Kudos to President Magufuli

Friday, 21 September 2018

Ajali na MV Nyerere iwe somo kwa taifa

See the source image
Tunaungana na ndugu na jamaa na watanzania wote kuomboleza msiba mkubwa uliotokea baada ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kwenye ziwa Nyanza. Dua na sala zetu ziko wa marehemu na ndugu na jamaa na taifa kwa ujumla. Hata hivyo, kama taifa na watu, tunapaswa kujifunza kutokana na makosa yetu. Kinachoudhi na kuumiza ni kwanini hatukujifunza toka mwenye msiba wa MV Bukoba iliyozama miaka yapata 22 iliyopita ikiwa imeteketeza zaidi ya watu 1,000. Je kama taifa, tumegeuka taifa lisilojali wala kujifunza? Je nini kitokee zaidi ili tujifunze? Naamini utawala wa sasa hautakuwa bubu wala sitting duck kama tawala zilizopita ambazo zilishindwa kujifunza tokana na janga la MV Bukoba.
Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi na kuwafariji ndugu jamaa na marafaiki wa marehemu. AMINA.

No comments: