Japo wengi hawajui, Ben Bill Nkapa alikuwa fyatu wa kupigiwa mfano tena personal friend wa Fyatu mwenyewe. Nakumbuka emails zake za mwisho alizoniandikia. Naona yule anatikisa kichwa kuwa nazua au kutaka kuwafyatua wasomaji wangu. Usifanye hivyo. Fyatu Ben alikuwa rafiki yangu taka usitake. Kimsingi, niliunganishwa naye na Fyatu mwingine ambaye pia ni rafiki yangu Dingi wangu Pio Nsekwa. Hayo tuyaache. Yanatosha.
Leo, kwa huzuni na majonzi, naandika waraka huu kumkumbuka Fyatu Ben. Kama raia wake na rafiki, nina jukukumu la kumkumbuka gwiji huyu aliyetoweka miaka mitano iliyopita. Wengi wanamkumbuka kwa ufyatu wake hasa kujiamini na kutoa hotuba ndefu tena zenye mashiko na zenye kujaa mapwenti. Wapo waliomuona kama mtu asiyefikika. Ukweli ni kwamba Ben alikuwa muungwana na down to earth sina mfano. Kwa wasiomjua, alikuwa tofauti na ninavyomueleza kama Fyatu aliyemfahamu.
Kwanza, nikupe habari mbaya. Yule dogo aliyekuwa akikuhusudu yaani rais Joni Kanywaji Malock si alikufa ghafla mwaka mmoja baada yako. Huu msiba ulitikisa taifa na dunia usipime. Wengi hadi leo hawajaamini kuwa gwiji huyu aliyesifika kwa kujiamini na uchapakazi alirejesha namba. Hata hivyo, aliacha alama ambazo zitachukua mamia ya miaka kusahaulika. Alianzisha miradi lukuki na kuipaisha kaya usipime. Baada ya kuondoka, makamu wake Bi Mkubwa Samia Solution alichukua ukanda. Maza anajitahidi usipime. Baada ya kushika ukanda, hajakaa hata kidogo. Anachapa kazi usipime. Baada ya Hapa Kazi Tu, alikuja na Kazi Iendelee. Na kweli, kazi inaendelea kindakindaki. Ukiachia politics za kukomoana na kupakaziana za wale wanaomuone maya na vivu, kaya imetulia. Ina amani na mshikamano na Bi Mkubwa wetu anazidi kuipaisha kaya. Mfano, lile daraja la Busisi ambalo sasa linaitwa JPM, lishakamilika zamani gani. Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nchonga nao, si haba, uko karibia ukingoni. Unakumbuka chimbuachimbua ya SGR? Basi, mwanangu, inazidi kupaa ikielekea Burundi na Rwanda. Miradi ni mingi aliyokamilisha Bi Mkubwa. Nakumegea hiyo kiduchu tu.
Mpendwa Ben, sasa tunaingia kwenye uchakachuaji, sorry, uchaguzi mkuu ujao. Chama twawala kishaandaa visu kupeta hata kama ni kwa bao la nkono kama alivyowahi kuseme Nipe Mapepe Ninaye kabla ya kuonyeshwa mlango. Kilishapata mpeperusha bendera yake ambaye ni Maza mwenyewe japo wapo wanaokosoa namna alivyopitishwa. Mambo ya Ngoswe tunamwaachia Ngoswe mwenyewe. Kama ujuavyo mambo ya mapinduzi mapinduzi hasa ya kifyatufyatu, kuna kitimtim cha kufa fyatu. Mafyatu sasa si haba. Wanajinoma kwa takrima na ukarimu vya muda wakijua wazi kuwa watafyatua njuluku za wanene sasa ili baadaye nao wafyatuliwe kwa miaka mitano ijayo.
Juzi si kiliumana. Walitokea wachumia tumbo na matapeli tena toka kwenye chama twawala wakataka kukinukisha. Mmoja ni yule jamaa wa kujipachika mavyeo makubwa ya utukufu kama uaskopo, udoktari, mengine mengi tena akipiga njulukub kwa kuwaibia mafyatu walioishiwa eti atawafanyia miujiza waukate wasijue utawakata.Si jama alikinukisha akijifanya eti kupinga utekaji na upoteaji wa mafyatu! Wanaomjua walimshangaa kwa namna alivyotaka kuwadanganya mafyatu akiwamo yeye mweyewe. Jamaa alilituhumu lisrikal na chama harafu akajifanya eti yeye ni mwanchama kindakindaki wakati ni msaka ngawira na twapeli wa kawaida. Jamaa alishukiwa usipime. Lile duka lake la kuuzia neno na roho si lilifungwa kiasi cha jamaa kutokomea na kuishia kubwekea kwenye mitandao. Mpaka ninapoandika, jamaa hatouonja tena uishiwa ambao nao alikuwa amepewa na mwendaze.
Mwingine ni yule jamaa mhuni mhuni aliyeibuliwa na mwendazake anayewaita wenzake wahuni kana kwamba yeye siyo. Huyu naye amekuja na mpya. Anapakaza eti hakuna haki kayani! Mafyatu tunajiuliza. Je, hii haki imeanza kutoweka hadi kutokuwepo lini na alikuwa wapi mbona hakuzoza? Kwa wanaokumbuka mwendaze alivyofumua kila kitu kiasi cha mafyatu kuanza kutoweka na kutoweshwa huku wengine wakimwagiwa shaba, anashangaa huyu jamaa alikuwa wapi. Fyatu sishangai. Si yeye ndo alikuwa jikoni mwa mwendazake akifyatua misimamo ya kuunga mkono kila kitu.
Mpendwa Ben, rafiki yako na mshirika wako Anna bado anadunda ingawa miaka ndiyo hiyo inayoyoma. Bado anamudu mikiki ya maisha kama wengine. Ila haonekani sana kama zamani. Cha mno, tunakumiss we acha tu. Tunamiss falsafa yako ya uwazi na ukweli ambao wakati mwingine, wasiokujua uzuri wala falsafa yako walidhani ulikuwa ufichi na otherwise.
Kwa vile uko kwenye pumziko la milele, naomba nisikuchoshe na mambo ya politiki. Japo, kwa ufupi, nimekupasha machache kati ya mengi yanayojiri huku uzimani. Naomba uwasalimie magwiji na mashujaa wetu walioko huko. Waambie tunawaenzi na kuwamiss sana kifyatu na kinomi. Unasalimiwa na best wako Pio Nsekwa. Siku hizi ameacha kuandika japo siyo kusoma. Huwa tunasalimiana mara kwa mara na kukukumbuka.RIP Ben Bill Nkapa my best friend.

Chanzo: Mwananchi Jtano iliyopita.
No comments:
Post a Comment