The Chant of Savant

Thursday 23 November 2017

Bila Kuwachoma Moto Hawa Matapeli, Wajinga Wengi Wataendelea Kuibiwa

Huyu ni mchungaji au mchunaji? Tanzania na Afrika kwa ujumla zimegeuzwa shamba la bibi kwa matapeli kutajirikia kwa kutumia utapeli chini ya jina la Yesu na upuuzi mwingine. Kwanini jamii isiwachome moto sawa na vibaka hawa vibaka na mibaka ya kiroho? Je nini mawazo na maoni yako juu ya utapeli huu mpya?

4 comments:

Anonymous said...

Kujibu hilo swali kwahitaji ufahamu usio wa kupumbazwa kwa halaiki. Yule Noah Trevor alishanukuliwa akisema "Instead of feeding the 5000 people like #Jesus did, today's '#prophets' are being fed by the 5000 hungry people." Swali lako la kwanza linajibika na hayo maandiko ya Noah kwamba mchungaji ni mchunaji na mchunaji ni mchungaji bila kumumunya maneno! Jamii ikishapumbazwa kwa halaiki kuanzia kule kwa munene wa PhD isiyohakikiwa ya kwamba msema kweli ni mpenzi wa Mungu au Allah tutategemea hawa vibaka na mibaka ya kiroho kuchomwa moto kweli? Utapeli huu mpya ni kumalizwa mara moja kwa kutumia watu wasiojulikana kuwamiminia mvua rasha rasha ile iliyomkuta munene wa wanasheria Tanganyika! No pun intended.
Wasalaaam.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Asante sana Anon umenena. Ila hili la wasiojulikana kuwamiminia risasi sidhani kama ni feasible hasa ikizingatiwa kuwa wote ni washikaji wanaofanya kazi moja ya kuwaibia walevi na wapumbavu wa Danganyika. Hili la bwana PhD mashaka sigusii. Sijui hata hicho chuo kilichoitoa kama ni halali. Kweli ukishangaa ya Mrema utaona ya kagufuli!

Anonymous said...

Salaamu Mwalimu Muhango,Mimi siwalaumu hawa Matapeli wa KIROHO kama nilivyokuwa nikiwaangalia hapo awali na simple reason ni kwamba WAJINGA NDIO WALIWAO,Kama walivyosema wahenga.Tatizo kubwa ni kuwaelimisha watu kjielewa kwamba wao kama ni watu katika masawala ya kiroho wawe na mwelewo wa wajitegemea wenyewe na kujiamini bila ya kuwahitaji watu wa kuwafikisha kwa MUNGU watu ambao wanajieleza kwamba wao ndio wawakilishi wa mungu Mungu na wanasema kwa jina la Mungu hapa duniani.lakini endapo watu hawatoelimishwa mueleo huo matokeo yake ndio haya tunayoyaona kwamba wajanja matapeli wa kiroho KAMA NI WATAFUTAJI RIZIKI ZAO WANAUTUMIA UJINGA WA WATU ILI KUJINUFAISHA KATIKA MAISHA YAO.Mwalimu Muhango,historia ya ulaya inatukumbusha somo ambalo katika nchi zetu za Afrika halisomeshwi mashuleni na kama linasomeshwa wanaolisoma hawalifanyii kazi kuweza kujielimisha wao wenyewe au kuwaelimisha watu wao.Nalo ni somo la watu ulaya katika karne ya 15 kuamua kutolipa kanisa kuingilia katika maisha yao ya kidunia kwa kupitia dini na kufikia kuiona dini ni ujinga mtakatifu,ujinga ambao unawakwamisha kusonga mbele katika maisha yao ya kijamii kimaendeleo na kidini pia na kufikia mueleo wa kwamba dini ni uhusiano binafsi kati ya mtu na anachokiamini na kukiabudu,na hatimae kanisa kujikuta liapoteza hadhi yake na nguvu yake katika kuathiri watu nguvu ya ujinga mtakatifu,ujinga mtakatifu ambao kanisa ulikuwa ukiutegemea katika kuwatawala watu kiroho na hatimae watu wa ulaya wakafikia hapa walipofikia katika maendeleo ya kijamii sayansi na teknolojia na kuikataa dini isingilie siasa,sayansi na teknolojia.

Mwalimu Muhango,"Ujinga mtakatifu" wa kidini ni sawa sawa na "üjinga mtakatifu"wa kikabila na uzalendo ukereketwa endapo hautopigwa vita kama unavyopigwa vita vya maradhi,ujinga(kukosa elimu)na umasikini,matapeli wa kidini na wanasiasa watakuwa msatari wa mbele kuutumia ujinga huo matakatifu katika kuwatawala watu na kujitajirisha.Swali muhimu linalojiuliza katika kadhia hii kwa nguvu ni hili je jamii zetu tunaweza kufikia kama walivyofikia wezetu wa ulaya kwa kuufuta ujinga huu mtakatifu wa kidini?Jibu hapana na simple reason kwamba wasomi tuliokuwa nao katika jamii zetu za kiafrika wengi wao wanaamini huu ujinga matakatifu wa kidini ukiongezea kwamba jamii zetu za kiafrika bado tunaishi katika hatua ya PRIMITIVE SOCIETY.NA JAMII YOYOTE AMBAYO INAYOENDESHWA KWA MIHIMILI YA KIDINI,KIUCHAWI NA KIKABILA NI VIGUMU KUSONGA MBELE.Tusisahau tu kwamba watu wa ulaya hawakufikia kuligeukia kanisa bila ya watu wao kujitolea muhanga katika maisha yao hususa mabingwa wao wa kielimu katika kulikosoa kanisa na kupambana nalo.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anon nashukuru kwa mchango wako pevu. Nakubaliana nawe kuwa bila kuelimishana na kujua ghilba na upuuzi ulioko nyuma ya miujiza, tutaendelea kuwa na watu maskini wanaoibiwa na majambazi hawa wa kiroho wakijiita viongozi wa kiroho wakati wana uroho wa kawaida. Hawana cha roho mtakatifu zaidi ya roho mtakakitu na mchafu wa utajiri hata kwa kuwaibia maskini. Sijui tufanyeje hasa ikizingatiwa kuwa mfumo wetu umeingiliwa na ujinga huu wa kuabudia vitu visivyoingia akilini?
Japo ulaya walifanikiwa, sijui kama Afrika tutafanikiwa hasa ikizingatiwa kuwa dini na serikli siku zote wamo kitanda kimoja wakitumiana. Utasikia kiongozi fulani akiwahimiza viongozi wa dini kuwafundisha wananchi mema kama kwamba wao ni wanyama au mataahira awasiojua mema na mabaya. Kwa sasa dini na viongozi wake wanasifika kunajisi watoto, kuzini na wake za waumini wao na uchafu mwingine na hakuna anayeshangaa. Dini nyingine zinaongoza kwa kuzalisha waganga wa kienyeji ambao si waganga chochote bali matapeli na wazinzi wa kawaida. Bila kuvunja huu mfumo na kuusuka upya, ukweli ni kwamba tuendako ni kubaya. Mimi huwa siwatofautishi hawa viongozi wa kiroho wanaobia watu kwa kusingizia miujiza sawa na washirikina wengine wanaoua watu wenye ulemavu wa ngozi yaani mazeruzeru.