The Chant of Savant

Friday 1 March 2019

Lowassa arejea CCM na kufanikiwa kulipiza kisasi kwa waliomuita fisadi papa

 Walipokutana Mwembe Yanga tarehe  15 Septemba, 2007 wakiwa na orodha ya mafisadi papa nchini akiwamo waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa, walisahau kitu kimoja au viwili. Kwanza, walikuwa wanaandaa kifo cha Lowassa kisiasa ndani ya CCM na Tanzania. Pili, walikuwa wamemtendea kosa ambalo asingeweza kulisahau maishani mwake bila kulipiza kisasi. Kwa wataalamu wa mambo, tulijua fika kuwa Lowassa alipojiunga na upinzani alisukumwa na sababu kuu tatu yaani:
Mosi, hasira baada ya kuenguliwa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais.
Pili, imani kuwa angeweza lau kushinda kupitia upinzani hata kushindwa bila kupoteza lolote zaidi ya upinzani.
Tatu, alitaka kulipiza kisasa kwa namna upinzani ulivyombomoa na kumtangaza kuliko mafisadi wengine uliotaja.
Tatu, alitaka kuukomesha upinzani na kujijengea nafasi maalumu kwa CCM ambayo, nayo bila shaka, ilijua kuwa alichokuwa akifanya kada wake huu kingeisaidia kwenye uchaguzi husika. Sababu ziko nyingi. Ila hizi tatu ndizo zingemfanya mchambuzi yeyote mahiri kutabiri kurejea tena kwa Lowassa CCM siku moja kama ambayo amefanya leo. Kimsingi, kama kuna aliyeuua upinzani si mwingine bali aliyeushauri kumpokea Lowassa. 
Sasa Lowassa ametimiza malengo yake yote. Kuna haja gani ya kubakia upinzani? 
KWA HABARI ZAIDI BONYEZA HAPA

No comments: