The Curse for Salvation

The Curse for Salvation

Tuesday, 30 December 2025

Tunataka usuluhishi, si usulubishi na usulutishi


Kwanza, nitoe salamu zangu, za Bi Mkubwa, na watoi tunapofunga na kuanza mwaka. Kipekee, nichukue fursa hii kuwakumbuka na kuwaombea ambao hawakuumaliza wala hawatauona mwaka mpya waliokufa ima kwa vifo vya kawaida au vya kufyatuliwa, waliotekwa, na kupotezwa hata waliowafanyia kitu mbaya nikiwataka waache na kumaliza na kuanza mwaka kwa nia safi kabisa.

 Tumalize mwaka na kuuanza mwingine kwa usalama si kwa kufungana kamba na kuumizana au kuitwishana mkenge. Turidhiane kweli kweli na si kuridhishana na kuendeleza upuuzi ule ule ili tusionekane hamnazo wala wanafiki waliojitoa ufahamu. Aaaamina.

Nije kwenye inshu. Mafyatu walipofyatua, si walifyatuliwa hadi kukawa kufyatuana! Baada ya kugundua kuwa kufyatuana na kufyatukiana hakuwafikishi mbali, sasa nasikia kamba za usuluhishi! Usuluhishi au usulutishi? Nani anasuluhishwa na nani na kwanini na ili iweje? Nifyatue wazi. Ili kuepuka kuendelea kufyatua, kufyatuana na kufyatuliwa, lazima huu usuluhishi uwe usuluhishi. Nani anataka usulubishi tena kwa usulutishi, ulushi na magumashi?

            Kama profesa emeritus wa migogoro na utatuzi wake, leo nafyatua lecture ya bure. Najitolea bure lau kusaidia mafyatu na kaya yetu tusiendelee kufyatuana na hata kunyotoana roho. Kitaaluma, tuna kitu kinaitwa give and take kinacholenga kufikia win-win situation. Ili kufikia hapa, mosi, lazima wahusika wawe wakweli. Wakubwa na wadogo hukosea. Waelezane ukweli kwa ukweli na uhuru na si kuzidiana ujanja, ujanja ujanja, na sanaa. Pili, waathirka lazima wapewe nafasi ya ku-vent au kutapika nyongo. Tatu, lazima watuhumiwa wawe na kifua si cha kupinga au kufyatuana bali kuwasikiliza wale waliowafyatua na kuomba msamaha au kuwajibika. Nne, lazima kuwepo na yule tunayemuita third party ambaye sina kimakonde chake. Huyu, lazima awe ni fyatu anayeaminiwa au wanaoaminika na wahusika wote. Sitaki niwachoshe na lugha za kitaaluma na kifyatu.

            Sasa, nini kifanyike?

            Hapa, kuna mambo kadhaa muhimu ya kufanya ndiposa usuluhishi, siyo usulubishi wala usulutishi, uanze.

Mosi, lazima tukiri kosa au makosa ambayo, kimsingi, ndiyo yanayosukuma kuwapo usuluhishi.

Pili, lazima iundwe tume––––si timu ya kufadhiliana, kulindana, kupendeleana, na kupeana ulaji wa dezo–––ya kuchunguza kadhia zima. Je, nani aiunde? Ili hii tume ikubalike kwa pande zote, lazima wahusika washirikiane kuiunda kuepuka na kuepusha mtuhumiwa au mhalifu kuwa mlalamikaji, mwendesha mashitaka, karani wa mahakama, mahakama, na hakimu katika kesi yake. Kwa waliosoma sharia, kimakonde, hii, ni katazo na uvunjaji wa haki usio kifani. Huitwa nemo judex in causa sua.

Tatu, kwa kuangalia mambo yanavyokwenda ambapo upande mmoja unataka kuutwisha mwingine mkenge uonekane makenge, nimewiwa kufyatua hii kitu lau nifungie na kufungulia mwaka. Hapa, nasisitiza kuhusu kuundwa kwa tume ya maridhiano si maridhishano, usuluhishi, siyo usulutishi n usulubishi. Nasema wazi. Tume yoyote ambayo haiakisi haya si tume bali timu ya kupendelea wale walioiunda ili kuwaepushia lawama wanazostahiki. Hapa, walalamikiwa lazima wakubalia lawama na kufanya hivyo siyo makosa wala udhaifu bali nguvu.  Kimsingi, timu kama hii haitatua tatizo bali kulikuza. Inakosa kile ambacho kimakonde tunaita impartiality, yaani kutoegemea upande. Tukumbuke, amlipaye mpiga zumari ndiye huitisha wimbo. Tahadharini hili.

            Nne, suala jingine nyeti ni je, ni nani amchunguze nani na kupata nini? Hapa, niseme wazi. Kama tutaamua kusuluhishana, tusuluhishane na si kusulutishana ili tusipoteze fursa na muda. Kuna usemi kuwa sometimesa conflict can present an opportunity if it is addressed constructively. Hivyo, tutafute chanzo cha yote na kukishughulikia kisayansi na kwa nia safi tukijiapiza na kuapa kutorudia uzwazwa uliotufikisha tulipofikishwa na waliotufikisha pale. Kusuluhishana kwa kweli si kupeleka kesi ya ngedere ya kula mahindi kwa nyani au kesi ya paka na panya kwa kwa chui.

 Tano, baada ya uchunguzi huru na wa kweli kukamilika, linakuja suala na swali la nani awe mshitaki na nani awe mshitakiwa? Tulenge kuepusha ukenge wa mshitaki kuwa mshitakiwa na mshitakiwa kuwa mshitaki kama ilivyo kwa sasa ambapo mkosefu anamlaumu aliyemkosea tena bila aibu wala sababu isipokuwa ukosefu wa aibu, utu, na mizania kimamlaka. Kwenye usuluhishi wa kweli, pande mbili zinakuwa na hadhi na kutenzwa sawa bila kujali nani ni nani.

 Sita, tukimaliza kujua pande mbili husika ambazo kimsingi na kitaaluma, ndizo hufanya kesi iwe ya kimahakama au ya usuluhishi, tunakuja na suala jingine. Je, nini adidu za rejea? Bila kuwa nazo, mambo mengi yasiyopaswa yataibuliwa na kufanya usuluhishi kuwa usulubishi kwa wasuluhishaji.

Mwisho, tukifanya hayo, tukumbuke. Pande mbili husika zina hasira na nyingine hata jinai. Hivyo, kila fyatu atajitahidi kuja na za kuja ili aonekane hana makosa. Je, nani atamfunga paka kengele bila kufanyiwa au kufanyiana ukenge?

Heri ya Mwaka Mpya.

Chanzo: Mwananchi Jtano, leo.

Wednesday, 24 December 2025

Busara na nasaha za Fyatu kwa mafyatu


Katika kufunga mwaka,, nalete somo la kifyatu si kwa mafyatu tu hata kwa wafyatuao mafyatu wasiofyatuka wakafyatua wawafyatuao. Hili ni somo rahisi lakini gumu lihitajilo ufyatu wa kiwango cha juu. Tuanze kujihoji na kuwahoji wengine. Nani aweza kuleta amani au haki kupitia dhuluma? 
        Amani haiwezi kukaa sehemu moja na shari wala mwanga na kiza. Adhaniaye anaweza kuviweka viwili hivi pamoja, anajidanganya na kudaganya wengine. Mwanga na kiza ni maadui sawa na upendo na chuki. Hata upendo upende vipi chuki, chuki haiwezi kuupenda au kuzaa upendo bali chuki. Japo hakuna uongo mzuri, kujidanganya ukadhani umewadanganya wengine ni hatari hata kuliko kudanganywa maana, waweza kushuku au kushukiwa ukaelewa ila siyo kujishuku.
            Mzee asiye na busara ni hatari kuliko mtoto mpumbavu kwani hana muda wa kujifunza ikilinganishwa na mtoto mwenye muda wa kuishi na kujifunza. Heri kisu butu kisichoshika kutu kuliko kikali kimalizwacho na kutu. Uzee unapogeuka au kugeuzwa uzezeta na uchumia tumbo, heri kufa mapema kuliko kuzeeka na kuishia kuwa hovyo kiasi hiki. 
        Mvi ni alama ya hekima. Ijapokuwa, wapo wengi walio nazo ila hovyo kiasi cha kutamani zingeota kwenye mwembe lau watoto hata ndege wale wapate hekima.
        Hebu tujifunze zaidi. Uongo na ukweli haviwezi kutangamana wala kuvumiliana. Ukweli ni ukweli na huweka huru wakati uongo ni uongo na humfanya auaminiaye mtumwa hata asifiwe au kujisifu vipi. Nani aliweza kulaza ubunifu na ubabaishaji kitanda kimoja? Ukifanikiwa, kitanda hata nyumba vitavunjwa vipande tokana na uadui wake.
        Sijawahi kudhani wala kushuhudia kujiamini na woga vikiishi pamoja na kupendana achia mbali kuwezekana. Ajiaminiye kuwa anaweza kuweka viwili hivi pamoja, siyo anajidanganya tu bali anajiaibisha na kuonyesha asiyo na akili wala busara. Nani aweza kuweka imani na shiriki pamoja pamoja kama ilivyo imani na uhalisia? 
        Chanya na hasi havitafanana hata vifananishwe vipi. Uchafu ni uchafu hata utukuzwe vipi bado ni uchafu.
Kwanini mja akifa hupelekwa mochwari kabla ya kuzikwa? Simpo. Uzima na ufu haviwezi kuwa sehemu moja kwa wakati mmoja. Kimoja kikiwepo, kingine hutoweka. Japo siku hizi, wapo wanaohalalisha haramu na kuharamisha halali, ukweli ni kwamba halali na haramu havijawahi kuwa mapacha wala marafiki. Utuli na uoza haviwezi kuwa washirika.
            Kadhalika, mwelevu na mjinga hawawezi kukubaliana wala kushindana. Ajuacho mjinga ni ujinga na mwelevu avijua vyote viwili. Heri uwe mwelevu ajifanyaye mjinga kuliko mjinga, tena juha, ajifanyaye mwelevu. Je, kuna ulevi mzuri wenye siha uwe wa urahibu au maulaji? Ulevi ni ulevi hata uitwe starehe. Ushuzi ni ushuzi hata uwe wa mfalme. Nani mpumbavu awezaye kuuachia mbele ya kadamnasi akajifisifia kafanya jambo jema? Je, hawapo wachafuao hewa kwa vinywa vyao tena usiowategemea?
            Kuna wakubwa walio wadogo kuliko wadogo walio wakubwa. Heri kuwa mdogo asiyependa ukubwa kuliko kuwa mkubwa mwenye uwezo mdogo katika kuutumia ukubwa. Tembo ana mwili mkubwa ila ana hasira kidogo. Vipi kuhusu nyuki? Nyuki na kijimwili chake kidogo, ana wingi wa hasira.
            Kuna waja wenye macho lakini vipofu na vipofu wanaoona mbali kuliko wenye macho? Hebu fikiria juu ya hili. Ukahaba si wa ngono bali hata wa siasa ni ukahaba. Kuna ulimwengu ambapo mizoga i hai na walio hai waweza kuwa mizoga hata wasichekane.
            Ubinafsi na ulafi ni ugonjwa wa vichaa. Kuna faida na mantiki gani kwa mja kujilimbikizia mali tena kwa kuwaibia na kuwaumiza wenzake ilhali aliikuta na ataiacha? Ni mwenye akili na busara gani aweza kuonea uchoyo kwa kile ambacho hawezi kukila au kukitumia na kimaliza? Najua hili halipendezi kusema. Ila kwa wenye akili ni shairi au wimbo mtamu. Apandeaye atashuka, na ajikwezaye atashushwa. Hivi mja ni nini hadi ajikweze huku akiwatweza wenzake?
            Je, wajua kuwa mja afarikipo huoza haraka kuliko viumbe wote isipokuwa minyoo na samaki? Kati ya kuku ambaye huungwa auawapo na kuliwa na binadamu ambaye huvishwa na kutupwa nani bora? Ni kipi bora kati ya maguvu na akili? Si kila kitu kinahitaji maguvu japo vyote uhitaji akili. Hujasikia wahenga wakiasa kuwa akili ni mali? Je, maguvu nayo ni nini? Moto waweza kuchemsha maji hadi yakayeyuka na kukauka. Je, maji hayazimi moto ukapotea? Umdhaniaye yu dhaifu aweza kuwa bora kuliko umdhaniaye kuwa mwenye nguvu.
            Heri mwenye njaa ya tumbo kuliko ya Kichwa. Heri aliyejishusha kuliko atakayeshushwa. Mpumbavu hujiamini anapopaswa kuchelea na kuchelea apaswapo kujiamini kwa sababu hana uwezo wa kujua mizania ya mambo. Yeyote akushauriye vitu vya hovyo, ujue anakuona hovyo na kukudaharau.
            Amuoneaye, kumdhulumu au kumuua yule ambaye asiyeweza kumuumba isipokuwa kumdhulumu, hujidhulumu, hujionea, na kujiua asijue japo hawafi siku na kwa namna moja. Kesho ni bora kuliko jana japo jana ndiyo iizayo kesho kama ambavyo kesho nayo kuna siku itakuwa jana. Heri ya mwaka mpya.
Chanzo: Mwananchi J'tano leo.

Sunday, 21 December 2025

Letter from Canada on nepotism


 In today’s letter, I’ll explore political nepotism and why does it not exist in Canada despite being racist. I’ll write an exclusive piece on this. Whereas Canada doesn’t have nepotism in the upper echelons of power, our southern neighbour, the US, is currently littered with it. Both countries use western democracy though differently.
        Canada isn’t only different from the US but also from Africa where colonisers introduced chaotic, choosy, and costly democracy that’s never worked meritoriously in Africa because it’s chimeric and a far-off imposition to Africa. Other than Botswana and somewhat South Africa, show me any African country with a functional democracy.
            Western democracy embeds and provokes intraparty affrays and fake jingoism for power but not serving the people as they portend and pretend to allege. Many so-called political parties are either kitbag property of their founders and owners, undemocratic, and veiled means of controlling resources for exploitation for a political cabal of self-seekers, their families, and friends in conjunction with foreign masters who fund democracy but not development. 
            Lucidly, colonisers introduced their colonised democracy to Africa to perpetually weaken, control, and exploit it. That’s why it's created family domination and monopolisation of power in many African countries. Why’s this democracy always depended on the west if it doesn’t serve its hidden interests as opposed to those of the African hoi polloi? Western countries are always generously happy to dish millions of dollars out to fund our elections.
            To make sure that recipients meet their standards, they dispatch electoral observers to Africa. Using their lens, once they’re satisfied with the results, they’ll declare it credible, free, fair, and transparent or not. Why don’t they allow us to observe their elections at least to learn how democracy is implemented and give our insignificant verdict? Former Zimbabwe President Robert Mugabe once wanted to send electoral observers to the US botched elections. My eye! The US flatly refuted and warned him not to repeat demean an ‘advanced’ democracy. Ironically, the same elections were marred with irregularities in the recent years wherein pro-Trumpian Americans attacked the ‘temple’ of democracy, the Capitol Hill.
            This brings us to an overtouted but convoluted riddle of the government of the people, by the people, for the people, a ding-dong of democracy, which worries me a lot. Who are the people, many, and what are they? Simply put, any binadams more than one are people. After winning twice, US President, Donald Trump filled many top positions in his government with family members. 
            Trump appointed his son-in-law, Jared Kushner, his senior advisor, Jared’ father, Charles Kushner, US ambassador to a peeved France (CNN, Nov. 30, 2024), Kimberly Guilfoyle who’s engaged to Donald Trump Jr since 2020 ambassador to Greece, and Massad Boulos—the father-in-law of Trump’s youngest daughter, Tiffany— senior adviser on Arab and Middle East African issues (US Today, Dec. 11, 2024) who also recently became the interceder in the DRC conflict.
        Ironically, when African Presidents replicates the same, it’s called nepotism! It becomes sacrilegiously antidemocratic while it's ‘our time to eat.” Let’s face it. Nepotism is nepotism. Period. It’s bad howbeit who employs, enjoys, entertains, or espouses it.
        When President Samia brutely appointed her daughter, Wanu and her son-in-law Mohamed Mchengerwa, Ministers or when President Museveni appointed his son Muhoozi Keinerugaba, the CDF and his wife Janet, Minister, it became big news globally. Tongue wagged with condemnations and pointless condescendence. In Equatorial Guinea, its long-serving President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo appointed his sons, Teodoro Nguema Obiang Mangue, Vice President and Gabriel Lima Mbega, Minister like his Togolese counterpart Gnassingbe Eyadema appointed his son Faure Essozimna Eyadema, who later inherited the presidency after his demise.
        In Ivory Coast, Alassane Ouattara appointed his younger brother, Téné Birahima Ouattara, Minister of Defence. In Congo, President Denis Sassou-Nguesso appointed his son Denis Christel Sassou Nguesso Minister in his government. What difference does such nepotism have from the one in the US or any monarchy? Isn’t it familydom?
        My simple argument is: if we want to become truly democratic, democracy must apply equally across the board failure to which means double standard and stinking hypocrisy.
        For western democracy to work effectively and equally, it must apply the same standards globally. Its selectivity, inequality, and veracity are its big undoing. We need to decolonise and deconstruct western democracy by diving back into our past to see how our precolonial institutions and systems worked judiciously as a viable and workable alternative to western democracy, which has become a mockery if not mere demockery, demagoguery, roguery.
Source: Daily Monitor Sunday today.

Wanawake Wasomi na Kitendawili cha Ndoa


Kuna swali huwa linatushughulisha kama wazazi na wanandoa tena wa muda si haba. Je, inakuwaje baadhi ya wanandoa hufanikisha mambo yanayowashinda wengi katika maisha ya ndoa? Tutaanza na mfano wa Malkia wa Uingereza marehemu Elizabeth (21 Aprili 1926 – 8 Septemba 2022). Pamoja na matatizo ya hapa na pale, malkia alibainisha kuwa inawezekana kufanikiwa kimaisha na katika ndoa jambo ambalo huwashinda wengi na kusababisha wawe na ndoa zenye changamoto na mazonge tokana mafanikio yao.
            Je, huwaje kukawa na watu waliofanikiwa kitaaluma, kiuchumi, na mengine lakini wakashindwa katika ndoa? Utamuona mtu ni tajiri lakini maskini wa ndoa. Mwingine ni msomi wa kupigiwa mfano lakini asiye na ndoa.
 Kuna wenye utajiri wa kuitwa utajiri lakini hawamo katika ndoa au ndoa zao zimevunjika. Jikumbushe watu waliofanikiwa kama vile Mfalme Charles wa Uingereza, Bill Gates, Donald Trump, Jeff Bizos na wengine ambao ndoa ziliwashinda. Walinganishe na watu wa daraja lao kama vile Warren Buffet na wengine ambao ni matajiri wenye ndoa za kupigiwa mfano. Je, kuna siri gani katika kushinda na au kumudu taasisi tata lakini nyeti ya ndoa?
            Maana, utakuta mtu maskini au asiye msomi ana ndoa imara kuliko ya tajiri ilhali wasomi na matajiri zinawashinda. Nenda mbele zaidi. Utakuta mama mrembo asiye na ndoa ilhali yule asiye mrembo anayo tena imara. Inakuwaje matajiri, wasomi, na warembo japo si wote wasiolewe lakini maskini, wasiosoma, na wasio warembo wakaolewa na kuishi kwenye ndoa imaara? Hapa kuna fumbo vile vile somo.
            Jiulize. Ni wamama tena matajiri au wasomi aka mishangazi–––japo hatupendi kushabikia neno hili––––wangapi wanaishi bila ndoa tena wengine wakitamani au kutangaza kutaka kuolewa wasiolewe? Wakati huo huo, unaweza kumkuta muuza baa akiwa kaolewa na anafaidi ndoa! Je, hapa ndipo msemo wa kuolewa majaliwa una maana zaidi? Je, nini kifanyike? Je, wazazi waache kuwasomesha mabinti zao ili waolewe au tubadili mtazamo juu ya wenzetu hawa?
            Japo hili haliongelewi,  kuna haja ya kuangalia mifumo yetu ya elimu inayowaandaa hawa waathirika. Mfano, siku za hivi karibuni kumekuwapo na madai hata visa vingi vya rushwa ya ngono kwenye baadhi ya vyuo. Hapa, tukiwa wakweli, waathirika ni akina mama. Kwanini tusibadili mfumo wetu? Mfano, hapa Kanada, si rahisi mwalimu kumtaka wala mwanafunzi kutoa rushwa ya ngono. Hii ni kwa sababu, hapa, tunao mfumo wa kutathminiana baina ya walimu na wanafunzi. Mwalimu anawatathmini wanafunzi ambao pia humtathmini. Pia, ikigundulika kuwapo kwa uchafu huu, mwalimu ataumia na kujutia maisha yake yote.
            Mbali na rushwa,  kuna tabia binafsi za wahusika hasa wale wasiopenda kuhenyekea maisha yao hadi wakashindwa kuona mbali kiasi cha kugeuza miili yao maduka ya kupatia baadhi ya huduma na mapato kirahisi wasijue madhara yake hapo baadaye. Hata hivyo, tunaonya na kusisitiza, si wasomi wote ni wa hivyo japo wapo wengi wa hivyo. Kwa wale wanaoshangaa kukuta msomi kaoa mama asiye msomi, hapa wanaweza kupata jibu.
            Tukiachana na tatizo la mifumo ya hovyo na kirushwa, tuangalie jamii kwa kujiuliza maswali haya. Je, hapa, tatizo ni wahusika pekee yao au jamii? Nini suluhu ya kadhia hii? Tutajaribu kujibu maswali haya chokonozi na tekenyeshi kifikra. Kwa mujibu wa American Boys and Men (2025), ni asilimia 50 tu ya wanawake wasomi wanaoolewa tena na wasomi wenzao. Nusu ya idadi iliyobaki, huolewa na watu wasio wasomi. Waliobaki wanabakia bila ndoa. Je, kama jamii, tumejiandaaje kukabili janga hili?
            Mwisho, kwa nchi zenye kufanya kwenye utafiti kama Marekani, tatizo tunaloongelea linaeleweka ukubwa wake. Je, kwa nchi zisizofanya utafiti, tatizo ni kubwa kiasi gani? Kama jamii na taifa, kuna haja ya kuyadurusu masuala kama haya ili kuweza kuwa na ndoa bora ili kupata taifa bora hasa ikizingatiwa kuwa ndoa ndizo huzaa wananchi ambao hutegeneza taifa. Kuna wakati tunadhani kuwa somo la ndoa linapaswa kufundishwa mashuleni kuanzia madarasa lau ya sita na kuendelea juu. Yawezekana kufanikiwa katika ndoa na mambo mengine. Je, tufanyeje?
Chanzo: Mwananchi J'pili leo.

Wednesday, 17 December 2025

Tulaani mabeberu mabarubaru na maburebure

 

Kuna mafyatu wanatubaparigaza na kutushangaza. Si mabeberu ‘wameleta’ vuguvugu na vurugu kayani!  ‘Wamehonga’ watoi na mafyatu wakiwashe na kukinukisha kiasi cha wote kunuka wakahujumu amani ya imani kupitia ‘vurugu’ eti ya kudai haki. Wamewadanganya kuwashinikiza mdai haki mkaponzwa. 
        Eti hamna haki! Haki gani katika kaya ya amani yenye ajira lukuki? Nani asiyepata haki hadi akataka aipate asiipate kwa vile haipatikani? Mbona hata wadudu na wanyama kayani wanaipata? Hujasikia chawa, funza, na kunguni wakitesa kama hawana akili nzuri? Hamuoni wanavyozifuja na kuzitabanga njuluku na ‘aslimali’ zetu huku tukisota? Haki gani mabeberu wanaweza kutoa ambayo hao maburebure hawatoi? Kama yupo asiye nayo, akaitafute ilipo badala ya kuhongwa kutuletea fujo na kutuudhi kwa raha zetu?
        ‘Wamewahonga’ ndumu, muguka, gongo, na ahadi za unyampala uchwara wauaji na watekaji wasiojulikana kuua na kuteka mafyatu na kuwapoteza mafyatu na mabarubaru wao. Kwanini kulaumu mabeberu bila maburebure wakati watekaji hawajulikani, au siku hizi wameanza kujulikana? Kawaulize akina bashiti walioshiti ukweli na uhalisia wakajifanya hamnazo wasijue kuna siku watalipa si kama walivyotegemea.
        ‘Wamehonga’ vyombo vya umbea kuandika umbea dhidi maburebure bila kuvisaza vile vya uhasama vinavyotumika kuhalalisha haramu na uovu vya kibeberu ya maburebure kwa maburubaru na mafyatu. ‘Wamehonga’ kila fyatu kuhatarisha maisha ya mabarubaru aka Gen Ziro na mafyatu.
        ‘Wamehonga’ madoktari ‘kudanganya’ eti walioambwa waue au kuficha namba ya waliouawa! Je, ni wangapi waliuawa na huu ubeberu wa maburebure?
         ‘Wamehonga’ wazazi kusingiziwa wamefiwa na watoi wakati hawakuuawa! Wamehonga mashehetani waliotishia kukata mafyatu vichwa kiasi cha kushindwa kutumia akili wakiishia kutumia njaa na utumbo. Hawa, ni wabaya kwelikweli.
        ‘Wamejihonga wakatugeuka bila makosa isipokuwa raslimali zetu. Hata hivyo, hawatutishi. Nani anahitaji fadhila na misaada yao wakati wanahitaji msaada kuwazuia waache kuhonga na kuharibu mafyatu wetu? Wamejihonga na kujitoa ufahamu na kuanza kutuwekea vikwazo ili tukwazike tujikwaze na wanaotukwaza watukwaze zaidi.
        ‘Wamehonga’ hata ndege watuzomee na kutushangaa. Kwanini tunafanyiwa na kufanyiana hivi kana kwamba sisi ni hamnazo au tumejitoa ufahamu na kuwa na kiherehere cha kunyotoana roho?      
 Mabeberu ‘wanatuonea’ wivu hasa sie wanaotuitao mabureburure wenye mamlaka ya kazi bure kiasi cha kutuzushia mambo ya ajabu. 
    Bure kabisa. Kufanikiwa, si waliwahonga hata wasioonekana wakawatekeka, wakawapoteza, na wakawaua mafyatu tena wasio na hatia ili tulaumiwe. Mwenye makosa anamlaumu asiye nayo. Asiye na makosa anamlaumu kila mmoja kwa kutoshirikiana naye wala kumsaidia kupata jawabu tunalosaka. 
        ‘Wameleta’ bunduki na kuwapa wasiojulikana wauaji wakaua mafyatu halafu wanasingizia ndata wetu watiifu wasioweza kuua hata inzi kama amruisha mkuu wao. 
        ‘Walihonga’ hata vyombo vya umbea vya kimataifa vikadai kuwa mbarubaru waliuawa kwa maelfu wakati waliouawa ni mamluki na si mafyatu wala mabarubaru wa kaya yetu ya peace.
        Hata ingekuwa kweli japo ni kweli, nani aliwaua kama siyo mabeberu waliomwaga njuluku? Kwani, yanawahusu nini? Mambo ya Ngoswe muachia Ngoswe nyie mabeberu hata kama wakati mwingine mnakuwa waungwana na kugharimia sirkal zetu na uchaguzi wetu ili tuwape dili za kuwapiga mafyatu. Hata kama kweli kama tuliua, kwani, tuliua wenu?
        Nani kawambia tuliua mabarubaru wetu? Sisi si wanyama kiasi hicho tuue mafyatu wetu. 
Japo wapo waliokufa, waliuawa na mabeberu siyo sisi walioonyesha ujahiri, ujuha, na uzwazwa vya hali ya juu. 
Ebo! Mbona tushaambwa kufa ni kufa na ni jambo la kawaida? Kwani, kwenu ubeberuni, sawa na ububuruni,mabarubaru hawafi kwa mibwimbwi au kujinyotoa roho? Eti wanataka tufanye mageuzi watugeuze majuha! Mageuzi kafanye nyinyi. Sisi hatuyahitaji kwa vile ni hatari kwa mstakabali wa kaya yetu ya amani hata kama ni ya imani. Acheni kutuonea wivu.
        Tunajua kwanini mnamchukia hata malkia wetu. Mnataka eti tuanzishe domoghasia yenu. Mbona pale kwa Chaz hawanayo ila mfalme mwenyewe mwana wa maza? Tukiteuana mnasema tuna upendeleo. Mbona Tarampu ameteua wakwe zake na vivyele vyake hamlalamiki? Ni kwa vile sisi siyo watasha siyo?
        Wamekuja na kuiba raslimali zetu lakini hawatosheki. Wameingia kimiujiza wakatusainisha mikataba ya uchukuaji ya ajabu ajabu. Hamtosheki wana hizaya nyie? Juzi, nilisikia mabeberu na mabuburu wakitaka kupenyeza hata udini! Ebo!                                
    Hamjui kuwa hizo dini mlizotuletea zilitukuta na zitatuachana tunajua kuwa mlizitumia kuingiza ukoloni hata uzwazwa kiasi cha kutuibia ardhi, madini, hata majina yetu? Mnadhani hatujui? Sisi siyo mataahira kama al Shabubu au Buku Haramu kugombania vitu visivyo vyetu wakati tukidharau vyetu. Sisi ni wazalendo ambao tuko tayari hata kumwaga damu kulinda ulaji, sorry, kaya yetu.
            Mkome na kukomaa kabla hatujawakomesha. Senzi nyie. Mnawapa watoi mibwimbwi wachukie wanene wapendwa na wawakosoe wakati hawakosei. Walaaniwe mabeberu na maburebure. Hivi nshameza vidonge vya kuzuia kuota nchana!
Chanzo: Mwananchi Jtano leo.

Wednesday, 10 December 2025

Mafyatu wanapokuwa kama kuku, mbwa, na wawafugao


 

Kuna hiki kisa cha binadamu, kuku, na mbwa. Mbwa alimfyatua kuku wa mwenyewe. Acha kuku, mbwa, na wenyewe walaumiwe na kulaumiana kwa kuku kufyatuliwa na mbwa! Mwenye mbwa alimlaumu kuku na aliyemfuga kwa kujiruhusu na kuruhusu aliwe. Kisa hiki cha kufikirika na kufikirisha. Kina maswali na mafunzo mengi. Kwanini alaumiwe mbwa na si yule aliyemfuga kuku au mbwa? Kwani, kazi ya kuku ni nini kama siyo kuliwa? Kwanini kuku alijiachia na kukubali kufyatuliwa? Kwanini ana nyama inayoliwa na siyo isiyoliwa? Je, walitaka mbwa ale nini na kuku aliwe na nani? Mbwa, akila kuku, ni kosa ila binadamu hapana! Kuku, japo kazi yake ni kuliwa na kutaga mayai yaliwayo pia, akiliwa, analaumiwa! Ebo! Kuku lake ni kuliwa bila kujali kaliwa na binadamu, kicheche au mbwa. Kuku ni kuku lazima ataliwa tu.

 Uzuri ni kwamba mbwa hakujilaumu na hatajakaa ajilaumu kwa kumfyatua kuku. Kuna mafyatu wanakosea. Wanapaswa kuomba radhi hata kutubia kuwalaumu kuku na mbwa kulana. Kwani, wanakosea kwa kudhani wanawazodoa kuku na mbwa wakati ukweli ni kwamba wanajizodoa na kujiambia wenyewe kama siyo mafyatu wenzao.

Kinachoendelea kayani na lawama hizi ni ile hali ya kuwatupia lawama kuku na mbwa wakati wahusika ni nyinyi. Hata kesi yake ipelekwe mahakama kuu, kuku hatashinda kesi wala kuwa na haki zaidi ya kufugwa na kuliwa. Kwanini mnataka kumpaka kitimoto lipstick mkidhani atarembeka? Kitimoto ni kitimoto. Mnamsumbua kitimoto bure kama mnamsumbuavyo mbwa kwa kula kuku na kuku kuliwa na mbwa. Nani anamjali kuku? Nani anamuombolezea kuku? Kweli, kuku ana haki au ni kwa vile kaliwa na mbwa? Kuliwa ni kuliwa. Kuku aliwaye na mbwa hata simba hana tofauti na yule aliwaye na mafyatu. Anafyatuliwa tu. Hivi, kweli hawa wanaomtetea kuku wanamtetea au kutetea mlo wao? Kigombacho ni pale fyatu anapowala mafyatu wenzake halafu akawalaumu kwa kujiruhusu kufyatuliwa naye bila wala yeye kujilaumu au kukubali kulaumiwa.

Juzi, nilisika maboksi na mashehena yakitika ka debe tupu. Huu uliitwa muujiza na wanaojifanya wana dini wakati ni duni. Ajabu ya maajabu, hawaongelei wala kuhoji. Inakuwaje mafyatu wanaongelea amani na kuitenga haki wakati hawa ni mapacha? Kunani hapa? Eti walitetea mafyatu wale kuku kwa amani wakati wakijiganya hawajui wala kuona haki ya kuku! Hivi mwenye mbwa anapokuwa mbwa mwenyewe mtasema nini? Je, kwanini kumdhalilisha mbwa ambaye yuko radhi kumfia bwana wake ambaye hawezi hata kumlilia? Mheshimu mbwa tafadhali. Kwani, ni kiumbe mwaminifu na anayelinda hata wahalifu wamfugao.

Jikumbushe yafuatayo ndipo unene. Mbwa hulinda mali zenye thamani kubwa lakini hufa maskini. Sindano hushona nguo nyingi lakini daima iko uchi. Kijiko huungua kuchota chakula na mchuzi. Nini hufuata baada ya mwenye kushiba kushiba kama siyo kukiosha na kukikausha? Hatushangai uongo unapogeuka uogozi na uongozi kuwa uongo? Najua. Wengi mlikuwa wakati wa Ticha Mchonga.  Muelewe. Mambo yamebadilika na kuharibika au siyo? Kubalini. Wakati ule, mliona nuru. Leo, mtaona kiza totoro mtake msitake. Si shehe Ruksa aliwaonya kuwa kila zama ina kitabu chake?

 Tafuta hicho kitabu ukisome uelewe. Najua wengi ni wasomi tena wenye PhD ziwe za kweli au za kuzawadiwa, kununua, na kuhongwa. Wangapi wayajua mateso ya kuzisomea na kuzipata baada ya kuhangaishwa na maprofesa wenye wivu kuwa utakuwa kama wao? Kumbuka. Unasimamiwa wakati mwingine jitu ambalo kiakili haliwezi hata kugusa sole ya kiatu chako. Jiumbushe. Ni committee chairs wa PhD unaowakumbuka ambao hata kufikiri namna ya kufikiri hawajui? Si ajabu mjinga kumfundisha msomi au mwenye macho kuongozwa njia na kipofu. Ndo mambo ya siku hizi. Tusizinguane wala kuhadaana na kugeuzana mazwazwa wakati tuna akili. Tusijitoe ufahamu na kufanya ukuku wa kumtetea kuku au umbwa wa kumla kuku wa wenyewe.

Naona yule anashangaa! Unashangaa nini mwenye macho kuongozwa na kipofu mwanangu? Amka uchangamke. Usilaumu wasiolaumiwa. Jilaumu mwenyewe. Ikizidi ikapungua, lalamika lakini si kulaumu. Kwani, ni kosa la jinai tena kubwa kuliko uhaini na ugaidi. Wakubwa huwa hawakosei. Wakikosea, hawakosei wala kukosolewa.

 Wenye mbwa, huwa hawaaibishwi. Unalaumu kwanini mbwa kala kuku! Ebo! Mbwa akila kuku ni kosa la kuku siyo mbwa wala mwenye mbwa. Kama ukitaka kuwaingiza wamilki, mbwa akila kuku, kosa ni la mwenye kuku ambaye hakumfunga wala kumtahadharisha na mbwa. Kazi ya mbwa, kama kicheche na mafyatu, ni kula kuku. Na kazi ya kuku ni kutoliwa na mbwa japo ataliwa na wengine bila kujali ni nani na kwanini. Naomba utie akilini. Hii dunia ni ya mbwa si ya kuku.

Acha nisiwachoshe kabla hawajanichoka, kunichosha, kuniteka, na kunitesa kabla ya kuniua. Wajue. Wakiniteka, nawateka tutekane kama ilivyo kwa sasa ambapo mtekaji na mtekwaji wote ni mateka wa utekaji. Hivi, leo, nimekunywa gongo kiasi gani?

Chanzo: Mwananchi Jtano leo.

Sunday, 7 December 2025

Letter from Canada à la authentic elections

 

There recently were botched and violet elections in Tanzania. Uganda is currently braced and geared for general elections next January. I wish it well. May these elections be credible, fair, free, and transparent. So be it. I’ve lived in Canada for over two decades. May I pull a leaf out of Canada’s book vis-à-vis how to conduct clear, credible, fair, and free elections? For, it offers positive insights. Thus, Uganda must (not can) learn and take a leaf from the Tanzania's lessons to avoid committing or repeating the same flaws.
            First, elections in Canada aren’t cutthroat and corrupts. For, voters vote for policies not parties and personalities. To win an election in Canada, present sound policies that respond to voters’ aspirations and interests altogether. Hence, the system here doesn’t allow, accommodate, or tolerate any sort of corruption or malpractices. Candidates squarely get what they deserve.
            Secondly, there aren’t expensive or pompous campaigns. In my town of approximately 4,400 people of about 17 years, I’ve never seen any campaign meeting. Not one, not once. When it is time for elections, the Electoral Commission set a date for elections. Public places are used to cast vote. 
                There are four ways of voting in Canada. One can vote on election day by going to a polling station and cast one’s vote or by advance polling days, which is before the voting day. If one doesn’t want to or can’t vote in the above category, can do so at any Elections Canada office or by mail. For those who want to vote in the last category,  provides his or her postal address to the Election Canada, which posts a voting kit ready for casting it.
            Thirdly, with such a system, there are no huge campaign meetings everywhere in the country. There also no chaos or cheating or rigged. Furthermore, there are no inducements or coercion since people here vote for policy not personalities or parties. This system has proved to be efficient and effective for both candidates and voters so to speak.
            Fourthly, Canada started voting in 1867. Canada is a multiparty country. It has many big and small political parties such as the Liberal Party of Canada, a centre-left political party that has historically been one of the two dominant parties in Canada; the Conservative Party of Canada, a centre-right political party that emerged from the merger of the Canadian Alliance and the Progressive Conservative Party; and the New Democratic Party (NDP), a left-wing party that advocates for social democracy and progressive policies.
            Others are the Bloc Québécois, a federal political party that promotes Quebec nationalism and advocates for the interests of Quebecers; and the Green Party of Canada, which focuses on environmental issues and sustainability, advocating for green policies and practices. These are the bigger parties, which are a must have in every general election.
            Other registered parties are the People's Party of Canada, a right-wing party that emphasises individual freedom and limited government intervention; the Christian Heritage Party, a socially conservative party that promotes Christian values in politics; and the Libertarian Party of Canada, which advocates for civil liberties, free markets, and minimal government intervention in personal lives, among others. Nevertheless, the top three are the dominant players in the politics of Canada.
            Fifthly, due to being corruption proof, I have never heard of any electoral corruption case. I tried to research in the archives and got none whatsoever. That said, that’s why Canada’s political system remains one of the world’s most stable and respected democracies.
            Sixthly, why are there no corruption in Canada’s elections? There are many answers among which are the fact that, in Canada as opposed to Africa, politics isn’t a moneymaking endeavour. Firstly, people run for political positions to serve people but not to serve themselves and families. Secondly, no politician, even though there can be a few, stays in a position for forlornly long. Specifically, since President Museveni came to power, Canada’s had seven Prime Ministers compared to our southern neighbour, the US with 8 Presidents.
            Finally, no party’s ever won more than 50-odd percent in four decades. Therefore, in Canada, neither party nor its leader has ever dreamt of winning with a bigger percentage as we recently evidenced in Tanzania where current President, despite bedlam and bloodbath, miraculously ‘won’ 98 percent! So, you know.
Source: Daily Monitor Sunday today.

Lugha yaweza kudumisha au kubomoa ndoa

   Tutaanza na kisa cha wanandoa A na B waliomo kwenye ndoa hatarishi. Wapendwa hawa wamedumu kwenye ndoa yenye misukosuko, visa, na visasi visiyo vya lazima kwa miaka sasa. Kwa umri wao na wa ndoa yao, ungedhani wangetulia, kulea watoto, na kujiandalia maisha ya utu uzima. Hata hivyo, si hivyo. Badala ya ndoa kuwa kimbilio, bahati mbaya, kwao, imegeuka mateso kwa pande zote. Kila uchao, wako kwa waganga, wachungaji, marafiki, hata wazazi kusaka ushauri juu ya namna ya kuboresha na kuokoa ndoa yao inayoyumba kwa muda mrefu.
            Katika kuwasikiliza, tuligundua yafuatayo ambayo wengi wanaweza kuyapuuzia wakitafuta mchawi wakati mchawi ni wao:
            Mosi, hawana siri. Ugomvi mdogo tu, kila mmoja anatafuta majirani, marafiki, ndugu, mashoga, washauri, na wengine kutafuta msaada! Kumbukeni. Mlipokutana na kukubaliana kuoana, mlikuwa pekee yenu. Mkivunja ndoa yenu, wao pia, hawataathirika zaidi ya kuwacheka hata kuwang’onga na kuwaona wa hovyo. Jifunzeni kutunza siri zenu hata kama mtaambiwa za wengine. Kama ni ushauri, siyo kila umuendeaye atakushauri vizuri. Mjue. Kila mtu ana ushauri ila si kila ushauri ni bora.
            Pili, hawaheshimiani. Tushaambwa. Heshima si utumwa na ni kitu cha bure chenye thamani. Msingi mmojawapo wa ndoa ni kuheshimiana. Hakuna uungwana unaoweza kukuza na kuzidisha upendo kama wawili kuheshimiana. Tunajua. Nyinyi si malaika. Pia, si mashetani. Mkiheshimiana, mtapendana na kuthaminiana na si kubomoana msijue mnajibomoa wenyewe. Msipoheshimiana, mtadharauliana na kudharauliwa hata na msiotegemea kama vile watoto wenu. Hata hao mnaowapelekea umbea juu ya tofauti hata ugomvi wenu, wanawananga na kuwadharau kwa uzembe huu. Não, wanayo yao.
            Tatu, wana lugha mbaya. Wanabagazana, kudhalilishana, kufokeana, na kutukanana tena mbele ya watoto wasijue wanavyowaharibu na kujiharibia. Kama matusi ndilo chaguo lenu za kuibua hoja na kupoza hasira, basi nendeni faraghani mtukanane mmalize na kuchoka. Kwanini kuwahusisha wasiohusika? Je, inasaidia nini zaidi ya kuongeza matatizo kwenu na wasio husika? Kama mna tofauti au ugomvi, nenda chumbani, au toka muende faraghani mfokeane hadi mchoke.
            Nne, hawaaminiani. Msipojiamini na kuaminiana, wengine hawatawaamini. Kuaminika huzaa kuaminika. Kadhalika, kutoaminiana huzaa kutoaminiwa. Kutoaminiana ni zao la kutojiamini. Je, mtaaminiwaje wakati hamjiamini wala kuaminiana?
            Tano, wanadharauliana. Watu wanaweza kuheshimiana bila kudharauliana. Katika hili, wahusika uheshimu mipaka yao na ya wenzao. Wadharaulianapo, mjue. Watadharauliwa. Kuliepuka hili, mhusika asijidharau, kudharauliwa, au kumdharau mwenziwe.
            Sita, wanashindana. Ndoa si mashindano bali kukubaliana kuishi na kufanya mambo pamoja kwa faida yenu wote. Kama mke ni mwili wa mume na mume ni mwili wa mke, nani awezaye kushindana na mwili wake? 
    Tunaposema mke na mume ni mwili mmoja, tunamaanisha matendo na siyo kuchukua miili miwili na kuiunganisha kibaolojia bali kijamii na kimahusiano. Ashindanaye na mwenzie, anashindana na yeye mwenyewe. Ni sawa na paka au panya kukimbiza mkia wake au mtu kukimbia kivuli chake. Hakuna mshindi wanandoa washindanapo.
    Sasa wahusike wafanye nini?
        Kuna njia nyingi za kuepuka hayo tuliyotaja hapo juu.
Kwanza, ni kuelewa kuwa hayajengi wala kuimarisha ndoa bali kuibomoa. Hivyo, jibu ni kufanya mambo kinyume. Kacheni mliyokuwa mifanya. Mtaona matokeo yake na kushangaa. Jaribu muone.
        Pili, fanyeni tathmini ya matendo na ndoa yenu. Katika kufanya hivyo, ainisheni hasara na faida (kama zipo) juu ya matendo yanu hatarishi.
        Tatu, kuweni wawazi baina kwelikweli ili kulijua na kuliona tatizo pamoja na kutafuta suluhu pamoja kwa sababu athari za matendo yenu huwaathiri pamoja. Dawa ya uchafu ni usafi. Na dawa ya migogoro ni amani na kukubaliana kuishi kwa amani na kuacha yote yale yanayowakwaza. Mjue. Mnajikwaza wenyewe. Hivyo, mwaweza kujiondoa kwenye vikwazo wenyewe mkiamua. Hamna mchawi bali nyinyi wenyewe. Je, wapo wangapi kama hawa?
        Mwisho, tunasisitiza. Waathirika badilini tabia na mwelekeo. Fanyani tofauti na mlivyozoea kufanyiana. Mtaona mabadiliko makubwa. Kimsingi, hakuna mchawi bali nyinyi wenyewe. Hivyo, msipoteze fedha na muda kutafuata mchawi. Mnaye baina yenu.
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.

Tuesday, 2 December 2025

Nimeamriwa kufungua hekalu la God la KGBJRJFRM


 Nikiwa sina hili wala lile, juzi, nilitokewa na Malaika wa Bwana akaniminyaminya na kuniamru nianzishe Kanisa ili kuikoa dunia hii inayoangamizwa na uzwazwa. Mwanzoni nilikataa kufanya hivyo nikidhani ni ndoto tu. Mara ya pili, si nilimezwa na samaki aina ya changu kwa siku tatu kule Manzese mpaka Bi Mkubwa alipostuka wakati nilikuwa napitia kwenye majaribio aliyopitia Yona yule mjanja aliyemezwa na Nyangumi wa kike kwa siku tatu. Hayo tuyaache.
         Baada ya juzi kusikia Askopo moja wa kujipachia ambaye duka lake la kuchuuza na kuuza roho za mafyatu waliokata tamaa na kutapatapa, si nikaijiwa na wazo la kifyatu la kufyatua njuluku kirahisi. Hapa, lazima nifyatue ukweli. Lazima nifyatue njuluku tena kiulani. Soon, sitaitwa Fyatu kapuku bali Fyatu mkwasi. Najuta. Sijui kwanini nilipoteza muda vyuoni wakati kuna fursa rahisi kwa hata vilaza na vihiyo kupiga njuluku ndefu! Maana, unene wa NGO kama hii ni wa kujipachika. Auhitaji kupiga shule mpaka ukafyatuka na kuonekana chizi.
            Kusema ule ukweli, tuache utani. Sikuamini kusikia madai ya ajabu kuwa ndata wetu waaminifu na watiifu waliokuwa wakilinda duka hilo la Ufu na Uendawazimu eti walikwapua mabilioni! Du! Wamejua kutufyatua! Inakuwaje kwa mwizi anaiba mwizi kama kweli njuluku ilipigwa? Kumbe mkuki ni kwa nguruwe!  Hekalu la Sir God na njuluku wapi na wapi wakati mwana wa Adam alikuja na kuondoka akiwa kapuku? Ajabu, wezi, sorry, wapigaji wenye roho mtakakitu wakimuita roho mtakatifu wanawafyatua mafyatu wasiofyatuka na kuhoji kuwa wanamhubiri mwana wa Adam huyu ambaye mie namjua kwa sababu ni wa ukoo wangu.
            Jina la kanisa langu linaitwa The Kasri of all God's, All Binadams and Jinni for Redemption and Jannah Firdaws Roho Mtakakitu Mtakatifu (KGBJRJFRMM). Usishangae urefu na utata wa jina la nyenzo yangu. Kuwapata mazwazwa wakaamini umepiga vitabu lazima utumie kimombo na majina marefu. Pia, lengo jingine ni kuunganisha din izote na kuepuka mchezo wa kutumia dini, udini, na udini kuwagawanya na kuwadhoofisha mafyatu japo hawafutuki na kushutukia huu ufyatuaji tunaotumia kuwafyatua.
        Kuwafyatua mafyatu vizuri, lazima nishughulikie matatizo yote Hivyo, wale wote wenye matatizo kama vile uzwazwa, umaskini, ugumba, uchungu, huzuni, mawazo, wasiwasi, waliovimbiwa, wenye njaa, waliotekwa, waliopotezwa nk.nk. Mie nitawapatia majibu ya matatizo yenu yote. Unatoa sadaka kidogo au kununua maji ya uzima na matatizo yako yote yanaisha hapo hapo. Mfano, shoo yangu ya kwanza ni kuahidi kumfufua Aminia Mfupa au kujifanya nimepooza halafu nikajitibu mwenye japo ukweli ni kwamba mganga hajigangi. Nitahakikisha natengeza maji ya uzima ambayo nitayajaza urahibu ili atakayeyaonja awe anarudi kununua mengine nami nafyatua njuluku. Hapa, dhambi iko wapi? Si tuliaswa kwa wajinga ndio waliwao?
            Najua wengi wataanza wivu wa kizwazwa. Watahoji kwanini mwana wa Adam alihubiri umaskini nami nataka njuluku. Simpo. Ufalme waliwao ni wa mbinguni. Sie, wajanja ufalme wetu ni wa hapa duniani. Msishangae. Kwanza, kuna vishawishi vingi ambavyo muovu sheitwan kaniletea. Mfano, ukifungua duka la kawaida TrA wanakuandamana wakati la kiroho hakuna kulipa kodi japo unawatoza wachovu kodi. Pia, kwa kutumia hii nyenzo, naweza kuingiza bidhaa zangu toka ughaibuni tena zisizo za kiriho na za wengine free. Hawa, nitakaowasaidia kutumia nyenzo yangu kupitisha bidhaa zao, lazima niwatoze kodi mwenyewe japo sitozwi. Nani hataki ulaji huu wa dezo tena unaotaka ubunifu na kutumia akili kiduchu?
            Kwa vile wachovu hawana njuluku kama nitakazowakamua, nitawahimiza wamtegemee Mungu awalinde. Ila nashauri wasishangae kwanini mimi nitakuwa nalindwa na mabaunsa. Ni kwa sababu shetani anayeniandama ahitaji kupambana na Mungu bali mabaunsa. Ili kuhakikisha nafaidi hii fursa na ubunifu mpya, nitahakikisha natumia hii kitu yangu kugombea urahis. Maana, nao nimegundua ahuhitaji elimu wala chochote isipokuwa urahisi na utayari kuhomola na kuhondomola. Hapa, lazima nijifunze kwa tapelo mmoja aliyewahi kucheza haka kamchezo. Si alijiunga na chata twawala hadi akazawadiwa uhishimiwa hadi alipolikoroga akataka kuwatumia waliomtumia ili watumiane wakaishia kumtimua na kufunga duka lake akabakia kubweka kama dogi tena akijifanya kulaani yale aliyokuwa akiyashabikia zama zile za Mwendaze. Hapa, nitachanganya duni na siasa japo twaonya kuwa havichanganyikani. Mbona vinachanganyikana. Upaswacho kufanya ni kupiga siasa ukiwa ndani ya chata twawala. Duni na siasa japo vyote ni duni, havichanganyikani kama uko upingajini kwa akina Tunda Lishe.
           Ili kupiga njuluku ndefu, nitaanzisha mradi wa Kutenda miujiza. Hapa, lazima ‘nifufue’ wafu na kuponya vilema. Naona yule anashangaa. Kwani, kufanya mazingaombwe, sorry miujiza ni vigumu hivyo? Si unacheza mchezo na kupandikiza vilema feki ambao mkipata mnagawana. Unacheza na miujiza? Ukiachia hadithi na ngano za kufikirika na amewahi kuitenda?
            Mwisho, nitajipachika mavyeo mazito. Kuanzia leo, naitwa Alhaj, Mtakatifu, Mchunaji, sorry, Mchungaji, Askopo, sorry, Askofu, Kardinali, Papa, Paroko, Bruda, Darwesh, Daktari, Profesa, Maulana Muadhama, Shehena, sorry, shehe Ulama, n.k, n.k, etc. Hivi, nani walinileta hapa Mirembe?
Chanzo: Mwananchi leo Jtano.