Ni wazazi wachache wavunao walichopanda toka kwa watoto wao. Hii inasababishwa na mambo mengi yakiwamo malezi, nyakati, na hata ujiga. Kila mzazi anataka watoto wake wafanikiwe kuliko hata yeye. Hivyo, anatoa kila kiwawezeshacho hata kwa kutojiwezesha asijue matokeo yanaweza kuwa kinyume. Hatupendi kuwakatisha tamaa wazazi. Ila wajue. Mambo yanabadilika. Hivyo, tunapaswa kuyakubali mabadiliko na kubadilika.
Leo, tutaongelea kitu ambacho tumekishuhudia kwa wengi. Tunajua fika. Siku hizi sawa na zamani, kila mzazi anataka awape watoto wake elimu bora. Je, ni wazazi wangapi wanajua maana ya elimu bora? Ni wangapi wanaweza kutofautisha elimu bora na bora elimu ambayo siku hizi imetawala? Ni wangapi wanafuata ughali wa shule na kuibiwa fedha zao na kuishia kujuta hata kuwalaumu watoto wamalizapo wasifikie malengo au matarajio ya wazazi?
Tutaanza na kisa cha mzazi mmoja msomi na tajiri. Huyu jamaa alisoma shule za Kayumba au zisizo bora kwa vigezo vya sasa vya kibepari. Hivyo, alijiapiza kuwa hatataka watoto wake wasome shule alizosomea yeye. Je, wako wazazi wangapi wa aina hii? Utamsikia mzazi akisema “sitaki wanangu wasomee shule nilizosomea wala kuishi maisha niliyoishi.” Kwa wajuzi, unashangaa. Maskini mhusika hajui kuwa ni maisha hayo hayo yaliyokufanya awe alivyo. Ni tofali gani laweza kufaa kujengea bila kupitia kwenye tanuri la moto? Ni dhahabu gani yaweza kuwa kito bila kupitia kwenye tanuri?
Wapo wazazi tena wengi wanapoteza fedha nyingi kuwasomesha watoto wao si kwa sababu ya ubora wao bali ughali na’usasa’ wa shule husika. Siku hizi, kuna English Medium na International Schools nyingi tu. Ajabu, wengi wa wanaomaliza shule hizi hata hicho kimombo hawakimudu uzuri hata wakikimudu, hawana stadi za maisha wala hawakidhi matarajio wala vigezo.

Wengi hawalioni hili hadi liwakute. Unampeleka shule ya kimataifa kufanya nini wakati hataishi kimataifa bali kitaifa? Kwanini kumfundisha mtoto habari za udongo wa mwezini na si wa aishipo wakati hataishi huko?
Ukiachia elimu, utamsikia mtu akisema “sitaki kufa bila kuwaachia watoto wangu urithi.” Ukimuuliza amaanishacho, anakwambia lazima awaachie majumba hata mashamba! Vya nini? Wao watajitafutia lini? Wengi wanaofanya hivyo hawakurithi chochote toka wa wazazi wao. Wako tayari kuibia kudhulumu hata kuuibia umma ili kuwaachia watoto urithi ambao wanaweza kuufuja hata kuuana wakiugombea. Kwani, kama utawafanyia kila kitu, akili na nguvu zao walizojaliwa watazifanyia nini?
Kama unaweza tena kihalali na kuwaandaa watoto wako si vibaya. Hata hivyo, wangapi wameacha utajiri lukuki kwa watoto wakaishia kuuvuja hata wengine kuuana kwa ajili yake? Chui na simba wana somo kubwa la maisha. Wazaapo watoto, huwalisha hadi wanapokua na kuanza kung’amua mambo. Kuhakikisha wanaweza kuishi bila kuwa tegemezi, huwafundisha kuwinda, kazi hatarishi na ngumu. Wanyama hawa, hukamata wanyama na kuwajeruhi halafu huwapo watoto wao wamalizie ili kujihakikisha kuwa wamefuzu tayari kuanza kujitegemea.
Kwa watoto wasio na maarifa wala uzoefu, kumalizia mawindo waliyoletewa na wazazi wao ni kazi hatari, ngumu, hata ya kuchukiza kwao. Mwanzoni, watoto huchukia na kuwaangalia wazazi wao wawasaidie nao wasiwasaidie. Taratibu, tokana na kuachiwa yale mawindo hai tena wakiwa na njaa, watoto hufuzu kwa kuwaangusha hata kuwaua wale wanyama walioletewa. Baada ya hapo, wazazi huanza kuandamana na watoto ili waone namna chakula kinavyotafutwa.
Je, ni wazazi wangapi wanawafundisha Watoto kazi walizofanya zikawafikisha walipo? Ni wangapi wako tayari kuwaudhi watoto wao kwa kuwaletea mawindo hai ili wamalizie? Kama humfanyi hivyo, mna sababu yoyote ya msingi kuwalaumu watoto ambao hamkuwaandaa au mliwaandaa vibaya? Je, hapa nani wa kumlaumu nani na kwanini?
Sasa nini kifanyike?
Mosi, wazazi wajue. Mambo yamebadilika tena sana. Hivyo, nao wabadilike kuendana na mahitaji na wakati vilivyopo.
Pili, wajue aina na nyakati za maisha ya watoto wao ni tofauti na zao.
Tatu, waanze kuwaandaa na si kuwaandalia maisha ya baadaye kwa kujifunza tokana na maisha yao wenyewe.
Nne, wasipeleke watoto shule tu bali wajue aina za shule na elimu wanakowapeleka na nini matarajio na matokeo yake.
Tano, kabla ya kuwalaumu Watoto, wazazi wajichunguze kuona ni wapi wamechangia katika kile kinachofanya wawalaumu watoto ambao nao kadhalika, wanawalaumu wazazi.
Sita, wazazi waache mashindano na miigizo katika kuwaandaa watoto wao. Mfano, wapo wazazi wanaowapeleka watoto kwenye shughule za bweni wakiwa wachanga kiasi cha kuwanyima fursa ya kukua na kufaidi utoto wao. Wengine wanawapeleka kwenye shule aghali kwa vile majirani au ndugu zao wamefanya hivyo, au wameambiwa au kusikia matangazo ambayo mengi ni ya uongo tu. Kwa tuliosomea matangazo, si chochote bali kitatange yaani, truth in adversement is an oxymoron.
Mwisho, msipoteze fedha zenu na muda wa watoto wenu kwa kuwaandaa visivyo na mkategemea mafanikio na kuishia na maanguko.
Chanzo: Mwananchi Jpili leo.

No comments:
Post a Comment