|
|
Jambo hili,
licha ya kumstua mume, lilimchanganya na kumwachia fikra nyingi asijue aambue
au kufanya nini. Je, tukio hili au kitendo hiki, kama ungekuwa wewe,
ungechukuliaje? Ungechukia? Ungefurahia? Ungechanganyikiwa au? Je,
linakufundisha nini?
Kimsingi, binadamu anapolala, licha ya kuota, anaweza kuwa macho kwa kiwango fulani kwa vile ubongo wake huwa haulali. Hivyo, kuna mambo mhusika anaweza kuwa akifikiria yakamrejea na akayafanya ima akiwa nusu usingizini au macho alivyofanya mwanandoa huyu.
Japo, hatuwezi kujua sababu za mama kumnusa vidole na masikio mumewe, tunajifunza mambo yafuatayo:
Mosi, mwenzi wako anafuatilia karibu kila jambo unalofanya, liwe kubwa au dogo, la maana, hata lisilo la maana. Licha ya kuwa haki yake, ni ishara kuwa anakujali na kukupenda vilivyo. Pia, inaonyesha kuwa yuko tayari kukukosoa, kukurekebisha, hata kukuboresha inapobidi. Hivyo, usimuewe vibaya wala kuhamanika. Kwani, hakuna aliye mkamilifu hasa katika masuala yahusuyo miili yetu.

Pili,
anaweza kuwa kanusa kitu. Hivyo, anatafuta kukielewa na kukirekebisha. Muhimu,
anafanya hivyo si kwa nia mbaya bali kukujua vizuri hata wakati mwingine
kutokujua vizuri, kukushuku, kuhisi, au kujifurahisha.
Tatu, hata kama hakwambii, kuna uwezekano mkubwa kuwa si kila anachokufanyia anakijua sawa nawe unavyomfanyia. Hivyo, baadhi ya vitendo, ima ni mrejesho au mwitikio wa matukio na matendo yako au hata yake.
Nne, anakufuatilia wakati mwingine kuliko unavyomfuatilia. Katika hili, akina mama wako mbali kuliko akina baba. Kimsingi, mkeo anakutunza kama vile ajitunzavyo au atunzavyo watoto wenu. Wakati mwingine, anafanya mambo kama haya bila kuhiari au kupanga. Hivyo, ujue. Mkeo si mnoko wala mwanga.

Ni wanandoa wangapi limewahi kuwatokea hili au
jingine lifananalo na hili? Mbali na hili, je, ni wangapi wanaangalia simu za
wenzao kujua namna wenzao wanavyozitumia? Uzoefu unaonyesha kuwa akina mama
ndiyo mabingwa wa kufuatilia matumizi ya simu za wenza wao japo, pia, wapo
akina baba wanaofanya hivyo.Tuliwahi kujadili namna ndoa zinavyoharibu ndoa na
namna ya kuzuia balaa hili. Hivyo, wahusika wajue wajibu huu na kuukubali hata
kama unaweza kuwa na ukakasi fulani hasa kwa wale wenye “mambo yao.”
Wangapi
wanawaruhusu au kutowaruhusu wenzao wasiguse, achia mbali kuziangalia hata
kuzipekuwa simu za wenzao? Wangapi wanawaficha wenzao simu zao? Japo unaweza
kuona kama uchimvi, mwenzio angependa kujua wote unaowasiliana nao na anaweza
kutaka hata nywila za baruapepe na simu zako. Je, ni
busara, salama, au hatari kumpa mwenzio nywila za baruapepe na simu yako?
Japo
unaweza kuona kama uchimvi, mwenzio ana lengo zuri la kukulinda wewe na ndoa
yenu. Hivyo, usijisikie vibaya akitaka kukujua kama ilivyo kwenye kisa
tulichoanza nacho. Anakuwa na nia nzuri ya kutaka kuhakikisha usalama wenu
wote. Kama tulivyobainisha pale juu, anakulinda kama kichanga japo wewe si
kichanga.
Kama hujui,
japo si wote, mwenzio anakuchunguza kila sekunde, saa, na siku. Yote ni kwa nia
nzuri. Kwa wanandoa wanaopendana na kuaminiana vilivyo, wewe ni mali yake naye
ni mali yako. Tusisitize. Hafanyi hivyo kwa nia mbaya au kutokuamini ingawa
wengine ni tofauti. Wakati mwingine, hata hajui kama anafanya haya.
Tusikutishe.
Tumalizie kwa kusema kuwa unachopaswa kujua
na kuzingatia ni ukweli mchungu kuwa saa zote uko kwenye mawazo yake na
ukochini ya uangalizi na uchunguzi muda wote katika maisha yako. Kama huna
“mambo yako” usiogope mwenzio kupitia mitandao au simu yako. Kuepuka au
kuogopa, hata kama huna, kunajenga shaka kuwa una “mambo yako” ujue.
Chanzo: Mwananchi Jpili juzi.
No comments:
Post a Comment