Juzi, baada ya kuupiga mma na ndumu kisawasawa si nikalikoroga likakorogeka, kunikoroga, na kuwakoroga Mafyatu wangu niliodhani mafala nisijue wananiona vivyo hivo! Kama munene wa Fyatuland, nilimtuma kiherehere wangu atangaze sera mpya.
Kwanza, nilitoa matangazo kuwa ningetoa taarifa muhimu utadhani nilikuwa nikiunda tume, sorry, timu ya kuchunguza timu ya kujichunguza na kuwafyatua mafyatu! Mafyatu waliganda runingani wakitegemea madini. Si waliambulia hasira na pumba. Kiherehere huyu aitwaye Aliyejuu
Mngojeeechemba,bila hata kufikiri na kuchanganya na zake, alizoza. “Mhesimiwa, Mtakatifu, Mtukufu, Msafi, Mpenda Mafyatu, Profesa Emeritus, Field marshal, Jenero, Mwanafalsafa, Muona Mbali, Mpendwa, Mwenye Udhu, Doktari Fyatu Mfyatuzi kanituma niwaletee habari njema. Kuanzia leo, tutaondoa sharia zinazotipa uwezo kutwaa mali na njuluku zilizopigwa ili kuwapa Mafyatu fursa na motisha kutengeneza njuluku bila kujali namna walivyofanya. Huu ndiyo unaitwa bora utawala bora.”
Kiherehere wangu alisema mambo mengi. Maskini, hakujua kuwa Mafyatu weshafyatuka. Ukiwafyatua, wanafyatuka na kukufyatua. Hata usipowafyatua, wanajifyatua na kukufyatua. Baada ya kiherehere kufanya kiherehere na kujifanya hamnazo, si nimezinyaka kuwa Mafyatu wanataka kufyatuka na kunifyatua na walaji wenzangu. Wanasema, mara hii, kitaeleweka hata kama hakieleweki. Wanataka kuzuia jinai ambayo niliyotaka kutenda na kuhalalisha.
Kwa tishio hili, nimeamuru wasiojulikana, lazima kijulikane. Natangaza rasmi. Yeyote asiyejipenda aingie mtaani ajue kilichowanyima ndege meno. Sikubali ufyatu huu kutaka kunifyatua nisifyatue? Sijui kwanini mafyatu wana akil ndogo kama kuku. Mnapewa fursa kupiga njuluku ndefu mnajifyatua ufahamu kama amfahamu dili zima!
Mifyatu kwa umbea na urongo, sina mfano. Si yapo Mafyatu yenye ntima nyongo na wivu yaliyodai eti sie wanene tumefyatua sana mali na njuluku za Mafyatu. Hivyo, tunajiwekea kinga iwapo siku moja tutafyatuliwa na kujikuta nje ya ulaji tupate pa kuangukia. Nani kawaambia? Yapo mafyatu yaliyokufuru yakidai eti katiba tukufu ya Fyatuland irekebishwe kuondoa kipengele kinachozuia Mafyatu kunifyatua mimi kama kiongozi wao. Hivi, kweli hawa wana akili? Sasa yakiondoa kipengee hiki hayajui kuwa Fyatuland itaingia kwenye machafuko tokana na wapenzi wangu kuchukizwa na kutishiwa na hila hii ya kifyatu? Mnataka wanene tule wapi? Mnataka mali zetu nasi na vitegemezi, na vigegemezi vya vitegemezi na maswahiba zetu vilindwe na nini dhidi ya kufyatuliwa na mafyatu wanaougua ugonjwa wa kufyatufyatuka hovyo?
Nilishawaonya Mafyatu kuwa Fyatuland ina wenyewe na wenyewe ni sisi. Sijui kwanini hawa Mafyatu hawaelewi inshu nzima! Kweli viumbe hawa wamelaanika sina mfano. Mliona wapi kiongozi wa kaya kama Fyatuland kushitakiwa kikatiba? Pamoja na Mafyatu kujifanya hamnazo, nina mpango mzuri wa kuwalinda Mafyatu wote. Mfano, kama kuna Fyatu atakayejiingiza kwenye ujambazi, uuzaji mihadarati, utakatishaji wa njuluku, na mengine kama haya, lazima mali na njuluku anazoita zake tuzitwae ili akome na kukomaa na kuacha uzwazwa na apigaji wa njuluku za Mafyatu.
Napanga kutoa elimu ya uraia ambayo itawapa ujuzi Mafyatu wa kutofautisha upigaji wa kalamu na ule wa silaha. Pia, lazima wajue kuwa kuna tofauti kati ya upigaji wa kisiasa na visasi. Hivyo, nikiri kuwa kiherehere wangu alikosea. Niliposema tufute sharia ya kutwaa njuluku zilizopigwa au kupatikana kiharamu, naamaanisha wale wasio wanasiasa. Kwanini Mafyatu hawajui kuwa siasa bila ‘kazi na dawa’, Fyatuland itakosa Mafyatu mahiri wa kuiongoza.
Inabidi Mafyatu waelimishwe na kuelimika. Wajue kuwa si kila ujambazi ni ujambazi. Upo uliohalalishwa na ule ulioharamishwa. Mbona wachunaji, sorry, wachungaji wanakunywa maziwa na kula nyama toka kwenye kundi la kondoo wao hamzozi? Kuongoza Fyatuland ni kazi kubwa inayompasa mwenye kuibeba kuwa na ukwasi ili asiaibishe kaya pale anapokutana na wanene wenye ukwasi wa kaya nyingine. Mfano, kiongozi wa Fyatuland, hapaswi kuonekana au kuwa kapuku. Akiwa hivyo, wachukuaji, sorry, wawekezaji, hawataweza kumwamini na kuwekeza. Hapa ndipo inapokuja diplomasia ya uchumi. Ili kuwashawishi wawekaji wawekao na kuchukua waa, lazima wanene wawe wananuka na kuonyesha ukwasi wa kufa Fyatu.
Hii inatokana na ukweli kuwa, ili kuwanasa wawekaji, lazima ufanane nao. Wao, wanakuja na njuluku, wengine mikoba mitupu na kuondoka na njuluku zaidi toka kwenye shamba la bibi, sorry, Fyatuland. Nimesemaje? Namaanisha kaya makini yenye kiongozi makini Fyatu Mfyatuzi mwana wa Mfyatuko mjukuu wa Mfyatuliko.
Huwezi kuvutia watega uchumi na wawekaji kama unanuka ukapuku. Lazima uwe na kila alama na sura za ukwasi. Njuluku huleta njuluku. Ukwasi huleta ukwasi. Uongo, sorry, uongofu huleta uongozi. Nani anaweza kumwamini kapuku akawekeza kwake? Si atajiuliza. Kama hawa uchumi wanao lakini wanaukalia, nitajuaje kama hawatakalia njuluku zangu. Lazima kuongoza kwa mfano. Ukitaka kaya yako itajirike, lazima ujitajirishe mwenyewe kwanza ili wengine waone na kuiga. Hii ndiyo sababu ya kutaka kuondoa sharia ya utwaaji njuluku za wanene.
Du! Hii gongo na mibangi, we acha tu. Badala ya kumwaga pwenti, tazama nimwaga pumba. Dharau kila kilichoandikwa hapa. Nilikuwa naota tu.
Chanzo: Mwananchi Leo Jumatano.

No comments:
Post a Comment