The Chant of Savant

Sunday 19 August 2012

Kwa hili Kikwete anastahili pongezi ingawa...



Kitendo cha rais Jakaya Kikwete kumwalika rais wa Malawi Joyce Banda kutembelea Tanzania  ni cha kupongezwa. Habari zilizotufikia ni kwamba rais Kikwete alitoa mwaliko huo wakati alipokutana kwa mazungumzo mafupi kando ya mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuia ya  ushirikiano wa nchi za Kusini Masharika  (SADC), huko Maputo Msumbiji. Tofauti na matamshi ya rejereja ya waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe na mbunge wa Monduli na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa waliotangaza vita wakati wao si amiri jeshi mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Kwa kitendo hiki Kikwete na Banda wameonyesha ukomavu na uzalendo wa namna yake. Ndiyo kunaweza kuwapo kutokuelewana juu ya Ziwa Nyasa. Lakini bado majadiliano ni njia muafaka kuliko milio ya bunduki. Nchi zenyewe zilizokuwa zikisukumwa zipigane ni maskini wa kutupwa. Heri Malawi na Tanzania kukaa meza moja na kutatua tatizo la umilki wa Ziwa Nyasa ingawa rais Banda alishikilia msimamo wake kuwa Malawi inamilki Ziwa Nyasa kwa asilimia mia. Kikwete hakujibu hili wala kulitolea ufafanuzi jambo ambalo limeacha maswali mengi kuliko majibu kuhusiana na msimamo huu wa Kikwete. Kwanini kama ni mradi wa utafiti wa mafuta usifanyike kama mradi wa pamoja wa nchi hizi mbili jambo ambalo litaongeza ushirikiano na kukuza ujirani mwema. Je hili litaingia akilini kwa nchi inayodai ziwa ni mali yake kwa aslimia mia?  Kwa kuanzia, kwa hili, tunampongeza rais Kikwete na mwenzake wa Malawi, Banda ingawa suala la umilki limewekwa wazi na Malawi huku Tanzania ikiishia kujikanyaga.

2 comments:

Anonymous said...

First time in history
mzee ma filter

Brownpphi said...

First time in history mzee ma filter