Tuesday, 28 June 2011

Mgao wasababisha vurugu Senegal somo kwa Watanzania


Wakati watanzania wakiendelea na ukondoo na kuahirisha tatizo kutokana na kuzoea kuteseka, wenzao wa Senegal wameamua kujikomboa. Juzi kulikuwa na ukatikaji wa umeme uliodumu masaa 24 katika baadhi ya sehemu. Hili kwa wasenegali wasio na mchezo na mtu lilitosha kuwatia hasira na kuingia mitaani ambako walichoma jengo la shirika la umeme la Senegal lijulikanalo kama Senelec.
Ikumbukwe. Kabla ya hapo kama siku tatu zilizopita, wasenegali hao hao walikuwa wameingia mitaani kumzuia rais wao Abdullaye Wade kutaka kubadili katiba ili aanzishe cheo cha makamu wa rais. Wanadai alilenga kuanzisha cheo hiki ili amteue mwanae Karim ambaye ni waziri katika serikali ili amrithi baadaye. Hii ni baada ya Wade kujaribu uhuni wowote bila kufanikiwa. Hata hivyo Wade aliachana na njama hii baada ya vijana kuingia mitaani na kuzusha tafrani. Je tatizo la Tanzania ni nini ambapo kuna mgao wa umeme kwa takribani miaka kumi sasa! Senegal wameweza. Sisi tutaendelea kuchezewa shere hadi lini! Hebu tufikiri pamoja. Senegal wamekosa umeme masaa 48 bila pesa yao kuibiwa kwenye ujambazi wa EPA wala wanaowalaza kizani kuingiza ujambazi wa Richmond. Je wangefanyiwa kama watanzania wa Danganyika hali ingekuwaje kwa hasira!
Kwa habari zaidi bonyeza hapa.

3 comments:

Anonymous said...

wacha kuchochea waTanzania watu wa Amani

Anonymous said...

Siasa za maji taka zimetuchosha.
kwe kwe kwe njo hapa upambane upo canada unachochea

NN Mhango said...

Anon namba moja na mbili siwachochei watanzania na amani yao. Wala sifanyi siasa za maji taka. Kupambana si lazima niwe Tanzania. Hivi ndivyo ninavyopambana na wakati wa kuhitajika kuvaa jezi ukifika mtaniona mitaani tu. Hata hivyo, silali kizani kama walioko huko. Ni suala la kuchagua kiza au mwanga. Kazi kwenu.