The Chant of Savant

Saturday 16 June 2018

Kukosekana makala za the Guardian, Nipashe na Tanzania Daima tokana na dhuluma ya Mbowe na Mengi

Image result for photos of mengi and mbowe
Image result for photos of reginald mengi


           Kama ambayo mmeona siku za karibuni, makala zilizokuwa zikitoka kila wiki kwenye Gazeti la Tanzania Daima na kijliwe na nyingine kwenye magazeti ya  Nipashe na the Guardian hazionekani  kwenye uga huu kwa muda sasa. Hit ni kutokana na kuacha kuandikia magazeti husika baada ya wenye magazeti haya kunidhulumu pesa nyingi ambazo ni malimbikizo ya kazi za takriban miaka mitatu. Hivyo, utawala wa blog hii unajisikia vibaya kufikia hatua hii ambayo, hata hivyo, haiepukiki. Kila nilipokuwa nikidai pesa zangu, wahariri wa magazeti husika walizoea kuniambia kuwa rais John Magufuli amehujumu biashara zao jambo ambalo naona ni dhuluma longolongo na ubabaishaji hasa nikaingalia haddi za wahusika. 
                  Badala ya kuongelea namna ya kunilipa, ulijengeka uadui wa ajabu. Mfano, wahariri wa Gazeti la Nipashe Gaudencia Mngumi na Edmund Msangi waliongoza katika uhasama huu usiokuwa na sababu yoyote bali dhuluma na kujikomba kwa mabwana zao. Sikutegemea watu  ambao wamekuwa wakijionyesha kama matajiri na watetezi wa haki za watanzania kama Freeman Mbowe na Reginald Mengi wangekuwa dhulumati wa kawaida wanaojionyesha kama watu wema wakati si chochote si lolote.

No comments: