Tutaanza na kisa cha wanandoa A na B waliomo kwenye ndoa hatarishi. Wapendwa hawa wamedumu kwenye ndoa yenye misukosuko, visa, na visasi visiyo vya lazima kwa miaka sasa. Kwa umri wao na wa ndoa yao, ungedhani wangetulia, kulea watoto, na kujiandalia maisha ya utu uzima. Hata hivyo, si hivyo. Badala ya ndoa kuwa kimbilio, bahati mbaya, kwao, imegeuka mateso kwa pande zote. Kila uchao, wako kwa waganga, wachungaji, marafiki, hata wazazi kusaka ushauri juu ya namna ya kuboresha na kuokoa ndoa yao inayoyumba kwa muda mrefu.
Katika kuwasikiliza, tuligundua yafuatayo ambayo wengi wanaweza kuyapuuzia wakitafuta mchawi wakati mchawi ni wao:
Mosi, hawana siri. Ugomvi mdogo tu, kila mmoja anatafuta majirani, marafiki, ndugu, mashoga, washauri, na wengine kutafuta msaada! Kumbukeni. Mlipokutana na kukubaliana kuoana, mlikuwa pekee yenu. Mkivunja ndoa yenu, wao pia, hawataathirika zaidi ya kuwacheka hata kuwang’onga na kuwaona wa hovyo. Jifunzeni kutunza siri zenu hata kama mtaambiwa za wengine. Kama ni ushauri, siyo kila umuendeaye atakushauri vizuri. Mjue. Kila mtu ana ushauri ila si kila ushauri ni bora.
Pili, hawaheshimiani. Tushaambwa. Heshima si utumwa na ni kitu cha bure chenye thamani. Msingi mmojawapo wa ndoa ni kuheshimiana. Hakuna uungwana unaoweza kukuza na kuzidisha upendo kama wawili kuheshimiana. Tunajua. Nyinyi si malaika. Pia, si mashetani. Mkiheshimiana, mtapendana na kuthaminiana na si kubomoana msijue mnajibomoa wenyewe. Msipoheshimiana, mtadharauliana na kudharauliwa hata na msiotegemea kama vile watoto wenu. Hata hao mnaowapelekea umbea juu ya tofauti hata ugomvi wenu, wanawananga na kuwadharau kwa uzembe huu. Não, wanayo yao.
Tatu, wana lugha mbaya. Wanabagazana, kudhalilishana, kufokeana, na kutukanana tena mbele ya watoto wasijue wanavyowaharibu na kujiharibia. Kama matusi ndilo chaguo lenu za kuibua hoja na kupoza hasira, basi nendeni faraghani mtukanane mmalize na kuchoka. Kwanini kuwahusisha wasiohusika? Je, inasaidia nini zaidi ya kuongeza matatizo kwenu na wasio husika? Kama mna tofauti au ugomvi, nenda chumbani, au toka muende faraghani mfokeane hadi mchoke.
Nne, hawaaminiani. Msipojiamini na kuaminiana, wengine hawatawaamini. Kuaminika huzaa kuaminika. Kadhalika, kutoaminiana huzaa kutoaminiwa. Kutoaminiana ni zao la kutojiamini. Je, mtaaminiwaje wakati hamjiamini wala kuaminiana?
Tano, wanadharauliana. Watu wanaweza kuheshimiana bila kudharauliana. Katika hili, wahusika uheshimu mipaka yao na ya wenzao. Wadharaulianapo, mjue. Watadharauliwa. Kuliepuka hili, mhusika asijidharau, kudharauliwa, au kumdharau mwenziwe.
Sita, wanashindana. Ndoa si mashindano bali kukubaliana kuishi na kufanya mambo pamoja kwa faida yenu wote. Kama mke ni mwili wa mume na mume ni mwili wa mke, nani awezaye kushindana na mwili wake?

Tunaposema mke na mume ni mwili mmoja, tunamaanisha matendo na siyo kuchukua miili miwili na kuiunganisha kibaolojia bali kijamii na kimahusiano. Ashindanaye na mwenzie, anashindana na yeye mwenyewe. Ni sawa na paka au panya kukimbiza mkia wake au mtu kukimbia kivuli chake. Hakuna mshindi wanandoa washindanapo.
Sasa wahusike wafanye nini?
Kuna njia nyingi za kuepuka hayo tuliyotaja hapo juu.
Kwanza, ni kuelewa kuwa hayajengi wala kuimarisha ndoa bali kuibomoa. Hivyo, jibu ni kufanya mambo kinyume. Kacheni mliyokuwa mifanya. Mtaona matokeo yake na kushangaa. Jaribu muone.
Pili, fanyeni tathmini ya matendo na ndoa yenu. Katika kufanya hivyo, ainisheni hasara na faida (kama zipo) juu ya matendo yanu hatarishi.
Tatu, kuweni wawazi baina kwelikweli ili kulijua na kuliona tatizo pamoja na kutafuta suluhu pamoja kwa sababu athari za matendo yenu huwaathiri pamoja. Dawa ya uchafu ni usafi. Na dawa ya migogoro ni amani na kukubaliana kuishi kwa amani na kuacha yote yale yanayowakwaza. Mjue. Mnajikwaza wenyewe. Hivyo, mwaweza kujiondoa kwenye vikwazo wenyewe mkiamua. Hamna mchawi bali nyinyi wenyewe. Je, wapo wangapi kama hawa?
Mwisho, tunasisitiza. Waathirika badilini tabia na mwelekeo. Fanyani tofauti na mlivyozoea kufanyiana. Mtaona mabadiliko makubwa. Kimsingi, hakuna mchawi bali nyinyi wenyewe. Hivyo, msipoteze fedha na muda kutafuata mchawi. Mnaye baina yenu.
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.

No comments:
Post a Comment