Thursday, 15 July 2010

Sofi, wakitunyima utatupa ?


Hivi karibuni bi mkubwa wangu alikuja na mpya. Alisema kuwa kuna shoga yake kamwambia kuwa siku hizi yeye na mumewe wana-sleep mzungu four baada ya kugundua kuwa anakisadia chama cha upinzani! Umbea niliounyaka ni kwamba wako akina mama wengi wameanza kutimiza upuuzi huu!


Anasema mama huyu alianza mkakati huu baada ya kuwaidhiwa na mwenyekiti wa kitengo cha akina mama cha Umoja wa Wanamama Tata (UWT) wa Chama chao Cha Maulaji (CCM siyo Chama Cha Mapinduzi) aitwaye Sofia Lion ambaye watani wake wanamuita Mpayukaji Msemahovyo wa kike kayani.

Niseme kwanza. Sina tabia ya kuwazodoa wala kubishana na wakubwa wa kaya hata kijiwe hadi wanichokoze au kugusa maulaji yangu. Hivyo wanapogusa maulaji yangu huwa sina cha msalie mtume wala kumradhi. Huwa natwanga kama sina akili nzuri. Raha jipe mwenyewe ati alijisemea Njaa Kaya ambaye siku hizi amempa raha na ujiko mwanae ambaye licha ya kuwa mweupe alikuwa hata hajulikani. Hayo tuyaache.

Mbona wao wanapowasaliti walevi hawaambiwi wanyimwe uhondo huu wa Mungu? Au ni yale ya mkuki kwa nguruwe. Hivi kama tungetenda haki si jamaa yangu Nkuu angebaka ukiachia mbali kufa kwa kiherehere alichowasakizia wanafunzi?

Huu ni ushahidi kuwa wakubwa, wake zao hata hawara zao wanataka kutawala akili za wake zetu kiasi cha kutudhalilisha na kutudhulumu haki yetu ya ndoa.

Sofi fyatu alipotoa mpya kuwa akina mama watakaoona waume zao wanaisaliti CCM basi wawanyime kitu ya Ngai Mulungu wetu, ukweli mimi sikujali.

Kwanza, sikudhani kungekuwa na wanawake fyatu na taahira kama yeye wakafanya kitu mbaya kama hii. Nilijua; ni mipayuko na kufilisika kimawazo kulikoanza kugeuka sera za wenzetu. Hivyo nilipuuzia; nikijua hili halitawezekana. Kumbe nilikosea! Sikujua kuna wanawake fyatu na hovyo wangeweza kutekeleza upuuzi huu.

Mie nimemwambia bi mkubwa personally kuwa kama siku akihama chama chetu cha familia cha Ugali Nyama na Maharagwe au Ufisadi Nongwa na Mizengwe (UNM) mie sitajivunga nitamuoa huyo Sofi maana nasikia hana mume. Akigoma nitamnyotoa roho nami nijinyotoe kuliko kutoa talaka hili wengine wafaidi.

Heri ya Sofi ambaye neno husband kwake ni msamiati mgumu. Heri yake anaweza kujivinjari na yeyote kwa vile yeye ni open cheque kwa kimombo. Kama atasema namkashifu nitaiomba mahakama atakaponishitaki aje na cheti cha ndoa na huyo mulume wake. Akitimiza masharti haya mawili basi niko tayari kufungwa maisha hata kunyongwa.

Mgosi Machungi ndiye ametoa mpya kwa kusema kuwa kwa vile Sofi ni kanunga fulani, anatumia mkakati huu kutaka wanawake wawasumbue waume zao ili yeye awanase. Maana Mgosi anasema cheo au elimu ya mtu haiondoi upumbavu wake. Hivyo kaa chonjo Sofi ana lake nyuma ya pazia.

Pia nimetoa ushauri kwa wale waliohujumiwa na mama hili, kwanza, waende mahakamani washitaki chama na baada ya hapo wajitoe chamani na kujiunga na UNM tuikomboe kaya inayozidi kuliwa na hawa nyemelezi wa Njaa Kaya.

Mbinu hii chafu na hatari, kama itapata washikaji, inaweza kuleta balaa hasa talaka na ukimwi ukiachia mbali uzinzi kwa pande zote. Hapa hatujaangalia kupungua idadi ya watoto. Huenda kama mbinu hii mfu ina faida basi si nyingine bali kupunguza ongezeko la watu hasa maskini ambao wenye nazo hawawahitaji kutokana na kuwasumbua kutaka wapambana ufisadi na umaskini. Hayo tuyaache.

Hebu fikiria. Piga picha. Mkeo ambaye ulimuoa kwa posa na kila makando kando bila ya chama kukusaidia, anataifishwa na chama hicho hicho ghafla.

Hebu fikiria mkeo kipenzi anakuwa na washauri wasiojua nini maana ya ndoa zaidi ya kuishi kama jiko la mchina. Unategemea nini bibi mkubwa anapotekeleza ushauri wa mashoga wenye akili mgando ambao kwao mume ni ulaji tena wa siku-kwa maana wanaweza kumchuna yeyote mradi wapate chao iwe pesa au cheo.

Nasikia mume wa shoga wa bi mkubwa hakuficha. Ana mpango wa kwenda kumwambia huyo aliyemgomesha mkewe ampe urodi hata kama aliyefanya hivyo ni changu maarufu potelea mbali atavaa silaha.

Je ni wangapi wataiga mfano wa dume hili la mbegu lililoamua kumtokea Sofi? Je hapa ukimwi utaacha kutumaliza hasa ikizingatiwa kuwa unasambazwa na wale tunaowaita viongozi wetu? Je watu wa namna hii wanafaa kuendelea kuwa kwenye ofisi za kaya hata kama wanajuana na waliowateua kutokana na waliyowafanyia?

Natamani ninkamate Sofi na kumfunga Segerea hata nimhamishie Afghanistan au Saudia akione cha moto.

Uchangu mwingine bwana unatia kinyaa. Unachefua hasa pale yule anayeueneza anapolipwa njuluku zetu za kodi. Hata kama sisi ni walevi na wasotaji wa kutisha, tuachieni burdani yetu yaani kitu ya Mungu. Mmeiba ma-EPA na ma-Richmonduli hatukusema. Mmetulangua na kutukatia maumeme mwaka mzima, manywaji na fegi tumenyamaza. Mmechakachua mafuta hadi magari ya dingi yanamgomea hatukusema! Mmepora pesa yote ya kahawa na kashata pale Bunch of Thieves (BoT) tumeuchuna mkaanza kuumbuana wenye .

Kwa vile mmegusa pabaya lazima tuseme tena kwa herufu kubwa. Kwanza nalaani ufisadi huu na uhujumu dhidi ya taasisi adhimu ya ndoa. Naapa kwa miungu yote. Tutatoana roho kabla ya ngoma kututoa roho.

Sofi, chonde chonde, acha nakusihi. Acha kabla ya kuona kiama kabla ya kukata roho. Hujui kitu hii ndiyo starehe pekee iliyobaki kwa walevi ambao ukapa unazidi kuwaadhibu huku wakubwa wakitanua na mibilioni ya kuusaka ulaji wakiwatumia vitegemezi vyao? Kwanini Sofi unafanya uchokozi hivi? Shida yako nini? Hivi kweli una mume au mshikaji tu? Mume anauma usiambiwe Sofi mwanakwetu mtoto wa
Kizaramizi. Wataka tuzaramie kwako na je utatuweza ambao bi wakubwa zetu wametupiga kibuti kutimiza amri yako?

Mie ningekushauri haya mambo ya ngono uachane nayo. Maana licha ya kukuaibisha huwezi kushinda vita hii. Kwanza, nashangaa. Siasa na ngono wapi na wapi? Mbona mke wa rafiki yangu Willy Silaha ni mpinzani wake kisiasa lakini hii haiwi tatizo kwenye ndoa yao na hawalali mzungu wa four?

Kama ni kunyimwa u-house basi wanyimwe wanaofanya na kulea ufisadi na siyo sisi tunaofaidi haki yetu ya kuweza kutumikia na kusaidia chama chochote. Hii ni haki yetu kikatiba. Mbona nasikia Sofi amesoma sharia lakini ni mweupe asiyejua katiba ya kijiwe chetu chakavu? Kuna haja ya kumchunguza. Huenda alipata ndingirii yake kwa kughushi au kutoa chau chau ya ngoni.

Sofi nasisitiza. Tangaza tujue utatupa ili tusifanye maandamano bure. Kwanza, tutajidai na mtu mwenye cheo kuliko sisi walevi. Sipati picha nami kukwea shangingi la wakubwa nikitanua! Ila nakuonya. Siyo tuje tukute mibuzi mikubwa mikubwa mienzio mtufunge bure. Na vitoto vitakavyozaliwa kwenye kitimtim hiki lazima viitwe chama au siasa.

Mara namsikia yule jamaa ambaye bi mkubwa wake amegomeshwa na Sofi akisema : “Acha niwahi nijitia uturi tayari na kuchukua zana zangu salama nienda kujivinjari na bi Sofi ili bi mkubwa wangu aliyenigomea akome.”

Jamani chungeni. Kuna miwaya na haijali cheo wala nini. Mwenzenu mie simo bi mkubwa wangu si mpuuzi wa kusikiliza upuuzi wa wapuuzi waliolewa ulaji.
Swali linaendelea. Sofi wakitunyima wewe utatupa? Nangojea jibu.
Khalas kweisine.
Chanzo: Tanzania Daima Julai 14, 2010.

3 comments:

Anonymous said...

Very good Mzee Mpayukaji. This woman is a prostitute per se. Yeye hafikirii zaidi ya kitovu chake na nonihino yake. Umempiga nilivyotaka.
Bravo

Anonymous said...

Akili zake hazina akili...nashangaa kwanini amepewa madaraka. Yaani ni si mzima kabisa; aangalie siasa za nje zipo vipi. Mama na baba wanaweza kuwa vyama tofauti lakini wakiwa nyumbani tofauti hakuna. Tuangali Gov.Schwarzenegger ni Republican mkewe Democratic tofauti ni vyama na si mambo ya unyumba.

Mimi ni mwanamke na nina haki ya kufata chama chochote na si kwa ajili ya mume wangu ebooooo!!

New Woman

Anonymous said...

Msimulaumu Sofia. Huyu ni changudoa wa kawaida anayetumiwa na Kikwete ambaye ni hawara yake kulipa fadhila.
Hamkuwaona akina Ritta Mlaki hawara wa Mkapa au Mary Nagu hawara wa Hassan Ngwilizi walivyoula?
Hawa wametumia nyuchi zao kuula na mawazo yao ni uchi uchi.