Juzi, katika kupitapita mitaani kutoa tongotongo, si
nikachekwa kiasi cha kudhani naanza kuchizika. Kwanza, kituko kilianzia uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Bole pale Addis. Baada ya kutua kama kawa, hutoa
tongotongo. Hivyo, nilikwenda kwenye ofisi za shirika la njiwa la Ethiopia lenye
watumishi wa hovyo sina mfano. Mstuko ndo usipime. Nikiwa nimejipanga mstarini
tayari kusikilizwa, niliomba msaada kwa abiria mwengine aliyekuwa mbele yangu
ambaye ni mmakonde kama mimi. Ukiachia yeye na wengine wachache, abiria
tarajiwa wa njiwa hiyo waliobakia walikuwa wachainizi!
Nilimuuliza jamaa kama kuna njiwa mbili
moja ya kuja Ufyatuni na nyingine ya kwenda Chaina. Jamaa alishangaa. badala ya
kujibu swali, naye aliniuliza swali. Si unajua tena mafyatu. Badala ya fyatu
kujibu swali langu, naye aliswalika swali. Alisema “kwani wewe unelekea wapi?”
Nilimjibu kuwa nilikuwa natia timu kaya. Badala ya kunipa jibu aliuliza tena
“kwani tatizo lako nini? Baada ya kuona hivyo, nikanywea na kuamua kujiondokea
nikangoja wakati ukifika wa njiwa wangu kupaa nitangoja mtangazaji anijuze ni
ipi.
Baada ya kusota muda mrefu na muda wa kupaa kuwadia, nilienda tena kwenye geti la kupandia. Kwa mara nyingine, nilikuta wachaina kibao. Hivyo, ilibidi nimuulize mfanyakazi mmojawapo kama njiwa iliyokuwa inaondoka ilikuwa inaelekea Chaina au Ufyatuni. Akiwa ameshangaa kidogo, alijibu kuwa ilikuwa inaelekea Ufyatuni na si Chaina. Du! Nilianza kuskuti lau nipate jibu nisipate. Basi, Fyatu nilifyata nikingoja pipa litue nione yaliyokuwa yakinisibu kuhusiana na hawa wachaina. Kutua, tu, nikasikia wengine wakitema uswa japo wakichainachaina.
Nilichukua
ndinga yangu kuzama zangu Utashani kwa wenzangu. We bwana! Kufika, si nikakuta
hata apartments za kupangisha baadhi yake zinamilkiwa na wachaina. Kabla mstuko
kuniisha si nikasikia mmoja akipita akisema ‘nauja ice cream!” “Du” nilijisemea
“utadhani niko zangu Uchainani na si Ufyatuni!” Baada ya hapo, maswali lukuki
yalianza kunishambulia. Hivi huu ndiyo uwekezaji au uchukuaji
kama siyo exportation of jobless army from Chaina?” Nisameheni kwa
kitasha. Maana, siku hizi hata Kiswahili naongea kwa taabu sana kiasi cha
kuandika haya madude kwa msaada wa mshikaji wangu Siri. Hayo tuyaache. Kwa
kuzingatia haya, kwanini Ufyatuni isiitwe Chaitan?
Mbali
na kuitwa Chaitan, maybe, chai tamu, lipo hili sekeseke na timbwili kama siyo
mtiti wa haya jamaa zangu waendesha baiskili za umeme au Toyo. Da! Hawa jamaa
walinikanganya hadi nikaongopa hata kuendesha ndinga yangu kwa wanavyoonyesha
umahiri wa kuvunja na kuvuruga sheria za barabarani.
Baada ya kusota muda mrefu na muda wa kupaa kuwadia, nilienda tena kwenye geti la kupandia. Kwa mara nyingine, nilikuta wachaina kibao. Hivyo, ilibidi nimuulize mfanyakazi mmojawapo kama njiwa iliyokuwa inaondoka ilikuwa inaelekea Chaina au Ufyatuni. Akiwa ameshangaa kidogo, alijibu kuwa ilikuwa inaelekea Ufyatuni na si Chaina. Du! Nilianza kuskuti lau nipate jibu nisipate. Basi, Fyatu nilifyata nikingoja pipa litue nione yaliyokuwa yakinisibu kuhusiana na hawa wachaina. Kutua, tu, nikasikia wengine wakitema uswa japo wakichainachaina.
Kwanza, nilijiuliza
kifyatufyatu. Inakuwaje mafyatu wazima wenye akili timamu kama siyo kuchizika,
na nguvu wafanye vitu ambavyo kwa kisambaa huitwa suicidal? Je ni
kuchizika, ukosefu wa akili timamu (UAT), ukosefu wa ubunifu au kujichoka na
kuchoka kuishi?
Pili, ni kwanini wahusika hawaoni denja wanayocheza nayo? Tatu,
inakuwajekuwaje wanene hawaoni balaa hili ambalo naona ni kama bomu linalotika
likingoja kuitafuna kaya? Nne, kwanini hawaoni uchafuzi wa mazingira mbali na
uwezekano wa kutengeneza kizazi au taifa la viwete tokana na uvunjaji wa sheria
na uendeshaji wa hovyo na hatarishi wa toyo unavyosababisha vifo vya
waendeshaji na abiria? Tano, imekuwaje tumejichoka na kuruhusu ghasia kuwa
ndiyo mfumo wetu wa maisha kama mafyatu?
Kusema ukweli, sikuamini kuwa fyatu mwenye akili timamu ana anayetaka kuishi angeweza kupanda haya majeneza yasiyofunikwa yaitwayo toyo. Sikuamini kuwa kidude kinachopaswa kubeba mafyatu wawili tena wakiwa, kisheria, wanapaswa kuvaa helmet kwa usalama wao, kingeweza kupakizwa mafyatu watatu na wakati mwingine wanne. Funga kazi ni pale niliposhuhudia abiria wakipanda haya madude ya kifo bila kuvaa helmets. Je, hapa tatizo ni wahusika au mfumo mzima usiofuata maadili wala sheria bali madili na shari? Kwa mujibu wa hali na jinai, kwanini Ufyatuni isiitwe Tanghasia?
Jambo
la tatu ambalo ningepata nilidurusu japo kwa ufupi ni upigaji wa kizwazwa na wa
kutisha, au tuseme wizi wa kimfumo. Mwajua kuwa juzi llikuwa Saba Saba? Siendi
kwenye historia yake na kuzaliwa kwa chata la TANU. Katika kutoa tongotongo, si
nikatinga nikiwa na lengo la kwenda kuwafaidi waanimo hasa lion. Kama kawa,
nilificha njuluku na rukono yangu bila kusahau wallet yangu ili wale washenzi
wasinisachi na kusepa. Kwa vile ni bonge la mjanja, njuluku niliweka sehemu
nyeti na kusepa. Kufika tu, huo msongamano usipime. Katika kusukuti, si
nilikuta kuwa ni wa kutengenezwa ili wahusika wapate kuuza hata tiketi feki na
kusepa? Nani alilistukia hili? Hili halikunihangaisha kwa vile ulaji na madili
ni sehemu ya mfumo wa Danganyika na Zaa inzi, we koma.
Nilitaka kushambuliwa na presha pale nilipolipia tikiti ya kuingilia na kuishia kulipishwa tena kuwaona waanimo? Je huu siyo uanimo kunipiga kuwaona waanimo wakati nshalipia kuingia kuenjoy kila kitu? Kumbe nina jet lag inayochizisha akili?
Kusema ukweli, sikuamini kuwa fyatu mwenye akili timamu ana anayetaka kuishi angeweza kupanda haya majeneza yasiyofunikwa yaitwayo toyo. Sikuamini kuwa kidude kinachopaswa kubeba mafyatu wawili tena wakiwa, kisheria, wanapaswa kuvaa helmet kwa usalama wao, kingeweza kupakizwa mafyatu watatu na wakati mwingine wanne. Funga kazi ni pale niliposhuhudia abiria wakipanda haya madude ya kifo bila kuvaa helmets. Je, hapa tatizo ni wahusika au mfumo mzima usiofuata maadili wala sheria bali madili na shari? Kwa mujibu wa hali na jinai, kwanini Ufyatuni isiitwe Tanghasia?
Nilitaka kushambuliwa na presha pale nilipolipia tikiti ya kuingilia na kuishia kulipishwa tena kuwaona waanimo? Je huu siyo uanimo kunipiga kuwaona waanimo wakati nshalipia kuingia kuenjoy kila kitu? Kumbe nina jet lag inayochizisha akili?
Chanzo: Mwananchi leo.
No comments:
Post a Comment