Kuanzia sasa, Fyatuland si jamhuri tena. Ni ufalme wa Fyatu Mfyatuaji awafyatuaye mafyatu atakavyo wasifyatuke wakamfyatua. Kuwafyatua vilivyo, juzi niliwafyatua mafyatu mkenge. Walinipigia kelele wanataka domoghasia aka demokrasia. Sikusita. Kwangu, hii ilikuwa fursa ya kuwafyatua vilivyo tena bila aibu wala huruma. Niliitisha uchaguzi ambao wapinzani wangu waliuita uchafuzi. Nilishangaa. Nani alimchafua nani wakati nilichofanya ni kufyatua? Ajabu, wengi wanaolalamika na kupiga zegele ni wale waliosusa sisi tukachukua na kuweka mwaa. Sasa twala. Viroho vinawauma kwa ngoa na wivu. Mshindwe kama mlivyoshindwa kwenye uchaguzi kumbaffuni kabisa. Kuanzia sasa, hakuna uchaguzi. Sitaki presha.
The Curse for Salvation
Wednesday, 26 November 2025
Rasmi natangaza Ufalme wa Fyatuland
Kuanzia sasa, Fyatuland si jamhuri tena. Ni ufalme wa Fyatu Mfyatuaji awafyatuaye mafyatu atakavyo wasifyatuke wakamfyatua. Kuwafyatua vilivyo, juzi niliwafyatua mafyatu mkenge. Walinipigia kelele wanataka domoghasia aka demokrasia. Sikusita. Kwangu, hii ilikuwa fursa ya kuwafyatua vilivyo tena bila aibu wala huruma. Niliitisha uchaguzi ambao wapinzani wangu waliuita uchafuzi. Nilishangaa. Nani alimchafua nani wakati nilichofanya ni kufyatua? Ajabu, wengi wanaolalamika na kupiga zegele ni wale waliosusa sisi tukachukua na kuweka mwaa. Sasa twala. Viroho vinawauma kwa ngoa na wivu. Mshindwe kama mlivyoshindwa kwenye uchaguzi kumbaffuni kabisa. Kuanzia sasa, hakuna uchaguzi. Sitaki presha.
Sunday, 23 November 2025
Can Museveni ‘fight’ over Indian Ocean?
Museveni speaks allegorically and philosophically. Besides, at his age, he speaks as if he does to his grandkids. Museveni is right. The Indian ocean is his simply because he enjoys its uses. His goods to and from abroad go through this ocean. Those naively lampooning him should know.
As for Muzei, he aims at warning the East Africans that they need to put their house in order. This reminds me of my book Africa Unite or Perish. Besides, of all African postcolonial president, it’s Dr. Kwame Nkrumah, Ghanaian founder who espoused Africa’s fast-track union while Julius Nyerere who outfoxed him preferred a bit-by-bit unification of Africa that’s never materialised.
In sum, before attacking each other, ask yourself. Who asked God to create water aka ocean for him or her and deny it to others? By the bye, why’d we fight over brine that we can’t even drink or shower with? Africa unite or perish. In this case in point, please, examine what is said not who is saying it. Museveni indeed is not supposed to be condemned but thanked for saying it honestly and point blank.
Source" Daily Monitor Sunday today.
Ni hatari wanandoa kuishi mbalimbali
Tokana na uzoefu, kwa kuona au kusikia, tunajua wanandoa wanaoishi maisha ya utengano usio na ulazima au sababu. Wanatenganishwa na aina na mihangaiko ya maisha kama kufanyia kazi sehemu tofauti. Pia, wapo wanaoishi mbali mbali tokana na mazoea na mila za baadhi ya jamii. Mfano, kuna jamii au makabila yanayoamini kuwa lazima wawe na mashamba na mifugo vijijini walikozaliwa. Hivyo, mara nyingi, mama ndiyo hupewa jukumu la kuangalia mali za familia huko kijijini. Utasikia mtu anasema kuwa mke wangu anaishi kijijini kuangalia ng’ombe au mashamba. Hukuoa wala mkeo kuwa mke wa ng’ombe, mbuzi, kuku, na mashamba bali mwenzi wako wa karibu anayepaswa kuwa nawe wakati wowote.
Japo wanalazimishwa na maisha, je, hilo ndilo jibu au njia pekee ya kuweza kuishi kwa ufanisi bila kujitesa hata kuwatesa watoto wao? Je, wanaofanya hivyo, wanajua madhara ya kufanya hivyo? Hivi, hakuna njia nyingine ya kuishi pamoja na wahusika wakakuza uchumi wao?
Leo, tunadurusu ndoa ya kuishi mbali mbali na madhara yake. Tunajua. Ili familia ifanikiwe na kustawi lazima iwe na kipato. Hata hivyo, kwanini uchumi uchukue nafasi ya mambo mengine? Kwa wanaojua raha na adha za ndoa, kuishi mbali mbali kunaweza kuwa chanzo kikubwa cha kuregarega na kuvunjika ndoa.
Kuishi mbali husababisha upweke si kwa wanadoa tu bali hata watoto kiasi cha kuleta changamoto katika malezi ya watoto. Wakikuyu Kenya na makabila mengine karibu yote ya Kenya ukiondoa ya Pwani, wana utamaduni wa kwenda mijini kutafuta na kuwaacha wake zao walee watoto peke yao. Nini madhara ya hili? Watoto huwa karibu na mama zao na kuwathamini kuliko baba zao japo huwahangaikia na kuwawezesha kimalezi kujiandaa kwa ajili ya maisha ya baadaye ambapo wahusika watakuwa wameishiwa uwezo kiasi cha kuwategemea wasipate msaada waliotegemea wala kukusudia.
Sisi ni wazazi. Tunajua mapenzi ya wazazi kwa Watoto ingawa wakati mwingine mapenzi yanaweza kuwajengea chuki dhidi ya wazazi wote au mzazi mmojawapo. Kwa uzoefu wetu, tunawashauri wazazi wasiwaishie watoto bali wawandae kuyapokea, kuyakubali, na kuyakabili majukumu yao ya baadaye watakapokua badala ya kujiumiza na kuwaumiza kwa kuwaandalia urithi wa vitu ambayo wengi huvifuja tokana na ukosefu wa uzoefu na maandalizi. Mnapowaishia watoto au kutaka muwaachie kila kitu, wakikua watafanya nini? Tunashauri wazazi wawafundishe watoto kujitegemea kwa kuwaandaa kifani na kisaikolojia bila kujiumiza ukihangaika na kuwaachia watoto eti mali. Japo si vibaya, je wao watakapokua watafanyia nini akili na vipaji vyao? Kwetu, urithi mkubwa kwa watoto ni kuwazaa, kuwandaa kwa kesho yao ambayo ni tofauti na ya wazazi tena wengi ambao hawakurithi hata kijiko zaidi ya kuzaliwa.
Hakuna urithi mkubwa kama vile kuzaliwa, kulelewa, na kuandaliwa kwa ajii ya maisha ya baadaye ambao ni bora kuliko fedha, mali, na vitu. Wapo wazazi waliolelewa na kusoma kwa taabu. Wakishapata fedha, huwaharibu watoto wao wakichelea wasipitie magumu waliyopitia wasijue ndiyo shule pekee iliyowafanya wafanikiwe. Kwa mfano, unampeleka mtoto International School kwa vile wewe hukuisomea au kushindana na majirani na ndugu. Akimaliza, unagundua umetengeneza kuku wa kizungu. Unafanya nini zaidi ya kumlaumu na kumuona mwanao kuwa mzembe usijue maandalizi aliyopata kule hayafanani na uhalisia wa maisha? Hili la malezi ya kisasa, tutalipa Makala yake maalum.
Mbali na ugumu wa malezi ya watoto, kuishi mbali mbali kunaweza kuwa chanzo cha vishawishi pande zote hasa lijapo suala la ‘stahiki’ ya wanandoa kimapenzi. Je, huwa wahusika wanafanyaje lijapo suala hili au tuseme tendo la ndoa ambalo katika ndoa ni lazima na muhimu? Ndiyo maana likaitwa tendo la ndoa. Hatupendi kuwahukumu, ila kuna uwezekano wa wanandoa wa aina hii kuwa na namna ya kulipata kiharamu japo si wote na pia, yawezekana wengine wakaishi pamoja na bado wakachepuka. Hilo, tunaliacha kama swali na changamoto kwa wanandoa kutafuta jibu.
Tumalizie kwa kusema. Ni hatari kwa wanandoa na watoto wao kuishi mbali mbali. Msihangaishwe na kesho ya watoto wenu. Kwani, kama mlivyoweza nyinyi, nao wataweza.
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.
Wednesday, 19 November 2025
Inakuwaje Fyatu Mzima Anajigeuza au Kugeuzwa Mdudu?
Kunguni na chawa ni mojawapo ya wadudu wachafu, na hatari bila kusahau wawafugao miongoni mwa viumbe waliolaaniwa tangu walipoumbwa. Ni dhalili, dhalimu, katili, na tegemezi. Hawana akili, aibu, maarifa, wala huruma. Ni hatari, hatarishi, na wabaya hakuna mfano. Hunyonya hata maiti na mizoga. Ni watumwa wa matumbo yao yasiyoshiba. Huishi kwa kunyonya wengine na kuwasababishia hasara, maradhi, mateso, usumbufu, na vifo. Maumivu ya mirija yao ni makali. Wanaweza kushindana na mbu na funza katika hili. Wanachukiwa na binadamu na wanyama kwa matendo yao ya hovyo na machafu. Ili waishi na kushamiri, wadudu hawa lazima kuwepo na uchafu na watu wachafu wa kuwafuga na kuwalisha kwa faida na sababu wasijuavyo japo ni hatarishi na za hovyo.
Mosi, nikiwa mkoa fulani pembezoni mwa kaya, nilimsikia kwa masikio yangu na kumuona kwa macho yangu yote matatu kupe mmoja ajiitaye kiongozi akiongopa mchana kweupe bila aibu wala hofu huku akijigeuza kupe ili kuwashinda chawa. Jamaa, alijitoa kimasomaso na kumpigia kampeni mgombea ‘pinzani’ akagoma kufanya hivyo kwa mgombea wa chama chake. Je, hakujua alichokuwa akifanya? Alihongwa? Alikuwa akijipendekeza ili apewe udohoudoho tena wa aibu? Si rahisi kujibu swali hili na mengine mengi.
Pili, nilijiuliza bila majibu. Inakuwaje fyatu mzima na akili zake tena mzito kuliko Kabwela anakubali, iwe kwa hiari, kuhongwa, hata kulazimishwa, kujigeuza au kugeuza mdudu. Ili iweje? Kwanini ukubali kuwa mdudu na siyo simba kama unapenda sana kuwa mnyama? Japo wadudu hawafanyi uchangudoa wa kimaadili, kidudu mtu ni changudoa wa kisiasa. Huvi ndiyo njia pekee iliyobaki ya kupata mahitaji, riziki, na ulaji wake? Wewe unamchukuliaje kidudu fyatu huyu? Matumbo yetu yasitufanye tufanyiwe vitu vibaya. Baya zaidi, wanaofanyiwa huu udhalilishaji wana watoi. Sijui wanawafundisha nini watoi wao na wengine?
Tatu, nilifyatuka na kushangaa, kukasirika, kuhuzunika, na kuudhika. Inakuwaje ‘kiongozi’tena wa chama kinachojiita pinzani, kumwacha mgombea wake, tena baada ya yeye kukacha kugombea urahisi, na kumpigia mgombea pinzani? Hivi hawa siyo wanachamana wa siri wanachojidai kupinga wakati wanaunga? Kweli, huyu anaweza kuaminika hata kwa wanyama?
Nne, zaidi ya kiongozi huyu muongo ambaye kwake uongozi ni uongo na uroho, ni nini kama siyo kunguni au kupe mtu? Je, anamdanganya nani zaidi ya kujidanganya mwenyewe akidhani anawadanganya mafyatu? Inasikitisha sina mfano kwa ‘kiongozi’ tena mzito kufanya mambo kikunguni na kikupe.
Tano, tumekuwa tukiwasakama chawa na wale wawafugao tusijue wataibuka hata funza, kunguni, na kupe waje kuturarua na kutuambukiza maradhi kama huyu kupe mtu ninayemjadili leo. Hivi, inakuwaje binadamu mzima mwenye akili timamu, macho, na mikono akatenda kama mdudu na asione aibu wala kuhisi uzito wa dhambi anayojitendea na kuwatendea wengine?
Sita, kinachogomba na kuuma ni ile hali ya mafyatu kufyatuliwa kuwa uchafu na uchafuzi huu nao ni uchaguzi. Uchaguzi gani usio na wapinzani? Uchaguzi gani ambapo vyama ABCD...Z ‘vinashindana’ vyenyewe. Katika mchezo huu mchafu, kinachoumiza zaidi ni kuunguza na kufyatua njuluku za mafyatu kwa viini macho. Si timu itangaze mteule yake badala ya kupoteza muda na njuluku za mafyatu kapuku? Hata hivyo, nisizoze na kulaumu sana. Hapa, wa kulaumiwa ni mafyatu au wanaowafyatua?
Saba, japo ni haki ya mtu kuchagua atatakacho, inakuwaje mja anajigeuza mdudu ili ajaze tumbo lisiloshiba asihofie Mungu na kesho? Je, hapa anayewafyatua mafyatu na mafyatu nani alaumiwe? Huku si kukubali kuliwa kwa hiari yao? Je, wakishafanya na kufanyiwa udhalilishaji huu, watakuwa na haki ya kulalamika au kulaumu? Wamlalamikie au kumlaumu nani wakati yote wanasababisha wao wenyewe kwa kukataa kufyatuka na kufyatua kiasi cha kujiruhusu wafyatuliwe hata na wadudu wasio na akili, maarifa, wala nguvu? Jamani, tunamkomoa nani ili iwe nini na kwanini? Kweli, mafyatu na ufyatu wetu tunashindwa hata kuwapondaponda au kuwasafishia mbali hawa wadudu ambao sasa wanaanza kujifanya hawahusiki na mateso yetu? Inakuwaje wadudu wanaonekana kutuzidi akili hadi tunakubali watufyatue tena kirahisi hivi?
Nashaurini mafyatu kuepuka uchawa, ufunza, ukunguni, ukupe, na ududu kwa gharama zozote. Kwani, mtajikuta pakanga kama kaya. Licha ya kudhalilisha na kuumiza, hali hizi hudumaza ubunifu na uthubutu kiasi cha fyatu mzima kukubali kujigeuza au kugeuzwa jidudu. Shame on you vidudu watu muwe wafugaji au wafugwao. Heri kufa njaa kuliko kukubali aibu, jinai, na shibe hii ya kudhalilishwa na kudhalilisha. Mtaliwa mkijiona. Shauri yenu. Sitaki, siku moja, mseme sikusema wakati nilisema kila mara. Inakuwaje Fyatu mzima anajigeuza au kugeuzwa mdudu?
Chanzo: Mwananchi Jtano leo.
Sunday, 16 November 2025
No longer at ease Tanzania island of peace––––Part three
How and where to start?
Accurate answers:
Practically, the authorities must earmark the parties to the conflict, release all detained opposition leaders, demonstrators, and pardon each other to build trust for reconciliation can start. Thereafter, the authorities must admit mistakes, then move together and move on.
Absolutely, there can’t be any reconciliation without the trio facing each other and telling the truth. The authorities must tell the whole truth and listen to other truths pertaining to the conflict at issue.
What are the root causes?
Demonstrators said clearly that they opposed (and still do) chronic abductions, corruption, despotism, forced disappearances, injustices, joblessness, murders, nepotism, partyism, the absence of the new constitution, and a truly Independent National Electoral Commission (INEC), which all stakeholders should equally and fully participate in its making. Such bottlenecks must be genuinely and practically addressed, and justice should be done and seen done.
Symptomatically, another problem revolves around the abuse of police forces and power and gross human rights violation as recently evidenced in the post-demo brutalities and bloodbaths. Thus, Tanzanians must persecute all the culprits regardless of their affiliations or positions as they immediately release those in custody.
Why fresh elections?
As per regional and international observers, which form the backbone of credible, fair, and transparent elections, there were no elections. They lacked important qualities such as credibility, fairness, peace, and transparency. For example, the Civic Front (CUF), one of at least credible opposition parties issued a scathing report demanding Tanzania to form a transition government that’ll conduct elections thereof since there wasn’t any election. So, too, the SADC observers concluded and reported that Tanzania elections didn’t meet standards. For example, there are reports that there were many more police officers at certain voting stations than voters.
Conclusion
Let’s agree. Tanzania is a horrible catch-22. To survive, the above recommendations, inter alia, must be worked on. Habits sometimes end up being faults. Demystify myths and move on Tanzania japo maji yameishamwagika. Fool me once, shame on me. Fool me twice, shame on you. The jury is still out though.
Epuka na Uogopa Uchoyo katika Ndoa
Binadamu anapaswa kuchunga hata kuepuka sana ubinafsi na uchoyo katika maisha na nyanja zote isipokuwa kwenye tishio la maisha na umilki wa mwenzi wake na mali zake. Tofauti, katika mali, binadamu anaweza kugawa, kuuza, kuhonga, kuazima, hata kuziharibu. Kwenye ndoa na uhai, hana chaguo isipokuwa kuwa mbinafsi na mchoyo. Kwa mfano, kwa wanandoa, ubinafsi tofauti na ulioonyeshwa hapo juu, unatosha kuiyumbisha hata kuihatarisha ndoa. Hakika, wanandoa hawapaswi kuwa na changu katika ndoa bali chetu. Hawapaswi kuwa na mimi bali sisi. Kwa wanaomkumbuka marehemu Malkia Elizabeth wa Uingereza, watakumubuka namna alivyokuwa ameolewa na mume Philip ambaye hakuwa mfalme kama yeye. Hata hivyo, tokana na dhana ya kuchangia na kumilki kila kitu pamoja kwa wanandoa, Malkia alimpandisha cheo mumewe asiyetoka kwenye ukoo wake wa kifalme na kuwa mwana wa mfalme.
Kuna vitu ambavyo wanandoa wanaweza kudharau hata kutokumbuka. Kwa mfano, mmoja kati ya wanandoa kujaliwa kipato kuliko mwenzie. Kama ndoa yako imo kwenye hali hii, basi adui yako namba moja ni mafanikio unayoyaita yako badala ya yenu. Je huwa unasema pesa yetu, gari letu, nyumba yetu au mali zetu au zangu? Je uliishamuuliza mwenzio hujisikiaje unapoonyesha wazi kuwa kila mtu ana chake na siyo chenu kama wanandoa? Kujibu maswali hayo, vaa viatu vya mwenzio au jiweke kwenye nafasi yake. Jiulize ungejisikiaje kama mwenzi wako angeendekeza tabia ya changu badala ya chetu?
Kunapokuwa, na changu na si chetu, basi kuna hatari kubwa kwa wahusika. Tunapoongelea hatari, madhara, na ubaya wa ubinafsi na uchoyo ni hapa. Mali na vitu vyote vinaweza kumilkiwa pamoja na kusiwe na tatizo. Isitoshe, tunaweza kuvitumia kuwasaidia wengine wasio navyo lakini siyo ndoa. Japo ndoa umeikuta na kuifungia hapa duniani, ni tofauti na vitu vingine. Hii ni kwa sababu, hata ulipende lako vipi, huwezi kulala nalo wala kushindwa kuwapa lift wenzako kwa kutumia gari hilo hilo ulipendalo. Hata upende vipi mashamba na wanyama wako, huwezi kulala navyo wala kuvitumia peke yako. Unaweza kuvinunua na kuviuza hata kuviazima kwa wengine. Unaweza kuvigawa hata kuvirithisha. Unaweza kuajili mtu au watu wengine kuvihudumia. Je unaweza kuajiri mtu mwingine kuhudumia mwenza wako awe wa kike au kiume kindoa?
Kwenye ndoa ya kweli, hakuna changu wala chako bali chetu. Hata hivyo, katika mfumo dume, tabia hii mara nyingi huwa nayo wanaume. Utamsikia mtu akisema, “nitakufukuza kwenye nyumba yangu” au “unafanya kiburi utafikiri wewe ndiye uliyejenga nyumba hii! Naweza kukuacha na kuingiza mwanamke mwingine.” Yapo mengi yanayosemwa kuhusiana na umilki wa mali. Kama nyumba yako au gari lako lilikuwa na thamani, kwanini hukuvioa? Kama una haki na jeuri hiyo, kwanini ulipoteza muda hata fedha zako kwenda kumtafuta, tena kwa kumbembeleza, huyo unayemtishia maisha kwa sababu ya vitu? Je hapa tatizo ni ukosefu wa kumbukumbu au ujinga wa kawaida na uroho?
Wednesday, 12 November 2025
Ole wa ‘mafyatu’mamluki waliotufyatua
Niwaonye tena kwa kinywa kipana na herufi kubwa. Komeni na kukomaa kabla hatujawakomesha, mkatokomea, na kukomea kuzimu. Msituzeee. Shauri yenu. Hatuchezi lijapo suala la amani ya imani. Yeyote anayepanga kukinukisha, atanuka yeye baada ya kumfyatua na kumzika hata kwenye makaburi yasiyojulikana. Ajue. Hata wale wasiojulikana wanaojulikana, sorry, wasioweza kujulikana, hawapendi uchochezi na uchokozi huu. Walaaniwe wote waliosababisha haya mambo.
Kaya yetu ni ya amani. Msituletee chuki, migongano, na uzushi wenu. Nani kawaambia tuna shida? Najua. Mnatuonea wivu. Ndiyo maana mnatuzulia kila uongo dhidi. Kuna waliongopa eti uchafuzi, sorry, uchaguzi wetu haukuwa huru na wa haki. Kwanza, unawahusu nini? Ungekuwa hivyo, ‘walioshinda’ wangeshindaje kwa aslimia mia?
Nisisitize. Mafyatu wetu hawawezi kuandamana tokana na kujazwa, sorry, kujaa imani ya amani mbali na kutokuwa na miguu ya kuchezea kwenda kuandamana. Hata uwanyanyase vipi, hawawezi kufanya hivyo. Kabla ya maandamano, hamkusikia mkuu mazeri akisema maandamano yatakuwa ya kwenda kuweka, kutiki, na kuchukua kama ilivyotokea tokana naye kuwa na maono hadi kutabiri matokeo. Wapo wanaodai eti matokeo yalipikwa? Loo! Mlitaka yaokwe au kukaangwa? Wengine waliongopa eti tulizima intanet! Kwanza, hakuna aliyezima intanet bali ilijizima.
Wengine walihoji kwanini tuliapishana haraka tena kwenye uwanja wa mageshi? Ebo! Walitaka tuapishane baada ya mwaka tena mbele ya wahuni kama hawa mamluki? Kwani, kazi ya mageshi ni nini kama siyo kupokea amri na kulinda chochote tena bila kupoteza muda kuhoji au kuwaza?
Wanaongopa eti kuna mafyatu wa kaya yetu waliuawa. Komeni. Sie siyo machizi, mahayawani, mataahira, wala makatili kuuana sisi kwa sisi. Sasa elewa na muamini kama alivyosema mazeri mwenyewe. Waliofyatuliwa wakafa ni mafyatu ya kigeni siyo wetu. Nani awezaye kumuua ndugu yake tena kwenye kaya ya amani?
Hatuna sababu wala shida ya kuandamana au kukinukisha. Kwanza, hatunuki. Pili, tunajivunia na kudumisha amani mshikamano wetu. Tuna demokrasia ya kupigiwa m,fano na iliyotukuka hadi, kama unapendwa, unashinda kwa asilimia mia. Tuna mafyatu wasiowahi hata kuua inzi. Hatuna ufisadi, umaskini, wala ujinga wowote unaowafanya wale mafyatu viumbe waliozoea kuandamana hata akiwanyea kunguru.
Eleweni. Tutailinda amani na mshikamano hata kama itahitaji kumwaga damu ya hawa mafyatu wa kigeni. Kwanza, nani kawambia? Sie siyo mazwazwa tuuane sisi kwa sisi. Sisi sote ni ndugu. Hatuna uchama, udini, ukabila, ueneo, ujimbo, wala chuki baina yetu.
By the way, kuna mafyatu waliwafyatua wasanii wetu kuwa ni wasanii na waongo, woga, na machangu! Kwani, kazi yao ni nini? Kuna mbwa walijiita simba. Kiliponukishwa kikanuka, wakarudia uumbwa wao. Uliona wapi murume akatoga masikio au kuvaa hereni na kuwa na uso kama mwananke akabaki kuwa mrume siyo buabua? Nimesemaje?
Sunday, 9 November 2025
Tanzania the Island of peace in pieces----Part II
There’s chaos in Kenya and Madagascar respectively where former survived after an opportunistic opposition joined the rut to douse fire. In Madagascar, the president was pulled down after soldiers refused to receive and execute stupid orders from above. Realistically, Tanzania had three routes, namely, to do as Botswana, Malawi, and Zambia did or make a fatal decision through Cameroon route ending up stuck in and with the Madagascar route.
Howbeit, Tanzania’s autochthonal abuses, depravity, endemic debaucheries. For instance, public appointments depend on surnames, know whom but not knowhow. Who’d stomach president appointing her son-in-law Minister for supervising elections? How’d such elections make any meaningful sense? Who’d love to hear president’s son being a link to all lucrative deals? That’s a root cause of troubles whereby the elite minority plunders and illicitly amasses wealth while the majority pointlessly suffers from their induced abject poverty.
Essentially, the CCM weirdly veered, stonewalled itself, strangulated all sort of freedoms, and bunged the angers of its people leaving no room for venting.
Essentially, Tanzania’s problems emanate from within. Firstly, when the CCM backed a stringent and workaholic outsider, John Magufuli in 2015, it blindly set itself in the collision course that left it bungled, injured, and moribund. Magufuli, the bulldozer, bulldozed its traditional networks and webs of eaters and movers.
Of all palpable victims is former CCM Ideology and Publicity Secretary and Ambassador to Malawi and Cuba, Humphrey Polepole, resigned and returned home with one mission, to revenge by spilling the beans up until he’s abducted and his whereabouts aren’t known. Polepole got the ball rolling, His exposes weren’t only daring and damaging but were religiously believed at face value. Instead of seizing this opportunity to seek to know how much Polepole knows, the CCM floundered and squandered this opportunity.
In a word, Tanzania was, and sadly, still is ripe for unrests shall all enumerated anomalies go be poo-poohed and unattended. The jury is still out. Thus, what those who haven’t faced the wrath of the browbeaten must quickly change.
Source: Daily Monitor today Sunday.
Jilaumuni kuwajengea watoto mazingira ya kuwalaumu
Leo, tutaongelea kitu ambacho tumekishuhudia kwa wengi. Tunajua fika. Siku hizi sawa na zamani, kila mzazi anataka awape watoto wake elimu bora. Je, ni wazazi wangapi wanajua maana ya elimu bora? Ni wangapi wanaweza kutofautisha elimu bora na bora elimu ambayo siku hizi imetawala? Ni wangapi wanafuata ughali wa shule na kuibiwa fedha zao na kuishia kujuta hata kuwalaumu watoto wamalizapo wasifikie malengo au matarajio ya wazazi?
Tutaanza na kisa cha mzazi mmoja msomi na tajiri. Huyu jamaa alisoma shule za Kayumba au zisizo bora kwa vigezo vya sasa vya kibepari. Hivyo, alijiapiza kuwa hatataka watoto wake wasome shule alizosomea yeye. Je, wako wazazi wangapi wa aina hii? Utamsikia mzazi akisema “sitaki wanangu wasomee shule nilizosomea wala kuishi maisha niliyoishi.” Kwa wajuzi, unashangaa. Maskini mhusika hajui kuwa ni maisha hayo hayo yaliyokufanya awe alivyo. Ni tofali gani laweza kufaa kujengea bila kupitia kwenye tanuri la moto? Ni dhahabu gani yaweza kuwa kito bila kupitia kwenye tanuri?
Wapo wazazi tena wengi wanapoteza fedha nyingi kuwasomesha watoto wao si kwa sababu ya ubora wao bali ughali na’usasa’ wa shule husika. Siku hizi, kuna English Medium na International Schools nyingi tu. Ajabu, wengi wa wanaomaliza shule hizi hata hicho kimombo hawakimudu uzuri hata wakikimudu, hawana stadi za maisha wala hawakidhi matarajio wala vigezo.
Ukiachia elimu, utamsikia mtu akisema “sitaki kufa bila kuwaachia watoto wangu urithi.” Ukimuuliza amaanishacho, anakwambia lazima awaachie majumba hata mashamba! Vya nini? Wao watajitafutia lini? Wengi wanaofanya hivyo hawakurithi chochote toka wa wazazi wao. Wako tayari kuibia kudhulumu hata kuuibia umma ili kuwaachia watoto urithi ambao wanaweza kuufuja hata kuuana wakiugombea. Kwani, kama utawafanyia kila kitu, akili na nguvu zao walizojaliwa watazifanyia nini?
Kama unaweza tena kihalali na kuwaandaa watoto wako si vibaya. Hata hivyo, wangapi wameacha utajiri lukuki kwa watoto wakaishia kuuvuja hata wengine kuuana kwa ajili yake? Chui na simba wana somo kubwa la maisha. Wazaapo watoto, huwalisha hadi wanapokua na kuanza kung’amua mambo. Kuhakikisha wanaweza kuishi bila kuwa tegemezi, huwafundisha kuwinda, kazi hatarishi na ngumu. Wanyama hawa, hukamata wanyama na kuwajeruhi halafu huwapo watoto wao wamalizie ili kujihakikisha kuwa wamefuzu tayari kuanza kujitegemea.
Kwa watoto wasio na maarifa wala uzoefu, kumalizia mawindo waliyoletewa na wazazi wao ni kazi hatari, ngumu, hata ya kuchukiza kwao. Mwanzoni, watoto huchukia na kuwaangalia wazazi wao wawasaidie nao wasiwasaidie. Taratibu, tokana na kuachiwa yale mawindo hai tena wakiwa na njaa, watoto hufuzu kwa kuwaangusha hata kuwaua wale wanyama walioletewa. Baada ya hapo, wazazi huanza kuandamana na watoto ili waone namna chakula kinavyotafutwa.
Je, ni wazazi wangapi wanawafundisha Watoto kazi walizofanya zikawafikisha walipo? Ni wangapi wako tayari kuwaudhi watoto wao kwa kuwaletea mawindo hai ili wamalizie? Kama humfanyi hivyo, mna sababu yoyote ya msingi kuwalaumu watoto ambao hamkuwaandaa au mliwaandaa vibaya? Je, hapa nani wa kumlaumu nani na kwanini?
Sasa nini kifanyike?
Mosi, wazazi wajue. Mambo yamebadilika tena sana. Hivyo, nao wabadilike kuendana na mahitaji na wakati vilivyopo.
Pili, wajue aina na nyakati za maisha ya watoto wao ni tofauti na zao.
Tatu, waanze kuwaandaa na si kuwaandalia maisha ya baadaye kwa kujifunza tokana na maisha yao wenyewe.
Nne, wasipeleke watoto shule tu bali wajue aina za shule na elimu wanakowapeleka na nini matarajio na matokeo yake.
Tano, kabla ya kuwalaumu Watoto, wazazi wajichunguze kuona ni wapi wamechangia katika kile kinachofanya wawalaumu watoto ambao nao kadhalika, wanawalaumu wazazi.
Sita, wazazi waache mashindano na miigizo katika kuwaandaa watoto wao. Mfano, wapo wazazi wanaowapeleka watoto kwenye shughule za bweni wakiwa wachanga kiasi cha kuwanyima fursa ya kukua na kufaidi utoto wao. Wengine wanawapeleka kwenye shule aghali kwa vile majirani au ndugu zao wamefanya hivyo, au wameambiwa au kusikia matangazo ambayo mengi ni ya uongo tu. Kwa tuliosomea matangazo, si chochote bali kitatange yaani, truth in adversement is an oxymoron.
Mwisho, msipoteze fedha zenu na muda wa watoto wenu kwa kuwaandaa visivyo na mkategemea mafanikio na kuishia na maanguko.
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.
Wednesday, 5 November 2025
Kumbe Mafyatu waweza kufyatuka na kufyatua wawafyatuao!
Haiwi haiwi, huwa na imekuwa! Si Nepali na Madagascar mafyatu walifyatuka na kufyatua kikaumana! Nani alitegemea mafyatu waliodhaniwa kutoweza kufyatuka au kufyatuliwa wangefyatuka na kufyatua wafyatuzi?
Watani wao waliwaita maiti. Hawakujua wangeweza kufufuka na kufyatuka wakawafyatua wawafyatuao! Hili liwe somo hata kama ni la kifyatufyatu. Hakuna aliye salama kama mafyatu watafyatuliwa wakafyatuka na kufyatua.
Huwa sipendi fujo wala dhuluma. Ni mpenzi kindakindaki wa haki ya kweli. Sipendi maigizo wala sanaa. Nachukia ngonjera, nyimbo, na mashairi vya sifa uchwara ilhali mafyatu wanafyatuliwa na matatizo yanayoepukika.
Fyatu ana nini hadi asifiwe na apende na kuridhika na kusifiwa? Waweza kuchukiwa na kusutwa hata kupondwa ukahadaika wapendwa. Hapendwi fyatu hapa. Ukiona mafyatu wanakupenda, jua kuna kitu wanataka kwako. Wakikusifia ukakubali, kubali na kupondwa ukubali hata kuchukiwa. Hayo tuyaache.
Leo, nitafyatua kisa cha Mafyatu waliofyatuka na kuwafyatua wawafyatuao huko kaya jirani ya Madagascar na Nepali hadi dunia ikafurahi, kushangaa, na kuogopa. Walidhani hawawezi kufyatuka na kufyatua.
Mafyatu si mawe yasiyobadilika. Ni wajanja usipime. Wanaweza kujifanya hawafyatuki wala kufyatuliwa ilhali wakipima situations na kudurusu namna ya kufyatuka lau kijulikane pale wafyatukapo wakafyatua kama walivyofyatua mafyatu wa Madagascar hadi dogo akakimbia ulaji wake kinomi. Sasa ishakuwa.
Nashauri tuache kuishi kwa mazoea tukijipa matumaini ilhali hali ni tete tokana na onyo dhahiri walilotoa mafyatu kuwa wakizidiwa, wanaweza kufyatuka na kuwafyatua wawafyatuao ambao wamepigwa na bumbuwazi wasiamini macho na masikio yao. Tujifunze toka kwa wenzetu.
Sasa nini kifanyike?
Jibu ni simpo. Wawafyatuao mafyatu wawajibike na kuonekana wakiwajibika kwa kuwatenda haki kabla ya mafyatu hawajafyatuka au kufyatuliwa zaidi na kufyatua zaidi. Wasikilizeni mafyatu na kujua matatizo yao ambao hata kuku wanayajua. Wawezeshe mafyatu badala ya kuwafyatua au kujifyatua akili kuwatisha mkidhani wanatishika wasifyatuke na kufyatua. Mafyatu wakifyatuka, huwa hawazuiliwi wala kufyatuliwa. Ukapuku umezidi ilhali waneneo wawafyatuao mafyatu wakizidisha ukwasi utokanao na ufyatuaji wa haki zao.
Nini kifanyike?
Ufyatuaji na matumizi mbaya ya mali na njuluku za umma vikomeshwe mara moja. Wajibikeni. Mjue, kama nyinyi, kila fyatu anataka amani na ufanisi. Je, amani yawezekana bila kutenda haki? Tendeni haki. Haki huleta amani na upendo, tofauti na dhuluma na ufyatuaji wa mali na njuluku za mafyatu huwafyatua mafyatu wakafyatuka na kuwafyulia mbali wawafyatuao.
Si mmeona wenyewe walivyofyatuka hadi kikataka kunuka pale jirani? Wanene walijifyatua wakatuma ndata kuwafyatua nazo zikafyatuka na kuacha kuwafyatua mafyatu na kuwaacha wawafyatue wanene wao. Je, hii maana yake ni nini? Jibu ni simpo. Mafyatu waliodhaniwa kufa wamefufuka na kufyatuka hadi kuanza kufyatuana na wale wasiofyatuliwa ambao kazi yao ni kuwafyatua mafyatu na mali na njuluku zao.
Ushauri wa bure
Mafyatu wakifyatuka, wote tutafyatuwana na kufyatuliwa. Hakuna fyatu au fyatuzi wala fataki atapona katika mfyatuko huu. Mafyatu weshazoea maisha ya kufyatuliwa. Hivyo, wakifyatuka au kufyatuliwa na kufyatua, watakaoumia ni wale ambao hawajazoea ufyatu isipokuwa kuwafyatua mafyatu wasijue nao wanaweza kufyatuka na wakafyatua kama walivyofyatua tena kwa kuchovya tu.
Nini zaidi kifanyike?
Wanene wawafyatuao mafyatu waache kiburi na kujidanganya kuwa mafyatu hawawezi kufyatuka wakawafyatua wakati ni rahisi kuwafyatua wakafyatuka na kufyatua hata kaya kwa ujumla. Mafyatu si mazwazwa. Ni wajanja. Wanajua mambo mengi. Wanajua nani alifyatua nini na ameficha wapi. Jiulize. Kwanini baadhi za mali mafyatuzi zimefyatuliwa. Wangezijuaje kama wasingekuwa wanajua? Usione mtego umeinama ukajifyatua na kukadhani hauwezi kufyatuka ukakufyatua. Mafyatu ni kama mtego ulioinama ukingoja kufyatuka au kufyatuliwa halafu ukafyatuke na kufyatua.
Kipi kifanyike?
Lipo la kufanya. Nalo, ni kuacha kuendelea kuishi kwa mazoea na kujifyatua ufahamu kwa kujipa matumaini yasiyokuwepo. Ukiona mwenzio kanyolewa, tia maji. Tujue hata kwa kulazimika kuwa mafyatu ni kama volcano. Huwa haifi bali hulala au kulazwa. Ila hufyatuka au kufyatuliwa ikafyatua na kufyatuka. Suala hapa si ni kama bali lini itafyatuka na kufyatua. Je, itafyatuka na kufyatua lini na vipi? Si rahisi kujua.
Hivyo, ajidanganyae na kuandaa mauti yake ni yule ajifyatuaye na kuifyatua ikafyatuka ikamfyatua bila na wakati asiotegemea. Kadhalika, Mafyatu wakiamua kuwafyuka au hata kufyatuliwa, ni wazi. Hakuna wa kuwazuia wala kuwafyatua. Kama volcano, watafyatuka na kufyatua tu na kuwaacheni majeruhi mkiwa mmefyatuliwa vilivyo bila kuamani.
Chonde chonde
Msijifyatue na kuifyatua volcano mkadhani mtaifyatua isiwafyatue mkafyatukia mbali. Kadhalika, mtawafyatua mafyatu waliofyatuka wawafyatue bure. Watawafyatua vibaya sana. Mjue. Kizazi fyatu cha sasa kina hasira. Chochote na yeyote na wakati wowote chaweza kufyatuka au kufyatuliwa kikafyatua wafyatuzi. Kwani, hakina cha kupoteza zaidi ya kuandika historia fyatu mpya na mbaya. Huwa siku zote nafyatua kuwa kuna siku tutafyatuana. Si yamefyatuka na kutimia! Naonya tena. Mafyatu wamefyatuka. Wawafyatuao wajiandae kufyatuliwa zaidi. Kumbe visa yangu ya kuishi Madagascar imeisha! Ngoja nijifyatue kabla hawajanifyatua.
Chanzo: Mwananchi Jtatu leo.