How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Friday 4 October 2024

Barua ya Wazi kwa Waziri, IGP, na Bosi wa TISS


Wapendwa,
Kwanza, nimshukuru mhe. Rahis kwa kuwapa muda mjitafakari na kufanya maamuzi kabla hajawawajibisha kuliko tumuwajibishe tokana na ushauri wangu. Sijawahi kuwasiliana nanyi. Hii ni mwanzo hadi kieleweke. Kwa uchungu, japo kichizani, nina hisia, mapenzi, maoni, mawazo, na haki kama nyinyi. Naomba niwaulize maswali yafuatayo nikiwakilisha mafyatu kama kiongozi wao:
            Kwanza, mna hisia kama machizi mnaowaangusha? Je mnaonaje hii jinai, kadhia, na kashfa isiyoisha ya utekaji, upotezaji, ufungaji, na uuaji wa mara kwa mara­­­–––kama wahusika, mnaionaje? Kama mnaifahamu na kuelewa, mmefanya nini kutatua na kukabiliana na janga hili? Mwajua wajibu wa nyadhifa zenu? Kama wazito, nini kazi yenu? Mmechukua hatua gani? Je nafsi zenu huwa zinawasuta? Wanaotekwa kupotezwa wangekuwa watoto, wake, ndugu, hata wakubwa zenu mgefanya nini? Mmewahi kuvaa viatu vya wahanga na wapendwa wao lau kihisia? Je, mmeshindwa tatizo hili, kwanini? Nini kifanyike kwa nafasi na nafsi zenu? Mnajua maana ya neno kuwajibika au mnangoja kuwajishwa? Kama hamjui, makelele na mashinikizo na ushauri vya bure kufanya maamuzi magumu mnavisikia na kuvielewa au la? Kama hamvielewi, kwanini? Kama mnavielewa, mmefanya nini au kwanini? Msaada gani mngetaka wahanga na umma wa machizi wahanga wawape kuepusha aibu kwenu, taifa, na bosi wenu na umma walioaamini dhamana hii? Mnataka wangapi wafe, kutekwa, kupotezwa, kuuawa, kuteswa, kudhalilishwa, kudhulumiwa, na kuhujumiwa iwaingie akilini? Je, mnapokea mishahara na marupurupu kwa nini? Mmewahi kujitathmini lau kiduchu? Kama mngeambiwa mjitathmini, mngejipa maksi kiasi gani, na kwanini na nini mungeamua? Kuna ugumu katika hili au mngependa/kutaka muwajibishwe?
            Mkitafakari maswali, mengine kapuni, ngoja nizamie historia iliyotukuka yenye mafunzo mengi ya mzee Ali Hassan Mwinyi (RIP Sana bro) walipouawa watu kule Kanda ya Ziwa––––mmojawapo akiwa [N]zegenuka kama sikosei––––hakungoja kuwajibishwa.  Roho ilimuuma. Nafsi ilimsuta. Imani yake ya kidini ilimkaripia. Nadhani hata washirika zake wa bedroom walimuonya. Kwanza, hakuhusika. Pili, hakuweza kuvumilia uoza. Tatu, alifanya maamuzi magumu. Nne alijiuzulu Januari 22, 1977. Tano, tokana na uadilifu, usafi, na weledi, baadaye kitendo hiki kilimwezesha kuwa dingi wetu kwa miaka kumi akiacha urathi uliotukuka. Sita, aliepuka kumfedhehesha bosi wake na kumtishwa mzigo wake japo haukuwa wake peke yake. Saba, alikubali yaishe kumondolea bosi wake taabu ya ima kuwajibishwa au kujieleza kama siyo kuonekana wa hovyo, asiyefuata sheria na viapo, au asiyewajali waliomwamini na kumpa maulaji aliyompa katika vicarious liability (kwa kisambachikwa wasomi wenzangu. Kama si wanasharia, niulize au waulize wenzangu walioko karibu yenu.
Tuache usomi kisheria, tuongee na kuulizana kichizani. Je mnajua kadhia hii? Kama hamjui, kwanini? Kama mnajua, inawafundisha nini? Je mnaielewaje na mantiki yake? Je mnaweza kuidurusu lau mpate somo na uamuzi mujarabu wenye faida kwenu, wahanga, na taifa? Mnaelewa madhara na uzito wake? Mmetafuta ushauri kisheria?
            Nataja majina. Bw. Hamad Yusuf Masauni, Camillus Mongoso Wambura, na Suleiman Abubakar Mombo mpo? Mwangojani?  Kwanza, mnaichukuliaje kashfa hii inayoishia milangoni mwa ofisi zenu? Inawahusu au la? Kama ndiyo, mwangoja nini? Kama haiwahusu, inamhusu nani zaidi ya bosi wenu? Mngependa au kupanga mujiwajibishe, kuwajibishwa, au kutaka hata bosi wenu awajibike wakati hahusiki moja kwa moja ingawa anahusika hasa ikizingatiwa kuwa ndiye aliwapa nyinyi maulaji? Kwa kashfa hizi za kinyama zilizogeuka donda ndugu, huwa mnalala usingizi kama mimi na wengine? Kama mnalala, kwanini? Kama hamlali, mpaka lini? Majina yenu ni ya dini hata kama ni za kigeni. Mnaamini kweli? Kama kweli, mmezitumiaje kuona mwanga? Je mmepuuzia imani zenu au ni waumini jina? Mlipoapishwa na mkaapa, mlibeba vitabu tulivyoaminishwa ni vitakatifu hata kama ni suala kujadilika? Kama mlivishika na kuviinua juu, mnavitenda haki au kuvihujumu mbali ya kujihujumu binafsi, taifa, bosi wenu, hata familia zenu mbali ya ufyatu na uumini wetu?
            Mkitafakari/kupanga kujibu maswali yangu­­­––––hata kama msiponijibu bali kujijibu––––tafakarini sana. Mngekuwa familia, jamaa, na ndugu za wahanga, mngetaka mfanyiwe nini au nini kifanyike? Je mmewahi kuwashirikisha washirika zenu wa bedroom kupata jicho la pili/ushauri? Juzi, nilimsikia bosi wenu ‘akiamuru’ vyombo vya uhasama, sorry, usalama vijichunguze. Je hii ni sahihi au vunga ili joto lishuke? Nani aweza kujichunguza akatenda haki hasa kama si mchizani na si malaika au Chizi Mchizani mwenye nguvu za ajabu za kanywaji? Je hii ni haki na sahihi? Je mmeshaurina naye au la? Kwanini? Kama mmemshauri, anasemaje  na mnasemaje? Je hili la kuwajibika, kujiwabisha, au kuwajibishwa ni gumu kiasi cha kuhitaji PhD kama yangu? Kati yenu na bosi wenu, nani mngetaka abebe hili zigo la kashfa na uchafu, maana naona Chakudema wameamua kukinukisha kama mbaya, mbaya japo ndata nao wametunishia misuli. Je watawazuia bila kukomesha utekaji na upotezaji machizani.
            Du!  Kumbe nafasi imejaa! Ngoja niishie kabla sijatekwa na kunyotolewa roho.
Chanzo: Fyatu Mfyatuzi.

No comments: