Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Liberal Peace Conflict, Gender, and Peacebuilding

Wednesday 26 June 2024

Maza Fyatua Bashee Baada Kumfyatua Nawander


Juzi mafyatu tulisuuzika roho baada ya kuvuja tuhuma za doktari Yah-yah Nawander kumbaki mwanachuo huko Shimiyu. I just wonder about Nawander. Sitafyatuka mengi. Uchunguzi haujakamilika. Sijui kama kesi iko kwa pilato au la. Tulisuuzika kufyatuliwa wanene wasiofyatuliwa lau kwa kutemeshwa ulaji bila kuwafunga. Doktari maza alimfyatua Nawander baada ya kutuhumiwa kufyatua Embedodo hadi maganda na kokwa tena kulikooza. Sijui Embedodo lilingiaje mchumani, kama hakukuwa na makubaliano? Je ni kweli jamaa alikula vyote hata mbegu iliyooza? Yaani mnofu wa Embedodo umeisha hadi fyatu mzima–––tena munene na doktari kama wa kweli siyo wa kugushi au honoris cause––––unahangaishwa na kokwa chafu? Huyu udoktari ni wa nini na aliupataje au ni ule wa akina Philo na Sofia? Je hii ni kweli au kuna namna? Je usingefanyika usodomu––––kama kweli ulifanyika––––Embedodo lililoanguka kwenye mchuma wa Nawander––––lingelalamika? Ajabu, nasikia mnaifungia twinter kwa kuhamasisha usodomu wakati wanene ndo wanaoufanya–––kama kweli Nawander aliufanya. Je hawa wanajuana na kukomoana nasi tunafyatuliwa changa la mato au ni siasa kama za kina Sir Baya? Mbona sielewi. Hayo tuyaache.
            Leo, kama kawaida ya mshauri wa maza asiyelipwa chochote isipokuwa kusukumwa na ufyatu na uzalendo, natoa ushauri kuntu tena bwerereee. Ushauri wenyewe ni huu. Fyatulia mbali Husaini Basheee aliyetuhumiwa na Mheshimiwa Luhager Mpiner tena kwa ushahidi kuntu unaoonyesha wazi jamaa alitengeza uhaba hadi sugar ikageuka shubiri! Mwe! Mmejua kutufyatua bila kujali tunaweza kufyatuka na kuwafyatua. Kabla ya Mpiner kumwaga mtama, nilikuwa nimehadaika nikatokea kumuona Bashee mzalendo kumbe wapi? Alivyokuwa akifyatuka na ‘kulaani’ uzembe utadhani alimaanisha! Kumbe sanaa. Sipendi kufyatua maneno mazito ila naweza kusema hii ni nifaki tosha. Sikutegemea fyatu aliyekuwa anafyatua mapofu 'kuwatetea' wafa kwa ngwamba angekuwa ndiye anayewaumiza mafyatu wa kaya yote.
            Doktari Mazeri, naomba nikushauri kumfyatua Basheee na akina Mwiguuu Nchember, Jan Makamber, na Riz One niliowataja siku zilizopita kwa sababu zifuatazo:
            Kwa ushahidi wa Mpiner, kuna kila dalili za upigaji njuluku ndefu kupitia kuongeza cha juu kwenye sugar, kutengeneza faida na rushwa kubwa kwa wanene na walanguzi wa sugar vilivyofanywa na Bashee ukiachia mbali Nchember. Alipojipiga kifua akitapika urongo mjengoni kuwa si waziri boya kumbe boyo! Je kuna mawaziri maboya? Kumbe na mtufuku rahis  anaweza kuteua maboya kweli? Kuna uboya kuliko ufisadi waziwazi tena wa kutumwa na akina Mood Doweji? Waziri anapogeuka broker, we acha tu apaswa kuwa mikononi mwa Takokuru kama siyo kunonihino kwenye debe lupango aungane na Nawander.
            Pili, kudanganya kaya na mjengo aliojifanya kuuita mtukufu wakati anaufanyia utukutu mbali na kutoa vibali vya kuagiza sugar nyingi kupita naksi iliyokuwapo kayani ni kosa la uhujumu wa uchumi. Ukimsikia jamaa anavyomtaja Sir God, utadhani anamwamini kumbe kamba! Kaya hii kweli ya sanii iko sema Kanjicholi. Haiwezekani umfyatue Nawander kwa masuala binafsi ushindwe Bashee ambaye skandali yake imeumiza umma wa mafyatu wote.
            Tatu, kutoa vibali kwa makampuni feki mengine yakiwa ni ya mamantilie ukiachia mbali la yule bilionea fisadi nauchwara wa kaya. Je haya makampuni siyo yake au mafyatu wake wapigaji njuluku ndefu ya makapuku wanaofyatuliwa na umaskini tena wa kutengezwa na akina Bashee, Nchember, na wenzake? Je huyu jamaa na wenzake wameishapiga njuluku kiasi gani? Je wako wangapi kayani? Je haya huyajui? Kama huyajui, ni kwanini? Kama unayajua, kwanini hufyatui? Je ni kweli unafaidika na akina Bwashee kama mafyatu wapingaji wanavyodai? Je kwenye bidhaa muhimu kama wese zinapigwa kiasi gani? Je Nchember na wenzake wameishapiga ngapi? Bandarini nako je? Vipi jamaa wa mbuga za waanimo na utalii? Madini nako vipi? Uhamiaji wajua?
            Nne, kusamehe kodi nusu trilioni tena kwa kaya kapuku. Ajabu, wewe maza unatembeza bakuli kukopa na kubomu hadi wengine wanakuita Vasco da Gama kama yule wa Musoga. Kuna haja gani kudhalilika hivi wakati uchumi tunao ila tunaukalia huku wengine wakiugawa kama huyu Bashee. Kwanza, kweli huyu ni mdanganyika na mzalendo kweli au ana uraia pacha? Je ni wale aliowahi kudai munene mmoja wa geshi kuwa kuna wageni wamepewa nyadhifa kuu kwenye ulaji wa juu? Pili, je huyu jamaa hawezi kuwa anauza hata siri za kaya na sirkal kwa maadui zetu wakiwamo magaidi kama vile al Shabubu?
            Tano, usipomfyatua, wapingaji wanaaamini kutakuwa na namna unavyofaidika. Wanataja zile pikipiki zilizoandikwa SSH, yaani Sasa Shida Hiyo au Seemingly Self-inflicted Hazard zilizosemekana kugawiwa bure nkoani. Wanadai hizi ndinga zimekula zaidi ya bilioni 50. Je hii njuluku ilipatikanaje? Zitolewe bure kwani duniani bado kuna cha bure? Kwanini sasa kuelekea kwenye uchakachuaji, sorry, uchafuzi, sorry, uchaguzi? Je nani mwenye hizi ndinga ambaye anaonekana kuwa mkwasi wa kutisha? Pamoja na Luhager kufyatuka kutuhabarisha na kutufumbua mato eti madame Spiker aka Spooker anamtunishia misuli kwa kumpeleka kwenye kamati ya madili wafanyie dili tuhuma zake! Kaya hii kwa maajabu, we acha tu.
            Kwa vile nawahi kanywaji, leo nakomea hapa. Hivi nimesema Bashee apandishwe cheo?
Chanzo: Mwananchi leo.

Wednesday 19 June 2024

Hii Kaya Sasa ya Chawa na Sanii

 

Siku hiji kaya yetu nageuka kaya ya sanii. Kila kitu ni sanii. Rahis nafanya sanii.  Wajiri nafanya sanii. Narudia neno nasema bungeni iliyopita. Natuma kampuni hewa. Nasamehe kodi. Kodi naingia fukoni yake. Sirkal nafanya sanii. Nakwenda bungeni. Nalialia na chovu naona yeye zalendo. Kama Pina nachambua yeye, naona fisadi kuba. Napoteza kodi. Nakwenda omba ghaibuni kama ile Tonya. Iko uliza wajiri ya kilimo na juluku na samaha ya kodi kampuni ya fukoni? Kama napigia yeye kelele, nageuka chura. Kama veve napiga kelele kama pinjani, chura nakaa kimya. Kama nazidi kelele. Yeye naonya hapana kanyaga guru vake nauza. Sasa iko ogopa sana.
         Kama rahis nageuka nyoka hapana umma umma sana? Kama nageuka chatu hapana kula vote na yote dugu yangu? Sasa mimi anza ogopa sana hii sanii. Bila fanya sanii mambo yako yote naharibika kabisa. Vatu nafanya sanii ili naishi. Nageuka chawa. Nyingine nageuka kunguni. Nyingine nakuwa fyatu nafyatua juluku ya chovu na sikini. Kila moja iko sanii. Kama hapana jua sanii, napotea na kuteseka vakati vote dugu yangu.
Juzi nakwenda Bombei kuona bibi na toto. Naacha yeye na toto moja nakuta toto tano na yote nakuwa sanii. Nakwenda sule nataka Ipad. Narudi Tanjania nakuta kila kitu sanii kila Swahili hata Hindi sanii. Sirkal nafanya sanii ya kupiga juluku. Naanzisha tozo na chango mpaka tumboni nauma. Kuku nakuwa sanii nataga yai ya rangi. Bila kuwa sanii, maisha iko tabu sana. Siku nafatuka ile mendazake Kufuli mimi dhani kaya kuwa ya Samier siyo ya sanii. Sasa kila kitu naona sanii. Profesa sasa nayo nageuka sanii ya siasa kabisa.  Iko mingi naingia siasa. Vatu nafanya sanii kwelikweli. Nafanya sanii ya nguvu sana dugu yangu. Kama nakopa juluku, nakausa damu. Hii naona penzi ya sanii.
         Rahis naye nakuwa sanii kubwa. Napenda sana sanii na sanii napenda sana yeye. Juzi nasafiri Korea na sanii mingi kwa juluku ya sikini ya kaya. Na vana kaya nafanya chura. Hapana lalamika kwanini aache vakulima. Toto sanii. Sasa naimba stari ya rap. Hapana soma suleni. Nataka tengeneja juluku kuba harakaharaka kama Kanjibhai. Vatu kuba sasa sanii nasifia sifia Samier. Kama nachukia au nakataa sifia yeye, nakufa sikini dugu yagu. Kama veve iko sanii, nasahau Mungu, Nasifia vatu nene. Vyuo sanii. Sasa natoa honoris causae kama jugu. Sasa kaya nakuwa ya doktori sanii mingi sana. Sanii nayo nakuwa sanii ya siasa. Nagombea bungeni. Natumia vana siasa fanya sanii kwa samier. Hii kaya basi iite saniiland. Hindi nakuwa sanii. Kama naongea swahili, nabukanya. Kama nakamatwa na data, naongea swahili kuliko Zaramo. Chukuaji nayo sanii. Sasa naita wekejaji. Ile miji kubakuba sana hesimiwa. Nafanya sanii. Napata tumboni kuba na kila kitu kubakuba. Nakuwa na nyumbani dogo mingi. Nyingine nabaka toto ya chuo. Yote hii sanii ya siasa.
            Sanii sasa mali kuliko dukani. Kama nataka juluku kuba, lazima iwe sanii ya siasa. Naendesa dukani na kugombea bungeni na kupiga juluku. Sirkal kila maka nanunua sangingi. Naharibu. Nauza mnada kwa bei ya sanii na sanii kuba napata deals. Kama veve sikini nafanya kazini na nastaafu, napewa kinua gongo ya sanii. Napewa kidogo. Kikuba naweka sirkal. Natumia kama hapana akili njuri. Chovu nalalamika. Veve nanyamaza kama chura. Sirkal nafanya sanii. Nasema navekea veve juluku yako! Kama nakupa yote nakwenda lewa pombe na kufa haraka. Je kama nanyima veve juluku yako, hapana tatizo fyatua veve na kufa haraka jamani? Hii yote sanii.
         Pinjani napiga kelele sana kama kisimani ya maji. Ile chura kuba naziba sikio. Napiga juluku toto, mama, na rafiki. Vote napiga juluku. Sikini sanii nalala sikini naamka tajir.  Sasa na pinjani nayo kama nageuka chura, nani tapiga kelele ile chura kuba na nyingine napiga juluku? Kama yeye chura, basi pinjani chemsa maji naunguza chura. Kama nafanya jusi, pinjani bana lango.
            Ile vatu ya dini nayo siku hizi sanii. Naimba nyimbo ya siasa sanii. Nasifia ile chura kuba napata juluku. Nyingine nafanya sanii. Nadanganya jinga nafanya ujiza. Napata juluku kuba. Naendesa gari kuba. Nalala kwa nyumbani kuba. Ile sikini nafanyia sanii naambia omba Mungu. Nafanya sanii. Naita ujiza. Kanji iko kataa ujiza. Vajinga ndiyo valivao dugu yangu. Chunga sana sanii ya dini na sanii ya siasa. Siku hiji sanii ya dini na sanii ya siasa nalala tanda moja. Kama nataka kuwa sanii, hapana chukia witu baya. Veve sifia. Kama napigwa kofi cheka. Kama juluku yako napigwa, sema mama namwaga juluku.  
            Sanii nyingine, sirkal nakopa juluku. Natumia wibaya. Hapana taka swali howo howo. Nafanya kataba hatari. Hapana taka swali. Nauza fyatu. Hapana taka swali. Nafanya kaya kama dukani yao, Chovu na fyatu natazama tu kama chura! Chama sasa nakula kitu yote. Kama nauliza nini bana? Nasema yeye chama twavala. Natavala na kula. Hiyo ndiyo kazi ya chama tavala. Kama napinga veve, iko adui ya kaya.
            Kama nataka kwenda bungeni, lazima sifia. Kama nanyimwa radi ya jimboni yako, napiga sarakasi jengoni. Kama nabana vaziri swali gumu, chama naita veve. Kama nabisa, nenda uliza ile Lwaga Mpini. Kama naleta domo kuba, ile chura nene nasema veve itengwe. Tena iko ongeza kuwa veve laani. Nakumbuka ile Nipe Pepe Nnaiye nasema jengoni? Nasema pinjani yote laana.
Du! Kumbe naota niko Bombei na nimegeuka Napharata karanāra bin Jātivādī bin Cōra! Bhagavāna manē madada karē.
Chanzo: Mwananchi leo.

Monday 17 June 2024

Misingi na Nguzo za Ndoa (2)

Leo tunaendelea tulipoishia kuhusiana na miiko na nguzo za ndoa. Karibuni tuendelee.
Maadili
Taaluma na taasisi yoyote lazima iwe na maadili ya kufanya ifanikiwe na kuheshimika. Ndoa kadhalika, lazima iwe na maadili vinginevyo haitafanikiwa au kuimarika. Kama ilivyo masharti ya udereva au uongozi, maadili ni nyenzo zinawezesha wanandoa kujifunza nini wafanye au wasifanye na kwanini. Maadili, licha ya kuwaongoza wahusika, huwapa fursa kuona madhara yanayoweza kuwapata wanapokiuka maadili ya ndoa kama tulivyogusia hapo juu juu ya changamoto na hatari za ndoa. Kuna usemi wa kimombo unaofasiri maadili kama kujua tofauti kati ya ulicho nacho haki kutenda na kilicho sahihi kutenda (ethics is knowing the difference between what you have a right to do and what is right to do). Pia, kuna busara nyingine inasema kuwa mtu asiye na maadili ni sawa nyamamwitu aliyeachiwa kwenye dunia hii (a person without ethics is a wild beast loosed upon this world).
            Tusisitize. Kama zilivyo nguzo nyingine, maadili ni muhimu au tuseme ni mojawapo ya matofali yanayojenga ndoa. Lazima wanandoa wayazingatie.
Miiko
Pamoja na mambo mengine, taasisi yoyote, ili idumu, ifanikiwe, na kuwa salama, lazima iwe na miiko yake ambao inaoingoza katika kuendesha mambo yake. Katika ndoa, miiko ni mojawapo ya nguzo zake. Kuna vitu mfano, hamuwezi kuitana au kufanyiana. Kuna kisa cha wanandoa katika nchi moja ya Amerika ya Kusini. Katika kisa hiki, mwanandoa mmoja alichukia hadi kufikia kutishia kuvunja ndoa kwa sababu mwenzie alijamba wakiwa kitandani wanaongea kabla ya kulala. Si kwamba hawa wanandoa walikuwa hawafanyi hivyo. Kilichogomba ni kanuni. Kila aliyetoa upepo alimtaka radhi mwenzake vinginevyo awe amelala fofo hajitambui. Hivyo, mwanandoa alioachia hewa na kushindwa kuomba msamaha, alikuwa amevunja kanuni moja kubwa. Jambo hili ni dogo, kama tulivyoonyesha hapo juu ila laweza kuwa na madhara makubwa kimahusiano kwani, lilitaka kuzaa makubwa kiasi cha kutishia ndoa ya wahusika. Hivyo, kanuni mlizojiwekea lazima mzifuate hata kama ni ndogo kiasi gani.
Upekee
Kama tulivyo viumbe. Kwa mujibu wa sayansi ya vinasaba (DNA science) kila mmoja wetu ana DNA tofauti na mwenzake na wenzake. Na ndoa kadhalika. Zina DNA za kipekee. Ndiyo maana hupaswi kufunga au kuendesha ndoa yako kwa kuiga ndoa nyingine. Hivyo, jambo mojawapo la muhimu ni kutambua na kuipa upekee ndoa yenu ili iweze kufanikiwa na kupambana na changamoto zake vilivyo bila ya kuigiza au kukopa japo si vibaya kujifunza kwa wengine wenye ndoa kongwe na zilizofanikiwa kuliko zenu. Hata hivyo, lazima muangalie mazingira na sababu za kufanya hivyo.
Siri na usiri
Japo siri na usiri (secret and secrecy) vinahusiana, havina maana moja. Ni rahisi kutengeneza siri japo ni vigumu kutunza siri kama hakuna nguvu ya ziada au sababu zinazokuzuia kufanya hivyo. Katika ndoa, siri na usiri vinakwenda bega kwa bega. Ili siri iwe salama, lazima kuwae na usiri. Na ili usiri uwepo lazima kuwa na siri ya kutunzwa. Ukiachana na misingi na siri za mafanikio ya ndoa hapo juu, msingi mwingine ni siri. Ndoa ina siri zake. Wenye ndoa pekee ndiyo waumbaji, watunzaji, hata wavujishaji siri. Tumegusia umuhimu wa kulishwa kiapo kabla au wakati wa kufunga ndoa. Mbali na kuwa ishara ya kukabidhiwa majukumu, kutoka hatua moja hasa ya chini kwenda ya juu, mantiki ya kiapo ni kutunza siri. Unadhani kinachofanya askari wawe watii wasitumie vibaya nguvu na silaha zao ni nini kama siyo kiapo na usiri wa kazi yao? Bila siri, hakuna taasisi. Ndoa siyo kama chumvi muazimane na majirani na marafiki.
        Kama ilivyo kwenye siri ya mtungi, muachie kata pekee ajue siri zake. Kama mume au mkeo ni tajiri au kafanikiwa katika jambo, huna haja ya kugeuza mafanikio yenu kuwa matangazo ya biashara. Wakati mwingine mafanikio yanaweza kuwa chanzo cha maanguko kama hayatahifadhiwa na kutumika vizuri. Kuna methali ya kiingereza isemayo kuwa thamani ya siri hutugemea dhidi ya watu unaopaswa kuitunza au kuiepusha (secret's worth depends on the people from whom it must be kept). Methali nyingine inasema kuwa kutunza siri yako ni busara lakini ukitegemea wengine waituinze ni upumbavu (to keep your own secrets is wisdom but to expect others to keep them is folly).
Wivu
Kama ilivyo petroli kwenye gari au mashini yoyote, ndoa bila wivu wa pande zote si ndoa bali maigizo. Kama tulivyodokeza hapo juu, binadamu ni kiumbe mwenye wivu wa kuzaliwa nao. Je itakuwaje utakapogundua kuwa mwenzio hana wivu nawe? Je ni kweli hana wivu au anao kwa mtu mwingine mbali nawe? Kwa wanaotoka Tanga wanajua. Kuna usemi kuwa siyo wivu tu bali hata limbwata kwa mume au mkeo linafaa ili muwe pamoja. Haya ndiyo mapenzi.  Mithali 6:34 inasema wazi kuwa wivu humfanya mtu achukie kiasi cha kutoonyesha huruma siku kulipiza kisasi. Japo si wote wanaoamini katika biblia, kuna ukweli katika aya hizi ambazo wakristo na waislamu huziamini. Tunaomba kutofautisha wivu huu na husda ambayo ni dhambi kama Muslim (V. 2) anavyoonya kuwa msichukie, kuwa na husda au kugeuka.
Chanzo: Mwananchi jana.

Wednesday 12 June 2024

Waziro wako wa fedheha aka njuluku anatuhujumu na kukuhujumu


Mtukufu Dk., Dk., Dk, Dk. Dk.Rahis.  Naambwa unazo PhD tano si haba.
Sina tabia ya kupongeza. Hivyo, kwa heshima na taadhima, nakuomba usishangae. Mie ni fyatu. Si msifiaji wala chawa. Hivyo, sianzi kwa mashairi, mapambio, ngojera wala kamba. Huwa namsifu Sir God pekee na siyo masanamu ya kuchongwa na machawa ili wapate kujaza mitumbo. Si kazi yangu, maana mie siyo chawa wala kunguni wa kujipachika uchawa wala mwenye kupwaya kamaadili na kitaaluma. Ni msomi kuliko Mwambukuzi. Ni fyatu kuliko Tunda Lishe na Pita Msingua mafyatu wanaosifika kayani. 
        Leo, nakuletea skandali ya mwishiwa Madilu Lameki Nchembuz ambaye hupenda kuitwa doktari. Nadhani ishainyaka. Niseme wazi. Anakuaibisha,  kukuhujumu, kutuhujumu, kukuchonganisha, na kukuchongea kwa mafyatu wanaoshangaa kwanini kumwacha aendelee kutia aibu na hasara kaya na hata mjengo wetu mtukutu, sorry, mtukufu. Hafai kwa lolote so to speak Unadhani mwendaze aliyemfyatua aliyemuumba na kumfyatua alikosea? Juzi iliibuliwa skandali mjengoni na mheshimiwa Joji Mwanisongo Lee ikimkariri Nchembuz akijisifu uzwazwa na uzembe. Hata kama muda umekwisha kuelekea uchakachuaji, Mwanisongo Lee ni jembe. Ningekuwa wewe, ningemteua awe waziri wa njuluku maana ana uchungu na njuluku na wakulima wetu.
         Mwanisongo Lee popote ulipo, nakupa kongole fyatu wangu. Unastahiki, kwani hukuogopa mvua wala jua. Ulicheza clip mjengoni ambapo Nchembuz anajisifu kuwasikinisha mafyatu na kuwatajirishi wakwepa kodi. Hakuna kilichoniudhi hadi nikalala njaa zaidi ya kupata kanywaji kuondoa hasira kama madame Kipaza sauti aka Spiker kushindwa kuunda kamati kumchunguza hata kumuondoa madarakani Nchembuz mbali na kuamuru takokuru imfyatue. Kama mjengo kweli ungekuwa wa mafyatu au kuwawakilisha hasa ikizingatia ndiyo wanaohujumiwa kwenye skandalii hii, ingeletewa hoja kumchunguza Nchembuz liwe somo kwa wengine. Ajabu ya maajabu, hakuna aliyeona skandali hii kama tishio kwa maisha ya kaya hasa kiuchumi. Tatizo nini?
        Ajabu!!!! Nchembuzi alipotakiwa kujieleza, siyo kujitetea, alipiga siasa na skandali ikafia hapo! Je zipo skandali nyengine kama hata kubwa kuliko hizi ngapi? Je kaya imeishapoteza njuluku kiasi gani? Ni mafyatu wangapi wapiga jembe waliokwishasikinishwa? Kama ningekuwapo mjengoni, ningekamata shilingi na kuhakikisha huyu fyatu anafyatuliwa tena bila maji. Je mtukufu rahis, umeridhia mchezo huu mchafu? Fyatua bila kuangalia nonihino usoni. 
        Ushahidi upo tosha na wazi. Unamuacha ili iweje na afanye nini zaidi ya kuendelea kuboronga na kuvurunda? Je unapanga kufyatua lini japo huwa hufyatui itakiwavyo nikikumbusha skandali za akina Riz One na Janwari Joseph Marope nilizokuletea ukaminya? Je kwenye uchakachuaji ujao, utatujibu nini tutakapomkumbusha skandali hizi na nyengine kama vile Deep Weed, Ngorongoro etc.? Je mhujumu uchumi huyu analipwa mamilioni, kupewa hekalu, shangingi, na wese bure kwa kazi gani iwapo amejifunga mwenyewe kuwa anahujumu kaya? Mafyatu twataka jambo moja tu, kuwajibishwa Nchembuz as soon as possible.
        Mafyatu, hadi leo, hatujaelewa uzwazwa na majisifu hata mantiki ya kunyamaziwa kana kwamba alichofanya Nchembuz ni haki. Je ni ile hali ya maadili kugeuzwa madili na baadhi ya mafyatu kujigeuza au kugeuzwa machawa wengine miungu? Je wanaachwa kwa vile wana sifa kuu za kujisifu na kukusifia kuwa umefanya mambo makubwa kama kukopa sana na kusafiri eti kuliko hata Vasco da Gama wa Musoga. Wee! Kausha. Heri lawama za mwenye busara kuliko nyimbo za wapumbavu na wasaka tonge. Mafyatu twasema wazi. Mummy, achana na masifa na kuteua kwa sifa na ithibati. Fyatua watie akilini hawa wanaotufyatua na kupiga njuluku zetu na kutusikinisha kwa uchoyo na uroho na roho mbaya zao.
            Clip aliyocheza Mwanisongo Lee ilimvua nguo mhujumu uchumi huyu ambaye mafyatu watafurahi kama utamtema haraka maanua anatia aibu na hasara. Nchembuz, doktari wa akina Philo na Sofia, sijui alipataje hiyo PhD maana, hata akiongea huoni dalili zozote za ubukuzi. Nadhani Mwambukuzi hakosei anapowaita vilaza. Wamelaza bongo hadi njuluku za mafyatu zaibwa wakiwa wamelala. Jamaa alibanwa inakuwaje anataka kuwatoza wafa kwa ngwamba kodi ilhali matajiri wanapeta. Hakutoa jibu lolote la maana zaidi ya kukusifia na kukusingizia kama gea yake ya kuendelea kuvurunda. Wizara si mali yake ya urithi kiasi cha kuchefua na kutia kinyaa.
            Kwa vile hii ni kaya ya mafyatu na wanene mpo kwa vile mafyatu tumewakasimisha na kuwaamini maulaji, lazima tuzoze hadi umfyatue na kutuletea fyatu anayefaa tena anayeweza kuwafyatua matajiri wasiolipa kodi. Kuna fyatu mmoja wa kaya ya jirani aliwahi kusema kuwa ukiona mafyatu wenye raslimali wakijipeleka majuu kubomu na kupangwa kama wanafunzi mbele ya mkuu wa shule, ujue kuna tatizo. Kwa kaya yetu, tatizo kubwa mafyatu wanaoloona limeota sugu ni kuteuana kwa sifa za uchawa na ukunguni. Inakuwaje fyatu mwenye PhD, tena si ya kuzawadiwa, anafanya madudu kuliko hata waliosoma ngumbaru? Sasa mafyatu tunazoza tena bila kumung’unya kuwa fyatu Nchembuz atumbuliwe haraka japo huwa unaonea kinyaa majipu usiyatumbue kama mwendaze.
            Leo sirongi sana. Muhimu, nasema wazi. Mummy fyatua huyu fyatu ili mafyatu wengine chawizi watie akili. Ukimfyatua usawa huu, mafyatu tutakumwagia kura za kula hadi uzimii. Hivi leo nimekunywa gongo kiasi gani?
Chanzo: Mwananchi leo.

Sunday 9 June 2024

Misingi na nguzo kuu za ndoa

Katika makala iliyopita tuligusia misingi na miiko baadhi ya ndoa. Leo tunaendeleza tulipoishia.
Uhuru
Ndoa inapaswa kuwa huru na isiyotegemea au kuingiliwa na watu wengine katika uendeshaji wenu. Mliapishwa wawili tu na si mia mbili. Hivyo, jukumu na wajibu wa kutunza kiapo chenu ni lenu. Si la watoto wenu, marafiki, wazazi, mashoga, na wengine hata muwapende, kuwathamini, na kuwaamini vipi. Ndoa ni kama sehemu zenu za siri. Hakuna apaswaye kuziona au kuzihudumia isipokuwa wanandoa wenyewe. Nani mpambavu huanika chupi zake hadharani?  Hivyo, ndoa inapaswa kuwa taasisi huru ambapo uhuru huu ulindwa kwa wivu na tahadhari kubwa. Tutoe mfano. Jamaa mmoja alizoea kuwapa marafiki zake siri za mwenzie. Moja ya siri alizotoa ilikuwa ni ukubwa wa maumbile yake na namna alivyojua shughuli.
    Katika hao marafiki, walikuwamo wakware waliokuwa wakimmezea mate mwenzie. Hivyo, kutotunza na kulinda siri za ndoa yake kuligeuka angamizi la ndoa yenyewe hasa wahusika walipokula njama kumuandamana mhusika. Binadamu tumeumbwa na kujipenda kuliko wengine. Mafanikio yako ni yako siyo ya kuwasimulia wenzako. Kitanda usicholalia, hupaswi kujua kunguni wake.
        Japo kuna kipindi mambo huzidi kiasi cha waliotanzwa kutafuta msaada. Katika ndoa, linapotokea tatizo, ni muhimu likashughulikiwa na wahusika peke yao tena kwa usiri. Ndiyo mana tunasema siri za ndani ziishie chumbani. Zisivushwe hata kuchungulia sebuleni. Hao mnaowafuata nao wana changamoto, kasoro, na matatizo yao. Kama ikizidi sana, wahusisheni wazazi wa pande mbili japo nalo hili linataka utafiti na umakini vya hali ya juu. Mnapozoea kuwapelekea watu matatizo yenu, mnayazidisha na kuyafanya yawe magumu zaidi kuliko mkiyashughulikia wenyewe. Mlipoamua kufunga ndoa mlifanya hivyo peke yenu japo baada ya hapo, mlitoa taarifa kwao kama sehemu ya hitajio la kijamii na kisheria. Kwenye changamoto, matatizo, na migogoro ya ndoa, msiwahusishe hata wapambe au mashahidi wenu. Hakimu wa kwanza wa kushgulikia changamoto na matatizo ya ndoa ni wanandoa wenyewe na mahakama yao ni chumba cha kulala.
Ithibati
Pamoja na miiko na misingi mingine, ithibati katika ndoa ni muhimu. Ithibati huonyesha kuwa mhusika anaaminika na anajiamini. Hivyo, zinapotokea changamoto katika ndoa yako, jambo kubwa la kwanza muhimu ni kujiamini. Hii hukupa fursa ya kufikiri na hata kufanya utatifi na kulidurusu tatizo ili ulipatie ufumbuzi. Mfano, unaweza kuchunguza au kutafiti chanzo au vyanzo vya tatizo. Mara nyingi, kama tulivyosema hapo juu, adui mkubwa wa ndoa ni wanandoa. Kadhalika, chanzo au vyanzo vya changamoto ni wao pia iwe kwa bahati mbaya, kutojua, kutokusudia, au kukusudia. Hivyo, sehemu ya kwanza kutafutia changamoto ni wanandoa wenyewe.
        Pili mwitikio na namna wanandoa wanavyopokea na kushughulikia changamoto zan doa yao ni muhimu. Hapa, unaepusha kumtafuta mchafu, wa kumtwisha lawama au kuepuka lawama kwa kufanya hivyo. Changamoto za ndoa ni sawa na maladhi mwilini. Ni mwenye mwili anayeyabaini hata kabla ya daktari. Hivyo, silaha imara ya kwanza kuelekea matatizo ni kujichunguza kwa wanandoa wanaokabiliwa nazo. Hapa, kunahitajika ukweli na uwazi ili kuepuka kufukuza tatizo au kutafuta suluhu mahali ambapo si sahihi au lilipo. Mfano, ukiwa unaumwa kichwa, huwezi kutafuta tatizo kwenye mguu. Lazima ukisikilizie kichwa hata kutafuta ushauri wa daktari juu ya kichwa siyo mguu.
Kanuni
Kama zilivyo taasisi nyingine, ndoa ina kanuni zake. Nyingi za kanuni hizi hazikuandikwa popote. Zinatengenezwa na wanandoa. Mfano, ni jambo gani hupenda kufanya bila kukosa wakati wa kuamka au kulala? Ni jambo gani wanandoa wanakubaliana au kutofautiana katika ndoa? Hata hivyo, methali moja ya kimombo inasema kuwa wanandoa wanaoimba pamoja huishi pamoja.
        Tutoe mfano wetu wenyewe. Siku moja tulinunua gari jipya aina ya Chevy Equinox. Baada ya kulinua, mmoja wetu aliamua atumie gari la zamani Kia Soul. Hata hivyo, kuna wakati tulikuwa tukibadilishana magari kulingana na tulipokuwa tukienda. Nkwazi alikuwa akiendesha Chevy zaidi na Nesaa akitumia Kia Soul. Kuna kitu tulitofautiana. Baada ya kununua Chevy Equinox, Nkwazi alinunua cover ya usukani nyeusi yenye manyoya. Nesaa hakuipenda hata kidogo akisema inaweza kutunza uchafu na ni vigumu kuisafisha. Mwishowe, tulikubaliana kuweka cover ya ngozi na changamoto ikaishia hapa. Kwa kanuni zetu, hatukujiruhusu kitu kitufarakanishe zaidi ya kukubali yaishe kwa msingi wa give and take kama tuutumiavyo kwenye taaluma ya utatuzi wa migogoro na kupata win-win solution au suluhu ambamo wote mnafaidika.
Mwisho, ukiangalia ukubwa wa changamoto, unaweza kuona ni kama jambo dogo. Si dogo. Kumbuka hata mbuni alianza na yai dogo mbali na mbegu za kiume na mayai ya kike visivyoonekana kwa macho. Mbali na hili, kanuni yetu kubwa ni kwamba asiyekubali kushindwa si mshindani na mshindwa wa leo anaweza kuwa mshindi wa kesho.
    Hivyo, ni vizuri kuzingatia msingi na nguzo za ndoa sawa na unavyofanya kwa taasisi nyinginezo. 
Chanzo: Mwananchi leo.


Wednesday 5 June 2024

Mafyatu Kumkaribu Rais Kuzindua Kijiwe

 

Baada ya kuona kuwa inawezekana kumfyatua, sorry, kumchengua rahis hadi anazindua mangomangoma ya Hamnazoo, mafyatu tunakula mkakati kumkaribisha kuzindua kijiwe chetu cha ndumuu. Naona yule anatikisa kichwa kuwa rahis na vijiwe vya bangii, sorry, nimesema bangili wapi na wapi? Hamkumuona arap Rooter wa kwa njirani akijinoma na mchekeshaji kwa Joji Kichaka akiwatosa wake. Ama kweli marahis tunao. Jamaa alikodisha pipa kwa bei mbaya akajaza familia na maswahiba wakaenda zao kutanua majuu kwa kodi za mafyatu. Hamkuona vibinti vyake na vinjukuti majuu? Halafu mnashangaa kwanini Afrika siku zote haiendelei! Kwa uzwazwa huu?

            Kimsingi, baada ya urahis kuwa rahisi hasa usawa huu wanene wanavyohaha na kufyatua maigizo ya kupatia kura ya kula, wanjanja ndo wakati wa kuwatumia kirahisi. Lazima tuwarahisishe japo wamejirahisi wenyewe. Hakumsikia profedheha Muongo aliyekataa msosi hotelini eti ‘kuokoa’ njuluku za mafyatu utadhani alianza unene jana? Tuliokua zama za mzee Nchonga, haya ni makufuru yaliyovunja miiko yote kimaadili. Nakumbuka mzee Ruxa alipomkaribisha Mic Jekson. Wee, tulizoza. Hakurudia.

Turejeee inshu. Nani asiyetaka kura ya kula hata ikibidi kuvunja protokali? Kwani,waziri wa michezo hakutosha kuzindua mangomangoma ya Chingaboy aka Hamnazoo aka kijana wa maza on top of mwana wa pekee wa Arushwa na Abuduli? Wasiojua, maza ni maza wa wanangomangoma mbali na kuwa mpenzi mhifadhi, mfadhili na mchambuzi mahiri wa mambo ya mangomangoma. Soon, nitamshauri fyatu mhariri wangu ampe safu ya kuchambua mangomangoma ili mafyatu waelewe uzuri. Mwaka huu tutashuhudia mengi. Wasiojua. jiulize kwanini, maza, kwanza, alisema jamaa ni kijana wake? Pili, zile ngomangoma siyo za mafyatu bali akina maza wa kisasa na kisiasa wasio na visasi wala madenguzi.

            Nilipoitisha kikao kumkaribu mheshimika, mtukufu, mpendeka, msikivu, mchapakazi, mwelewa, doktari mwenyewe, mmwaga njuluku, fyatu mmoja alidai ninamdhalilisha. Nilimfukuza kigwenani na kumtangaza adui nambari wani wa kaya. Kama Katiba inampa kila uwezo hadi wa kimuungu wa kuweza kuumba na kufuga chawa, nani atamzuia kudhamini na kufungua kijiwe au kucheza nchiriku tena unaomsifia kamwaga njuluku tusizoziona? Kwani yeye siyo binadamu wala fyatu? Ukisikia usikivu na kujishusha­­­­––––siyo kujirahisisha––––kama mafyatu pingaji wanavyoweza kudhani––––ndiko huku. Huku ndiko kupenda mafyatu kiuchakachuaji japo kwa muda hadi kura ya kula ivunwe. Upendo au usanii? Apples and oranges.

            Mbali na hayo, siku hizi, siasa zinahitaji kiwango kikubwa cha usanii. Hivyo, si vibaya rahis kuwa msanii awatumiaye wasanii wenzake. Mmemsahau Njaa kaya kwenda kubembea kule Jomeika utadhani huku hakuna! Mmesahau? Siku hizi ikuu si kukuu tena bali playground ya wasanii? Kesho, sitashangaa kuwaona wakuu wa nkoa na wilaya wakifungua hata vigenge vya kuuzia ulabu kama siyo mmea sorry, mazao yatokanayo na mimea hata kigodoro. Tumeelewana?

            Tulikubaliana kumwalika rahis. Tumepanga tumpongeze kwa kuzindua ngoma nzuri kama hizi. Pili, tuutamtungia wimbo wa kumpongeza anavyomwaga njuluku na ni simba jike. Hamnazoo aliimba kuwa wamaza ni ngurumbili na nusu. Sisi tutaimba kuwa mamaza hasa maza mwenyewe, ni ngurumbili mia. Tatu, maza ana roho ya chuma. Nani alijua kuwa anamilki runinga binafsi? Tutamtaka ataje miradi yake yote ukiwemo ukwasi wake na namna alivyoutengeza na kuuchuma.

            Tutampongeza namna maza anavyowahusudu mafyatu maskini kama vile wauza madafu, mitumba, na udohoudoho mwingine hadi wengine wakiruhusiwa kuuzia hata pale ikuli. Nadhani umenielewa. Pia, tutamuomba mafyatu hasa Fyatu Mfyatuzi atutaje siku hiyo kama alivyowataja wasanii. Mafyatu wamenipa mbinu ya kumvutia maza ili anitaje. Lazima nianze usanii. Nitaanza kuimba mapiano na singeli na kimatress nikieleza anavyovutia kura. Nitamsifia kuwa ni goddess kama wale wa Misri zamani pia kuwakumbuka wasanii. Tutampa maza outing ya nguvu kuliko dingi anavyompa.

            Kabla ya kumaliza, lazima nimshawishi maza, atumie kipaji chake cha kujua mangomangoma na wanamangomangoma kusoma vitabu vya watunzi na waandishi wetu wa vitabu nchini waliododa na kusahaulika huku usanii  ukipewa thamani kuliko ilmu.  Tutamwambia katatizo ka kaya. Inakuwaje wasanii tena waimbao ngonongono watajirike lakini waandishi wa vitabu wafe maskini? Je tatizo ni kaya kupenda na kutukuza mambo haya? Hamjaona orodha ya short time guest houses, vilabu, na madanguro vilivyo vingi kuliko mashule hadi tunapeleka vitegemezi kwa majirani walioamua kutopenda mambo haya. Hamuoni vijigazeti vya udaku vinavyotajirisha wasanii wengi kuliko vitabu vya kiada? Mie mwenyewe niliwahi kuandika kitabu cha kiada kikauawa kwa sababu ambazo sikuambiwa.

            Tutamshauri maza, aanze kuandamana na waandishi wa vitabu badala ya wasanii.  Ikishindikana, tubadilishe shule na vyuo vyote kuwa vya sanaa huku wizara yake ikihamishiwa ikuu. Wajanja wanawekeza kwenye ilmu, sie kwenye mipasho! Sijui nani katuroga yarabi? Je tamasha la Hamnazoo kaandaa yeye au katumwa na maza aanze kampani za kampeni kabla ya kipenga? Hivi, uchaguzi, sorry, uchakachuaji ni lini? Kaeni chonjo. Nshaonya.

Chanzo: Mwananchi leo.

Tuesday 4 June 2024

Yet another baby in the house!!!!

 Yoo-hoo, Africa Is Yowling

ISBN9789956554379
Pages104
Dimensions203x127 mm
Published2024
PublisherLangaa RPCIG, Cameroon
FormatPaperback

YOO-HOO, AFRICA IS YOWLING

by Nkwazi Nkuzi Mhango

Yoo-hoo, Africa Is Yowling is an awakening chant, aiming to shed light on Africa’s losses and explore ways to reclaim its rightful place. Nkwazi Mhango critically examines the continent’s struggles with corrupt leadership, emphasizing how those in power mismanage resources. Despite Africa’s abundant potential and resources, it remains inexplicably impoverished. The central question posed by the tome is this: How can a continent so richly endowed become a dejected entity? The book challenges prevailing narratives that perpetuate Africa’s perceived poverty, urging Africans to think differently and act positively for their own development and the well-being of future generations. In its nostalgic critique, the book confronts societal ills and condemns those who hinder progress. It encourages Africans to boldly advocate for their rights, rejecting deceptive practices, defunct ideologies, and other hindrances. Ultimately, Yoo-hoo, Africa Is Yowling serves as a wake-up call – an urgent plea for Africans to rise, reclaim their agency, and shape a brighter future.

 BOOK PREVIEW
British Pound£
Paperback
£15.00 

ABOUT THE AUTHOR

Nkwazi Nkuzi Mhango

Mhango is the author of Saa ya Ukombozi, Nyuma ya Pazia, Souls on Sale, Born with Voice, Africa Reunite or Perish, Psalm of the Oppressed, Perpetual Search, Africa’s Best and Worst President: How Neocolonialism and Imperialism Maintained Venal Rules in Africa and ‘Is It Global War on Terrorism’ or Global War over Terra Africana?: The Ruse Imperial Powers Use to Occupy Africa Militarily for Economic Gains, How Africa Developed Europe: Deconstructing the His-story of Africa, Excavating Untold Truth and What Ought to Be Done and Known, Africa’s Dependency Syndrome: Can Africa Still Turn Things around for the Better?, Our Heritage, Family Friend of Animal and Matembezi Mbugani (Children’s book co-authored with his wife Nesaa).

Sunday 2 June 2024

Waishiwa Wasiwe Madoktari au Wabukuzi

Kaya yetu si ya watata wala aihitaji utata,  kuringa, na kuringishiana ujuha. Ni kaya ya mafyatu. Hii inatosha. Siku hizi, kila fyatu anataka aitwe ima doktari au profedheha hata kama hajui kusoma na kuandika ilmradi tu ujiko na kujimwambafy. Hawajui wanavyotusononesha sie tusiobahatika kuwa madoktari wala maprofedheha ingawa ukiwauliza wamefanya nini cha mno, wote ngoma droo. Leo nitafyatua hii tabia hatari katika kutawala. Nitadurusu tabia chafu ya kuringa, kuringishiana, na kutishiana usalama na ulaji kayani na njengoni.
            Pili, ukiwa na waishiwa wasomi, watahoji upigaji wa wanene kiasi cha kuwanyima raha na kuwatia presha wakidai wagawane vinginevyo hakieleweki. Kama chawa wanashibishwa, kwanini wao wasishibishwe?
            Tatu, ukiwa na watawala wabukuzi watabukua kila kitu tofauti na mbumbumbu watakaobungabunga kila kitu na mambo yakaenda.  Haiwezekani wanene wasomeshe vitegemezi vyao ughaibuni halafu waje kushindana na wabukuzi mjengoni au kwenye sirkal. Ili kaya iendelee, tunahitaji mabingwa wa kusema ndiyo,kusifu na kupongeza bila kusahau kuimba mapambio. Haiwezekani maza awe doktari halafu mruhusu madoktari wengine kuja kushindana naye. Doktari anapaswa kuwa mmoja tu kayani.
            Ili kunogesha mambo, tokana na kasheshe, vimbwanga, na vituko nionavyo njengoni, napendekeza sifa mojawapo ya kuwa muishiwa iwe ni kuwa bingwa wa kupiga kanywaji na mmea ili akienda huko vimbwanga, vimbweka, na vituko viongezeke kuwaburudisha mafyatu wasifyatuke wakawafyatua.
            Nne, kushusha viwango vya elimu vitafanya tuzalishe wanene wengi na kugeuka kaya ya wanene tuondolewe kwenye orodha ya kaya kapuku. Tukiondoa ulazima wa kula mabuku, tutaondoa ulalamishi wa waliobukua wakakosa ajira. Wabukuzi ni walalamishi utadhani warugu, wee koma. Si mnamuona Mwambukuzi anavyolalamika? Angekuwa hajabukuwa taabu ingekuwa wapi? Wabukuzi hawafai. Kwanza, si woga. Pili, ni mafyatu wanaoweza  hata kuhoji uraia wa rahis na mgongano wetu mtukutu, sorry, mtukufu.
            Tano, tutaondoa presha na mikikimikiki ya kughushi, kuficha, au kuumbuliwa siri zinapofichuka. Hii inawapa taabu sana mafyatu wetu kiasi cha wengine kufyatuliwa na ugonjwa wa presha ya moyo. Nani anataka kupoteza mafyatu wake wanaowanenepesha wanene kwa kulipa kodi na tozos? Tukiondoa ulazima wa kuwa na shahada za vyoo, sorry jalala, sorry, vyuo vikuu, tutakuwa tumeondoa na kishawishi cha kughushi, urongo, na kujimbwafy na kuwakoga mafyatu mbali na kuokoa njuluku zinazopoteza kuzalisha modktari ambao kazi yao ni kuongea mineno migumu na mambo ya kufikilika na kutufanya tuchukie kutazama kipindi cha runinga njengoni.
            Sita, wabukuzi wanajidai sana. Wanaongea kiswanglish kigumu kiasi cha mafyatu kutonyaka wasemacho njengoni. Wanatunga sharia mbovu, sorry, ngumu kwa mafyatu na zinazowahudumia na kuwalinda wao. Juzi, kuna aliyeniudhi nusu nipige teke runinga yetu. Alisema eti yeye ni doktari wa Philo na Sofia! Yaani, bila aibu unatwambia kuwa una nyumba ndogo? Kama unawatibu hao akina Philo na Sofia wako, sisi inatuhusu au kutusaidia nini? Mwingine naye aliniacha hoi alipodai eti yeye ana bachela sijui ya madudu gani. Yaani, umri wote huo bado wewe ni bachela tu? Mwingine naye eti ana masta. Hivi masta kwa kisambaa siyo bwana? Nani anataka ubwana njengoni?
Kwa kuangalia wale wajimwabafaio kuwa ni madoktari wa Philo na Sofia, nagundua kuwa kaya inawapa njuluku ndefu bila sababu kiasi cha kuwa na nyumba ndogo. Bila hivyo, nani angesomea kuwatibu akina Philo na Sofia? Kesho, tutawasikia wengine wakijidai wao ni madoktari wa Halima na Husna. Mwingine eti doktari wa akina mama! Wako wapi wa akina baba? Tunataka wabukuzi madoktari wa Mafyatu siyo vimwana jamanini. Hii maana yake ni kwamba tupunguze mishiko na marupurupu ya waishiwa ili waonje tunavyofyatuliwa na dhiki zitokanazo na unene na vimbwanga njengoni.
            Saba, tukiwa na waishiwa darasa la saba au ngumbaru tutakuza lugha ya kaya na kuweza kuwasiliana na mafyatu kirahisi. Tutaua lugha za kikoloni zinazozidi kuua waishiwa wetu. Hamjawaona wakibukanya kiswanglish wanavyotoka jasho kiasi cha kupandisha presha ya shinikizo la moyo?
            Nane, tutapunguza idadi ya waishiwa wanaouchapa njengoni tokana na kuboreka kwa kiswanglish na mineno mingine migumu inayowatia usingizi hadi wanauchapa njengoni. Juzi kuna doktari mmoja alikuwa akiwasilisha na kujisifu sijui yeye alimaliza udoktari wake na extinction ya akili yake asifikaye kwa upigaji na kujidai hata kwenye uzwazwa. Kitegemezi changu si kiliniuliza nini maana ya extinction. Bila kujivunga nilikiambia kuwa yule jamaa alikuwa bingwa wa kuzima moto chooni, sorry, chuoni. Vitegemezi vya siku hizi vijanja kama simu janja. Kesho yake si kilikwenda kikamuuliza ticha wake akaniumbua bila kujua!
            Chonde chonde, njengo ujao, tuhakikishe tunachagua ngumbaru na kuachana na madoktari wa akina Philo, Sofia. Nimesemaje  eti nami ni doktari?
Kwanza, elimu yetu yenyewe Iko Chumba cha Umauti (ICCU). Hivyo, hatutaki waishiwa wabukuzi kama Mwambukuzi. Wataleta ubukuzi na kuzuia panyabuku kubukua wabukuavyo.
Chanzo: Mwananchi j'tano iliyopita.


Misingi na nguzo kuu za ndoa

Kama ilivyo nyumba, ndoa ina misingi yake. Kama ilivyo taasisi yoyote, ndoa ina nguzo hata miiko yake ambayo wanandoa wanapaswa kuizingatia na kuilinda. Hapa, tutaongelea misingi mikuu ya ndoa ambayo tunaidadavua kama ifuatavyo japo kwa uchache na ufupi ili kukuachia fursa na wakati muafaka kufanya utafiti binafsi na huru wewe mwenyewe. Pia, tuwe wakweli kwako. Sisi kama binadamu, pamoja na taaluma zetu, bado ni wanagezi tunaojifunza kila siku pamoja na kufundisha. Hivyo, hatuwezi kuwa na majibu ya maswali au matatizo yote tunayoibua tokana na taaluma na uzoefu wetu hasa ikizingatiwa kuwa nafasi tunayopata ni finyu mbali na kutokuwa safu.
Upendo wa kweli (true love)
Hivyo, wanaofunga ndoa, wahakikishe wanapendana kwa dhati na kwelikweli. Ndoa siyo lelemama wala jambo la muda kama urafiki na mahusiano mengine. Kama tunavyoonyesha hapo juu, ndoa ahitaji upendo tu bali upendo wa dhati na kweli. Baada ya kufungwa ndoa, upendo na utayari hupimwa na changamoto za ndoa ambazo leo hatutazigusia.Tusisitize. Lazima kuwe na upendo wenye pembe kuu mbili yaani udhati na ukweli.  
Uaminifu wa dhati (true trust)
Msingi wa pili wa ndoa ni uaminifu hasa ikizingatiwa kuwa ndoa ina majaribu na mitahani mingi iwe ya kijamii hata kiuchumi. Hivyo, wanaofunga ndoa, wahakikishe wanaaminiana na si kuaminiana tu bali wahikikishe wanaaminika pia. Kwanini uaminifu ni lazima na muhimu katika ndoa? Chukulia mfano inatokea hali ya kuyumba kiuchumi, ugonjwa, kesi, na mengine kama hayo. Kama wahusika hawaaminiani juu ya kupendana, hakuna atakayejitoa au kumvumilia mwenzake. Hakuna mtihani mkubwa kama kuyumba kiafya au kiuchumi. Hebu fikiria mwenzako wakati mnaoana alikuwa nazo. Mara ghafla unatokea mkwamo kiuchumi. Kwanza, waliowazunguka wataanza kujua kulingana na maisha yanavyobadilika. Hivyo, wapo watakaotaka kujua kunani. Hapa ndipo msingi mwingine wa usiri au kutunza siri za ndoa unapoingia na kufanya kazi au kukosekana na kuharibu kila kitu. Wahenga wanatuasa kuwa siri ya mtungi aijuaye kata. Na hapa tusisitize. Ni kata pekee apaswaye kuijua na kuitunza siri ya mtungi.
        Katika mkwamo, siri za ndoa zinapofuja, wapishi watakuwa wengi na kuharibu mchuzi. Kimsingi, unapokosekana uaminifu ambao hutokana na kuenda sambamba na kutojiamini wala kuchukua tahadhari dhidi ya hatari dhidi ya ndoa, ndoa itayumba hata kusambaratika. Kama zilivyo taasisi zozote, lazima ziwe na kanuni (rules) maadili (ethics), ithibati (integrity), miiko (taboos) uhuru (independence), upekee (uniqueness), uaminifu (tust), usiri (secrecy) na wivu (jealousy). Ndoa ikikosa au kupungua vitu hivi hugeuka tegemezi na hatarishi. Ndoa inayoendeshwa kwa itegemezi ushauri matakwa ya wasiohusika si imara wala salama. Japo hatukani kuwepo kwa wana familia, jamii, wengine. Si washirika katika ndoa. Ndoa si ushirika na haina wala aihitaji ushirika. Ndoa inapoanza kuendeshwa kwa mawazo, misukumo, na ushauri wa marafiki mashoga, hata ndugu, ujue iko hatarini. Ndoa ni ya wanandoa. Ndiyo wajuao misingi miiko, siri thamani, na umuhimu wake. Ndoa si klabu. Ina misingi sababu na siri zake. Ndoa ni kama serikali. Ndo maana huiingii bila kuapishwa, kuonywa, na kupewa majukumu. Hapa mantiki ni rahisi na wazi. Wanandoa ndiyo wanaojua sababu za kufunga ndoa. Ndiyo wanaojua thamani na umuhimu wake pia waathirika wa kuvunjika au kushindwa kwa ndoa yao. Ndoa ni kama utajiri. Inapotokea tajiri kufilisika, muathirika wa kwanza na mkuu ni yeye na siyo marafiki wala nguvu zao. Hivyo, tufahamu kuwa wanandoa ndiyo wajenzi hata wavunjaji wa ndoa. Kimsingi, adui wa kwanza wa ndoa ni wanandoa wenyewe hasa pale wanapokiuka misingi yake.
        Kwa leo tutamalizia hapa. Tukijaliwa na kupata fursa, tutaendelea na misingi na nguzo nyingine za ndoa. Tusisitize. Ndoa ni kama jengo. Kama itajengwa kwenye misingi na ikaongezewa nguzo imara, itadumu. Kama itajengwa bila msingi au kwenye msingi na nguzo hafifu, itaporomoka itakapokumbana na changamoto hata ziwe ndogo kiasi gani.
Msingi mkuu wa kwanza wa ndoa ni upendo, maana bila upendo hakuna ndoa na kama ipo ni majuto na mateso tena ya kudumu. Upendo ndiyo cheche inayoanzisha hitajio la kufunga ndoa. Hii haina maana kuwa hakuna misingi mingine muhimu. Ipo, ila upendo ndiyo msingi wa kwanza. Kama ndoa ni dini, basi upendo ni imani. Maana bila imani hakuna dini. Bila upendo wa kweli, hakuna mapenzi bali kutakana, kutumiana hata kuzidiana kete tu, maana mtaishi katika gereza. Tunadhani neno ndoa ni ndoana hutokana na uwepo wa ndoa zisizo na upendo wa kweli. Ndoa zenye upendo wa kweli ni kama pepo hata ziwe na chamgamoto kiasi gani. Tutoe mfano mwingine. Kama ndoa ni mchuzi, basi upendo ni viungo. Kukiwapo upendo, msingi, nguzo na mambo mengine hufuata kirahisi. Kwa kimombo husema things will fall into place.
Chanzo: Mwananchi leo.