Tutaanza na kisa ambacho tulishuhudia kwa ndugu yetu mmoja. Huyu bwana, kuna kipindi alichishwa kazi. Hivyo, alianza kuamka kila asubuhi akielekea mjini kusaka vibarua ili mkono uende kinywani. Mambo hayakwenda kama alivyotaka wala kupanga. Hivyo, ulipita muda bila kuwa na namna ya kujiingizia kipato. Hata hivyo, alifanikiwa kumtafutia mkewe kibarua kwa ndugu yake. Mama alifurahi kupata kibarua na kuingiza lau kipato. Hata hivyo, yule mama ambaye tunasema ni mpumbavu, alianza kumuona mumewe kama hamnazo na asiye na ujanja wa kuhangaika na kupata kipato.
Siku moja alidamka, kama kawaida yake akijiandaa kwenda kwenye kituo cha daladala ili aende zake mjini kuchakalika. Kwa bahati mbaya, siku ile hakuwa hata na nauli. Hivyo, alimuomba mkewe nauli. Badala ya mama kumpa nauli, alimjibu “mwanamme mzima unaomba nauli kwa mkeo! Mwanaume gani suruali.” Kwa busara na upendo, yule bwana hakukasirika wala kujibu zaidi ya kuumia ndani na kufunika kombe mwanaharamu apite.
Kwa vile tabia ile ilituudhi, tulimwita jamaa kando na kumpa nauli bila hata kumpa pole kwa kuhofia tungeamsha uchungu hata kumwaga mafuta kwenye moto. Pamoja na kumhifadhi ndugu yetu huyu, kile kitendo kilituudhi na kutufedhehesha. Cha mno, kile kitendo kilitupa somo kuwa, katika ndoa, kuna wanandoa wengine wanabomoa ndoa zao kwa mikono yao.

Badala ya mama kujiuliza angekuwa yeye angefanya nini, aliamua kujivua na kumvua mumewe nguo tena mbele ya watu. Katika hali hii, mume akipata fursa ya kutosha, je hawezi kulipiza kisasi kiasi cha kuanza unyanyasaji katika ndoa. Je hapa chanzo na wa kumlaumu zaidi ya mkewe ni nani japo naye, kama mume, anapaswa kupima mambo. Je ni wangapi wanatumia lugha chafu kama hizi dhidi ya wenzi wao? Je wanafaidikaje na tabia hii chafu?
Hapa kuna mambo kadhaa ya kujifunza.
Hapa kuna mambo kadhaa ya kujifunza.
Mosi, kupata na kukosa, yote ni majaliwa na aliye nacho leo anaweza asiwe nacho kesho na asiye nacho akawa nacho.
Pili, kuna haja ya kuvumiliana hasa wanandoa wanapopata mitihani ya kimaisha ambayo ni mambo ya kawaida yanayoweza kuwajenga au kuwabomoa.
Tatu, kupata si ujanja na kukosa siyo uzembe au ujinga. Kwanin watu wa namna hii hawahoji ni kwanini watu wengine wanaishi kwa muda mrefu wakati wengine wanaishi kwa muda mfupi?
Nne, upendo baina ya wanandoa unapaswa kuvuka vitu vidogo kama vile kipato, elimu, na mengine kama haya. Kwani, kila mmoja anaweza kuwa nayo au asiwe nayo.

Tuliwahi kudurusu kisa cha mwanandoa mmoja aliyesoma akaishia form four failure aliyejiona msomi sana kuliko mumewe ambaye hakumaliza hata la saba. Huyu mama toka familia maskini, alianzishiwa biashara na mumewe huyo huyo asiyesoma na kufikia hata kumilki biashara yake na gari.
Baada ya kujiona kapata, alianza kumdharau mumewe hadi kufikia kumtamkia “wewe hukusoma.” Ajabu ya maajabu, wakati wanakubaliana kuoana, alijua fika kuwa mumewe alikuwa kaishia darasa na tano. Kwa waliosikia kisa hiki cha hovyo, walijiuliza ni kwanini hakumkataa alipomchumbia tokana na kutokuwa na elimu aliyotaka ijapokuwa naye hakuwa nayo?
Ukiunganisha kisa cha ‘mume suruali’ na cha ‘wewe hukusoma’ unagundua mambo mengi ambayo ni hatarishi na sumu katika ndoa. Mfano, mwanandoa aliyemwambia mwenzie ni mume suruali, naye alikuwa katokea kwenye familia maskini. Je kwanini hakujiuliza kuwa hata baba yake alikuwa mume suruali na hata mama yake mke gauni?

Kwa yule aliyemwambia mume hakusoma, utakuta wazazi wake pia hawakuwa wamesoma ukiachia mbali kuwa hata naye hakuwa amesoma. Katika ndoa, epukeni tabia ya nyani kutoona nonihino lake. Epuka kuwa kama mbwa chihuahua (chiwawa) kiumbe mwenye kubweka sana asishambulie wala kujihami anapokabiliwa na adui. Kwenye ndoa, epuka kumhukumu mwenzio kabla ya kujihukumu.
Kama mmejaliwa au mmoja wenu kajaliwa talanta fulani, zitumieni kwa upendo na usawa bila kudhalilishana, kunyanyasana, kutukanana, na kuvunjiana heshima. Leo, unaweza kumuona mwenzio hafai wakati nawe hufai na kesho mkaachana ukajikuta umemkimbia mjuzi na kumkumbatia mamba. Hivyo, kabla ya kuhukumu au kutuhumu, fanya hivyo kwako mwenyewe kwanza. Hiyo ndiyo busara ya leo.

Chanzo: Mwananchi Jpili iliyopita.
No comments:
Post a Comment