The Chant of Savant

Sunday 25 August 2013

Kijiwe chajadili kashfa za Ruanda


BAADA ya kijiwe kuipata kuwa kuna kipande cha kaya karibu na kaya yetu kina mpango wa kuivamia au kuichezea kaya yetu, tumekutana kutoa shinikizo na ushauri wa haraka.
Tunafanya hivi kushauri yeyote anayeota ndoto za mchana kuwa anaweza kutugeuza DRC nyingine akome na kukomaa. Japo kaya yetu imegeuka ya hovyo kutokana na uongozi mbovu na kutamalaki kwa ufisadi na ubabaishaji, kama wazalendo wa kaya hii, kijiwe kimeamua kutoa tamko kali kuwalaani wote wanaodhani we are there to be taken for a ride. Try whatever megalomania you surely will regret hugely.
Hakuna kitu kiliwachukiza wanakijiwe kama tabia ya kijikaya hiki maskini kulhali kutumia uongo na upuuzi kutuchafuria kaya. Hata kama kaya yetu ishachafuliwa na mihadarati, usanii na ubabaishaji, hii haimhusu yeyote nje ya mipaka ya kaya yetu.
Mara Mbwa Mwitu analianzisha baada ya kugundua kuwa wanakijiwe wote wana ndita usoni kama ishara ya kutoa taarifa kwa wabaya wa kaya yetu kuwa they mean business. Anasema: “Wazee mmeipata mpya ya kufungia mwaka?”
Mipawa anajibu, “Ngosha, mpya gani hiyo nawe?”
Mbwa Mwitu anajibu, “Kumbe husomi vyombo vya udaku siyo! Hukusikia eti Ruanda inadai kuwa bi mkubwa Salama Shari Njaa Kaya ni Mhutu?”
“Kwani akiwa Mhutu kuna ubaya gani? Hata wangesema ni Mmakonde it is okay for me. Lililo baya ni vitisho vya kitoto vinavyotolewa na hiki kipande cha ardhi eti kuna siku wataishikisha kaya yetu adabu wakati wao wenyewe hawana adabu zaidi ya adhabu ya kunyotoana roho wao kwa wao,” Alijibu Msomi Mkatatamaa.
Kabla ya kuendelea, Kapende anachomekea: “Usishangae kesho ukasikia wakisema kuwa na mumewe ni Mhutu kama siyo Al Shabaab kama Kinamna anayemaliza ndovu wetu na bado wanampa ukuu.”
Anaendelea: “Kinachomponza jamaa yetu ni tabia yake ya kusema bila kufikiri mbali na huruma ya kijinga. Si ni yeye aliyelainisha kaya nyingine za Afrika Mashariki kuwapokea hawa wauaji na wapuuzi kwenye jumuia yao mfu ambayo nayo imekufa hata kabla ya kutungwa mimba.”
Mgosi Machungi hajivungi. Anakatua mic: “Tinapaswa tijilaumu kwa kuendekeza hivi vijipande vya aidhi. Tilimtengeneza M7 naye akamtengeneza Ka-Game sasa kanataka kutileta game la vita wakati ni mchovu asiyeweza kutufanya kitu. Wathubutu waone cha moto.”
Msomi anaamua kukamua tena: “Kimsingi hapa wa kulaumu ni watuwala wetu wanaoendekeza ubinafsi. Hata hivyo, hakuna cha vita wala nini zaidi ya vita ya maneno machafu na ya kipuuzi. Wapigane wakati wanaishi kwa kuombaomba kwa wafadhili?”
Mpemba haridhishwi na jibu la Msomi. Anakwanyua mic: “Yakhe usifanye nchezo na hawa mabeberu wanaopenda kutumia watawala wetu ili kupata madini yetu. Mie nkikumbuka Congo wanavyoghasiwa naona waweza kutufanyia kitu mbaya tusipoanka.”
“Una maanisha nini kusema kutufanya kitu mbaya? Sisi tutamfanyia kitu mbaya kama tulivyomfanyia mwenzie Idd Amin. Hivi kweli hata kama ni kuwa wachovu tokana na ufisadi kweli tunaweza kupigwa na kipande cha ardhi kisicholingana na hata Mkoa wa Tabora? This is but too much so to speak openly, clearly and whole heatedly na madudu mengine mengi magumu,” Msomi anajibu.
Mzee Ndevu anaingilia: “Japo si mpenzi wa Njaa Kaya, kwa msimamo wake dhidi ya vipande vya nchi amenikuna. Angeonyesha jeuri hii hata kwa mafisadi na wauza unga nadhani angeweza kuheshimiwa na kuaminiwa sina mfano.”
“Mzee umevuka mipaka. Mambo ya ufisi ahadi na mihadarati ni untouchable. Kama hujui sasa jua. Wao wanaangalia masilahi binafsi. Unadhani asingetukanwa angeweza kuchukua hatua kama vile kuwatimua wahamiaji haramu? Hebu angalia alivyowanyamazia wahamiaji haramu waliojazana mijini toka Asia. Hadi atukanwe ndipo awajibike?” Kapende anaongeza.
Mgosi anaamua kupigilia tena msumari wa moto: “Tikubaliane. Jamaa ni bingwa wa kulipiza visasi hana lolote. Kama angekuwa ni mtu mwenye kujali masilahi ya kaya nadhani hichi kiinchi kidogo si tishio kama ufisadi na rushwa hata mihadaaati.”
Mbwa Mwitu anachokoza Mgosi: “We acha rongo rongo. Muulize Kanji kama kweli wahamiaji haramu wameshughulikiwa.” Anaongea huku akimtazama Kanji ambaye anaonekana kuudhika. Anajibu: “Mimi si hamiaji haramu. mimi nazaliwa pale taa ya Sutu (Kisutu). Hata kama iko Hindi nahamia haramu nakuja pata riziki kwa njia ya panya mi zaliwa hapa hapa bwana.”
Mzee Maneno anaamua kukamua mic: “Nasikia kuna wenye vyeo vikubwa kwenye lisirikali.”
Mipawa anajibu: “Hukusikiaga yule meya aliyesababishaga wenzake watimuliwe kwenye chata la mafisi na mafisadi? Mbona tuliambiwa alikuwaga mrwanda au kwa vile amejirekebisha na kutubia. Hivo, dhambi zake kusamehewa na kuwa raia?”
Mbwa Mwitu anamchokoza Kanji: “Hebu Kanji saidia mimi. Je, kuna mbunge Mswahili huko kwenu India?”
Msomi anaamua kujibu hata kabla ya Kanji kujibu: “Mbunge Mswahili India! Mbona kuna Waswahili waitwao Jarawa wanatumiwa kama wanyama na magabacholi kuwafanyia utalii kwenye kisiwa cha Andaman? Achana na mbunge. Sina hakika hata kama kuna genge la nazi la Mswahili India. Jamaa walivyo wabaguzi Mswahili hawezi kuwa na hata choo kule.”
Kanji kuona mambo yanazidi kumwia magumu anaamua kujikata kisilesi kwa kuja na sanaa kama za Njaa Kaya. Anasema: “Mimi iko wahi peleka toto jamati. Acha wahi yeye. Onana siku ingine ee?”
Mipawa hamkawizi: “Nendaga jamatini mpangage jinsi ya kuhonga mafisadi wetu. Kuna sehemu yenye ubaguzi kama jamatini? Yaani hata dini ni kikabila?”
Anaondoka huku akisema: “Sisi si baguzi.”
Mipawa hamkawizi: “Kesho kutwa njoo tupange wewe kumuozesha kijana wangu Masunga binti yako Shiofta.”
Tanzania Daima Agosti 25, 2013.

2 comments:

Anonymous said...

he he he he kweli hicho kijiwe cha walevi wasio jua vita.ninyi mnafkiria unene wa pua ndo wingi wa kamasi. ka nchii kadogo ilaa mziki wake mkubwa. utauliza nchi ka Zimbabwe angola Namibia mauonja huko drc congo 1998. nyie nikuafumua vitambi tu ubavu hamna wa kusimama na Rwanda. tz inachukua wiki mmoja tu kwisheni. kila siku mnaimba vita vya AMINI walopigana hio vita wote wazee wameshastaafu tayari hao wa sasa makuruta tu maana hawajawahi kuskia milio ya silahan kubwa siku wakiskia ni nduki hapo. Rwanda haivamiwi inavamia aduii tunamkuta kwake tunampa kisomo. wadhahifu nyie sana wachovu. kama kweli wewe muandishi usbanie hii commenti thanx tunaanzisha mjadala hapa.

mdau Kigali mpenda nchi makazi boxini kusaka chake

Anonymous said...

Mkuu toka Kigali hujui unachosema. Rwanda si nchi ya kupigana na Tanzania wewe. RPF yenyewe ilishindwa na mchovu Habyarimana hadi ikamvizia angani itaweza mama wa vita? Tazania ikiamua kupigana na Rwanda dunia haitairuhusu kujidhalilisha hivo. DRC mlikwenda kuiba na kuchezea wachovu. Hata mwizi mobutu msingeweza kumtingisha. Hata hao wahutu walioko huko wanawanyima usingizi kwa vile kuna siku watawatokea kinoma,