How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Monday, 13 August 2012

"Maficho" ya Dk Ulimboka nchini ni maficho au mtego?


Juzi vyombo vya habari vilirusha habari za kurejea kwa Dk Steven Ulimboka toka Afrika Kusini alikopelekwa kutibiwa baada ya kutekwa na wanaodhaniwa kuwa Usalama wa Taifa,kumtesa na kujaribu kumuua na hatimaye kumtupa kwenye msitu wa Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. Wapenda amani na mageuzi wamefurahi kusikia Dk Ulimboka amerejea akiwa mzima. Wengi wanangoja kusikia akiwataja wale waliomfanyia unyama na kujaribu kumuua. Kurejea kwa Ulimboka akiwa mzima ni jambo na kuendelea kuishi au tuseme kuwa salama ni jambo jingine. Maana wale waliomteka ambao wanadaiwa kutumwa na ikulu na ikulu yenyewe bado wapo. Sababu iliyopelekea kutekwa na kujaribu kuuawa bado ipo pale pale-kutetea maslahi ya madaktari. Je Ulimboka ni salama pamoja na kudaiwa kupelekwa mafichoni? Je kuna maficho salama nchini Tanzania ambapo serikali iliyopaswa kumlinda Ulimboka ni mtuhumiwa namba moja? Je kwa kutekwa na kutaka kuuawa huku wahusika wakiendelea kula kuku bila kushughulikiwa si ushahidi tosha wa kimazingira kuwa wakiamua kumuua wanaweza- na watafanya hivyo ili kuficha aibu zao.Swali kuu la kujiuliza ni: Je ni uamuzi wa busara kwa Ulimboka kurejea nchini bila kuona hatua zikichukuliwa dhidi ya wahalifu waliomteka? Je ni busara kwa Ulimboka kurejea bila kuhakikishiwa usalama wake? Time will surely tell.

No comments: