Kuna kisa
cha mama mmoja aliyeukwaa uheshimiwa.
Tulipata kisa hiki kwenye pitapita zetu kwenye tarifa mitandaoni na
kuthibitisha kuwa ilikuwa ni stori ya kweli. Tuliweza kudurusu na kujua hata
jimbo analotoka katika mkoa mmoja wa Kanda ya Ziwa. Huyu mama, kwa kusaidiwa na
mumewe, alitumia raslimali za familia kuukwaa uheshimiwa ambao, hata hivyo,
uliishiwa kuwa uishiwa. Hii ni kutokana na kuvurunda na kuivunja ndoa yake
baada ya ukubwa kumpanda kichwani.
Pili, alianza kwenda ughaibuni akiandamana na waheshimiwa wenzake wa kiume na maafisa wakubwa wakubwa wa serikali. Huko, walikaa kwenye mahoteli ya bei mbaya wakila na kunywa na kulala pamoja. Ghafla, uzalendo ulimshinda. Alianza mahusiano yasiyo na heshima na waheshimiwa wenzake. Walipika na kupakua kiasi cha kunogewa. Jambo hili, lilimpelekea kutokuwa na hamu na mumewe kiasi cha kuanza kuanzisha kasheshe hadi ndoa ikavunjika.
Tatu, badala ya mafanikio kufanikisha ndoa, yalifanikisha kitu kimoja tu ambacho ni kuivunja ndoa na kuacha majuto na mateso si kwake tu bali mume na watoto na hata ndugu na jamaa.
Japo si wengi wala wote wanaojitokeza kueleza ukweli huu wa aibu na uchungu, je hawapo? Je ni akina mama wangapi wenye madaraka wamevunja ndoa zao? Je kwanini ni wanawake ambao ni wahanga wa madaraka au kuna na wanaume? Jibu laweza kuwa sababu ni kwamba jamii yetu inatawaliwa na mfumo dume ambapo wanaume wana uwezo wa kufanya watakalo na wasifanywe kitu na wenzi wao wa kike.
Katika kudurusu kisa hiki, je nani wa kulaumiwa. Je ni mfumo au mhusika mwenyewe? Je hii inatoa somo gani kwa wale ambao hawajaingia na yakawakuta haya yaliyomkuta dada huyu ambaye wakati anaupata uheshimiwa alikuwa mdogo miaka 30 na ushei? Je hiki hakiwezi kuwa kikwazo kwa wanawake wengi ambao wangetaka kuingia siasa? Je wahusika wachague kipi kati ya madaraka na ndoa? Wakati mkitafakari kujibu maswali hayo hapo juu, tunaweza kuwapa mwangaza au ujanja wa kufanya uamuzi bora. Tutatoa angalizo kuwa madaraka ni ya muda na ndoa ni ya kudumu. Kwa mwenye akili safi na busara, atachagua cha kudumu na kuachana na cha muda. Je ni wangapi wanaweza kuchagua ndoa na kuachana na madaraka? Je hatuhitaji kubadili mfumo wetu wa kisiasa ili kulinda ndoa za waheshimiwa wetu na kuwahakikishia usalama akina mama ili wawe na mazingara salama na sawa kushiriki katika siasa? Je hili ni tatizo la watu binafsi au la jamii kwa ujumla pamoja na mfumo wake? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Pamoja na kwamba makala hii inahusika na ndoa za waheshimiwa na madhara wapatayo, inawakilisha dhana nzima ya madaraka kijinsia. Kwanini wanaume wanapopata madaraka hayavunji ndoa zao? Kwanini madaraka ni tishio kwa ndoa za akina mama wengi japo si wote? Je nini kifanyike?
Je katika kudurusu kisa husika, wewe kama mwanandoa, unamsikitikia, kumlaumu, kumhukumu, au kutojali kwa vile hayakuhusu? Je ungekuwa wewe, ungechagua nini na kwanini? Tunauliza maswali hii kutaka kuwaelimisha wasomaji wetu kuwa madaraka si uheshimiwa tu bali ni dhana mtambuka. Kuna haja ya wanandoa kushirikiana katika jambo hata kama ni madaraka au mafanikio vinginevyo, yanaweza kugeuka maanguko si kwa mmoja bali wao, watoto wao, na hata wazazi, mafarafiki na familia zao.
Tumalizie kwa kuwataka wahusika na jamii kwa ujumla kukomesha na kuepusha balaa hili kwa ndoa litokanalo na mfumo dume na fisasdi. Kwenye nchi za magharibi, waheshimiwa huchunguzwa sana na kupewa adhabu kali wanapopatikana kuvunja kanuni za maadili wanazopaswa kuzifuata. Hata hivyo, wana mazingira mazuri ya kuwezesha waheshimiwa kulinda. Nasi, baada ya kugundua tatizo hili, kama jamii yenye akili timamu, tuchukue hatua kulikomesha ili kuepusha mateso kwa familia nyingi na wanandoa mbali na kuwepo mazingira magumu kwa wanawake kufanya siasa kwa uhuru bila kuchelewa yaliyompata mhusika kwenye kisa husika.

Baada ya kujaa mjengoni, kwanza,
mama alianza kuzinyaka na kuuonja unono na utamu wa ukubwa. Mshahara alipata si
haba tena kwa mamilioni. Milioni tano kwa mwezi mbali na marupurupu lukuki
kiasi cha kuondoka na si chini ya milioni kumi kwa mwezi.
Chanzo: Mwananchi j[pili.
No comments:
Post a Comment