The Chant of Savant

Saturday 3 April 2010

Tumuunge mkono Mpendazoe



Mbunge wa zamani wa Kishapu Fred Mpendazoe amefungua pazia. Ameamua kukung'uta vumbi toke kwenye laana akiiacha laana mlangoni mwa CCM. Ametupa faida moja kubwa kusema kuwa alikuwa akiishi kwa matumaini yasiyokuwapo. Pia alihitimisha shutuma kuwa serikali ya sasa ni fisadi kutokana na kuwa tunda la pesa ya wizi na ufisadi na uchafu wa kila aina. Watanzania tusiwaangushe wazalendo walio tayari kujitoa mhanga kutetea maslahi ya taifa letu.
Tuchukue fursa hii kumpongeza Mpendazoe na kuwapa changamoto wale wote waliotuaminisha kuwa ni wapambanaji dhidi ya ufisadi. Wakati wa kujitoa ni sasa na pia kuonyesha matendo badala ya maneno.
Pia nawakaribisha kusoma kitabu changu cha SAA YA UKOMBOZI ili muone utabiri wangu juu ya kuporomoka kwa himaya chafu itokanayo na ujambazi wa EPA.
Pia Mpendazoe alinifurahisha aliposema CCM imevamiwa na wafanyabiashara mbwamwitu wanaoitumia kupata madaraka ili kuendelea kutuibia na kuficha uchafu wao. Hapa nadhani ndipo ilipo siri ya kuwa na watu kama Mohammed Dewji,Nazir Karamagi, Andrew Chenge na wengine waliohujumu taifa letu. Kesho msishangae kusikia Idris Rashid akigombea ubunge bila kusahau Yusuf Manji na wezi wengine.
Hakika hatua ya kishujaa ya Mpendazoe ni changamoto na suto kwa akina Samuel Sitta, Dr. Harrison Mwakyembe, Anne Kilango Malecela, John Malecela, Lucas Selelii, Eng. Manyanya, William Shelukindo na kundi lao.
Kila la heri mwana mwema na shujaa na mzalendo wa kweli FREDRICK MPENDAZOE.
Hakika CCM si mama wa yeyote aliasa MwL. Julius Nyerere.

No comments: