Tuesday, 21 June 2011

HONGERA DK WILLY MUTUNGABlog hii inachukua fursa hii kumpongeza jaji mkuu wa Kenya Dk. Willy Mutunga kuchaguliwa kuwa jaji mkuu wa Kenya. Pamoja na kuwa rafiki yetu wa karibu, tunachukua fursa hii kuungana naye kwenye adhimisho hili la utumishi wa umma uliotukuka.Kwa tunaokukumbuka ukiwa Mkurungenzi mtendaji wa Kenya Human Rights Commission pale Valley Arcade Lavington kabla ya kwenda kuwa mkurugenzi wa Ford Foundation pale Kenyatta, tunajua unyenyekevu na uwazi wako. Tunaokujua kama Mutunga na si daktari wala jaji mkuu, tunajua ni aina gani ya mtu na mchapakazi Kenya imepata hasa kipindi hiki cha kuanza kutekeleza katiba mpya ya Kenya. Tunaamini mchango wako utakuwa somo na changamoto kwa nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazoendelea kutawaliwa na ubabaishaji, ukale, usanii na majaribio.
Kila la heri na Mungu akuongoze na kukufanikishia kila chema ulichodhamiria kuitendea Kenya.
Dk Mutunga, tunaamini utakuwa chemi chemi ya mageuzi na ukombozi wa Kenya kama ambavyo umekuwa siku zote.
Ni rafiki yako Nkwazi Mhango

No comments: