Delonising Education

Delonising Education

Saturday, 30 September 2017

Kujenga uzio ni kumaliza tatizo la 'danganyikanite'....?

Watasha husema kuwa ukiwa na nyundo, kila kitu hugeuka msumari. Hivi karibuni walevi walishangilia sana kabla ya kushangaa na kujishangaa baadaye baada ya wataalamu kutoa maangalizo yao. Hii ni baada ya munene kutangaza kuwa kule kwenye machimbo yam awe aina ya Danganyikanite kuzungushiwe uzio as soon as possible ili kupambana na upigaji.  Japo hii ni strategy poa, je ndiyo jibu au jipu wakati wapigaji wengi wanakuwa ndani ya uzio huo huo wakifanya vitu vyao chini ya mgongo wa kuajiriwa? Nani mara hii amesahau wataalamu tuliowaona mbele ya pilato juzi wakishitakiwa kwa kutumia utaalamu wao kuwasaidia wapigaji wa almas kule Maganzo na Mwadui kwa ndugu zangu akina Nkwingwa na Ngw’adira? Je hapa tatizo ni nini? Kwa vile mimi nimesomea masuala ya intelligentsia na usalama, nitatoa angalizo langu la kitaalam.
            Kwanza, unapojenga uzio kwenye kichwa unaweza kudhani kila tatizo linahitaji uzio na si mifumo huru yenye kuweza kuzuia maovu kama vile Katiba Mpya na sheria nyingine. Ndiyo maana unaweza kuondoa wapigaji aina moja ukaweka wapigaji aina nyingine. In simple parlance, kwani hao ndata si walevi? Je mipaka nayo mtaweka nyuzio?  Unapojenga uzio, ni rahisi kuwapa nafasi maadui bila kujua kuwa unafanya hivyo. Mfano, unapoweka watu wako wasioguswa kama vile kibashiteshite, wakiamua kukutumia, na of course lazima wakutumie, unajikuta pakanga bila kutegemea. Muulize mzee Mchonga. Alipotangaza ujamaa, akadhani waliokuwa wamemzunguka walikuwa wajamaa. Kustuka, kumbe alikuwa amezungukwa mbwa mwitu na fisi pamoja na utaua wake usiopigiwa mfano.
            Pili, tunapopanga kujenga uzio, kuna mambo fulani fulani tunayopaswa kuzingatia. Mfano, je upigaji wote husaidiwa na kutokuwepo uzio au husukiwa kwenye ofisi zetu? Nitatoa mfano mdogo kuhusiana na wizi wa fedha ama benki au zinapokuwa zikipelekwa au kutolewa benki. Wapigaji lazima kwanza wawe na mtu wao wa ndani anayewapa data zote ili wapange ni wapi pa kutekelezea mpango mzima.kwa vile benki kuna uzio na vya moto vingi, huwa wanavizia njiani au kuingia kwenye benki wakati ambapo walinzi hawako chonjo au kuhakikisha wenye funguo za sefu wapo ndani ili wakiingia wawateke na kuwalazimisha kufungua sefu.  Mbali ni hiyo, ukitaka kujua namna uzio usivyo big wala real deal rejea namna wanaharamu fulani wa ndani wakishirikiana na wa kigeni walivyoweza kupitisha twiga uwanja wa ndege tena mchana kweupe.
            Ushahidi kuwa uzio si muarobaini uko kila sehemu. Rejea namna wakora walivyofanikisha kuinigiza vichwa vya treni bandarini mchana kweupe na kutoweka. Hapa hujagusia upigaji uliokuwa umetamalaki bandari ambapo scanners ziligeuzwa mapambo. Rejea jinsi bwimbwi lilivyokuwa likipitishwa hivyo kwa staili hiyo hiyo ya kugeuza scanners scammers. Kwani bandari na viwanja vya ndege havikuzungushiwa nyigo? You know what I mean.
            Je kutokana na ukweli kuwa uzio si jibu wala muarobaini, nini kifanyike? Mlevi anashauri mtunge sheria za kiwajibikaji ambapo kila mlevi atapaswa kueleza namna alivyopata ukwasi wake; na kama akishindwa kutoa maelezo, adakwe na kuswekwa ndani huku ukwasi husika ukitaifishwa. Mzee Mchonga aliweza kujenga mashule, hospitali, zahanati na viwanda walivyoharibu waliomfuatia si kwa miujiza bali kutunga sheria na kuendesha mfumo kama huu.
            Pili, jenga mifumo inayoweza kubaini ufisadi ambapo walevi watapewa jukumu kisheria kuripoti kila ukwasi au ufisadi pale wanapoushuku Rejesha kale ka mchezo ka Mzee Mchonga ka kuchongeana unapohgisi kuna mtu anapiga njuluku za umma. Huwezi kuwa na jamii ambayo inaruhusu mlevi kulala maskini na kuamka tajiri ukazuia ukwasi. Kimsingi, rejesha sheria ya maadili ili ipambane na madili ambapo kila mlevi lazima awe anatangaza kipato chake kila mwaka.
            Kukomesha ubishi na kukata mzizi wa fitina, lisilikali liwe na mamlaka na lihakikishe; linawachunguza wafanyakazi wote waliowahi na wanaofanya kwenye sehemu nyeti za upigaji kama vile TRA, viwanja vya ndege, bandarini, mipakani na wizara husika tena wengi walioajiriwa kidugu.
            Mwisho kabisa, wanene wanaposhughulikia kadhia hii ya upigaji, wahakikishe hakuna kulindana kama ilivyotokea kwa wanene waliobariki upigaji kwa miaka mingi wao wakiwa wanatanua ughaibuni au kujitwalia baadhi ya mali kama vile machimbo ya makaa ya mawe ya kule Kiwila kwa akina Twambombo tununu. Pia epuka upendeleo kama ulioonyeshwa kwa baadhi ya watuhumiwa wa kughushi hadi zoezi zima likauawa kwa sababu ya wahalifu wachache wenye connection na wanene kibashiteshite kiasi cha kutoguswa. Kwa leo naishia hapa. Kama ni msaada nimewapa bure.
Chanzo: Nipashe J'mosi leo J'mosi.

No comments: