The Chant of Savant

Thursday 30 August 2012

Matonya: Kioo cha jamii iliyoharibikiwa


INGAWA marehemu mzee Paulo Mawezi almaarufu Matonya anaingia kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kwa kile Waingereza waitacho ‘the whole wrong reason’, ameacha somo kubwa kwa wenye kufikiri.
Taarifa zilizotufikia ni kwamba mzee huyu maarufu kama alama ya umaskini na ufisi wa taifa letu amefariki dunia. Mzee huyu mwenyeji wa Dodoma alikuwa kivutio kwa wengi jijini Dar es Salaam ambako yalikuwa makao makuu ya shughuli zake za kuomba.
Kipindi fulani alimtoa jasho Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa wakati ule, Yusuf Makamba alipomwamuru ahame na kuachana na shughuli za kuomba kwa sababu alikuwa akilidhalilisha taifa. Matonya hakukubali ‘kufa kibudu’. Alipambana na Makamba hadi kumtishia kuwa angemng’oa kwenye nafasi yake. Kwa wenye kuuona ukweli, Matonya alikuwa bora kuliko Makamba. Kwani imeandikwa kuwa ajikwezaye atashushwa na asiyejikweza kupandishwa.
Sababu kubwa aliyotoa Matonya ni kwamba, akina Makamba walikuwa walafi wanaokula kwa mikono na miguu bila kunawa huku wengi wanaowanyonya wakiangamia. Matonya aliwaona akina Makamba kama ombaomba waliojisahau hadi kujipa haki ya kuwafukuza wenzao. Matonya aliomba na kuwafikishia mke na watoto wake wakati wenye madaraka huomba na kuficha Uswisi.
Anayetilia hili shaka ajiulize walioficha pesa tena kwa mabilioni ya Kitanzania ni nani kama si wale ombaomba wenye masuti? Ni ombaomba walafi na wenye roho mbaya kuliko Matonya ingawa ombaomba ni ombaomba hata kama amevaa manyang’unyang’u au suti.
Hivyo, kuomba kwa Matonya ilikuwa ni haki yake. Na kweli, kuomba ni bora kuliko kuiba au kujihusisha na ufisadi, mihadarati na jinai nyingine ambazo zimelifikisha taifa letu hapa lilipo. Kwetu sisi Matonya alikuwa matunda ya siasa za kifisi na ubabaishaji. Pia alama na kumbukumbu kwa wenye akili kuwa mambo hayakuwa sawa. Ni bahati mbaya kuwa watawala wetu hawakujifunza suto lililotokana na shughuli za Matonya.
Badala yake walitaka kutumia maguvu kumficha ili asiwaudhi wao na wageni wao, hasa wafadhili. Hakika huu mchezo umekuwa ukiendelea hata nje ya nchi ambapo wazungu huja Tanzania na kupiga picha za watu maskini na kuzipeleka kwao kutengeneza mabilioni kwa kisingizio cha kuhamasisha watu wao matajiri kuwachangia waswahili wenye dhiki. World Vision linaongoza kwa jinai hii. Inashangaza ni kwanini mamlaka zetu haziwazuii hawa wafanyabiashara ya nafsi za watu kupiga hizo picha.
Tukirejea kwa Matonya, alikuwa shujaa aliyewabana watawala wetu. Hata walipowaficha maskini wengi vijijini, yeye alikharifu hujuma hii na kujitokeza na kuomba, hasa jijini Dar es Salaam ambako ni moyo wa nchi.
Matonya atakumbukwa Dar es Salaam, Dodoma na Morogoro (alikoweka makao yake ya muda baada ya kutimuliwa kwa muda mfupi na Makamba kabla hajamdharau na kumshinda na kurejea Dar).
Kifo cha Matonya ni pigo kwa taifa, hasa maskini aliowawakilisha kwenye uso wa nchi kwa kung’ang’ania kuomba badala ya kuiba. Inashangaza watawala wanaosifika kwa kuombaomba kumfukuza ombaomba mwenzao. Je, ni kwa sababu hakuwa ombaomba mwenye suti au anayetumia kalamu?
Ingawa kwa jicho la kawaida Matonya alionekana kuwa mtu wa kawaida, hakuwa mtu wa kawaida. Matonya alikuwa supastaa wa kweli tofauti na hawa masupastaa uchwara wa maigizo na wa siasa wanaochafua maadili na kuwa chanzo cha maangamizi ya umma.
Matonya alikuwa kioo cha jamii iliyoharibikiwa. Jamii ya ufisi, unafiki na kujisahau. Hakuficha udhaifu wake wala mahitajio yake. Alipeperusha bendera ya watu maskini. Matonya alikuwa bora kuliko majizi na majambazi ambayo yameuza rasilimali zetu hadi kufikia kuuza hata bendera yetu.
Alifanya kazi hata kama ilidharaulika tofauti na majambazi na matapeli wanaopewa kazi ya heshima wakaidhalilisha kwa ufisi upogo na uroho wao. Matonya hakuwahi kuibia benki kama wale majambazi wa EPA.
Matonya alihubiri dini ya kweli ya umaskini utokanao na unafiki na ufisi tofauti na wahubiri wengi wa dini ambao ni matapeli. Kama kuna pepo basi asipoingia Matonya hawa majambazi wenye suti wataishia kwenye moto wa aina yake.
Ingawa Matonya alikuwa ombaomba asiyevaa suti kama wale wanaovaa suti, anapaswa kuenziwa kwa kuwa darasa na kioo cha jamii kwa wenye akili na uzalendo. Matonya alikuwa ombaomba wa kutengenezwa na ombaomba wenye masuti. Maskini hakuomba dola wala yen.
Yeye aliomba ili kuishi na siyo kuomba kwa tamaa na roho mbaya kama wanaoomba mabilioni wakayaficha ugenini au kuyatumia kutafuta ukubwa. Kwa Matonya maisha yalikuwa rahisi na ya wazi tofauti na ombaomba wenye mamlaka, ambao hufanya maisha yao kuwa magumu na kujiona miungu.
Matonya hakuomba rushwa iwe ya dola, shilingi, ngono, au ardhi. Matonya hakuomba rushwa ya kusomeshewa watoto wala kutoa upendeleo katika kazi au mtihani. Matonya hakuruhusu mkewe au mtoto wake kutumia nafasi yake. Hatujui kama watoto wake walikuwa ombaomba au vinginevyo tofauti na wenye madaraka ambao hugeuza mali ya familia, ukoo na marafiki hata waramba viatu wao.
Matonya hakuwahi kutoa ajira kwa upendeleo, udugu, rushwa, udini wala jinai yoyote itendwayo na waitendao chini ya kivuli cha madaraka. Matonya hakuhusika na wizi kule TRA, Tanesco, BoT, Maliasili, Uhamiaji, Bandari na kwingineko kunakosifika kwa wizi. Hakuhubiri kutenda miujiza ya kitapeli wala kuwaibia wanyonge, hakuhubiri maji na kunywa mvinyo.
Kama Matonya angegombea urais ningempa kura yangu. Kwani Matonya hakuwa binadamu tu bali mwakilishi wa kweli wa wanyonge. Matonya hakuwakilisha tumbo lake wala kupewa posho za makalio, usingizi na umbea. Ingawa Matonya alionekana kuomba na kula dezo, ukweli ni kwamba alitoa jasho kupewa alichopata. Nenda kapumzike mzee Matonya ulikuwa changamoto kwa wenye akili na udhu.
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 29, 2012.

Tulikataa futari na mashindano uchwara


“Hili kampuni la simu lenye kila dhambi ya ufisadi eti lilitaka kutufuturisha. Kwanini msitupe huduma bora badala ya kutuhonga vipilau na upuuzi wenu? Ukipiga simu unaambiwa ongeza salio halafu wanakata pesa yako hata kabla hujaongea,” alianza kulalamika Dk. Mzee Maneno.
Dk. Mchunguliaji: “Wakati juzi namdeep shemeji yenu si walinikata shilingi 1,000!”
Dk. Machungi: “Mgosi siyo kudeep bai kupeep.”
Mchunguliaji: “Nilisema hivyo makusudi kuona kama mnajua kimombo. Hata wewe mgosi wapitia Mombo ukienda Lushoto, lazima ujue kimombo.”
Machungi anazidi kuongeza uhondo: “Hujui kuwa kishambaa na kingeeza ni lugha moja?”
Mbwa Mwitu hakubali: “Mgosi sasa huo uongo wa mchana. Unakuwa muongo kama wanasiasa!”
Machungi anakula mic tena: “Mgosi si uongo. Hujawahi kusikia wazungu wanasema why? Wasambaa tunasema kwai.”
Kijiwe hakina mbavu kwa jinsi magwiji hawa wa vituko wanavyopeana mistari.
“Jamani mie naona tungejadili hili la mikampuni mijizi inayotoa huduma chafu na kuwaibia watu kila siku huku serikali ikiinyamazia,” alipendekeza Dk. Profesa Msomi Mkatatamaa.
“Kweli msomi umelonga. Maana walevi wamekuwa kama mataahira. Ajabu makampuni haya ya kitapeli eti nayo yanafuturisha watu! Futari au hongo tena ya pesa chafu ambazo kuzila ni ukafiri tosha.” alirai Dk. Mipawa.
Profesa Msomi anaongezea msumari kwenye madai yake: “Mimi naona kama baadhi ya watawala wetu wanafanya biashara na hii mikampuni. Maana badala ya kututumikia sisi wanaitumikia hii mikampuni yao ya wachukuaji wanaowaita wawekezaji. Uwekezaji gani wa kutupa huduma chafu na kuchukua kila kitu?”
Wakati kikao kinaendelea aliingia Dk. Shemihiyo, mdogo wake Dk. Machungi (huyu ni memba mpya aliyetokea Lushoto) akiwa anatabasamu.
Baada ya kutuamkua alitoa dukuduku lake: “Wagosi, nimepewa ujumbe na kampuni ya simu ya kuwataarifu kuwa mnakaribishwa kwenye futari Ijumaa ijayo baada ya swala laswir.”
Dk. Profesa Mkatatamaa anadakia hata kabla Shemihiyo hajamaliza: “Yale yale tuliyokuwa tukiongelea. Yaani mikampuni yenyewe mijizi na haina huruma nasi sasa huu uumini wa kutufuturisha unatoka wapi kama siyo rushwa na kutufanya majuha tena makafiri?”
“Dk. Prof Msomi unashangaa makampuni tapeli na jambazi kufuturisha! Hukusikia wanasiasa wachafu tena mafisadi wanaonuka kwa rushwa na ufisadi nao wakifuturisha na kujipiga vifua kuwa wamefanya jambo la maana wakati ni ukafiri wa kutosha?”
Dk. Mpemba ameguswa pabaya: “Yakhe usemayo nkweli. Siku hizi hata futari na dini havina maana tena wallahi. Kula mwenye fedha anafedhehesha dini kwa fedha zake. Juzi sie ntaani kwetu tulikaribishwa kwenda futuru na rahisi tukasusa isipokuwa waroho wachache.”
Dk. Mbwa Mwitu aliamua kukwanyua mic: “Dk. Mpemba, shehe na ustaadhi kama wewe ungeenda hakika, licha ya kuwa kafiri ungegeuka shehena badala ya shehe.”
“Dk. Mbwa Mwitu wasema kweli wallahi wabillahi. Siku hizi mashehe na wasomi wa dini tu-wachache. Mie nlihifadhi koraani yote na kusoma fikh. Hivo najua dini vilivo. Sikusoma popote eti mtu asokuwa nsilamu kufuturisha. Afuturisha vipi wakati yeye hafungi wala kuishi angalau kwa haki achia mbali kuwa muumin au muuminat?”
“Dk. shehe ustaadhi hafidhi Mpemba umenena. Mimi nilikuwa nashangaa sana kuona watu wasio na dini isipokuwa ufisadi eti nao wakifuturisha. Dini imegeuzwa mchezo wa kamari ambapo kila mwenye nazo hucheza. Huwezi kufuturisha mtu wakati wewe ni mchafu na wengine ni makafiiri mie sina mfano.
“Huwezi kuiba pesa ya umma au ukatajirika kwa mihadarati halafu ukafuturisha. Huu ni ukafiri ingawa mie siyo Mwislamu.”
“Allah Subhana anasema kwenye surat Kaffirun kuwa; ‘hamuabudii ninayemwabudia. Siabudii mnachokiabudia. Mna dini yenu. Nina dini yangu’.” Alikariri aya Dk. Shehe Mpemba na kuwaacha watu vinywa wazi.
Aliendelea: “Wao waabudia pesa na wizi, uchafu, rushwa na dhulma. Kwanini wataka kuwaingiza watu wema kwenye dini yao hii chafu? Ajabu watu nao wajipeleka kama vile hawana macho!”
Dk. Mbwa Mwitu alichomekea: “Kuna fisadi ambaye sitaki kumtaja anayefanya kazi serikalini ambaye anajulikana kwa wizi na uasherati wake. Eti naye alitaka kutufuturisha. Nilimpa pasonali wazi wazi.”
Akiangalia huku na huku na huko aliendelea: “Kama kawaida yangu nilimpa wazi na kumuuliza; nani kawaambia tuna njaa ya futari? Tuna njaa ya maendeleo na kutendewa haki finish.”
Huku kijiwe kikionesha wasiwasi juu ya maneno ya Dk. Mbwa Mwitu ambaye tunamjua, kama jina lake hawezi kukataa kitu na kama ana dini basi dini hiyo ni ulaji, Dk. Machungi alichomekea: “Sisi ni maskini kwei akini si maskini wa mawazo.
“Hatitumii matumbo yetu waa masabui kufikii kama wao. Yaani mmegeuza kaya yetu kuwa kaya ya upuuzi! Hatihitaji hongo bai tinataka haki na huduma safi. Hakuna ukafii kama kufutuu pesa chafu ya wizi na ujambazi.”
Akiwa anaendelea kusema, mara Mzee Maneno alinong’ona: “Huyu mwenzetu naye anataka kutufanya majuha. Pamoja na kuzaliwa na wazazi waswalihina huwa haishi maeneo ya kigogo kukamata kitimoto. Huyu hawezi kukataa futari hata kama ni ile itokanayo na pesa za bangi, miunga, bia, kamari, wizi, rushwa na ufisadi.”
Baada ya kuona mada inaanza kuharibika kutokana na baadhi ya wenzetu kuanza kuwasengenya wenzao, mzee mzima ambaye nilikuwa kimya muda wote niliamua kuokoa jahazi. Nilikohoa kidogo na kubwia kahawa yangu kidogo na kuendelea: “Jamani, naona kama mnaanza kutoka nje ya mada. Sasa nitawarejesha. Yote mliyoongea kuhusiana na dini kugeuzwa nyenzo ya kutolea rushwa ukiachia mbali kudhalilishwa, mie nadhani tutoe azimio.”
Nilikatua kashata na kuendelea: “Kwanza tulaani mchezo huu mchafu wa kugeuza dini kitu cha kuchezea. Pili tulaani uroho na upogo wa watu wetu. Tatu tuhakikishe haya makampuni ya simu yanayotuibia huku yakitupumbaza na bahati nasibu na mashindano uchwara yanafurushwa kayani mwetu. Nne viongozi wote mafisadi wanaoyakingia makampuni haya kifua tuhakikishe wanatimuliwa.
“Tano, tumrejee Mwenyezi Mungu huku tukijitahadhari na uroho, usanii kama wa wale wanaokataa kuhesabiwa utadhani hawatahesabiwa. Nasema mtahesabiwa hata mkiwa maiti. Hata mkihama nchi tutawafuata huko na kuwahesabu. Yule jamaa Mrundi anayegomesha walevi aitwaye Pondwa lazima apondwe na kunyea debe.
“Acha niishie kwenda kumzika rafiki kipenzi chetu ndugu yetu mzee Matonya. Sijui wapenda kuzika nao watakuja au kwa vile huyu alikuwa havai suti kama wao basi hafai.”
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 29, 2012.

Wednesday 29 August 2012

Mchungaji au mchunaji, injili au unga?







    Hapo juu ni hekalu jipya la anayejiita mchungaji Getrude Rwakatare lillilozinduliwa huko Mbezi Beach  nje kidogo ya jiji la Dar es salaam hivi karibuni. Wengi wanajiuliza. Huyu ni mchungaji au mchunaji? Je huu utajiri wa ghafla ameuchuma wapi na kwa muda gani na kwa kufanya nini? Kweli Tanzania imegeuka nchi ya wanyang'anyi ambapo mtu anaweza kulala maskini akaamka tajiri na hakuna anayeuliza. Je Rwakatare anafanya biashara gani na analipa kodi kiasi gani? Tuna haja ya kuuliza hasa baada ya kugundulika kuwa Rwakatare ni mmojawapo wa watu waliokamatwa wakitumia umeme wa wizi. Jumba kama hili ukilijenga kama hapa Kanada ujue utatozwa kodi hadi ukome. Isitoshe huwezi kuwa na utajiri ambao hauna maelezo kabla ya mamlaka ya kodi kuuweka mikononi hadi utoe maelezo yanayoeleweka ulivyochuma. 

Monday 27 August 2012

Ngono inapotumika kama silaha dhidi ya ukandamizaji



Wanawake nchini Togo wametakiwa kutojamiiana na waume zao kwa wiki moja ili kumlazimisha rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe Eyadema kuachia madaraka.
Baada ya Eyadema aliyerithi madaraka toka kwa baba yake aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 37 hadi alipokutwa na mauti, kuonyesha kutopenda upinzani, wanawake wameombwa wawasusie waume zao hili likiwa ni shinikizo wa Eyadema. Wengi wanangoja kuona matokeo ya aina hii mpya ya upambanaji kwa ajili ya haki za kidemokrasia. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Saturday 25 August 2012

Mtu wa kwanza kwenda mwezini afariki


Neil Armstrong dies at 82. (Getty Images)


Jina Neil Amstrong likitajwa wengi hukumbuka 1969  mwaka ambao Amstrong alikanyaga kwenye uso wa mwezi na kuwa mtu wa kwanza kufanya hivyo. Tukio hili liliripotiwa dunia nzima na kuondoa hekaya nyingi za kweli na uongo juu ya mwezi. Tangu wakati ule sayansi ilikua na kuweza kufikia kuanza kwenda kwenye sayari nyingine za mbali kama Mars.
Amstrong rubani wa majaribio wa Kituo cha Utafiti wa Anga za Juu cha Marekani (NASA) amefariki akiwa na umri wa miaka 82. Baada ya kuwa mtu wa kwanza kwenda mwezini na kupata umaarufu dunia nzima, Amstrong hakulewa sifa. Mwaka 1971 alijiuzulu kazi katika Nasa na kuamua kwenda kufundisha unajimu chuo kikuu cha Cicinnati. Amstrong hakupenda makuu wala sifa zaidi ya kujiishia maisha yake binafsi kama mstaafu yeyote. Kwa habari zaidi kuhusiana na msiba huu BONYEZA hapa.



Friday 24 August 2012

Somo toka maisha ya marehemu mzee Matonya

Picture
Ingawa marehemu mzee Matonya aliingia kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kwa kile waingereza waitacho wrong reason, ameacha somo kubwa kwa wenye kufikiri. Taarifa zilizotufikia ni kwamba mzee huyu maarafu kama alama ya umaskini na ufisi wa taifa letu amefariki dunia. Mzee huyu mwenyeji wa Dodoma alikuwa kivutio kwa wengi jijini Dar Es Salaam ambapo yalikuwa makao makuu ya shuguli zake za kuomba. Kipindi fulani alimtoa jasho mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam wa wakati ule Yusuf Makamba alipomuamuru ahame na kuachana na shughuli za kuomba kwa sababu alikuwa akilidhalilisha taifa. Matonya hakukubali kufa kibudu. Alipambana na Makamba hadi kumtishia kuwa angemng'oa kwenye nafasi yake.

Sababu kubwa aliyotoa Matonya ni kwamba akina Makamba walikuwa walafi wanaokula kwa mikono na miguu huku wengi wakiangamia. Hivyo, kuomba kwa Matonya ilikuwa ni haki yake. Na kweli, kuomba ni bora kuliko kuiba au kujihusisha na ufisadi, mihadarati na jinai nyingine ambazo zimelifikisha taifa letu lilipo. Kwetu sisi Matonya alikuwa matunda ya siasa za kifisi na ubabaishaji. Pia Matonya alikuwa alama na kumbukumbu kwa wenye akili kuwa mambo hayakuwa sawa. Ni bahati mbaya kuwa watawala wetu hawakujifunza suto lililotokana na shughuli za Matonya. Badala yake walitaka kutumia maguvu kumficha ili asiwaudhi wao na wageni wao hasa wafadhili. Hakika huu mchezo umekuwa ukiendelea hata nje ya nchi ambapo wazungu huja Tanzania na kupiga picha za watu maskini na kuzipeleka kwao kutegeneza mabiloni kwa kisingizio cha kuhamasisha watu wao matajiri kuwachangia waswahili wenye dhiki. World Vision linaongoza kwa jinai hii. Inashangaza ni kwanini mamlaka zetu haziwazuii hawa wafanya biashara ya nafsi za watu kupiga hizo picha.

Tukirejea kwa Matonya, alikuwa shujaa aliyewabana watawala wetu. Hata walipowaficha maskini wengi vijijini, yeye alikharifu hujuma hii na kujitokeza na kuomba hasa jijini Dar Es Salaam ambapo ni moyo wa nchi. Matonya atakumbukwa Dar Es Salaam, Dodoma na Morogoro (alikoweka makao yake ya muda baada ya kutimuliwa kwa muda mfupi na Makamba kabla hajamdharau na kumshinda na kurejea Dar.)

Kifo cha Matonya ni pigo kwa taifa hasa maskini aliowawakilisha kwenye uso wa nchi kwa kung'ang'ania kuomba badala ya kuiba. Inashangaza watawala wanaosifika kwa kuombaomba kumfukuza ombaomba mwenzao. Je ni kwa sababu hakuwa ombaomba mwenye suti au anayetumia kalamu?
Nenda kapumzike mzee Matonya ulikuwa changamoto kwa wenye akili na udhu.

Thursday 23 August 2012

Kuna watu wana hasira waking'atwa na nyoka huwang'ata nyoka pia!



Jamaa mmoja nchini Nepali ametoa kali baada ya kung'atwa na nyoka aina ya Cobra. Baada ya kung'atwa jamaa alipandisha hasira na kumfukuza nyoka hadi kumkamata. Wajua alifanya nini baada ya kumkamata nyoka? Jamaa alimng'ata nyoka hadi kumuua. Hiki ni kituko si cha kawaida. Maana tumezoea kusikia mtu aking'atwa na nyoka na mwenye kung'atwa kumpiga nyoka na kumuua lakini si kumng'ata kama ilivyotokea kwenye kisa hiki. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Wenye swimming pool mngefanya nini hii ingewatokea?



Nchini Afrika Kusini ndama wa kiboko mwenye miaka miwili amekuwa mgeni asiyetegemewa kwenye swimming pool ya mtu mmoja. Ndama huyu aliyeandamana na mama yake aliyekuwa akienda mateneti kujifungua, aliachwa na mama yake kiasi cha kupotea. Mama alikwenda hospitali (mwituni) kujifungua na kurejea na kichanga chake huku akimpoteza ndama yake mkubwa. Hivyo, ndama alilazimika kuzurura hadi alipofanikiwa kupata bwawa la kuogelea la mtu na kujichimbia mle. Je mgeni huyu ungemkuta kwenye bwawa lako la kuogelea ungefanya  nini? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Wednesday 22 August 2012

Waliouza bendera yetu Iran watajwe


INGAWA Watanzania hawakushupalia kashfa ya Tanzania kuiruhusu Iran kupeperusha bendera yao kwenye meli zake za mafuta baada ya kuwekewa vikwazo kimataifa, kashfa hii inafichua uoza wa serikali.
Je, hili nalo limefanyika kwa ridhaa na heshima yao au dharau na hujuma kwao? Ni jambo la hatari na kujidhalilisha kuruhusu bendera ya nchi kutumiwa na nchi nyingine kufanya biashara hatari.
Hii ni biashara hatari ikizingatiwa kuwa, jumuia ya kimataifa ilipitisha azimio la kuiwekea vikwazo Iran, nayo ikakubali hatua hii, vinginevyo ingeshupaa na kutaka itendewe haki kama kweli haki yake imekiukwa kuliko kujificha chini ya bendera za nchi nyingine.
Bendera ya taifa, ni alama na kitambulisho cha taifa chenye thamani kuliko kitu chochote, ikiwemo hata taasisi ya urais.
Hivyo, anayechezea alama hii awe mtu binafsi, shirika na hata mamlaka, anapaswa kuchukuliwa kama msaliti na mhaini ambaye adhabu yake, ni kifo chini ya sheria ya Tanzania.
Kiongozi yeyote asiyejua umuhimu wa bendera yetu kiasi cha kuiruhusu ichezewe na kuuzwa kama karanga kukidhi tamaa za kipumbavu na kifisi za baadhi ya maofisa wa serikali, hafai kuendelea kuwa hata kuitwa kiongozi wa taifa.
Kuendelea kuwa na watawala wa namna hii, hakuna tofauti na kulibaka taifa.
Asiyechukizwa na kitendo cha bendera yetu kutumiwa na taifa jingine kuficha uchafu wake, hapaswi kuitwa hata Mtanzania achia mbali kuwa kiongozi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa bendera ya taifa, si vibaya kuwataka wananchi waamke na kuwawajibisha viongozi wasiolinda maslahi ya taifa kiasi cha kuruhusu bendera yetu kutumiwa na taifa jingine kuepuka kuumia kiuchumi wakati sisi tunaweza kuumizwa na upogo huu.
Kwa kuzingatia umuhimu wa bendera kama alama ya taifa, ni ajabu kuwa Watanzania, hata waliposikia habari hii ya kuudhi, hawakuhamanika kuiwajibisha serikali inayojiita yao.
Je, haya ni matokeo ya ujinga, ukosefu wa uzalendo, woga au ufisadi wa kimawazo kiasi cha kushabikia kila upuuzi unaoingiza pesa hata kama hiyo pesa hawaipati?
Rejea imani kuwa ujanja ni kupata na hapendwi mtu. Je, Watanzania tumekubali kuwa wa hovyo kiasi hiki hata kwenye maslahi ya taifa na vizazi vijavyo?
Hili lingetokea kwenye nchi zenye watu wenye mwamko na kujua heshima na stahiki ya nchi yao, lilitosha kuiondosha serikali iliyoko madarakani.
Maana hata ukiangalia utetezi uliotolewa na serikali, ni wa kichovu na uongo mtupu.
Kinachokera na kuamsha hasira, ni utetezi uliotolewa na serikali baada ya kubanwa kuhusiana na kashfa hii.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Bernard Membe alikaririwa akisema kuwa kama serikali itagundua kuwa meli 36 za Iran zilisajiliwa, basi itafuta usajili huo!
Hii ni ajabu. Kumbe wanajua hata idadi ya meli zilizobebeshwa bendera ya taifa letu halafu wanajifanya hawajui!
Eti wanasema, kadhia hii imesababishwa na wakala aliyeko Dubai! Ala!
Huyu wakala hata hawasemi atachukuliwa hatua gani wala hawana mpango wa kuchunguza kadhia hii.
Ni ajabu kukuta serikali na mamlaka yake zinajua kuwa wakala huyu aliyetambuliwa kutoka visiwani, bado hajakamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu na uhaini haraka sana iwezekanavyo ili kurejesha heshima ya serikali na taifa.
Wameshindwa hata kuomba msamaha wala kulaani uchafu na ufisi huu. Je, namna hii hayajajengeka mazingira ya kuipiga mnada Tanzania hata kwa makundi ya jinai kama inavyoanza kubainika baada ya vigogo wa vita wa Somalia kuanza kuwekeza nchini?
Kesho utasikia kuwa makundi ya kigaidi ya Al Shabaab, Al Qaeda hata Boko Haram yanatumia bendera ya Tanzania kwenye makambi yao ya kuandalia magaidi wa baadaye.
Huu ni ushahidi kuwa, kwa uongozi huu nchi yetu si salama hata kidogo.
Maana tangu serikali ya sasa iingie madarakani, imekuwa na sifa ya kufanya madudu na kukumbwa na kashfa.
Kashfa ya kwanza ilikuwa Richmond ikifuatiwa na Dowans na sasa Iran.
Tunapelekwa wapi Watanzania? Je, tunaogopa nini kuwawajibisha watawala wetu ambao wamethibitisha kuwa madarakani kwa bahati mbaya na kwa ajili ya maslahi binafsi?
Sitashangaa kesho nikisikia kuwa, baadhi ya mawakala wa kununua mafuta toka Iran ni makampuni yenye ushawishi kwa wakwasi watu walioko madarakani kuchuma badala ya kupanda. Sitashangaa kusikia makampuni ya mafuta yaliyoibuka hivi karibuni yakifanya biashara na Iran.
Kimsingi, kama hatua hazitachukuliwa kwa wahalifu walioweka maslahi na mustakabali wa taifa, hatari itathibitisha dhana kuwa tunaongozwa na watu wasio na uzalendo wala visheni ukiachia mbali kutochelea kinachowakuta baada ya kuachia madaraka.
Hii itajenga picha kuwa, watawala wetu ni wagumu wa kufikiri na kuelewa, hasa kutokana na kutanguliza matumbo yakiwaelekeza kwenye maslahi binafsi badala ya mustakabali wa taifa.
Kwa hili la kuuza bendera yetu kwa taifa lililowekewa vikwazo, ni ushahidi kuwa sasa Tanzania inaweza kuuzwa na kila jambazi kiholela na kwa yeyote bila kuchukuliwa hatua.
Tulianza na ujambazi wa rada, tukaja kwenye wa EPA na hatimaye wa IPTL, Richmond, Dowans na sasa tunauza bendera ya nchi yetu kana kwamba hatuihitaji!
Yuko wapi rais kutoa maelezo ya kina na kutoa msimamo wake na serikali yake juu ya kuwashughulikia hawa wahalifu? Kiko wapi chama tawala kutoa maelezo tena yanayoingia kichwani au kuwa tayari kuwajibika?
Jamani, wako wapi Watanzania kutaka maelezo na uwajibikaji? Je, tumekuwa wa hovyo kiasi cha kuuzwa na kila jambazi kwa amtakaye na bei atakayo?
Tubadilikeni haraka kabla hatujabadilishwa na mahitajio ya wakati huu, tena kwa nguvu na aibu.
Waliouza bendera yetu kwa Iran lazima watajwe na kushughulikiwa haraka, vinginevyo serikali iwajibike.
Vinginevyo, itajenga dhana kuwa hao ni mawakala au washirika wake katika hujuma hii kama haitawashughulikia.
Je, Tanzania imekuwa rahisi hivi kiasi cha kuchezewa na kila kibaka?
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 22, 2012.

Tanzania - Iran Saga:Implications for E. Africa


When it surfaced, it was treated just like any other rumours. But Tanzania’s re-flagging Iran ships is now an open secret. It came to light that Iranian tankers were flagged by Tanzania and Tuvalu in order to avoid and escape nippy and biting sanctions extended to Iran. By doing so, Tanzania, a member of the East African Community, was intentionally and maliciously breaking international law. So too, Tanzania was seriously endangering the security and economies of the whole region. Tanzania, just like anyone else, knew that Iran was sanctioned due to its stance of aiding terrorist groups and clinging on its nuclear weapon programs. Currently, East African countries are facing a threat from Somalia’s Al Shabaab whose terrorist operations have already seen two countries namely Kenya and Uganda attacked at various times. Kenya with its friends is currently in Somalia trying to flush, if not to wipe, out Al Shabaab.
Recently, the Senate in the US was pressuring President Barack Obama to extemporarily slap Tanzania with sanctions as a punishment for re-flagging Iran. A letter from SenatorsMark Kirk (R-IL) and Bob Menendez (D-NJ) was quoted by the Cable as saying, “ The actions of the Tanzanian and Tuvaluan ship registries directly undermine the international community's ongoing diplomatic efforts to prevent Iran from obtaining nuclear and ballistic missile technology, and appear to be in violation of the legislation you just signed into law.” Tanzania is not a parvenu in the EAC. If sanctions are applyied on it, such a move will mean that other East African Countries trading with Tanzania are likely to be directly and indirectly affected. This will not only curtail economic development in the bloc but will also cause diplomatic confusion especially for landlocked countries using Tanzania’s harbours to import and export their commodities.
More on re-flagging Iranian tankers, Tanzania admitted to have caught redhanded and promised to deregister 36 tankers. Interestingly, when the government was cornered it said that it was not awared of such national humiliation-cum-sabotage. To save its face, Tanzania blamed the whole fracas on the so-called Dubai-based the Tanzania Zanzibar International Register of Shipping. If anything, Zanzibar’s status in the EAC is going to create many problems if not addressed legally and timely. For there are some matters that are non-union it can use either blindly or purposely to sabotage the EAC. Given that there are some grumblings and confusion over the union between Tanganyika and Zanzibar currently chances are that Zanzibar knew what it did. It might have ignored the consequences knowingly that if Iran paid it handsomely the monies will end up in its coffers at the expense of the whole region. Circumstantially, this means Zanzibar is open for whoever has a big purse even if that person is Al Shabaab. Evidentially, it means that if Iran pays Zanzibar to accommodate Al Shabaab Zanzibar will comply. These being the possibilities for Zanzibar to gain money, being an island, proves to be a very good strategic area for Al Shabaab and other terrorist groups shall they want to use provided they have cash for their operations. Is this going to be a precursor of so much to come?
Looking at who is bearing responsibility, Zanzibar is likely to scot-free. Reports have it that Zanzibaris government under the influence of one undisclosed former Zanzibari president, Zanzibar entered in agreement to re-flag Iran’s tankers. Up to now Zanzibar has three living former presidents namely Ali Hassan Mwinyi who also saved as union President, Salmin Amour and Amani Abeid Karume. Despite all, Zanzibar is not in the limelight and does not face any hostilities to answer questions resulting from this scandal. It is Tanzania that is running the show when it comes to responsibility. Iran ship re-flagging by Zanzibar is like the case involving a doli incapax or juvenile whereby he commits the crime but the parents bear all consequences. If such a child is not caned is likely to commit even gravier crimes than the one he has already committed.
As the heat kept on rising on the matter, Tanzania’s foreign affairs minister Bernard Membe was quoted by BBC as saying, "If it is confirmed that the ships flying Tanzania's flag are indeed from Iran, we will take steps to deliberately obliterate the registration.” Again, despite all these braggadacios the dent had already been made. For such admission US authorities have the evidence it need to prove and warrant sanctions shall it decide to. Tanzania to avoid punishment for abeting with Iran will all depend on the mercy of the US and the international community.
Although Tanzania’s international relations policy is the matter of its sovereignity many still wonder how Tanzania could take such suicidal and selfish stance ignoring the consequence the regional can suffer from its move. Knowing how Iran has secretly been supporting terrorist groups to destabilize countries with the view that Islamic sentiments would comeforth and have a say in the government,why didn’t Tanzania think about its neighbours especially Kenya that has been under Al Shabaab’s attack? With such better- than- thou mentality will EAC be safer?
Source: The East African Executive Magazine August 22, 2012.

Kumbe na waheshimiwa wanakula kaya!


Walianza na kashfa ya kulala mjengoni huku wakilipwa posho ya kuuchapa, wakaona haitoshi.Wakaja na madai ya kuongezewa posho ya makalio, wakaona hii haichangamshi. Maana walevi licha kushangaa kuwa makalio nayo yanalipwa posho waliona kama wizi na ujambazi wa kutumia madaraka badala ya bunduki.Walikuja na kashfa ya kula rushuwa wakaona hii cha mtoto.Sasa wamekuja na kubwa ya kuvuta sigara kubwa na kunusa bwimbwi. Haya si maneno yangu. Ni maneno ya naibu wa Microphone Johab Ngudai.
Mama Microphone bint Speaker Annae Shemamba Makida Makida ambaye inaelekea anatoka ukoo wa mgosi Machungi Shekiango naye amekuja na mpya yake. Aliwapasha wale wabunge wa underwear au misukule akiwataka watoke usingizini na kuingia kwenye kimbembe cha kugombea kura za kula badala ya kutegemea nonihino zao ingawa naye aliupata uspiika kwa njia hiyo hiyo ya nepi. Leo hili siyo hoja, another day.
Turejee kwa wala majani. Kama wao wanavuta mibangi na kubwia bwimbwi kwanini wasiuze hiyo midudu? Kumbe ndiyo maana wameshindwa kuondoa biashara ya mibwimbwi kwa vile wanauza na kubwia? Ila sisi walevi tukujivutia vijibangi kidogo ndata hao na kiherehere chao. Badala ya kuwasumbua wala bwimbwi wanaojipa raha kama w alivyoshauri mkuu wa kaya, kawakamateni hao wanaokula vvyote, bwibwi, majani na kodi zenu. Wala unga hawamwibii mtu. Siyo kama hawa wanaosema nipe kura yako nikuibie kula yako. Kama nyinyi kweli walume si mkavamia mjengo na kuwatoa nje mkiwa mmewafunga pingu na uhishimiwa wao? Juzi mlimuogopa yule mla rushwa Ommy Badwell. Nyinyi na Takokuru hamna maana kabisa. Nawaona kama vibaka mliojivalia magamba. Lakini siyo kosa lenu bali kaya yenu. Maana kwa masikio yangu juzi nilimsikia mkuu mwenyewe mzee wa sanaa Njaa sorry simalizii, akimtetea mzee wa Vijisenti Endelea Chenga kuwa wainglishi waliomchunguza na kukuta kuwa alikwapua eti walikosea tena kuchapisha. Huyu jamaa naye kweli mpuuzi. Yaani jitu zima na kubwa lenye cheo kikubwa linadanganya kitoto! Mwe! Tumekwisha kama wakuu wetu ndiyo hawa!
Kaya yetu haishi vituko. Juzi nilitaka kujinyotoa roho kama siyo bi mkubwa kunibembeleza kuwa nikifanya hivyo atabaki mpweke. Kwa hiyo wapenzi wa mipasho na kijiwe mshukuruni huyu bi mkubwa maana ningejinyotoa roho msingepata mtetezi wala mpashaji wa hawa wala majani. Basi mpigieni makofi tafadhali huku mkijipanga kuwapiga makofi wala majani na wabwia unga wanaokula kodi zenu. Wajua kwanini nilitaka kujinyotoa roho? Si pale yule jambazi Koshita Muhalu aliyeiba njuluku kule Urumi akiwa sijui balozi sijui mwakilishi alipoachiwa na pilato. Jitu linaiba mifweza tena kwa mabilioni, linafunguliwa kesi uchwara halafu wanasharia wa lisirikali wanafanya mchezo mchafu linashinda na kulipwa pesa ya wale wale lililowaibia. Tunakwenda wapi? Mapilato wetu nao wamegeuka kama vyangu. Leo wanatishwa na lisirikali wanatoa hukumu za ajabu ajabu. Hamkuona walivyowahujumu matabibu na wapiga chaki?
Anyway, leo hayo siyaongelei. Nitaongelea hili la wahishimiwa wa mjengoni kuvuta mibangi na kubwia miunga. Hivi mlitegemea nini kutoka kwa watu waliopata uhishimiwa kwa njia ya rushwa, kuchakachua au chupi? Hivi kama tunafanya uchunguzi wa walioiba kura za kula au kuhonga na kuchakachua si mjengo utabaki na miviti tu? Hawa wavuta wabangi wanaowakilisha matumbo yao wanapaswa ima wakimatwa wanavuta mibangi wafikishwe kwa pilato ingawa mapilato wamegeuka kuwa voda fasta au watunge sheria ya kuruhusu watu kujivutia mibangi na kubwia miunga ili bei zake zishuke nasi tufaidi. Kumbe ndiyo maana wawekezaji sorry wachukuaji wanaiba kwenye kaya utadhani shamba la bibi tena bibi mwenye chizi na kipofu! Sasa kama wahishimiwa wanaingia mjengoni wakiwa wamevuta mibangi mnadhani watashindwa kuwa na mawazo ya kibangibangi? Tena nakumbuka mmoja niliyekuwa nikimjua anavuta bangi akiwa mjengoni ingawa alisharudisha namba mwendazake. Wajua nani huyu? Mtoto wa njini msiseme dito.
Kwa utaalamu wangu wa madawa niliosomea kule Ujerumani nikapata shahada ya PhD in Medicine isiyo ya kughushi kama za akina Buttoks Masaburi, Makorongo Muhanga, Meli Nyago, Doedodos Kamaliza na wavuta bangi wengine. Nakuta kuwa ndiyo maana wahishimiwa wanapenda kulala mjengoni. Hii ni kutokana na kile tunachokiita kitaalamu effects of consuming and abusing and overusing and nonihono drugs and bwibwiz. Nadhani jamaa zangu akina Stivi wahasira na Joni Kombahaha mnanipata. Maana nyinyi kwa kuchapa usingizi mjengoni utadhani baby aliyezaliwa jana au nyoka aina ya kifutu! Hata mgoshi Machungi aliwahi kuniambia kuwa yule mzee wa Kisambaa nadhani mwamjua aitwaye Jose Makambale alikuwa anakula ndumu ndiyo maana alikuwa akipayuka hovyo hovyo. Inawezekana hata huyu jamaa Njaa Kaya mwenyewe anaweza kuwa anakula majani maana ile anguka anguka sieewi eewi. Anyaway nitamuuliza mgosi Machungi wa Kiango aniambie tena. Sasa jamani kama watunga sharia tena wanaoitwa wahishimiwa wanakula mijani na kubwia mibwimbwi hao watoto wetu mashuleni si wataogea? Au ni kwa vile wengine wanaokula mibangi na kubwia mibwimbwi wakizaa watoto na watoto wanakuwa wameishaathirika na mibwimbwi yao? Ndiyo maana mnawaona mitaani wanatembea matako nje na kujichorachora kila upuuzi huku wakiimba nyimbo za vurugu na kelele au al maarufu rafu.
Mie kuna kipindi nashindwa kuwatofautisha kati ya walaji na wapingaji. Maana nao ukisikia mikakati yao utajua kuna ukombozi. Badala ya kuleta mageuzi wanaleta mashauzi. Maana tangu waanze kupiga mikelele yao mara tutaandamana mara tutateka kaya mara tutapinga lile kumbe nao wanavuta mibangi! Mbona wahishimiwa wa upingaji hawakulaumu wala kukana kama nao hawali hiyo midude? Mimi nilishangaa kusikia eti Chakudema inadhaminiwa na gabacholi wa chama magamba. Hivi huu siyo uamuzi wa kibangibangi? Mtu unapinga chama chake halafu eti anajifanya anaku-love. Kama anawa-love si ajiunge na nyinyi? Au ni kwa vile anajua kuwa wote ni walaji tena wa majani na bwimbwi? Tusipoangalia mtatuingiza mkenge na kuiteketeza kaya yetu. Jamani tisiogopane. Lazima tiambiane ukwei, wapingaji nanyi mnaboa ingawa mchango wenu ni mkubwa lakini siyo kama inavyotakiwa. Tusilamu wapingaji peke yao. Hata walevi mnaboa kwa ujuha wenu wa kuwa watazamaji wakati kaya yenu nanyi mkiliwa tena mc hana kutwa.
Juzi nilisikia eti al Shabib wameishaanza kuwekeza mipesa ya uharamia kwenye kaya yenu ili baadaye wagombee urahisi. Aka! Mie simo! Acha nikambomu huyu mhishimiwa kipisi cha bangi kabla hajaingia kwenye mshangingi wake. Na ndata yule naona anatunyemelea kumbaff. Ngoja nione kama atatukamata wote ili kiumane kudaaadeki.
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 22, 2012.

Tuesday 21 August 2012

Is it the beginning of the end of Assad?


Qadri Jamil, Syria's deputy prime minister, speaks during a news conference in Moscow, August 21, 2012
If anything, many analysts and obeservers have been trying to pin down the fable as to when Syrian strongman, Bashar al Assad will leave the scene or fall from grace to no avail. But the way things look, Assad is in his last moments in power. No doubt that the world of peace lovers, peacemaker and peace builders would like to see Assad being shown the door if not killed. News that reached us is that Assad's exit is up to the grab. Having gotten in power after the death of his father, Assad has been ruling Syria just like his person estate. What has been going on since  the mass uprising has proved how Assad lacks sense of reason and humanity. He has been using his majordomos to kill innocent people indiscriminately for long. Now that the time is up for the Assad to hit the road, we can easily say that this is the beginning of the end of Assad. More on Assad's exit please CLICK hither.

Now it is true Zenawi is no more



After many speculations complication and machinations about the health of Ethiopia PM Meles Zenawi, the curtain has now fallen. The government announced the death of Zenawi just yesterday without going into the specifics of the cause of his death nonetheless. Again, Zenawi will be remembered as the guy who changed Ethiopia in both good and bad ways.  On the one hand, he ruled with the iron fist. This has no doubt about it. On the other hand, he ushered in some economic and fiscal changes. Many projects were constructed under his watch. So too, corruption dogged his administration especially the role his wife, Azeb Mesfin played in corruption. She got a moniker of Queen of Mega namely the Queen of Mega corruption. Now that the man is gone, it is time for Ethiopia to forge ahead by learning from his mistakes. He was neither an angel nor was he a devil. Who was Meles Zenawi? The answer depends on who is answering the question based on what he or she chose from Zenawi. For more information about the death of Zenawi, please CLICK here.

Sunday 19 August 2012

Kwa hili Kikwete anastahili pongezi ingawa...



Kitendo cha rais Jakaya Kikwete kumwalika rais wa Malawi Joyce Banda kutembelea Tanzania  ni cha kupongezwa. Habari zilizotufikia ni kwamba rais Kikwete alitoa mwaliko huo wakati alipokutana kwa mazungumzo mafupi kando ya mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuia ya  ushirikiano wa nchi za Kusini Masharika  (SADC), huko Maputo Msumbiji. Tofauti na matamshi ya rejereja ya waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe na mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa waliotangaza vita wakati wao si amiri jeshi mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Kwa kitendo hiki Kikwete na Banda wameonyesha ukomavu na uzalendo wa namna yake. Ndiyo kunaweza kuwapo kutokuelewana juu ya Ziwa Nyasa. Lakini bado majadiliano ni njia muafaka kuliko milio ya bunduki. Nchi zenyewe zilizokuwa zikisukumwa zipigane ni maskini wa kutupwa. Heri Malawi na Tanzania kukaa meza moja na kutatua tatizo la umilki wa Ziwa Nyasa ingawa rais Banda alishikilia msimamo wake kuwa Malawi inamilki Ziwa Nyasa kwa asilimia mia. Kikwete hakujibu hili wala kulitolea ufafanuzi jambo ambalo limeacha maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na msimamo huu wa Kikwete. Kwanini kama ni mradi wa utafiti wa mafuta usifanyike kama mradi wa pamoja wa nchi hizi mbili jambo ambalo litaongeza ushirikiano na kukuza ujirani mwema. Je hili litaingia akilini kwa nchi inayodai ziwa ni mali yake kwa aslimia mia?  Kwa kuanzia, kwa hili, tunampongeza rais Kikwete na mwenzake wa Malawi, Banda ingawa suala la umilki limewekwa wazi na Malawi huku Tanzania ikiishia kujikanyaga.

Saturday 18 August 2012

Salma Kikwete huwa anaandamana na mkalimani?


Elimu ya mke wa rais wetu inatia shaka. Wengi wangependa ajiendeleze angalau aendane na wakati na majukumu na changamoto za kuwa mke wa rais. Kwa hali ilivyo hana muda wa kujiendeleza zaidi ya kuendeleza ziara hata bila umuhimu. Wengi wanashangaa huwa anaongea lugha gani huko au anaandamana na mkarimani anayelipwa kwa pesa ya walipa kodi. Je umefika wakati wa kuanza kuangalia na sifa za first lady ili kuepuka kuwa na first lady kihiyo anayeweza kutumiwa vibaya na wasaka ngawira? Tuzidi kumshauri first lady wetu kwenda shule ili aende na wakati. Madaraka yana mwisho lakini elimu haina. Ni ushauri wa bure tu.

Friday 17 August 2012

Hii picha inakufundisha nini?


Si maneno yangu. Kuna rafiki yangu kaniambia kuwa Jakaya anamwambia Zuma kuwa: Mbona wewe unaweka hadharani badala ya kuchukua kimya kimya kama sisi?  Mwenzio huwa mwenzio huwa sitangazi nyumba ndogo. Kweli watanzania usanii wanauweza. Maana jamaa aliponipa hii nikaona heri niwamegee na wengine ingawa najua wapenzi wa magamba itawaudhi. Tusameheana. Tabia ya mtu huwezi kuificha hata kama unampenda kiasi gani. Hamuoni jamaa pembeni alivyostuka na kujitoa haraka. Ni kama anasema: Wazee yenu siyawezi ngoja niangalie upande mwingine nisijehesabiwa  nanyi kundi moja. Je nini siri ya hawa vizee kutozeeka na kujiona vijana? Je ni ili vimwana wawapende? Unagundua nini vichwani mwao? Mmoja ananyoa kuficha kipara. Na mwingine anaweka piko kuficha mvi. Ngoma droo.

Tanzania na kukodi midege mibovu, Ethiopia inanunua mpya

Air Tanzania 5H-ATC aircraft at LanseriaA Dreamliner Boeing 787 lands at Bole International airport in Addis Ababa, Ethiopia, Friday, Aug.17, 2012.
Hiyo hapo juu ni ndege mpya aina ya Boeing Dreamliner mali ya shirika la ndege la Ethiopia. Ethiopia imenunua ndege kumi za aina hii na inakuwa taifa la pili duniani kupokea ndege hizi baada ya Japan. Ni aibu kuwa Tanzania, kutokana na kukosa uongozi wa kizalendo na wenye visheni,imekuwa ikiunguza mabilioni kwenye kukodi mikangafu ya ndege. Yote hii inasababishwa na kundi dogo la watu wanaoendekeza ten percent badala ya uzalendo. Inashangaza kwa nchi yenye raslimali nyingi kuliko Ethiopia kutokuwa na hata shirika lake la ndege. Rais wetu na mkangafu wake mara nyingi amekuwa akisafiria ndege za nchi nyingine bila hata kuona aibu. Ni bahati mbaya kuwa tunakodisha midege mibovu kutokana na kuwa na watu wenye fikra mbovu na mafisi wanaotanguliza matumbo yao badala ya taifa wasihangaike na mstakabali wa taifa. Ethiopia hii ambayo tunakamata watu wake wakikimbia maisha magumu inazidi kupiga hatua kwenda mbele wakati sisi tunapiga mbio kurudi nyuma. Je nani aliliroga taifa letu hadi likawa na watawala wenye tabia za panya za kutoboa hapa na pale ili mradi matumbo yao yajae? Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Thursday 16 August 2012

Wakati Kenya wameamka Tanzania waendelea kuuchapa!


Jiji la Nairobi jana lilishuhudia maandamano ya wafanyabiashara wazawa kupinga wamachinga wa kichina kuendesha biashara za viosk. Wakati wachina wakiendelea kutawala biashara ndogo ndogo ya kimachinga maeneo ya Kariakoo jijini Dar, jijini Nairobi hawakaribishwi wala hawataachwa kufanya biashara hiyo ambayo ni ya wazawa wenye mitaji midogo. Machinga wa Kenya wanasema wazi kuwa wachina wamepewa tenda za kutosha za kujenga madaraja, barabara na urari wa biashara baina ya nchi mbili haulingani ambapo China huzoa pesa nyingi toka Kenya ikilinganishwa na Kenya inayopata kutokana na biashara baina ya nchi hizi mbili. Je tatizo hapa ni wakenya kutetea haki zao au watanzania kutojua na kutokuwa tayari kutetea haki zao? Je hapa nyenzo ni mwamko wa wakenya au usingizi wa watanzania?

Kwa hili la majaji tunamuunga mkono Lissu

[8D6U6245.JPG]
Baada ya kuingia serikali zinazoongozwa na watu wasio makini, baadhi ya nyadhifa zilizokuwa zikiheshimika zimeshuka hadhi, kukosa hata kuchafuliwa. Mojawapo ya nyadhifa zilizochakachuliwa na kukosa hadhi ni ujaji. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliliona hili kiasi cha kulitolea ufafanuzi baada ya kuonekana kama anashambulia mahakama. Heri Lissu ameliona hili na kujitoa mhanga kulizungumzia. Watanzania si kwamba hawakuliona wala kulijua hili. Waliliona na kulijua sema waliogopa makahama. Kwenye mabaa hata kwenye madaladala watu wanaongelea uoza huu. Siku hizi kumuona jaji na kumalizana naye si jambo la ajabu. Zamani cheo cha jaji kilitisha na kuheshimika hakuna mfano. Ila siku hizi, ujaji hauna tofauti na ukuwadi wa kawaida baada ya kuona watu wachafu wakipewa hadhi hii. Si uongo wala uchochezi. Majaji wengi walioteuliwa kwa wingi na utawala wa sasa kwa kuzingatia kujuana au kulipana fadhila wamechafua sifa ya ujaji. Wapo majaji wenye kila aina ya madoa kiasi cha kushangaza umakini gani ulitumika kuwateua. Wapo walioshiriki kikamilifu kwenye wizi wa fedha za umma kama vile EPA. Wapo wenye tuhuma za wazi wazi za kutoa rushwa au kuingilia mahakama katika kutoa haki. Wapo ambao ni vihiyo wasio na ujuzi wa kutosha kuwa majaji. Wapo ambao ni wazee waliovuka umri wa utumishi lakini wakapewa ajira kishikaji. Wapo walioteuliwa si kwa sifa bali dini, jinsi zao hata mitandao yao. Hawa pamoja na baadhi ya mabalozi, wakuu wa wilaya na mikoa hata mawaziri, wamechafua hadhi ya utumishi wa umma. Hili licha ya kuwa pigo kwa haki na utumishi wa umma, ni kashfa kwa serikali na ofisi za umma. Kama kuna jambo ambalo wananchi wanaweza kufanya, ni kushinikiza mfumo huu mchafu wa kishikaji na kifisadi unateketezwa huku walionufaika nao wakiwajibishwa. Lissu amewataja wengi. Tunangoja kusikia wakienda mahakamani kumshitaki. Kwa wale wenye udhu wa kutosha tutasikia wakijiwabika. Maana kwa madai na utetezi uliotolewa na Lissu wamechafuka kiasi ambacho hawawezi kusafishika. Sasa nini kifanyike? Tuondokane na tabia ya kumpa rais madaraka ya kufanya uteuzi wa majaji maana imeyatumia vibaya kuwafadhili na kuwalinda marafiki na washirika zake. Badala yake iundwe tume ya kuajiri majaji kama inayofanya kazi nchini Kenya kwa sasa ambapo nafasi za majaji kuanzia jaji mkuu hutangazwa na wanaozihitaji huwasilisha maombi na kuhojiwa na kupitishwa au kukataliwa.

Wednesday 15 August 2012

Walijua basi la dola 10,000,000?

Dunia hakosi vituko kila uchao. Sayansi inazidi kusonga mbele huku nchi zilizotangulia zikiendelea kuongoza kwenye mashindano ya sayansi. Jana tulikuwa tukiongelea vyoo vinavyoweza kubadili kinyesi kuwa makaa hata mafuta. Leo tunaongelea basi linaloweza kukimbia kilometa 250 kwa saa.

Barua ya wazi wa spika Makinda




MPENDWA Anna Makinda Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
 Samahani sitakuita Anne kama unavyopenda kuitwa nikizingatia kuwa wale waliozaliwa wakati wakao walikuwa wakipewa majina bila kutumia manjonjo ya kiingereza.
Ndiyo maana watu wa umri wako ni akina Katarina siyo katheleen au Josephina siyo Josphine nakadhalika.
Kwa mara ya kwanza nakuandika barua hii ingawa si mara ya kwanza kukuandika tena kwa kukuchambua siyo kukupongeza.
Nimewahi kuandika mara nyingi juu yako. Mfano, kukaripia pale ulipomnyamazisha mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema alipodai kuwa waziri mkuu ni muongo. Ulijua hoja yake tena bila staha.
Katika hili niliandika pia kukulaumu kwa kuburuza Bunge na kuwafanya wawakilishi wa wananchi kama watoto wa shule. Hilo lilipita ingawa nilidhani ungenijibu kama siyo kutoa angalau maelezo yanayoingia kichwani. Lakini hukufanya hivyo.
Pia nimewahi kuandika kukutaka ukanushe kuwa wewe si chaguo la mafisadi hasa baada ya kutokea uvumi kuwa wakati akienguliwa mzee wa viwango Spika aliyekutangulia Samuel Sitta, ulipitishwa na mafisadi ili kuepuka kurudiwa kwa kile kilichomng’oa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Bahati mbaya hukujibu wala kukanusha.
Niliwahi kukuandika nikikushutumu kutumiwa na muhimili mmoja wa dola yaani utawala kinyume cha maagizo na kanuni za mgawanyo wa madaraka (separation of power) na utawala bora (good governance). Kadhalika, hukukanusha wala kujitetea.
Niseme ukweli nilitokea kutokupenda achia mbali kukuheshimu. Pamoja na mapungufu yako yote niliyowahi kuelezea kuanzia kutokuwa na elimu ya sheria wala uwezo wa kuliongoza Bunge, juzi ulinifurahisha kiasi cha kuandika waraka huu wa kukupongeza.
Nakupongeza kwa mambo makuu mawili kumruhusu Naibu wako Job Ndugai kuwatolea uvivu wabunge akisema kuwa baadhi yao wanaingia bungeni wakiwa wanatoka kuvuta sigara mbali mbali (ambazo zilitafsiriwa kama bangi au sigara kubwa na kunusa vitu vingine ambavyo wengi tulitafsiri kama unga au madawa ya kulevya. Ulitumia njia nzuri kwa vile Ndugai ni mwenzao anawajua nani anavuta au kunusa nini ukiachia kumchukua au kuchukuliwa na nani.
Uzuri wa sakati hili kuonyesha kuwa ni kweli hakuna mbunge hata mmoja aliyejitokeza kukanusha hata kulaani. Nakupongeza kwa hili na Ndugai pia ingawa sikubaliani naye kuhusiana na kauli yake kuwa hajui idadi ya watoto alio nao.
Hili lilimwonesha kama mtu asiye na maadili kwenye ndoa na familia yake maana yeye kwa dini yake haruhusiwi kuwa na wake wengi. Alisema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo cha Televisheni kimoja hivi karibuni. Hili tuliache si hoja ya leo.
Pili, ulikaririwa ukiwapa nasaha wabunge wa viti maalumu kuacha kubweteka na kuuchapa usingizi wa pono na kuridhika na viti hivyo ambavyo ulisema vinawadhalilisha. Wengi wanaona ushauri huu kuwa wa kinafiki kwa vile nawe ulipata usipka kwa njia hiyo hiyo ingawa ulipigiwa kura.
Hili nilishaliandikia sana. Ni ukweli usiopingika kuwa umma unawaona wabunge wa vitu maalumu kama wanyonyaji na mizigo kwa mlipa kodi. Imefikia mahali wanaitwa misukule! Unawaona hivyo kutokana na ukweli kuwa hakuna wanayemwakilisha bali jinsia zao. Maana kama ni kusema eti wanawakilisha wanawake, ni uongo.
Maana wanawake wanaume watoto na watanzania wote wanawakilishwa na wabunge wa kuchaguliwa majimboni. Ingekuwa wabunge husika wanawakilisha wanaume tungesema wanawake wanahitaji wawakilishi.
Dhana hii imefanya baadhi ya watu kuviita viti maalumu astagffirulah, viti vya chupi. Kuna udhalilikaji kama huu? Wengi wanahoji wanamwakilisha nani bungeni iwapo wanawake sawa na wanaume wanawakilishwa na wale waliowachagua?
Pia ukiangalia mizengwe inayotumika hata rushwa kuwapata wabunge hawa unaishiwa imani na ushawishi nao. Nani anapinga kuwa kupitisha hadi kuchaguliwa hugubikwa na vitendo vya rushwa kama ilivyowahi kudaiwa huko Mbeya miaka mitatu iliyopita kuwa wanawake wanatakiwa rushwa ya ngono ili kupitishwa? Nani alikanusha tuhuma hizi?
Hata ukiangalia chimbuko la viti hivi unagundua kuwa ni udhalilishaji mtupu. Chini ya mfumo kandamizi wa chama kimoja, baada ya kugundua wingi wa wanawake kama wapiga kura, chama kiliwatengea wanawake na vijana nafasi za kuwadhibiti na kuwafuatilia huku wakichongeana na kuchukiana ili wasitishie maslahi ya wanaume.
Hata ukiangalia waliokuwa wakichaguliwa katika nafasi hizi ima walikuwa wake wa wakubwa, nyumba zao ndogo (hasa pale wanawake wasioolewa walipopitishwa kirahisi na vyombo vya juu vya chama) au waliojipendekeza kwa chama.
Kimsingi, wanawake na vijana walipewa viti vya upendeleo ili wavigombee na kusahau kugombea nafasi nyingine zilizokuwa zimemilikiwa na wanaume. Hii ilikuwa ni sawa na kuwapa mbwa mfupa halafu ukaiba kwenye lindo lao. Bahati nzuri Makinda umewahi kuingia kwenye mikiki ya kugombea ubunge jimboni na ukashinda. Hivyo, unaongea kutokana na uzoefu usioweza kutiliwa shaka.
Kwa ufupi viti maalum ni udhalilishaji na utekemezi visivyo kifani. Kwa maana nyingine wanaovipenda na kuvitegemea licha ya kujidhalilisha, wanaonesha kuwa ni watu tegemezi wasio na ubavu wa kwenda majukwaani kupambana na wanasiasa wenzao.
Kuhusu la wabunge kuvuta na kunusa vitu vinavyodhaniwa kuwa mihadarati, hili nalo si jambo jepesi. Kuna haja ya kuunda utaratibu wa kuwachunguza wabunge walevi wa aina yoyote ili waumbuliwe na wale waliowachagua wawajibishe kwenye chaguzi zijazo. Huenda hii ndiyo sababu kubwa ya kufanya baadhi ya wabunge kulala lala hovyo bungeni.
Kwa ufupi, nakupongeza Makinda hata kama sikubaliani nawe kwa mambo mengi. Kwa ujumbe huu mfupi, naomba niishie hapa nikikushauri ubadilike na kuwa spika wa viwango.
Kila la heri na pongezi kwa mara ya pili. Wako akukosoaye ili ujirekebishe na kuepuka aibu.
Chanzo: Tanzania Daima Agosti 15, 2012.

Tuesday 14 August 2012

Meya wa Toronto matatani kwa kuvunja sheria za barabarani



Meya wa jiji la Toronto Rob Ford amejikuta matatani baada ya kugunduliwa akiwa anaendesha gari na anasoma jambo ambalo ni kosa la jinai kwa sheria za Kanada. Ford alikiri kuendesha huku akisoma ingawa alijaribu kujitetea kuwa ni mtu mwenye shughuli nyingi. Hivyo hujikuta ana mrundikano wa kazi. Je angekuwa meya wa jiji la kiafrika angekamatwa? Wenzetu hawana mchezo na sheria na hawajui cheo cha mtu. Miaka minne iliyopita waziri mkuu wa zamani  wa jimbo la New Foundland and Labrador, Danny Willilams alijikuta matatani alipokamatwa na askari mdogo wa usalama barabarani na kutozwa faini pamoja na kuomba msamaha. Ingekuwa Afrika maofisa wa polisi kama hawa waliowakamata wakubwa hawa wangeishia kutimuliwa kazi kama siyo kuonywa kama wangeonewa huruma. Tujifunze na tubadilike kwani madaraka ni mali ya umma na si mali binafsi kama wenzetu wanavyoyatumia vibaya barani Afrika. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Ziwa Camargue huko Ufaransa


Hili ziwa ni tofauti na mengine ingawa tofauti yake kisayansi ni jambo la kawaida. Maji ya Ziwa hili ni mekundu tofauti na maji ya maziwa mengine duniani. Ziwa hili ni kivutio kutokana na maji yake ambayo ni matokeo ya kisayansi ya chumvi kwenye ziwa. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Monday 13 August 2012

"Maficho" ya Dk Ulimboka nchini ni maficho au mtego?


Juzi vyombo vya habari vilirusha habari za kurejea kwa Dk Steven Ulimboka toka Afrika Kusini alikopelekwa kutibiwa baada ya kutekwa na wanaodhaniwa kuwa Usalama wa Taifa,kumtesa na kujaribu kumuua na hatimaye kumtupa kwenye msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Wapenda amani na mageuzi wamefurahi kusikia Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima. Wengi wanangoja kusikia akiwataja wale waliomfanyia unyama na kujaribu kumuua. Kurejea kwa Ulimboka akiwa mzima ni jambo na kuendelea kuishi au tuseme kuwa salama ni jambo jingine. Maana wale waliomteka ambao wanadaiwa kutumwa na ikulu na ikulu yenyewe bado wapo. Sababu iliyopelekea kutekwa na kujaribu kuuawa bado ipo pale pale-kutetea maslahi ya madaktari. Je Ulimboka ni salama pamoja na kudaiwa kupelekwa mafichoni? Je kuna maficho salama nchini Tanzania ambapo serikali iliyopaswa kumlinda Ulimboka ni mtuhumiwa namba moja? Je kwa kutekwa na kutaka kuuawa huku wahusika wakiendelea kula kuku bila kushughulikiwa si ushahidi tosha wa kimazingira kuwa wakiamua kumuua wanaweza- na watafanya hivyo ili kuficha aibu zao.Swali kuu la kujiuliza ni: Je ni uamuzi wa busara kwa Ulimboka kurejea nchini bila kuona hatua zikichukuliwa dhidi ya wahalifu waliomteka? Je ni busara kwa Ulimboka kurejea bila kuhakikishiwa usalama wake? Time will surely tell.

Sunday 12 August 2012

Kurudi kwa Dk Ulimboka sawa je wabaya wake hawatammaliza?


  1. Watanzania wapenda amani na haki walifurika kwa furaha kumlaki shujaa wao Dk Steven Ulimboka anayesemekana kutekwa, kuteswa na hatimaye kujaribu kuuawa na wale aliodai walitumwa na ikulu baada ya kuonekana kuwa mwiba kwa serikali wakati wa mgomo wa madaktari. Ingawa ni haki yake kurejea nchini, kuna haja ya kujiuliza maswali kidogo kuhusiana na hili. Je wabaya wake hawatataka kummaliza ili kukwepa kuumbuliwa? Je ana hakikisho gani la usalama? Je ni busara kurejea bila haki kutendeka? Kwa Tanzania ilivyogeuka nchi ya utawala wa hovyo, blog hii ina wasi wasi na usalama na maisha ya Ulimboka. Maana akina Ramadhan Ighodu na Jack Mughendi Zoka bado wapo na waliowatuma wapo na wanajulikana kwa kulipiza visasi. Time will surely tell.

Kashfa ya meli za Iran: Ni rahisi kuinunua na kuiuza Tanzania kinyemela


An Iranian oil tanker - archive shot, 2004

Ingawa watanzania hawakushupalia kashfa ya Tanzania kuiruhusu Iran kupeperusha bendera yake kwenye meli zake za mafuta baada ya kuwekewa vikwazo kimataifa, kashfa hii inafichua uoza wa serikali yetu. Ni jambo la hatari na kujidhalilisha kuruhusu bendera ya nchi kutumiwa na nchi nyingine kufanya biashara hatari. Bendera ya taifa ni alama na kitambulisho cha taifa chenye thamani kuliko hata urais. Ni ajabu kuwa watanzania, hata waliposikia habari hii ya kuudhi, hawakuhamanika kuiwajibisha serikali inayojiita yao. Hili lingetokea kwenye nchi zenye watu wenye mwamko na kujua heshima na stahiki ya nchi yao, lilitosha kuiondosha serikali iliyoko madarakani. Maana hata ukiangalia utetezi uliotolewa na serikali ni kwa kichovu na uongo mtupu. Eti wanasema kadhia hii imesababishwa na wakala aliyeko Dubai! Ala! Huyu ajenti hata hawasemi atachukuliwa hatua gani wala hawana mpango wa kuchunguza kadhia hii. Wameshindwa hata kuomba msamaha wala kulaani uchafu na ufisi huu. Je namna hii hayajajengeka mazingira ya kuipiga mnada Tanzania hata kwa makundi ya jinai kama inavyoanza kubainika baada ya vigogo wa vita wa Somalia kuanza kuwekeza nchini?  Kesho utasikia kuwa makundi ya kigaidi ya Al Shabaab, Al Qaeda hata Boko Haram yanatumia bendera ya Tanzania kwenye makambi yao ya kuandalia magaidi wa baadaye. Huu ni ushahidi kuwa kwa uongozi huu nchi yetu si salama hata kidogo. Maana tangu serikali ya sasa iingie madarkani imekuwa na sifa ya kufanya madudu na kukumbwa na kashfa. Kashfa ya kwanza ilikuwa Richmond ikifuatiwa na Dowans na sasa Iran. Tunapelekwa wapi watanzania? Je tunaogopa nini kuwawajibisha watawala wetu ambao wamethibitisha kuwa madarakani kwa bahati mbaya na kwa ajili ya maslahi binafsi. Sitashangaa kesho nikisikia kuwa ajenti wa kununua mafuta toka Iran ni kampuni ya mwanamke Rahma Kharoos Kasiga anayehusishwa na Jakaya Kikwete naye asikanushe. Sitashangaa kusikia kuwa kampuni ya mwanamke huyu ya RBP Oil ikifanya biashara na Iran. Kimsingi, serikali yetu inaongozwa na watu wasio na uzalendo wala visheni ukiachia mbali kutochelea kinachowakuta baada ya kuachia madaraka. Viongozi wetu ni fedhuli na wagumu wa kufikiri na kuelewa hasa kutokana na kutanguliza matumbo yakiwaelekeza kwenye maslahi binafsi badala ya mstakabali wa taifa. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.

Saturday 11 August 2012

Kikwete kwa vituko hakuna mfano

Wakati mananasi nchini Tanzania yanaoza na kuuzwa kwa bei ya kutupa kutokana na serikali kutowawezesha wakulima kupata soko na bei nzuri, rais wao anachekelea vya wenzake kama anavyoonekana kwenye shamba moja nchini Ghana alipokwenda kuzika na baadaye kutalii. Kinachopaswa kumsuta ni ukweli kwamba wakati akifurahia maendeleo yaliyofikiwa na wakulima wa mananasi wa Ghana, ni ukweli kuwa jimboni mwake pale Chalinze wakulima wanaendelea kuwa maskini pamoja na kuzalisha mananasi kwa wingi. Hakina aliyempangia kutembelea shamba hili amejua kumstuka Kikwete. Sijui kama ameipata au ni yale yale ya kujifanya huwa hasikii wala hajali.


Kumbe paka ana akili kuliko mbwa hata kama wote wanafugwa!


A video of a cat outsmarting a dog by jumping on a surfboard has gone viral (YouTube)

Katika picha hii mbwa alijaribu kumfukuza paka. Baada ya paka kuona amezidiwa alimua kuyaingia maji na kumuacha mbwa akikata tamaa na kurejeza zake nyumbani.

Friday 10 August 2012

Tanzania kuna mfumo-kristo au mfumo-islam au bangi za wanaodhani hivyo?



Nikiwa napita pita kwenye wavuti wa Jamii Forums jana nilikutana na hoja kuwa 'mfumo-kristo umeleta umaskini nchini Tanzania. Hoja hii ilinivutia na kunichochea kuandika yafuatayo kama majibu kwa wale wanaoota mchana na kutafuta visingizio badala ya kukabiliana na tatizo lenyewe.
Niliandika:
Huo uislam na ukristo zaidi ya kuleta utumwa na ukale umeleta nini? Tatizo la Tanzania si mfumo kristo wala dini bali utawala mbovu. Ukiangalia ufisadi uliofanyika chini ya utawala wa Benjamin Mkapa, Ali Hassan Mwinyi na sasa Jakaya Kikwete, unashangaa maana ya mfumo-kristo kama kweli upo nayo ipo.
Ukiangalia watuhumiwa wakuu wa ufisadi kama vile Andrew Chenge, Edward Lowassa Idd Simba na Idris Rashid wote ni wa dini zote. Tutafute jawabu sahihi la tatizo letu badala ya kutafuta visingizio. Inashangaza mtu mwenye akili timamu kusema eti Tanzania inaongozwa kwa mfumo kristo wakati rais na makamu wake ni waislam. Mtu wa namna hii ima hajasoma na kuelimika au ni kasuku anayejipayukia bila kufikiri wala kufanya utafiti. Huu upuuuzi "wa mfumo kristo" sasa umegeuka kuwa wimbo kwa watu wasiokuwa tayari kufikiri sawa sawa. Nendeni vijijini muone watanzania wanavyoumia bila kuangalia dini wala watokako. Kuna haja ya kuacha uvivu wa kufikiri na kutafuta visingizio. Tatizo la Tanzania ni utawala mbovu wa kifisadi unaoendekeza kuombaomba na kutumia vibaya. Nyerere aliwahi kusema kuwa uchumi mnao lakini mmeukalia. Wajinga walitafsiri kipuuzi na kukosa maana na nafasi ya kukabiliana na changamoto ya umaskini. Hakuna cha mfumo kristo wala islam.

Fareed Zakaria nabbed plagiarizing


CNN's foreign show host Fareed Zakaria was recently was nabbed plagiarizing. He made an apology however the dent had already been made. AP reported the scandal as follows:

NEW YORK (AP) — Columnist and TV host Fareed Zakaria has apologized for lifting several paragraphs by another writer for use in his column in Time magazine. His column has been suspended for a monthZakaria said in a statement Friday he made "a terrible mistake," adding, "It is a serious lapse and one that is entirely my fault."In a separate statement, Time spokesman Ali Zelenko said the magazine accepts Zakaria's apology, but would suspend his column for one month, "pending further review.""What he did violates our own standards for our columnists, which is that their work must not only be factual but original; their views must not only be their own but their words as well," Zelenko said.Media reporters had noted similarities between passages in Zakaria's column about gun control that appeared in Time's Aug. 20 issue, and paragraphs from an article by Harvard University history professor Jill Lepore published in April in The New Yorker magazine.In Zakaria's column, titled "The Case for Gun Control," he began one paragraph with the sentences: "Adam Winkler, a professor of constitutional law at UCLA, documents the actual history in 'Gunfight: The Battle Over the Right to Bear Arms in America.' Guns were regulated in the U.S. from the earliest years of the Republic."A corresponding passage in Lenore's New Yorker essay, titled "Battleground America," begins: "As Adam Winkler, a constitutional-law scholar at U.C.L.A., demonstrates in a remarkably nuanced new book, 'Gunfight: The Battle Over the Right to Bear Arms in America,' firearms have been regulated in the United States from the start."In Zakaria's statement, he apologized "unreservedly" to Lepore, as well as to his editors and readers.Besides serving as an editor-at-large at Time, Zakaria is a Washington Post columnist and the host of CNN's foreign-affairs show, "GPS." Source

My take is clear.If you look at what Zakaria says and writes, sometimes, you find that he is not worth what he seems to worth so to speak. I was his fan. But as the days lapsed, I found something amiss in his clout. Rules, especially academic ones, are strict and must be obeyed mutatis-mutandis. To be referred to as an academics or a guru, one needs to know all this. If anything, playing "within the rules" is what makes an academic an academic apart from making him edgier. I would respect a person who attribute whatever he uses in his work even if it means to say he did not toil a lot. This is how we were taught at universities. I maybe wrong. Again, academics is about disciplined and following the rules religiously. Plagiarism or purloining, for an academic is like a suicide for his fame, knowledge and career. Suspending Zakaria is not enough. He should be fired. For he does not qualify to do what he was doing. They are many academic who are out there seeking to do a job best.

Jamaa amekata miaka 38 bila kuoga, kisa?

mtoto wa kiume! Kichaa au imani?

Huyo jamaa hapo juu aitwaye Kailash Singh (66) ametoa mpya kwa kukaa miaka 38 bila kuoga wala  kunyoa ndevu. Kisa?Aliweka nadhiri kuwa ataoga siku akipata mtoto wa kiume. Singh ameingia kwenye kitabu cha maajabu ya dunia cha Guiness kuwa mtu anayeongoza kwa kunuka. Pamoja na yote  hayo yeye hajali hadi apate mtoto wa kiume. Kwa habari zaidi BONYEZA hapa.