kuwa mimi ni wa hovyo ni kweli.

Baada ya kukumbuka blunder hii nilijiona dikteta kama M7 wa UG na Mutalaka wa Dziko la Bwino ambao waliwapa ulaji wadogo zao, watoto wao hata wake zao. Hata hivyo hatutofautiani ikichukuliwa kuwa Bi Mkubwa naye ana ulaji wake wa Ki-NGOs unaotokana na nafasi yangu ya kuwa mwenyekiti wa kijiwe.

Mie katika ndoto yangu nilimpiku Mutalaka wa Dziko la Bwino. Kwani yeye alimteua mdogo wake Peter wakati mie niliteua makumi ya watu wangu wa sirini na hadharani. Pia Mtalaka hana kitegemezi chake kinachotesa kwenye Chama chake kama mimi nilivyo na kitegemezi kinachotesa kwenye kijiwe changu cha kahawa. Mutalaka ana PhD ya kusotea wakati mie ninayo ya kugawiwa. Yeye alisotea mie nikapata kiubwete. Upo hapo mwanawitu?

Pia katika ndoto hii niliota tukimuangukiwa Kanji al maarufu Rostitamu yule Mhindi wa kijweni ambaye alisababisha upotevu wa mapesa kibao ya kahawa kwenye mchoro wa HEPA kipindi tukielekea kwenye uchaguzi wa kijiwe. Maskini wanywa kahawa hawakujua kuwa ponjoro huyu alitumiwa nami kutekeleza mchezo mzima ili nisijulikane na kuumbuka!

Huwezi kuamini kuwa niliota kuwa Dungong Denjaman Makapu Tunituni alikwenda sehemu sehemu akachafua hewa! Niliota nikimzaba makofi Tunituni kama yule jamaa wa Chama Cha Mafisadi aliyefumaniwa kule Igunga akila urodi wa kada wa chama chake.

Hawa jamaa wana hatari. Yaani kada anakula uroda wa mke wa kada na bado wanaendelea kuwa makada badala ya kukandamizana na mapanga! Kama ni njaa na dharau na kujidhalilisha na kudhalilishana huku kumezidi.

Mie naapa haki ya nani, hata kama ni nabii Suleimani. Nikikuta unakula urodi wa nke wangu napiga mipanga bila kujali kuwa naweza kunyongwa. Heri kunyongwa kuliko kuwa shahidi wa bi mkubwa kuliwa urodi wangu. Lo! Acha niachie mambo ya urodi hapa nisijeleta balaa kwa wasomaji. Kama mmeudhika mezeeni pia someni nisemayo na siyo niandikayo.

Ngoja niendelee kuwasimulia ndoto yangu. Niliota, kumbe kumekucha!
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 21, 2011.

Tuesday 20 September 2011

Wafe wangapi tustuke?

Ingawa ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islander huko Nungwi inaweza kuitwa mpango wa Mungu, ukweli si mpango wa Mungu bali uzembe, kutojali, ujinga, woga, roho mbaya na uroho wa binadamu.

Mimi siamini kuwa Mungu alitaka mamia ya watu wateketee. Hivyo basi, badala ya kumlaumu au kumtwisha Mungu mzigo, namlaumu mwanadamu hasa serikali kwa uzembe usio kifani. Mwaka 1996 Tanzania ilikumbwa na msiba mkubwa wa kuzama kwa MV Bukoba. Wengi walidhani hili lingetustua na kutukumbusha kuwa kuna haja ya kufuata taratibu, kanuni na sheria hasa kuzingatia haki ya kuishi ya mwanadamu. Ni ajabu na bahati mbaya kuwa hatukujifunza.

Katika mkasa huu huwezi kulaumu serikali peke yake. Hata raia wa kawaida wanaokubali au kulazimika kujazwa kama dagaa kwenye vyombo vya usafiri nao wana sehemu yao ya lawama. Kwa mujibu wa masimulizi ya manusura ni kwamba hali ya meli na jinsi ilivyokuwa imepakiwa mizigo na watu kupita ujazo vilikuwa wazi kwa kila mtu. Ni bahati mbaya sana kuwa watu wetu wamekubali kutendewa kama wafadhiliwa hata wanapolanguliwa na kukamuliwa na wenye kutoa huduma!

Nchi yetu ina mfumo mbovu wa kubanana karibu katika kila Nyanja za kimaisha. Ukiangalia kwenye nyumba za kupanga, magari ya abiria, bajaj, viwanja, madarasani, hospitalini na hata maofisini, tunasongamana na kuridhika na hali hii. Inatisha na kukatisha tamaa sana. Ukienda mahospitali kwa mfano, unakuta wagonjwa wanalazwa zaidi ya mmoja kwenye kitanda. Magerezani ndiyo usiseme. Ni kwenye nyumba za ibada tu ambamo hatubanani kutokana na kuibuka kwa madhehebu mengi na kupungua kwa waumini. Zaidi ya hapo kila sehemu ni kubanana. Ni ikulu tu ambapo hakuna kubana pakiwakilisha maofisi ya wakubwa yenye kila neema kuanzia viyoyozi, samani aghali na makandokando mengi.

Barabara zimejaa mikangafu na madereva feki huku wanaovunja sheria wakitozwa rushwa. Hali inaachwa iendelee bila kujali madhara yake hasa kukithiri kwa ajali za barabarani. Nani anajali iwapo wakubwa wanasafishiwa barabara wanapotaka kupita? Nani anajali iwapo wakubwa wanatumia ndege na si usafiri wa kawaida? Nani anajali msongamano na mbanano kwenye madaladala iwapo wakubwa wanasafiri kwa magari ya bei mbaya tena kwa kujinafasi? Hii ndiyo roho mbaya na uroho ninavyomaanisha kwenye makala hii.

Ukondoo au woga wa umma kutenzwa kama wasio na haki kwenye nchi yao ni sababu nyingine ya kuwepo kwa maafa kama ya kuzama meli huko Nungwi. Hakuna ubishi. Wasafiri wa meli husika waliona fika kuwa meli ilijazwa sana lakini waliogopa kujitetea kwa kuanzisha hata vurugu kuzuia kupakiwa kama wanyama au watumwa. Hawa kimsingi hawajui haki zao na kama wanazijua wanaogopa kuzidai. Huu ndiyo ukondoo na ujinga. Kondoo hunyenyekea hata kwenye machinjio. Binadamu hapaswi kutenzwa kama kondoo.

Tatizo jingine ni kukithiri kwa rushwa kama alivyokiri rais hivi karibuni kuwa kila sehemu kumetamalaki rushwa. Wenye vyombo vya usafiri na utoaji wa huduma nyingine wanapata pesa kiasi cha kuhonga wamtakaye na kwa kiasi cha fedha watakacho. Kama siyo ilikuwaje mamlaka husika hazikuwa na maafisa wa kuthibiti usalama kwenye bandari? Kimsingi, ni kwamba walikuwa. Lakini hawakuona hatari iliyokuwa inawakabiri wasafari wa meli ya Spice Islander kwa vile rushwa ilikuwa imewapofusha kiasi cha kuwauza wenzao. Sijui kama roho zao haziwasuti kwa dhambi waliyobeba kwa usaliti na uroho. Mara nyingi wanaomilki vyombo kama hivi wana uwezo wa kuvunja sheria bila kukamatwa kutokana na kula na baadhi ya watendaji wa serikali. Hawa wameifanya serikali kuwa mali yao na si mali ya wananchi.

Unafiki ni tatizo jingine hapa. Mwandishi anakumbuka maneno ya Katibu mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Kenya (Central Organization of Trade Unions (COTU) Francis Atwoli, aliyekaririwa akiwakemea wanasiasa waliokuwa wakimiminika kutoa salamu za rambi rambi kwa wakenya waliounga kwenye ajali ya moto uliotokana na kulipuka kwa bomba la mafuta kwenye kitongoji cha Sinai jijini Nairobi.

Ajali zinapotokea utawaona wanasiasa wakija na viapo na dua na maneno ya faraja wakijua fika kuwa wao wamechangia kwa kiasi kikubwa ingawa na wananchi kwa tabia yao ya ukondoo hawaikwepi dhambi hii. Atwoli aliwatuhumu watawala kwa uroho na kutokuza uchumi, kuondoa umaskini na kuwa na mipango mizuri kama vyanzo vya maafa kwa jamii inayoendeshwa na njaa na umaskini. Kwanini wanasiasa ambao wamekabidhiwa jukumu la kusimamia sheria hawatimizi wajibu wao? Hili ndilo lilikuwa swali kubwa la Atwoli. Je ni kwa sababu mara nyingi wao kutokana na nyadhifa zao hawakumbani na adha hizi hivyo haziwahusu?

Tatizo jingine ni ubinafsi wa kupindukia. Watu hasa wenye madaraka wanapoteza muda mwingi kwenye kuchuma kiasi cha kuwapuuzia wenzao na haki zao. Kama hili lingetokea kwenye nchi zilizoendelea, waziri wa uchukuzi hakuwa na kazi tena. Lakini nani atawajibika au kuwajibishwa iwapo wote hali ni ile ile? Utamsikia waziri akijitetea kuwa yeye hakuwa nahodha wa meli ile! Lakini iko chini ya wizara yake? Ubinafsi wa kupita kiasi utatumaliza. Hamkushuhudia waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania wakiendelea na sherehe zake ilhali wakijua taifa limekumbwa na msiba mkubwa? Nani anajali?

Mjadala huu hauwezi kuisha bila kugusia uzembe. Maovu yaliyotajwa hapo juu yana mama mmoja yaani uzembe. Nani angetegemea nchi yenye vyombo vyote vya dola, upelelezi na udhibiti kushindwa hata kujua idadi ya abiria waliokuwa wamepanda meli husika? Tunaambiwa 600, 800 na sasa imefikia kulipotiwa 3,00! Ukweli ni upi? Je huyu mwenye mali kama hakuwa na idadi inayojulikana kwa mamlaka zote husika, alikuwa anakatwaje kodi ya mapato? Je alikuwa analipa kiasi alichokuwa akitaka au kuna wakubwa walikuwa na ubia kwenye biashara hii kiasi cha kutolipa mapato? Namna hii kweli tunaweza kujikomboa kiuchumi?

Wafe wangapi tustuke iwapo waliokufa mwaka 1995 kwenye ajali ya MV Bukoba haikutustua? Laiti hada ndege ya rais ingekuwa inajazwa hivi au maisha yake kuwa ya msongamano huenda angeelewa hili. Lakini si hivyo. Yeye anaishi raha mstarehe tena kwa kodi za hawa hawa wanaoteketea kwenye misongamano.

Chanzo: Dira Septemba 2011.

Siku mlevi aliponusurika kifo cha bajaj ya ambulansi

Sijui niite zali la mentali au mentali ya zali? Nashindwa kuiita hii ndude bajaj ya ambulansi au ambulansi ya bajaj.

Siku hiyo gongo yote niliyokuwa nayo kichwani ilinitokea puani nikaona nilimuona Ziraili yule mjumbe wa kifo na makucha yake akitaka kuninyakua. Pamoja na kujeruhika kijogoo nilimkaripia Ziraili nikisema aende kwa mafisadi wanaofisha watu bila sababu.

Tuligongwa na kujikuta ICU nikiwa na michupa ya maji hewa na damu bila kujitambua. Badala ya kutundikwa michupa ya gongo si walinitundika ya damu utadhani mimi mumiani! Kweli shida mwanaharamu! Nani alidhani nguli wa gongo kama mimi ningekaa hospitali wiki mbili bila hata kuonja gongo? Aminini nilikaa kule na kuondoka na kunguni. Waweza kuamini tulikuwa tukilala watatu kitanda kimoja? Aminini ilikuwa hivyo.

Turejee kwenye masahibu yangu. Siku ya ajali ya kugongwa na gari la mwishiwa fulani aliyekuwa akiwahi kutanua na dogo dogo zake nilikuwa nimeutwika mma kama sina akili nzuri. Nilipata ile gongo ambayo huwa tunaipima kwa kibiriti. Nakumbuka. Rafiki yangu Shemboza alininunulia mapupu tukapata bangi kidogo ndiyo ngoma ikatoka kwenda home. Kufika maeneo ya Friends Corner na shangingi la shangingi wa kisiasa likanivaa mwanakwetu. Kilichofuatia ni kuletewa ambulansi ya bajaj. Wakati huo sikuwa nimepoteza fahamu. Nilimuangalia dereva mwenyewe aliyekuwa akiendesha hiyo ambulansi na kugundua kuwa hakuwa dereva kitu. Dereva mwenye aliooneka alipata leseni kwa kutoa rushwa kama alivyosema mkuu.

Tuache utani. Huwezi ukaamini kuwa hiki kituko kilitokea karne ya 21 ya sayansi na teknolojia kwenye nchi inayojidai kuwa mbele kimaendeleo miongoni mwa nchi zilizosahaulika katika maendeleo. Huwezi kuamini kuwa hadi ninapoandika yameishawakuta wengi makubwa kuliko haya. Hebu wafikiri jamaa zetu wa Zenj walionyongwa na mafisi wenye meli na maafisa wa bandari walioruhusu mkangafu ule kubeba watu zaidi 6,000. Baada ya kugundua yaliyotokea kwangu na baadaye niligundua kuwa kumbe teknolojia tunayoambiwa inamaanisha kitu kingine kabisa. Sikujua kuwa kumbe ni teke linalokujia toka kwa watawala ambao mie kwa gongo zangu huwaita watu wala watu. Wao wanapanda mashangingi kwenda kutanua na madege kwenda kuchunguzwa afya hasa mafua.

Tuendelee na masahibu yangu ambayo kimsingi ni ya walevi na makapuku wote. Nashukuru Mungu sikunyotoka roho. Baada ya kukaa hospitalini kwa wiki tatu na kuwekewa POP nilirejea nyumbani nikiwa nimepigika. Kwanza wajua maana ya piopio? Hii ni Plaster Of Paris kwa wale waliosoma uganga. Mie niliusomea udaktari lakini nikaamua kukatiza masomo baada ya walimu wangu kunionea wivu kwa nilivyokuwa nawazidi akili.

Mambo ya Piopio tuachane nayo. Baada ya kufika nyumbani ugonjwa wangu uliongezeka baada ya kugundua kuwa kumbe pesa ya kulipia matibabu yangu ilikopwa na mke wangu kwa mpemba muuza genge. Hebu fikiria. Umaskini huu! Yaani mke wangu Cha Utamu anakwenda kukopa pesa kwa muuza genge! Walikubalianaje na nini hadi muuza genge akawa mfadhili wetu. Hili hadi sasa linaniumiza roho hasa nikifikikumbuka mpemba huyo huyo alivyokuwa akitania kuwa siku moja atakuwa mkwe wa binti yangu Mwapombe. Kumbe aliyekuwa akilengwa si Mwapombe bali Cha Utamu aliyegeuzwa Cha Wote na umaskini! Wasomaji nishaurini. Ungekuwa wewe ungefanyaje?

Nakumbuka kipindi fulani baba mwenye nyumba alitaka kututolea vyombo nje. Mke wangu alijivuvumua na kulipa akidai kuwa alikuwa akicheza mchezo wa akina mama wa upatu. Je ni upatu au upato ambapo wenye nazo hupata toka kwa vitu vyetu tusio nazo? Je ni wangapi yameishawakumba au yatawakumba usawa huu ambapo ukapa na ukete vimealikana kutunyotoa roho? Huwa nikiangalia haya yote huwa natamani niwe kama wale jamaa wanaojitoa mhanga kwa kujifunga mabomu na kuwalipua wabaya wao. Mie kwa hasira nilizo nazo, kama nikiamua kuwa gaidi, nitakuwa radhi hata kujifunga bomu kumlipua kuku wako achia mbali wewe. Yaani jitu linatumia vijisenti vyake kumpata mke wa mnywa gongo! Inauma wajameni.

Sisi wanywa gongo tuna masahibu we acha tu. Si juzi jamaa yangu Shemtashua alimtaliki mke wake baada ya kudanganywa na mganga kuwa ana nuksi hivyo akienda naye faragha nuksi itamtoka. Bila kujua kuwa hakuna cha nuksi bali siasa nuksi jimama nalo likaachia na kuambulia talaka. Hayo tuyaache yana wenyewe.

Nirejee kwenye safari yangu ya kwenda hospitali. Baada ya kupakizwa kwenye kijimkweche ambulansi bajaj mara dereva akaondoa bajaj kwa fujo. Kwa vile barabara zenyewe zimejaa mikweche na mashimo, ilibidi akatize mitaa ya Mwembechai upande wa Makulumla. Kufika mitaa ya Kiyungi si akakutana na ngalangala linalotoka Uzuri kwenda Kariakoo likiwa wangu wangu. Kilichofuatia usiniiulize maana sijawahi kusimuliwa. Baada ya kufungwa piopio na kupata fahamu, pamoja na masahibu yangu hasa kukaa muda mrefu bila kuonja, nilianza kujiuliza maswali. Je hali hii itaendelea hadi lini? Je nchi hii ni ya nani kati ya sisi tunaoambiwa ni yetu wakati si yetu?

Hakuna kitu kinanisumbua kama ile pesa niliyolipiwa na mke wangu. Maana pamoja na kudhalilika kote huko, nilikuja kuponea kwa mchua mfipa na si hospitalini nilikotoka na ukurutu na kunguni kibao.

Kama kuna kitu kimeongezeka kwangu licha ya mihasira kutokana na urafiki wa bi mkubwa na muuza genge ni ile hali ya kusikia wanasiasa uchwara na matapeli wakijidai eti wameleta maendeleo. Haya ni maendeleo ya kwenda mbele au kurudi nyuma? Wakati wao wakihomola na kuwa matajiri wa mijumba, migari, mifugo na miakaunti nje, wamenimegea kunguni niliotoka nao kwenye hospitali ya kueneza badala ya kutibu magonjwa. Kibaya ni kwamba unalipia magonjwa haya na kunguni!

Nimalizie kwa kuwaletea habari njema kuwa nina mpango wa kwenda Pakistan kujifunza kujifunga mabomu ili nije niwalipue wanaosababisha upuuzi huu.
Msinichulie serious. Natania.

Chanzo: Dira Septemba 2011.

Thursday 15 September 2011


HIVI karibuni, Rais Jakaya Kikwete, alikiri waziwazi kuwa nchi inanuka rushwa. Alikaririwa akisema: “Sasa hivi kila kona rushwa, ukienda barabarani polisi wanaomba rushwa, watendaji wakuu wa serikali wanachukua rushwa na makandarasi nao wanatoa rushwa ili waweze kupata zabuni. Ni tatizo, lazima tuikemee, itatufikisha kubaya.”

Kukiri kwa Rais Kikwete kuwa nchi inanuka rushwa kila kona na idara, hakutoshi. Ni jambo la kufurahisha kuwa hatimaye rais amekubali kuwa serikali yake imejaa rushwa. Pia ni jambo la kuhuzunisha kuwa na rais mwenye tabia ya kulalamika bila kuchukua hatua. Kukiri na kulalamika haitoshi. Kinachotakiwa ni rais kuchukua hatua. Rais na wapambe wake ambao wamekuwa wakiwachukulia kama wachochezi hata maadui waliothubutu kusema hili. Sasa ni wazi kuwa maji yamefika shingoni.

Kama alivyokiri rais, ni kweli kwa sasa kila kona kuna rushwa. Ikulu kuna rushwa, bungeni kuna rushwa, mahakamani kuna rushwa hata makanisani.

Kwenye NGO kuna rushwa na hata Misikitini kuna rushwa. Kama rais analijua na kuliona hili, kwanini alalamike badala ya kuonyesha amefanya nini kupambana na uchafu huu anaokiri kuuona na kuujua? Je, kulalamika ni jibu au ulegelege ambao wapinzani wanausema kuwa serikali ya Kikwete inao?

Kwa ukumbusho tu, rais aliwahi kukiri mwenyewe kuwa ana orodha ya majambazi, wauza unga, wala rushwa na wahalifu wengine. Cha ajabu ni kwamba, pamoja na mamlaka aliyo nayo, rais hajawahi kuwashughulikia angalau hata mmoja. Sasa kama rais anakiri kuwa anawajua wahalifu tajwa na hawashughulikii, wananchi wasio na mamlaka wala vyombo vya dola wafanyeje? Je, hii haiwezi kuwa mwanzo na mzizi wa watu kujichukulia sheria mkononi huku wateule wake wakizivunja hata kudharau mahakama kama ilivyotokea kwa katibu wa ardhi, Patrick Rutabanzibwa?

Hebu tuangalie nukuu nyingine ya rais Kikwete, aliyekaririwa akisema: “Katika sekta ya ununuzi wa mali za umma ndiyo kabisa, wanaagiza mali za serikali kwa kuongeza gharama, kuweka cha juu, ili wakifanikiwa waweze kugawana huku wakifahamu kwamba fedha zinazotumika ni za serikali. Lazima watendaji kama hao waangaliwe kwa umakini sana kwa sababu wanaweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.”

Kumbe rais anajua hata sekta zinazokumbwa na mdudu rushwa kwa viwango vya kutisha lakini hachukui hatua! Swali linaloulizwa kila wakati ni kwanini rais hataki kuchukua hatua? Kwenye ngwe yake ya kwanza hakuchukua hatua. Hii ni ngwe ya lala salama. Je, rais atawashughulikia lini hawa wahalifu aliowageuza ‘souvenir?’
Mwandishi nguli, Mark Twain, alituachia wosia kuwa: “Ni heri kustahiki heshima ukaikosa kuliko kuwa nayo wakati hustahili.” Hatutaki rais wetu afikie huko. Maana kwa cheo chake na hadhi yake, si mtu wa kulalamika bali kutenda. Ingawa watu wakimkumbuka marehemu baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, wanaonekana kufikiri kurudi nyuma, ukweli ni kwamba alituachia urithi usio kifani.

Nyerere hakuwa mtu wa kulalamika lalamika bali kutenda bila kujali kuna watakaomlaumu au kumpenda. Yeye aliangalia haki badala ya upuuzi mdogomdogo kama kujuana na kuogopana.

Rais anapolalamika, licha ya kujidhalilisha, anatoa mwanya kwa wahalifu kuendelea na ‘business as usual.’ Maana wanajua alivyo legelege na mwoga. Hatutaki kuamini kuwa rais wetu ameshafika huko hata kama anaelekea huko au alifika zamani kutokana na haya tunayoshuhudia. Je, hicho ndicho kile alichosema Edward Lowassa, kuogopa kufanya maamuzi magumu? Je, haya ndiyo maamuzi magumu wazee wa CCM walimtaka rais afanye ? Kwanini rais anakuwa mwepesi wa kufanya maamuzi magumu angamizi kama kuendelea kuvumilia ufisadi na uhalifu mwingine? Je, rais wetu anataka akumbukwe kwa hili baada ya kuwa ametoka madarakani? Je, kuna namna rais ananufaika na jinai hizi yarabi? Sitaki kuamini hivyo hata kama ni hivyo.

Rais wetu ana mapungufu. Ni binadamu anayepaswa kupewa msaada. Leo tunaongelea kukithiri kwa rushwa kila sehemu. Inashangaza hata naye anahusishwa, si mara moja wala mbili, tena bila kukanusha na akifanya hivyo anafanya mzaha kama tulivyosikia juzi juu ya hongo za suti. Kuwa mke wa Kaisari hupaswi kutuhumiwa. Kutuhumiwa tu kunatosha kujiwajibisha. Kutofanya hivyo ni kuonyesha ni kwa jinsi gani mtuhumiwa asivyo msafi. Je, hii ndiyo sababu ya rais kuendelea kukalia ushahidi aliosema alipewa na wahusika anawajua? Je, anaogopa na yake yasifichuke? Bila kuja na utetezi wa maana kuhusiana na kadhia hii, makaripio na matusi ya watetezi wake hayatafua dafu.

Katika sakata la kushutumiwa kuhongwa kwa mfano suti tano, ningekuwa rais, mtu wa kwanza kumfukuza kazi alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, ambaye ametoa utetezi uchwara kwa mihemko badala ya kuingia kwenye madai na kuonyesha ukweli ni upi. Huwezi kumuita balozi mpuuzi bila kutaja upuuzi wake ni upi. Mbona mabalozi haohao wanapotoa misaada hamuwaiti wapuuzi? Dawa ya kuepukana na ‘upuuzi’ huu ni ‘ku-deliver’, badala ya kupuuzia kuwachukulia hatua mjaarabu wanaohujumu uchumi na taifa letu. Huwezi ukawa tegemezi, ukaotesha mapembe. Wanaokufadhili watayakata. Na isitoshe, uzoefu unaonyesha kuwa serikali ya sasa inapotuhumiwa, hurukia kuwaita wazushi, waongo na wapuuzi, wanaofanya hivyo.

Nani amesahau kuwa, Dk Willibrod Slaa, alivyoitwa mchochezi, mmbea, mpuuzi, mzushi na majina mengi mabaya kabla ya ukweli kuumka na kuwaacha watuhumiwa uchi wakivuana magamba? Kwa kuangalia historia hii, tukubali, tusikubali kwenye tuhuma lengwa kuna ukweli hata kama si mia kwa mia.

Nani mara hii kasahau ‘List of Shame’ ambayo imegeuka jinamizi kwa serikali na chama cha Kikwete huku naye akihusishwa? Haya ndiyo mambo ya kujadili kuangalia ni kwanini rais wetu anakuwa mtu wa kulalamika badala ya kuchukua hatua. Je, yeye ni salama? Je, nyumba yake na waliomzunguka nao ni salama? Tusimuogope wala kumdanganya kama watetezi na washauri wake. Wao wanatetea kitumbua, nasi tunatetea taifa.
Chanzo: Tanzania Daima Septemba 14, 2011.
WAHAMBA nathi (ulitembea nasi)
Oh wahamba nathi (oh ulitembea nasi)
Oh wahamba nathi, siyabonga (oh ulitembea nasi, twakushukuru)
Siyabonga Jesu (tunakushukuru Yesu),
Siyabonga ngonyama yezulu (twakushukuru samba wa mbingu)
Siyabonga Kakaramba- tunakushukuru mkuu

Nawashukuru walevi
Walitembea nami nawashukuru
Nawashukuru kwa ujinga wao
Nawashukuru kwa kuwauza kama Yesu
Nawashukuru mwamba wa dili mie
Nawashukuru kama mkuu
Mkuu naye anashukuru walevi na wabongolalalanders
Tunashukuru kuwalamba ninini lolo lolo lalalala

Mwanzenu baada ya kugundua kuwa kumbe kaya imegeuka kaya ya madili badala ya maadili, nami nimeamua kuchonga dili langu.

Soma taratibu akina mgosi Machungi wasikusikie wakatia kichumvi. Nina mpango wa kumuuzia kijiwe mwarabu fulani kibopa uchwara. Ameniahidi bonge ya msuli, suti, kandambili na makando kando mengine ya dezo.

Pia katika dili hili sitakula peke yangu. Bi mkubwa atanunuliwa bangili za shaba na batiki mtindo mmoja. Ili kuhakikisha tunajadili na kula vinono wakati wa dili husika, mwarabu ameahidi kutuletea tende na mafuta ya zeituni ili tukarangize nyama ya kijiwe. Ilikuwa atupe tiketi za ndege twende kujinoma kwa mama lakini tumeona hii ni kuharibu fweza bure. Sisi tutamalizia mambo yetu hapa hapa kayani bila kujali nani ataingizwa mkenge.

Mie nina usongo na njuluku na kuukata haraka. Kama atatokea anayetaka kununua watumwa sina neno. Nitapiga bei hata akitaka na wanywaji kahawa nao nawasha kulaleki!

Sijutii uamuzi huu. Kama wakuu wa Danganyika na Bongolalaland wanauza kaya kwa suti na upuuzi mwingine nina kosa gani kuwauza wanywa kahawa waliokwishapigika? Hivi ni kosa kwa fisi kuwararua kondoo au nyoka kung’ata kisigino?

Kama wengine wameuza wanyama tena kwa kuwavusha kupitia viwanja vya ndege vyenye kila ulinzi bila kufanywa lolote, mie nina kosa gani kuuza kijiwe. Ajabu wanyama walipotoroshwa eti walevi wakaambiwa eti hawajui walipelekwa wapi wakati hata wadudu wanajua kuwa walipelekwa umangani.

Sasa kama madege hata ya kijeshi yanaweza kuingia yakatua na kupaa hao uhasama wa taifa wanafanya kazi gani kama siyo kuiba kodi za walevi? Hiyo mamlaka ya anga inaangaza nini kama madege yanaweza kuja na kuzoa wanyama wetu yatakavyo?

Ajabu nyingine ni kuripotiwa kuwa yule ponjoro aliyewezesha dili hili ametoroka akiwa kwenye dhamana! Hii maana yake ni nini kama siyo kudharau mahakama na mapilato wake kama alivyofanya nshomile Ruta hivi karibuni. Ponjoro ametoroka au ametoroshwa ili wazito wasiumbuke ikizingatiwa kuwa yeye ni dagaa aliyekuwa ameletwa na mapapa.

Mara hii mmesahau sinema ya Chauda na uuzaji wa mashamba ya wagosi kule Tanga? Nani hajui kuwa Chauda alitoroshwa ili kulinda siri za wanene kama ilivyo kwenye zali hili la k utorosha mahayawani wetu? Kama rada na makompyuta yamechemsha, kwanini nisiuze kijiwe ambacho mlinzi wake ni Mungu mwenyewe? Huu ni wakati wa kuuza. Hii ni kaya ya kuchuuzana. Bila kuucha mtu au watu huukati bali utakukata.

Nitachofanya, nikishapiga bei kijiwe nachukua hisa kwenye biashara ya Mwarabu atakayoianzisha kwenye kijiwe. Hivi ndivyo wakubwa tunavyokula. Siogopi cha Weeklick au nini nauza tu.

Najua dili hili litapita na hakuna atakayenistukia kwa vile kwenye kijiwe hatuna mabalozi wa kuandika madhambi yetu na kutuma kwao kama jamaa aliyewalipua jamaa wa kuuziana taasisi kwa bei ya suti. Msijeninukuu vibaya. Mie sisemi yaliyosemwa ni kweli au uongo. Nitajuaje wakati madili yao hayanihangaishe isipokuwa hili langu la kuuza kijwe kwa kasi na ari, mori na nguvu mpya.

Wengi watasema naunza kijiwe kwa bei ya kutupwa kwa kuhongwa upuuzi kila aina. Hata wakiniona mie ni mpuuzi anayehongwa upuuzi mie najifanya sisikii. Nikiona wanoko wamezidi namtuma my waifu wangu Silvia kuwatukana wote wanaoishikia bango ulaji wangu. Nitamwambie awaite wapuuzi wao na mama zao.

Mi nilivyo na usongo wa fweza hata mtu akitaka kumnunua bi mkubwa namuuzia. Si bora mshiko bwana kuliko uchovu wakati unaona waliokuwa wachovu jana wakiukata na kuula?

Mie sina roho wala akili nzuri. Sina tofauti na wale jamaa zangu wa mlimani ambao huwaambia watoto wao: umekataa kuiba utakula mafi yako. Jamani nawatania hata kama ni kweli tumezee. Ndiyo mila zenyewe nyingine chafu au siyo meku upo hapo? Yethu mbesa kwanza.

Mie mbele ya fweza ni sawa na mbwa mbele ya nyama au fisi mbele ya fupa. Mie na Yuda hatuna tofauti. Sioni taabu kuzoea vipande thelathini na kumuuza mama yangu hata dingi yangu. Hebu fikirieni. Kama naweza kuwauza madingi wangu wanakijiwe ni nani niwaonee huruma wakati hawajionei huruma?

Kama dili langu litabumburuka wala sitawaita watakaokuwa wanituhumu kuwa wapuuzi. Watetezi wangu hasa bi mkubwa Silvia atasema tuhuma hizi zitalenga kunichafulia jina. Kwanini watakaonituhumu wanichafulie jina wakati nikijua fika hawawezi kugombea kuongoza kijiwe? Najua wenye akili watauliza: kwanini yeye na si wengine?

Najua wengi watanicheka kwa kuuza kijiwe kwa zawadi za misuli, tende na mafuta ya zaituni. Huo ndiyo uwezo wangu wa kufikiri hata ukionekana ni wa hovyo. Si ninauza change? Hata nikigawa kama wale wanaogawa madini na wanyama shauri yangu. Nyie yawahusu nini? Waache Wanakijiwe walalamike. Maana, ndiyo wenye mali. Hata hivyo nani anajali? Mali ya umma haiumi ati. Mmesahau mara hii. Yamefanyika mangapi tena zaidi ya haya? Nani mara hii anajisahaulisha ujambawazi wa HEPA, EITISIELO, AIPITIELO, Dowanis na Richmonduli? Juzi nilisikia wakiuza hata ofisi za mapilato bila hata kuhofia! Nikisema mnaliwa mnasema natukana. Situkani. Huo ndiyo ukweli hata mkiuita upuuzi.

Kuna jambo moja linashangaza hata hivyo. Mbona hao watasha wanaowatuhumu wakubwa wanapotoa misaada yao hatuwaiti wapuuzi? Hapa mpuuzi ni yule anayewaita wenzake wapuuzi na kupuuzia ukweli kuwa naye ni mpuuzi? Hilo mie sijibu. Mtajibu wenyewe.

Like gari ni kama la Maiko Reiza. Ngoja niende kumuuliza ukweli mwingine.

Chanzo: Tanzania Daima Septemba 14, 2011.

Tuesday 13 September 2011

Leo nafikiri kama mbuzi na si mlevi

Sithi Hosana, hosana, hosana,
Kuwe Nkosi yamakhosi.
Hosana, hosana, hosana.
Hosana, hosana, hosana, hosana.
Siyaguqa phambi kwakho, sizinikela lamuhla.
Thumel’uMoya oNgcwele, uzasikhanyisela, Sithi...
Sicel’uthando, lomusa enhliziyweni zethu.
Ibizo lakho, lidunyiswe, emhlabeni lasezulwini, Sithi...
Siyabonga, Baba wethu ngokusithanda
kwakho konke, Sithi...

Naomba nisitafsiri bali niende kwenye yaliyonikuta.

Juzi mwenzenu nilifaidi sana. Nikiwa zangu kwa Mama Betty nikipata kanywaji si akajitokeza fisadi mmoja toka chama fulani cha mafisadi anayegombea ulaji kule Igungaa lilikodondoka gamba la Kagoda. Jamaa alinipiga kwa makulaji ya nyama ya mbuzi sina mfano! Niliagiziwa mbavu, salala na figo nikajichana kama sina akili nzuri. Jamaa alitaka eti anipeleke Igungaa nimpigie debe. Hakujua mie japo mlevi bonge la mjanja. Nani afanye unepi kama wale waandishi makanjanja wanaotumikia mitumbo yao zaidi ya nchi? Sorry nimesahau. Alitaka eti niandike makala safi kwa wanywa gongo kumpamba ili anunue magazeti yote na kuyasambaza kule Igungaa asijue wengi wa wapiga kura hawajui kusoma wala kuandika!

Kwa wanasiasia uongo hili si tatizo hata kidogo. Ingekuwa nchi za wenzetu hiki ni kile wanachokiita bull’s eye. Hivyo, wange-barnstorm kuhakikisha watu wanapata angalau elimu ngumbaru.

Turejee kwa mpuuzi huyu. Hakujua mie ni msomi wa kupigiwa mfano ingawa PhD yangu nimeipata kwenye chuo kikuu cha Gongo! PhD yangu ya gongo ni kali kuliko zile za vyoo vikuu ambazo husababisha wenye nazo kuuibia umma kama mbuzi avamiavyo shamba. PhD ya gongo haigushiwi na kila juha ili aitwe daktari wakati ni kihiyo kama Msampuri anayefikiri kwa makalio. PhD ya gongo haigushiwi. Iga ufe kwa supu ya mawe si kanywaji ka kudandiwa na kila juha sawa na PhD yake.

Baada ya kujichana nyama mulua ya mbuzi nilianza kufikiri ni kwanini wanadamu humfuga na kumla mbuzi. Jibu rahisi nililopata ni kwamba wanadamu huwala mbuzi, kondoo, kuku na hata chamanki nchanga kwa vile wanawazidi akili. Je nyama ya mbuzi haiwakomeshi kwa uchoyo wao kwa kuwasababishia kuvimba miguu. Je nyie mliwao hamounekani na kufikiri kama mbuzi? Msiseme nawatukana kuwalinganisha na mbuzi ingawa ni hivyo. Kwanini mnaliwa? Hili ndilo swali langu la leo.

Mbuzi hawauawi kwa risasi kama swala na mbarapi. Lakini bado hufa tena kifo cha taratibu cha visu na manyanyaso. Je si bora kuishi kama swala kuliko mbuzi? Mbuzi hupigwa kwa mijeledi na kufungwa kamba. Swala wake mkuki au risasi lakini baada ya shughuli. Mbuzi na kondoo ni viumbe wa hovyo wasio na kumbukumbu. Ukimfokea mbuzi wakati anakula mahindi shambani mwako anadhani ni miaka mingi iliyopita. Ukirudia kumfokea anadhani ni jana. Hadi atie akilini hadi jiwe litu kichwani mwake hata kumvunja ubavu. Hiyo ndiyo akili na kumbukumbu ya mbuzi. Mbuzi hana kumbukumbu, na kama anayo basi ni ya muda mfupi sawa na wadanganyika ambao kila uchapo uchafuzi hukirimiwa gongo na mapupu kama jamaa alivyonifanyia akidhani nami ni mbuzi. Mie nilivibukanya vilaji vyake na sasa namtolea nyodo. Kama yu mjanja basi aje anipasue tumbo achukue uchafu wake. Mie hata kama mlevi ni mjanja tena bonge la mjanja niishie kwa gongo kuliko takrima za kipuuzi na ufisadi kama wa Ewassa.

Nazidi kujiuliza. Je hawa ndata wanaokuja hapa kwa Mfuga Hyena na kuwatoa wauza gongo na wala bwimbwi mitaa ya Mnazi Mmoja Lumumba uchache kwa vile wanavunja sheria si mbuzi? Watashindwaje kuwa mbuzi iwapo nao wanatenda jinai kwa kutumia jinai wakijua fika wakidakwa kibarua kinaota nyasi? Hawa nao ni mbuzi. Maana mbuzi huwa hafikiri wala kuwa na kumbukumbu zaidi ya kulialia meeee. Unampiga mtu bao ukimatwa unalia meeee! Meee ndio muziki wa mbuzi. Ndiyo maana mbuzi hula majani bila kufikiri kubadili sawa na hawa watenda jinai waishio kwa jinai wasibadilike. Je hawa si mbuzi binadamu? Je hawa wanaojilimbikizia mimali wakijua wakati waja wa kuwanyang’anya hiyo mimali na kuwatupa lupango umekaribia siyo mbuzi? Unafanya ufisadi halafu ukivuliwa gamba unaanza kulia meeee! Ndugu zangu wa magamba mpo hapo? Unachangisha pesa ya kuwahonga waishiwa ukimatwa unalia meeeee! Mbuzi mkubwa hata kama una cheo.



Nazidi kuwaza. Kwanini mbuzi hunya na kulala humo anyamo? Jibu rahisi ni kwamba ni kwa sababu yu mbuzi. Je hawa wanaochezea ofisi za umma wakijua fika si za urithi wana tofauti gani na mbuzi au kuku anyae na kulala pale aliponyea? Maskini mbuzi hana kesho ns kama ipo ni mashaka mtupu. Yake ni leo leo maana hajui kama kesho atapona kisu hata kama karidhika na kamba! Mbuzi ni mbuzi hata akae kwa bilionea bado atakula majani na kuitwa mbuzi. Mbuzi ni mbuzi hata awe tajiri miongoni mwa mbuzi wenzake. Mbuzi si mjanja mbele ya majani hata kama anayala. Huenda majani yangekuwa na miguu yangemkimbia.

Ingawa nami naweza kuitwa mbuzi hata kuwekwa kwenye kundi la mbuzi kutokana na kuwa mtumwa wa gongo. Je mtumwa wa gongo na mtumwa wa ufisadi nani mbaya zaidi kwa taifa? Hakika naona mbuzi kila mahali. Naona mbuzi wanono na waliokonda. Naona mbuzi wakilia lia meee kwenye kiza na umaskini wasijue la kufanya kwa vile wao ni mbuzi. Jamani, mbuzi ulimkosea nini wadudi hadi ukaridhika na umbuzi?

Leo siongei na wanywa gongo kama kawa. Naongea na mbuzi wangu. Nyie mbuzi, mtaacha lini umbuzi wa kuliwa mkijiona? Nanyi mbuzi muwalao mbuzi wenzenu mwadhani ni ujanja? Mbuzi ni mnyama mwenye kumbukumbu kidogo. Hata ukimletea demokrasia badala ya kuchagua mbuzi mwenyewe amuongoze atamchagua fisi! Je wawachaguao wawalao wana tofauti gani na mbuzi? Mbuzi ana nafuu kwa vile ni hayawani na hajihangaishi na kubadili mwelekeo wa maisha yake. Mawazo yake yameganda kama ya yule mama wa mjengoni ambaye bado hajui kuwa mambo yalishabadilika na ibada za sanamu zilishaondolewa! Hamumuoni akicheza Makidamakida? Yule naye ni mbuzi wa aina yake tena wa shughuli kama waliwao. Hamkumuona juzi akimteua fisi Ewassa kuwachunguza mbwamwitu wakati yeye ni fisi?
Chanzo: Dira Septemba 2011.

Rutabanzibwa anangoja nini ofisini?


Baada ya katibu mkuu wa wizara ya ardhi Patrick Rutabanzibwa kupatikana na hatia ya kuidharau mahakama na kuhukumiwa, wengi wanaamini wakati wake wa kuachia ngazi umefika. Maana, hata kama ni vigumu kujisuta kutokana na ulaji uliomzunguka na usugu wa kupenda kula uliowajaa watendaji wetu, sifa na jina lake vimeishachafuka vilivyo. Hivyo, Rutabanzibwa hana haja ya kungoja apigiwe makelele na kutungiwa mashairi na nyimbo au kuandaliwa maandamano ndipo ajiwajibishe. Pia angefanya haraka kuachia madaraka ili kumpunguzia mzigo rais aliyemteua kutokana na kuwa mengi ya kufanya. Swali linaloulizwa ni je atawezaje kukaa kwenye ofisi ya umma wakati aheshimu sheria za nchi anazopaswa kuzilinda na kusimamia? Je rais anayehimiza uwajibikaji kila siku atamfumbia jicho?

Jina la Rutabanzibwa lilianza kusifika kwa wanahabari kutokana na kuhusishwa na kashfa mbali mbali kuanzia IPTL hadi ya hivi karibuni ya uuzaji viwanja. Hata hivyo, pamoja na Rutabanzibwa kutajwa kwenye kashfa nyingi, aliendelea kubakizwa madarakani. Hakuhangaika kukanusha wala kujitetea. Hata anapojaribu kujitetea kama alivyofanya kwenye kashfa ya sasa, anafanya hivyo kujionyesha kama mjanja anayeongea na watu wasio na akili wala uelewa wa lolote isipokuwa atakalo yeye. Hii laweza kutafsiriwa kama kiburi cha hali ya juu. Na pili hii inaweza kuchukuliwa kuwa shutuma zilizotolewa dhidi ya Rutabanzibwa ni za kweli ndiyo maana hakuhangaika kuzikanusha wala kujitetea. Hili, kimsingi, limekuwa likiwaudhi na kuwasumbua watanzania wengi hasa wapenda haki ambao wanashangaa ni kwanini mhusika hachukuliwi hatua hata kuwajibishwa.

Nani mara hii kasahau au kusamehe kashfa aliyotuhumiwa kwayo Rutabanzibwa ya kusaini mkataba wa hatari kwa taifa wa IPTL ambao umegeuka donda ndugu kwa taifa? Nadhani bado watanzania wanakumbuka yaliyofanyika mjini London wakati wa kashfa hii.

Kwa kosa alilopatikana nalo hatia Rutabanzibwa, anapaswa kuwa mfano kwa watendaji wengine wanaodhani mahakama za Tanzania zipo kuwaadhibu watu wadogo na kuwakingia kifua na kuwaogopa wanaojiona wakubwa. Rutabanzibwa ameonyesha mfano mchafu hakuna mfano. Naamini hata rais aliyemteua hataweza kumvumilia tena kutokana na aina ya kosa alilotenda hasa akiwa mtumishi wa umma wa ngazi ya juu. Kudharau mahakama si kosa dogo. Hata hivyo, mahakama imekuwa na huruma sana kwa kumpa adhabu yenye uchaguzi kati ya kifungo au kulipa faini. Vinginevyo alipaswa apewa adhabu zote ili liwe somo kwa wengine wanaodhani mahakama ni chombo cha kudharau na kuchezea.

Kadhalika kutokuwajibishwa au kuwajibishwa kwa Rutabanzibwa kutatoa fursa kwa watanzania kutathmini upya msimamo na maagizo ya rais ambaye amekuwa akijitahidi kuwaaaminisha kuwa yuko kulinda maslahi kanuni na sheria za nchi kwa mujibu wa kiapo chake cha utumishi. Hii ni fursa adimu ambayo inaweza kutumiwa na rais kurejesha heshima yake kuhusiana na ambavyo amekuwa akiwashughulikia watuhumiwa wa kashfa mbali mbali.

Ukiachia kupatikana na hatia ya kudharau mahakama, Rutabanzibwa ni mmoja wa maafisa wa juu wa serikali wanaotuhumiwa na kashfa nyingi kuanzia kipindi cha awamu ya tatu. Ingawa wengi wanaona kama Rutabanzibwa analindwa, kipindi hiki hakuna sababu yoyote ya msingi inayoweza kutolewa ni kwanini asiachie ngazi. Kwa msingi huo, rais ambaye kikatiba ndiye aliyemteua, anapaswa kuzingatia kuwa kuendelea kuwa na mtu asiyetii sheria wala kuheshimu mahakama kutamshushia hadhi na kufanya umma uwe na shaka naye. Hivyo, jambo la maana na la haraka kwa rais kufanya ni kumwajibisha ingawa hatuna utamaduni huu kutokana na mifano mingi ya ambao wameishatuhumiwa bila kuwajibishwa.

Rutabanzibwa anapaswa kuwa mfano. Na si mfano tu. Anapaswa kuwajibishwa haraka ili kuonyesha jinsi rais anavyochukia kuwa na watu wasioheshimu sheria na mahakama. Maana hatuwezi kuwahimiza wananchi wetu wafuate na kuheshimu sheria wakati sisi tunaowahimiza ni mabingwa wa kuzivunja na kudharau taasisi halali za umma.

Kuna haja ya watu kama Rutabanzibwa kuadhibiwa vikali kutokana na kuanza kujengeka mazoea kwa baadhi ya walevi wa madaraka kudharua taasisi za umma. Hivi karibuni, katibu mkuu kiongozi Philemon Ruhanjo, alionyesha dharau ya wazi kwa bunge na rais wa nchi kwa kumrejesha kazini mtuhumiwa wa ufisadi, katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini David Jairo katika mazingira yanayoonyesha wazi kupindwa sheria.

Kwa kumshikisha adabu Rutabanzibwa, litakuwa onyo kwa wengi wanaodhani kuwa wao hawaguswi.
Chanzo: Dira Septemba 2011.

Thursday 8 September 2011

EAC: Is Northern Sudan Welcome?

Can Bashir be trusted? Photo courtesy


News that North Sudan has recently presented its application to join East African community is indeed a bad joke. Though unity is healthy, the unity of a lamb and hyena is not.

We must not allow ourselves to be taken for a ride by our rulers who in the past accepted and fast -tracked the memberships of some suspicious members without consulting with the hoi polloi. We should make sure that they don’t consent to North Sudan’s membership.

Machinations and bulldozing the hoi polloi have already started. Richard Owora Othieno, the head of corporate communication at the EAC Secretariat said in interview that the Secretary General, Dr Richard Sezibera has circulated the information to all member states asking ministers to chart the way forward.

"As per the normal procedure, Dr Sezibera circulated the Republic of Sudan's communication to Partner States; so we expect the Council of Ministers to take note of this development and give guidance on the way forward," Owora said.

North Sudan should not be admitted to EAC. First of all, North Sudan’s ruler, Omar Hassan Bashir is wanted by the ICC for committing genocide in Darfur. Thus, by admitting North Sudan, EAC will be abetting with the genocidaire..

If one looks at North Sudanese, excluding Darfur and Nuba Mountains, North Sudanese despite being African believe they are Arabs - not Africans even though they are typically black. It also should be noted that for generations, these Africans calling and regarding themselves as Arabs killed and tortured South Sudanese simply because they were black and Christians.

At one time, North Sudan allegedly sanctioned the killing of South Sudanese, guaranteeing the killers a place in paradise. Unfortunately for North Sudan, it has nary issued any apology or recanted this sacrilegious abuse to humanity. It is ridiculous and dangerous to admit Africans to the EAC who despise Africans and deny being African. For those who know the history and mindset of North Sudanese “arabs” will agree with me that being an African in North Sudan is synonymous with being a slave.

Economically, North Sudan has nothing to offer to EAC except conflict and more problems. While EAC members are gasping for improving the lives of their people, currently North Sudan has some programs that involve resettling Arabs and other Gulf nations in North Sudan under the arabization move by North Sudan.

There is yet another fact. Why should North Sudan hurriedly apply even before South Sudan that is a natural member of East Africa? If North Sudan is accepted, it must be understood: it will be an outright provocation for South Sudan to shy away from EAC. Comparably; EAC needs South Sudan more than North which has always forced its people especially black to join Arab League.

In essence, North Sudan, thanks to losing oil revenues after South Sudan went solo, is desperate and bankrupt. This can be seen on how its currency is cascading now. Therefore, it is looking for green pastures from East not to mention exporting its problems to other coutries. Refer to North Sudan being run by a dictator who has always hidden his face behind Islamic rule.

North Sudan, just like other Arab states, believes that one key member of EAC, namely Tanzania, committed genocide or tribal cleansing in Zanzibar in 1964 during the revolution of Zanzibar that toppled the Arab minority and apartheid regime. Refer to this linkhttp://www.youtube.com/watch?v=4lpY8_mKvjk. This is a crime to refer to revolution-cum-liberation of Zanzibar as a crime against humanity in Zanzibar. If North Sudan is admitted, Zanzibar that is the party of the United Republic of Tanzania will never make do with this blasphemy –cum-abuse to its independence and wellbeing.

North Sudan is using its vastness to dupe EAC members to think it is a good market. But looking at the current size of the economy of North Sudan and its dependent on Arab goods, and the mindsets of its people, North Sudan is not a big deal to have within the fold.

The expansion of the market has always being a driving factor for EAC members when it comes to admitting a new member. This should not dictate everything. For, in the end, we are going to admit loss-making and blood-letting new vampiric members like North Sudan.

Apart from the facts listed above, North Sudan is not a signatory of ICC whereby EA is. And thus, shall North Sudan become a member; its ruler become will put EA in conflict with international community.

What happened during the promulgation of the new constitution in Kenya should not be repeated by allowing Bashir the chance to stroll and jabber the way he wants. In sum, EAC should not be turned into the area for criminals like Bashir to stroll and chest beating. Apart from being a pariah state, North Sudan has always openly supported Islamic fundamentalism. Refer to the harboring of Osama bin Laden and condemning the emancipation of Iraq from the fangs of Saddam Hussein.

Source: The African Executive Magazine September 7, 2011.

Ningekuwa Jakaya ningebuni dhana ya kuvaa gamba

Tukiacha unafiki sanaa na kujidanganya, hakuna gamba nene na zito kama Jakaya Kikwete miongoni mwa magamba yaliyopo nchini na kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa mujibu wa List of Shame ya Dk. Wilibrod Slaa ya Mwembe Yanga ya Septemba 15, 2007. Hasa tukiangalia chanzo kilichoibua magamba ambayo kwa sasa CCM kimeshupalia, tunagundua kuwa hakuna gamba isipokuwa Kikwete. Hebu tukumbushe kwa kujierekeza kwenye mkutano wa hadhara kule Mwembe Yanga Dar es salaam wa Septemba 15, 2007 ambapo msemaji mkuu ni Dk Wilibrod Slaa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Bila woga, Dk. Slaa anawataja mafisadi wanaolisumbua taifa letu. Katika orodha hiyo kuna Jakaya Kikwete kama kiongozi na mnufaika mkubwa wa ufisadi huu hasa ule ujambazi wa EPA.

Baada ya CHADEMA kufyatua kombara hili, wengi wa waliotuhumiwa mafisadi walitishia kwenda mahakamani kujisafisha ingawa baadaye waligwaya. Katika kundi la waliofurukuta kutishia kwenda mahakamani Kikwete hakuwemo. Yeye, kwa sababu azijuazo na kwa makusudi mazima, alichagua kukaa kimya! Wanasheria hapa wanasema circumstantial evidence applies though silence is not necessarily to plead guilty.

Je ni kwanini Kikwete alichagua njia ya kukanganya na ya hatari ya kujikanyaga na kukaa kimya kama hakushiriki? Je kweli hakushiriki ufisadi wa EPA ambao unamshusisha hata mtangulizi wake yaani Benjamin Mkapa? Je hakunufaika na ufisadi huu? Je Kikwete atajificha nyuma ya ukimya hadi lini na kwanini kama hakushiriki wizi wa EPA? Je hii ni mbinu salama huko tuendako ambako kiongozi wa zamani anaweza kufikishwa mahakamani kama ilivyotekea Malawi na Zambia?

Iwe ni kwa woga, kujikomba au unafiki wa kawaida, wengi wamekuwa wamkimshauri rais Kikwete kuwatimua mafisadi ilhali wakijua hawezi kufanya hivyo kutokana na sababu nyingi tu. Kimsingi, tunapaswa kumwambia Kikwete, tena bila kuzungusha wala kumung’unya maneno, kuwa naye ajitimue. Je kwa siasa uchwara kama alivyosema Rostam Aziz mnufaika mkuu wa ufisadi, Kikwete atajitimua au umma umtimue? Kwani yu gamba tena nene. Kwa lugha rais ni kwamba Kikwete ni gamba-kikwazo. Najua hawezi kujivua gamba mwenyewe hadi pale yaliyotokea Libya, Misri na Tunisia yamfike mlangoni mwake. Je itawezekana wakati watanzania nao ni magamba kwa namna yake? Japo inataka ujasiri wa mwendawazimu, potelea mbali, acha niwe wa kwanza kumvisha kengele paka kwa kumtaka ajivue mwenyewe kabla ya kuwavua wengine magamba.

Je inaingia akilini kumwambia gamba awavua magamba wenzake wakati lao ni moja nyuma ya pazia? Je anao ubavu wa kuwavua wenzake magamba akabaki salama? Je akiwavua wenzake magamba yeye atabaki salama hasa ikizingatiwa kuwa wanajua mambo yake mengi ambayo asingependa mtu yeyote ayajue hasa wananchi anaowaaminisha kuwa anafaa wakati hafai? Tuache utani. Hivi tunategemea CCM imvue mtu gamba wakati chama chote ni magamba matupu hamna mtu mle bali agamba?

Leo tunalalamika ulanguzi wa mafuta na umeme wakati nyuma ya pazia tunaowalalamikia ndiyo hao hao wanufaika.

Leo tunapiga kelele kumtaka Kikwete awashughulikie mafisadi kama wale wa EPA wakati ameingia madarakani kwa pesa hiyo hiyo ya EPA iliyowezeshwa na wawezeshaji wake! Ni ajabu na aibu. Wanaodhani ninamzushia wajiulize swali jepesi la kwanini Kikwete tangu shutuma za kuingia madarakani kwa pesa ya EPA ziibuke hajawahi kujitetea wala kuzijadili kama ni za uongo? Je ukimya hautoshi kutupa ukweli? Hivi mnadhani Kikwete ni mtoto mdogo kiasi cha kuzushiwa akubali jambo ambalo hakutenda? Can he allow himself to go down in flames? Tabia ya binadamu inajulikana awe mweusi au mweupe mtawala au mtawaliwa. Mtu yeyote akizushiwa jambo hawezi kunyamaza yaishe. Ukiona kanyamaza jua kuna ukweli kwa kiasi kikubwa kuliko uongo. Je ukimya wake unamaanisha nini zaidi ya kuthibitisha madai na shtuma? Je watanzania watakomaa lini na kuuangalia ukweli kama ulivyo hata kama unauma?

Ukiachia mbali kushiriki ufisadi wa EPA, Kikwete anakuwa gamba zito kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma hasa kupenda ziara na kuwaachia wateule wake wajifanyie watakavyo. Rejea kujaza mawaziri mizigo wengi kwenye baraza lake la mawaziri. Hivi mawaziri kama Hussein Mwinyi, William Ngeleja, Ezekiel Maige, Vuai Shamsi Nahodha, Hawa Ghasia, Celina Kombani, Sofia Simba, Jummanne Maghembe, Shukuru Kawambwa na manaibu wao wanapaswa kuwa ofisini wakati wamevurunda kupita kiasi?

Pamoja na kustumiwa kuwa yu dhaifu na serikali yake ni legelege, Kikwete ameendelea kulegea zaidi kiasi cha kukatisha tamaa kwa watanzania. Uchumi unazidi kuporomoka huku ufisadi ukiongezeka kama ilivyofichuliwa hivi karibuni bungeni ambapo mamia ya wanyama yametoroshwa huku serikali ikiangalia na kujikanyaga. Leo tunaongelea mamia ya wanyama waliotoroshwa siku moja. Je wameishatoroshwa wangapi na kwa muda gani bila kujulikana? Je ni madini kiasi gani yameishatoroshwa kwenye mchezo huu?

Kikwete ameshutumiwa kuwa mbabaishaji. Ajabu ameendelea kuwa mbabaishaji zaidi. Angalia alivyojikanyaga hivi karibuni kuhusiana na watuhumiwa wa magamba kukataa kata kata kujiondoa kwenye nyadhifa zao. Hata mmoja aliyejitoa bado anaendelea kutesa huku akishirikishwa kwenye kampeni za mrithi wake kule Igunga! Huku ni kujipiga mtama na kuthibitisha madai kuwa siasa za sasa ni uchwara. Rostam aziz kadai na hakuna aliyempinga wala kumkaripia! Hii maana yake ni kwamba anachosema rostam ni kweli.

Hata hivyo tunaweza kumpongeza Jakaya kwa kuruhusu joka kuu yaani CCM ifie mikononi mwake. Kama ataendelea na kasi hii ya kukiua chama ipo haja ya kumsamehe makosa yake baada ya wapinzani kuchukua nchi na kuilekeza inakopaswa kuelekea.

Hakika ningekuwa Kikwete ningebuni na kutangaza sera ya kuvaa magamba zaidi badala ya usanii wa kujivua magamba.

Chanzo: Tanzania Daima Septemba 7, 2011.

Tangu leo sitacheka tena

Baada ya kugundua walevi wamenuna kwa matatizo huku wezi wachache wakichekacheka, nimeamua kununa kuwaunga mkono. Kwa sasa wanamtamani rais Nunanuna na mbabe baada ya Chekacheka kuwaingiza mkenge. Pia ukichekacheka hovyo kama mwenye kiharusi, unatoa nafasi kwa mafisadi na majambazi kukuzoea kiasi cha kukutumia. Kuchekacheka kunafanya watu wengi wakudharau na kukuona kama mtu ambaye si makini wala serious. Hivyo, nimeamua kuchukia kinyume cha kucheka. Nafanya hivyo kama sifa mojawapo ya kuweza kupewa kura na walevi ambao uchaguzi ujao watafanya kinyume.

Nani amesahau kuwa muhula ule walevi waliangalia vicheko, ahadi za uongo na bashasha wasijue hata shetani ni bingwa wa kucheka? Kwa vile walevi wameishachoka urembo na mashauzi, imebidi nianze kununa ili nionekane, kwanza sicheki hovyo na pili nina sura mbaya kama yule rais mbabe bingwa wa mipasho na ubishi wanayemtamani.

Kuna msemo kuwa what matters is not how big your house is but how big your heart is. Nami nasema. No matter how big your smile is but how big your wrinkles are. My heart rich in angers not in dribs and drabs but full of the same. Hivyo, walevi wajiandae kuwa na rais anayenuna hata kwenye harusi na siyo yule waliyezoea anayecheka hata kwenye msiba. Tunahitaji mabadiliko. Mpayukaji I am for changes big changes so to speak. Kupitia kununa, niko tayari kuondoa kiza na kuleta mwanga. Sasa wapiga kura watachagua vicheko kwenye kiza au kununa kwenye mwanga. Mie nitawanunia mafisadi na kuwakamata hata kama baadhi yao watakuwa mke au watoto wangu na washirika zangu.

Kupitia kununanuna wauzaji wa wese waliojigeuza walanguzi hawatawanyonya wala kuwachezea watu wangu kwa kuwalangua wese. Nitakachofanya kwa wale watakaojifanya wana magamba manene ni kunyongelea mbali kabla ya kuruhusu vurugu za wese kuinyonga serikali yangu. Hakuna kitu kinanifanya ninune hadi kupata saratani ya akili kama kuona watu wangu wakilanguliwa wese wakati kwenye nchi za jirani bei ni za chini.

Kwa vile nitakuwa nanuna nuna hovyo, nchi nyingi hazitapenda kunipa mialiko. Hivyo sitasafiri wala kutalii hovyo na kupoteza pesa nyingi za walevi. Kwa vile nitakuwa nimenuna kila saa, hata mshirika wangu wa bedroom hataandamana nami iwapo nitakuwa na ziara ya lazima ughaibuni.

Pia kwa kununanuna naamini hata mawaziri nitakaowateua kwenye serikali yangu hawatafanya madudu kwa kuogopa nisiwapasukie. Hivyo, mawaziri vilaza kama Bill Ngelanija, Milima ya Kigoma, Makorongo Muhanga, Safia Lion, Hawa wana Ghasia, Semakombania, Shukrani kawa Mbwa, Jfour Majembe, Emmy Nchimvi, Bill Luku-mvi, Meli Nyago, Vurumai Nahodhi, Hosseni Mwuinyi, Stevu Wa Hasira na wengine hawataweza kunigeuza zoba la kuibia walevi kama ilivyo sasa.

Hata magabacholi wanaojichekesha kutokana na kuitikia vicheko hawatanipata. Maana akijifanya anataka appointment ya kukutana nami namtolea mihasira yangu na kumsweka lupango bila kuuliza. Bila kufanya hivyo, huwezi kuendesha kaya. Mara hii mmesahau mzee Mchonga alivyokuwa akinuna? Juzi nilikuwa nikipitia hotuba zake baada ya kuutwika. Nilisikiliza hotuba moja kamambe alipokuwa akitoa sifa za rais mpya baada ya mzee Ruksa. Alisema wazi. Lazima rais ajaye awe anachukia rushwa na akisema nachukia rushwa, ukiangalia usoni mwake unaamini kabisa huyu anachukia rushwa. Alionya kuwa kusema nachukia rushwa au nitawapeleka Kanani si jambo la maana iwapo anayesema hivyo anachekacheka na kuonyesha wazi anavyowatapeli walevi.

Sasa mimi nasema. Nachukia rushwa na ufisadi. Si kuchukia tu. Ukinitajia ufisadi ua rushwa nanuna nusura ya kupasuka. Mie nisemapo nachukia rushwa, inabisi mnielewe. Nikigundua kuwa waziri wangu hata mtoto wangu au mke wangu amekula rushwa au kuwa fisadi, lazima nimnyonge. Heri kumpoteza mpenzi au mtoto wangu kuliko kujiingiza kwenye vitendo vichafu na kupoteza heshima yangu.

Isitoshe, nikishachaguliwa kuwa rais ambaye si rahisi kama ilivyo, nitahakikisha naandika katiba upya na kutamka wazi wazi kuwa atayekula rushwa au kufanya ufisadi anyongwe mara moja. Pia nitahakikisha katiba inatamka wazi kuwa kwa mtumishi wa umma kushikiwa kunatosha kumuondoa mtu kazini au ofisini ili sheria zichukue mkondo wake. Hivvo ningekuwa nimeishaapishwa, watuhumiwa wote wa rushwa, ufisadi uwe wa fedha au elimu wangekuwa lupango wakingojea kunyongwa kama siyo kupigwa risasi kwenye viwanja vya Jangwani ili wengine wajifunze na kupokea onyo toka kwa rais Nunanuna Mpayukaji PhD isiyo ya kupewa wala kughushi.

Pia nitakapokuwa nimewashawishi walevi kwa ndita zangu na kuchaguliwa kuwa rais, nitahakikisha bunge linaendeshwa na spika mwenye elimu na hadhi na si vikaragosi vya mafisadi. Nitahakikisha bunge linakuwa na meno na hadhi badala ya kuwa rubber stamp ya kupitishia bejeti uchwara na madili ya mafisadi wakubwa wakubwa kama ilivyo katika baadhi ya nchi kwa sasa.

Juzi niliongelea majambazi manne yaani Ngelanija, Milima, Ruhani-njoo na Devil Jahiri. Kama ningekuwa rais tayari wangekuwa marehemu.ninaposema marehemu nieleweke, siyo kisiasa bali kibaolojia. Na nazidi kuwaahidi walevi kuwa mkombozi wenu niko mlangoni nachungulia ikulu kuja kuondosha uchafu na kuparejesha kuwa patakatifu pa patakatifu toka kwenye kuwa patakataka pa patakitu.

Wale wauza bwimbwi wakae mkao wa kuliwa. Mie sitashughulika na biashara hii haramu kwa kuwapiga baadhi ya watu vijembe. Nitanuna na kukamata wauzaji na kuonyesha hadharani ili nisipoteze muda wa majibizano ya kitoto. Sitataja majina ya wauza bwimbwi. Watajitaja wenyewe siku nikiwaonyesha kwa umma bila kujali nyadhifa zao au kama ni makafiri, mashehe, maaskofu au watakatifu. Mie nitasema kwa vitendo. Hivyo wauza bwimbwi kaa mkijua kuwa nikichaguliwa ndiyo mwisho wa biashara zenu.

Kwa kutumia kanuni ya kununa, nitahakikisha kila mwananchi anataja mali zake. Najua walevi wengi hasa wa uswekeni watataja chawa na mapanya kama mali zao. Poa kuliko wanaotaja au kuficha mahekalu ya wizi. Kwangu maskini anayekula jasho lake ni bora kuliko jambazi anayeishi kwa kunyonya wenzake kama kupe. Pia nalaani ule msemo wa kipumbavu kuwa mtaji wa maskini ni nguvu zake. Mtaji wa maskini ni raslimali za nchi yake. Kwanini mtaji wa maskini iwe nguvu yake ilhali mtaji wa wezi wenye madaraka ni jasho la maskini?

Hivi nikiwa rais mafisadi si watajinonihino kwenye nguo zao?

Naona Rahma ananibeep ili twende kujivinjari kwenye kiza.
Usimwambie mtu.

Chanzo: Tanzania Daima Septemba 7, 2011.

Tuesday 6 September 2011

Barua kwa Edward Lowassa




Mpendwa waziri mkuu aliyeachia madaraka kutokana na kujiingiza kwenye kashfa ya Richmond, Edward Ngoyai Lowassa (MB).

Salamu sana na habari za siku nyingi? Leo naomba nichukue fursa hii adimu na muhimu kuwasiliana nawe kwa njia hii ya waraka wa wazi. Najua una mambo mengi ya kufanya na kufikiri hasa ikizingatiwa unakabiliwa na shinikizo la kujivua gamba.

Naandika waraka huu kutokana na kuadimika kwako kwenye vyombo vya habari siku hizi. Mbona umekuwa kimya sana? Je unatafakari jinsi ya kujibu mapigo au kujivua gamba kama yule "mwarabu" wa waziri mkuu aliyetajwa na Bangusilo Ibrahim Msabaha? Je ule mpango ulioripotiwa mwezi jana kuwa unapaswa kujivua gamba kama Rostam Aziz na kama hutafanya hivyo mwenyewe utavuliwa gamba unauchukuliaje? Je unadhani ni danganya toto au watafanya kweli?

Mpendwa,lazima nikiri na kusema ukweli. Hakuna siku nilihuzunika kiasi cha kumwaga chozi kama alivyofanya mkeo kama siku ili niposhuhudia kwenye runinga ukitoa hotuba yako ya mwisho ukiwa waziri mkuu. Namkumbuka, mama Regina, kama alivyoitwa wakati ule. Sikujua kumbe umama unakwenda na cheo! Utasikia mama nonihino. Kila aendeko heshima na makandokando. Wengine wamefikia kuenziwa sawa na waume zao. Ila madaraka yakitimka nao hutokomea. Cheo cha mumewe kikishatimka na umama unapotea na kuja ugumba wa madaraka!

Hata hizi NGO za uongo na ukweli za kuchumia utajiri wa haraka huchangiwa baba akiwa madarakani. Akishakitoa NGO inadoda kama vile haijawahi kuwepo. Nikikumbuka Equal Opportunity and Trust for First Lady (EOTFL) ilivyododa sasa naamini kweli cheo ni dhamana. Nikimbuka mbwebwe za jamaa aliyetangulia akitisha vyombo vya habari na alivyonywea sasa, naamini kweli avumaye baharini papa. Bahati mbaya, wengi wa namna hii hili huwa hawalijui hadi linapowakuta! Hayo tuyaache ndiyo wizi wa kisasa na kisiasa.

Mpendwa,hata kama miaka imeyoyoma, picha hii mbaya sana huwa inanijia mara kwa mara kiasi cha kuninyima raha. Najua wewe huwa hutishiki kirahisi ingawa ukibanwa sana hufanya maamuzi ya kustukiza na yenye kustua. Je una mpango wa kutustua kwa kujivua gamba kwenye dakika za majeruhi kama alivyofanya Rostam? Je una mpango wa kuachia ngazi kwa kustukiza kama ulivyofanya wakati wa kuutema uwaziri mkuu au unangoja uvuliwe gamba kwa aibu na fedheha? Mie, hata kama si mshauri wako wa karibu wala mwandishi wa habari wa kukusifia na kukusafisha, nashauri ujivue badala ya kungoja kuvuliwa. Je kati ya hayo niliyoshauri hapo juu una mpango gani ndugu yangu?

Mpendwa,baada ya kuona umekaa kimya sana, nilijawa na wasi wasi kiasi cha kuanza kuwaza: kama utavuliwa ulaji wako ndani ya chama, kweli utakuwa na nguvu tena hata za kuweza kugombea urais kama wengi wanavyosema? Huoni, kama utavuliwa gamba kwa nguvu, utatimiza unabii wa Nape aliyesema kuwa lazima mvuliwe magamba wewe na Andrew Chenge na mkitoe? Maana, Nape alisema kuwa samaki huwa na nguvu akiwa majini, ila ukishamtoa majini si chochote si lolote. Kwanini hukumjibu hata kwa vijembe? Hayo tuyaache.

Mpendwa, nakumbuka ulipoulizwa kipindi fulani ueleze mipango yako kuhusiana na kujivua gamba kwa mwenzio ulisema kuwa muda ukifika utaweka mambo hadharani. Je utatimiza ahadi yako hii lini wakati muda unazidi kuyoyoma?

Mpendwa,uliwahi kung’aka kwa vyombo vya habari kuwa wewe ni rafiki mkubwa wa rais Jakaya Kikwete na urafiki wenu hakuanzia barabarani na wala hautavunjwa na vyombo vya habari. Je kwa sasa una msimamo gani kuhusu hili hasa ikizingatiwa kuwa urafiki wenu haukulenga kwa wewe kuwa gamba? Je unadhani rais ataendelea kujichafua kwa kulinda urafiki wako au msimamo wa chama na maadili badala ya madili?

Mpendwa, juzi juzi nilisoma sehemu fulani mtetezi wako akisema eti wewe ni mchapa kazi wa kupigiwa mfano. Ajabu jamaa huyu mbumbumbu asiyejua anachosema wala kuandika alisahau kuwa watu wanajua kati ya pumba na mbegu linapokuja suala la uchapa kazi! Bahati mbaya watu wengi wanakuelezea kama mchapa kazi wa kupigiwa mfano bila kutoa mifano ya kazi zako nzuri zaidi ya zile unazoshutumiwa kuzifanya! Je jamaa alimaanisha kazi zako kama vile Richmond na kutafuta mvua kule Thailand?

Mheshimiwa, naomba unisamehe kwa muda wako nitakotumia kuwasiliana nawe. Leo ni maswali mengi kutokana na kutokuwa na nafasi ya kuja Monduli kukuhoji. Nakumbuka juzi juzi uliwaonya wakubwa wa chama chako na serikali kwa kusema eti wana ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi magumu hata kama watalaumiwa. Je wewe una mpango wa kufanya uamuzi gani mugumu kati ya kujivua gamba na kutimka au kuvuliwa na kutimliwa? Je unangoja nini wakati muda unazidi kuyoyoma?

Sambamba na kuonya juu ya ugonjwa wa kuogopa kufanya maamuzi magumu, nakumbuka: ulimshauri waziri mkuu, Mizengo Pinda, kupunguza wizara yake kutokana na kuwa kubwa kupita kiasi ingawa hukuona wala kufanya hivyo wakati ikiwa chini yako. Je umeishamkumbusha tena kufanya hivyo kutokana na ukweli kuwa tangu utoe ushauri huo, tuseme; ulipuuziwa au kuwekwa chini ya busati? Je ni kwanini hukuliona hili ulipokuwa incharge wa wizara hiyo?

Ingawa hili si jipya kwako nami, unajibuje tuhuma kuwa ulijilimbikizia mimali lukuki iliyopatikana kinyume cha sheria? Maana ni miaka mingi tangu tuhuma hizi zitolewa bila kujibiwa. Naomba nawe ufanye maamuzi magumu lau ujibu tusikie upande wako. Na je unajiteteaje kuhusiana na tuhuma kuwa ulililingiza taifa kwenye kiza na hasara ya mabilioni kutokana na kupigia debe kampuni feki la Richmond? Naomba nitumie ushauri wako uliowapa wenzako kuwa wasiogope kufanya maamuzi magumu hata kama watalaumiwa. Je wewe una mpango gani wa kujibu tuhuma ili usionekane mnafiki wa kuona ya wenzio wakati yako huyaoni? Hilo la kujivua gamba tuliache.

Je una mpango gani wa kutoa maelezo au tuseme utetezi kuwa watoto wako waliajiriwa na Benki kuu kutokana na ushawishi na nafasi yako serikalini? Je una habari kuwa ni makosa kutumia cheo chako kuwanufaisha ndugu au wanao? Je huu nao ni sehemu ya uchapakazi wako?

Samahani katika waraka huu nitakuwa nakwenda mbele na nyuma. Hivyo naomba unisamehe na kunivumilia kwa hili. Maana mambo ya kujadili ni mengi na ya muda mrefu.

Naomba nimalizie waraka huu kwa kuomba lau nami unijibu hata kwa mafumbo kama utaweza. Pia naamini kuwa kwa muda uliobakia kufikia kusuka au kunyoa, usipotumika vizuri, kuna hatari ya wewe kugeuka historia mud si mrefu. Mungu apishe mbali na kila la heri ingawa maji yameishafika shingoni na mbuzi hawezi kuimbia kisu.

Chanzo: Dira Agosti 2011.

Saturday 3 September 2011

Aliyeiroga Tanzania sasa marehemu





Mkuu wa mkoa wa Rukwa Daniel Ole Njoolay akikabidhi ambulansi ya "kisasa" aina ya bajaj kwa mkuu wa wilaya ya Mpanda, Dk Rajab Rutengwe (kushoto). Ambulansi za miguu mitatu zimesambazwa na serikali kusaidia kutoa huduma za afya vijijini ambapo mkoa wa Rukwa utapokea miguu hii mitatu 20. Picha na Hamza Temba

Bila aibu wala wasi wasi serikali yenye kusifika kwa kununua mashangingi kwa ajili ya viongozi na watumishi wake hata wa chini eti imesambaza utitiri wa ambulansi za miguu mitatu nchi nzima katika karne ya 21. Jamani, kwanini wao wanapata pesa ya kununua mashangingi hata kutoa misamaha ya kodi na kuwatesa watanzania hivi? Pamoja na matusi yote haya ya nguoni bado watanzania wanaendelea kuichagua Chama Cha Mafisadi! Je hapa mgonjwa tena wa akili zaidi ya wananchi ni nani? Je watawala nao wanaowavua nguo wananchi hivi bado nao ni wazima? Je aliyewaroga watanzania ni nani? Hakika kama yupo mi marehemu na hakuna wa kuwazindua toka kwenye 'ufu" huu.

Hivi mabilioni ya EPA, Meremeta, Buzwagi, SUKITA, ATCL, THA,NBC na mengine mengi yaliyoibiwa na watawala wakishirikiana na majambazi wa kihindi yangeweza kununua magari mangapi ya kusafirishia wagonjwa?

Ukiangalia na ukweli kuwa watawala watu huangalia cha mbele kabla ya kinachokusudiwa, kuna uwezekano hii ni biashara ya kigogo mmoja akishirikiana na makuwadi wa kihindi. Kuna haja ya kuchunguza sana wizi na udhalilishaji huu wa mchana. Maana waliofanya hivi hawana uchungu wala heshima kwa nchi na watu wake na si waaminifu hata kidogo. Karne ya 21 ambapo wenzetu wanatumia Air ambulance, sisi tunaletewa kituko kiitwacho bajaj! Nahisi kupasuka.

Bado hapa Jakaya Kikwete anajisifia kuwa ameleta maendeleo ya kurudi nyuma kwa watanzania nao bado wanaendelea kumvumilia. Hivi uchafu huu wangefanyiwa walibya hata wamisri wangemfanya nini rais wao? Maana ukiangalia viwango vya maisha katika nchi za Maghreb ambazo zimejikomboa hivi karibuni na kulinganisha na marehemu Tanzania ni kifo na usingizi.

Hizi bajaj zinachekesha licha ya kusikitisha. Hivi huyo anayemhudumia mgonjwa atakaa wapi? Maana ambulansi si kusafirisha mgonjwa haraka tu bali hata kumhudumia. Je hilo vumbi na jua havitammaliza huyo mgonjwa kabla ya kufikishwa huko Hospitali kuandikiwa dawa na kuambiwa akanunue? Hapa bado hatujaangalia barabara zilizojaa misongamano na madereva feki ambao bila shaka watakigonga hiki kibajaj na kumuua dereva na mgonjwa wake. Tuache utani. Hivi aliyebuni upuuzi huu ana akili nzima kweli?

Kuna haja ya kutafakari na kubadilika haraka kabla hawa watu hawajatuzika hai. Je hawa wanaoogopa kuingia mitaani kudai haki zao hawafi kwenye huduma mbovu za jamii ukiachia mbali kufa kwa ugonjwa moyo wakifikiri jinsi ya kubangaizi na kufisidi ndiyo waishi?

Friday 2 September 2011

Jambazi anapojilinganisha na Yesu!

Ni muda mrefu tangu kijiwe kikutane kujadili mambo mbali mbali. Hii ni kutokana na wajumbe wetu kusambaa sehemu mbali mbali duniani kusaidia ukombozi wa nchi mbali mbali. Hivi karibuni mwenyekiti nilikuwa kwa mama kuwahamasisha vijana wampindue maana anakula bure na kulala bure yeye na ukoo wake.

Msomi Mkatatamaa alikuwa Masri ambako tulikwenda pamoja na kumpindua Huseni Kibaraka. Kwenye msafara huu nami nilikuwapo kabla ya kuondoka mwezi Mei kwenda zangu AbortAbad kwenda kumkamata Msama bin Burden ambaye tulimnyotoa roho. Kumbuka mimi ni SEAL ingawa hii ni top secret. Hivyo, unaposoma usome kwa sauti ya chini ili watu wasikusikie hasa mafisadi wakakimbia kwa kujua ninawatafuta.

Pamoja na kwamba baadhi ya wajumbe wetu wako kule Libya ambapo Mlamali Kashafi tumeishamwangusha, kijiwe kitaendelea bila wao kuwepo. Kwa taarifa nilizo nazo ni kwamba Msomi mkatatamaa yumo mjini Cairo kusaidia utawala mpya wa Libya kuunda serikali mpya. Yeye ndiye mshauri mkuu anayeniwakilisha mwenyekiti.

Kikao cha leo cha kijiwe ni kujadili na kumlaani Devil Jaa Hilo aliyenakiriwa hivi karibuni akijilinganisha na Yesu mtoto wa Maria. Hivyo mjadala wa leo pamoja na kuegemea kwenye ufisadi na usanii wa Njaa Kaya, kitaangalia mambo mbali mbali hasa wakati huu ambapo kaya iko kizani huku mapanya yakiendelea kuiguguna kama alivyonaswa Jaa Hilo akitaka kufanya kwa kisingizio eti cha kuwahonga waishiwa. Huyu naye anafikiri kwa masaburi au makali kwa wale wasiojua msamiati mpya wa masaburi. Ikumbukwe. Hapa hatumaanishi yule jambazi Masampuri aliyewatukana waishiwa kuwa wanafikiri kwa makario.

Baada ya kukutana baada ya muda mrefu, tunapata kahawa haraka haraka kukazia swaumu zetu na kuanza shughuli.

Mbwamwitu analianzisha aningia akiimba wimbo wake aupendao sana.

Anaimba,

Watu wa dunia hii mie wamenishinda,
Wakiingia kanisani wanahubiri na kuimba sana,
Wakitoka nje wanakwenda uza miunga.
Wakiingia ofisini wanajisifu na kuiba sana,
Wakitolewa wanaanza kusema eti wao ni Yesu,
Mambo mambo mambo
Mambooo mambo mambo, mambo yamenishinda.

Baada ya kumaliza kuimba wimbo wake alioanza kuuimba alipomaliza kusoma habari inayomhusu Jaa Hilo na Ruhani Njoo, anampasia gazeti Mchunguliaji, Mbwamwitu anakwanyua mic na kuzoza.

“Waheshimiwa wajumbe, leo nina hasira sana. Hasira zangu zimesababishwa na kuona jambazi mmoja mwenye maulaji eti akijilinganisha na Yesu baada ya nduguye na fisadi mwenzie aitwaye Phil Ruhani Njoo kusaliti ofisi yake na yule aliyempa ulaji bila kufikiri asijue ni jizi.”

Kabla ya Mbwamwitu kuendelea kunema, mzee Maneno anaingilia, “We unaongelea Ruhani Njoo na Jaa Hilo badala ya wale mahabithi wawili yaani Bill Ngelanija na mtoto wa Adimu Milima ya Kigoma ambao Njaa Kaya anajitahidi kuwaokoa!”

Mzee Maneno anamkabidhi kipisi cha sigara kali mzee Ndevu na kuendelea, “Hapa bila walevi kushinikiza mahabithi wote wanne wasulubiwe utakuwa ni usanii na usaliti kama kawaida. Wanakaya tutaendelea kuliwa.”

Mara miguno inasikika huku mzee Ndevu akisema, “Astaghafullahi eti tunaliwa! Matusi hayo mzee Maneno pia chunga maneno yako.”

Mzee Maneno haombi msamaha anaendelea, “Ndiyo tunaliwa. Sasa tunaliwa vipi msiniulize. Kama tusingekuwa tunaliwa si tungekwenda huko maofisini na kuwachoma hawa majambazi lau kwa kahawa.”

Kila mmoja ananyamaza kidogo kusukuti aliyesema mzee Maneno. Ni kijembe babu kubwa.

Tukiwa wote tunafikiri jinsi ya kumjibu, Mbwamwitu ambaye ana unywanywa wa kuongea hasa ikizingatiwa kuwa aliingiliwa na mzee Maneno anakula mic. “Waheshimiwa sana. Mzee Maneno kasema ukweli. Tena amefikiri kwa ubongo na si masaburi. Ametonesha donda ili waathirika tuumie na kuamka na kujihami. “

Anakunywa kahawa yake na kukatua kashata na kuendelea, “Mie narudia, mnaliwa.”

Kabla ya kumaliza, Mchunguliaji hajivungi, anamnyang’anya mic na kujibu, “Kama kuliwa unaliwa wewe na hao akina Njaa Kaya, Ruhani Njoo, Jaa Hilo, Milima ya Kigoma na Ngelanija na wenzake. Kwani hatujui kuwa wanatumiwa na mabwana zao watokao ughaibuni kuja kuchukua kwa kujifanya wanawekeza?”

Akiwa anatweta Mchunguliaji anaendelea. “Mie siliwi na kama kuna anayetaka kuliwa aliwe mwenyewe siyo mimi.”

Mpemba kaguswa pabaya. Anaingilia kwa ulaini kabisa kutokana na Mchunguliaji kunyamaza ili kuona ujumbe wake umefikaje. Mpemba anasema, “Yakhe kwani kuliwa tusiii? Mbona kama kuliwa wote twaliwa! Wala kodi zetu, wachangishana pesa yetu kupitisha upuuzi na wizi wao. Je huku si kuliwa jamani?”

Kabla ya swali lake kujibiwa, Mgosi Machungi anachip in, “Mgoshi kama kujigh’wa ni kuibiwa basi nao wanajigh’wa. Mie aiposema kujigh’wa niizani yale mambo ya kwenu ya popobawa.”

Kabla ya Mgosi kuendelea Mpemba anaingilia, “Yakhe hayo mambo ya popobawa yalikuwa ya Chama Cha Makafiri na Salimuni Amri yule kidhabu aliyetaka kututesa kwa vile eti tu wapemba.”

Mpemba anaendelea, “Mie naona hata hao akina Ruhani Njoo, Jaa Hilo, Ngeleza na Milima ya sijui Kigoma sijui Ujiji sijui Maneromango ndiyo mapopobawa wenyewe wanaokula pesa yetu. Mie nanchukia huyu ruhani haswa nkizingatia maruhani walivotuibia kura kule Zanzibar. Sasa waiba pesa nchi nzima ati. Hawa ni majambazi yatumiayo kalamu kuwaibia wanakaaaya wallahi.”

‘Wanakaya siyo wanakaaya. Hujui wanakaaya ni wavuta bangi Ami?” Anatania Mbwamwitu.

Mwenyekiti nami sitaki kuonekana kihiyo au mwoga kama Njaa Kaya. Nakula mic. “ Jaa Hilo ambaye ni jaa kweli hivi karibuni alitoa mpya alipofanya makufuru ya makufuru kwa kujilinganisha na Yesu pale jambazi mwenzie alipomwokoa kutokana na kashfa yake ya ujambazi na kuwasingizia waishiwa wabuge. Mie nasema, Jaa Hilo si Yesu bali Yuda atake asitake. Kusum ibn al muthnaka.”

Nabwia kahawa kidogo na kuangalia huku na kule na kuendelea. “Sasa nasema. Nenda kawambie wote kuwa nitawapindua kama nilivyowapindua akina Kibaraka, Kashafi, Bin Ali au kuwajeruhi kama tulivyomfanyia yule habithi wa Yamani Salehe.”

Wajumbe hawana mbavu kutokana na ninavyoongea kwa mamlaka na kujijazia ujiko.

Naendelea, “Njaa kaya na hao nyani wake hana jipya hata kama amejifanya kufuta uamuzi wa habithi Ruhani Njoo. Msitu ni ule ule na nyani ni wale wale. Hivyo hata huo uchunguzi tuliokuwa tumeambiwa ni usanii na utoto wa kawaida uliokuwa ukifanywa na watu wazima kimwili lakini watoto kiakili.”

Naona ndata wanakaribia, hivyo kila mtu atimke kivyake tukikutana tena tuwatokee hao majambazi na kuwaangukia kipopo.

Jaa-hilo na Ruhani-njoo mnanipata? Kumbaff sana.

Chanzo: Tanzania Daima Agosti 31, 2001.