The Chant of Savant

Wednesday 27 July 2011

JK na Pinda walivyotesa na Uongofleva!



Hii picha hapo juu ni picha ya mwaka ya blog hii. Sijui jamaa waliipigia wapi? Ingawa ni utani unaweza kubeba ujumbe mzito kuwa watawala wetu bado wanafanya mambo ya kitoto. Je wao wanapojiona hupata somo gani? Wanafanya utoto kweli au wanasingiziwa? Hivi kwa mfano Pinda kuwaambia wabunge kuwa kashfa ya wizara ya nishati na madini haivumiliki na JK kuendelea kuwaacha walioiasisi yaani William Ngeleja na naibu wake Adam Malima si utoto? Je kutoana kafara si utoto? Rejea kutolewa kwa bangusilo Ibrahim Msabaha, Edward Lowassa, Rostam Aziz na juzi juzi David Jairo huku wahusika wakuu wakiendelea kunema. Je kuna utoto kama huu jamani? Je Kikwete na Pinda wataacha utoto lini? Hebu tubadili namna ya kuuliza maswali. Picha hii inaonyesha usanii wa hali ya juu. Je usanii wa Kikwete bado ni mali au utoto na pigo la kihistoria kwa taifa? Hii ndiyo maana tumeona tutumie Uongofleva kuwakilisha ujumbe kulingana na aliyesanifu picha alivyolenga kuonyesha utoto wa hawa jamaa.
Kazi kwenu kutafakari wakati mkifaidi picha hii ya mwaka ya blog hii.

5 comments:

emu-three said...

Kama kuna kitu kimeongoza kwa kutia doa serikali ni hili tatizo la umeme, naona kilikuwa kicha cha kuchakachua `mali ya walalahoi' lakini sasa kimegundulika, na watu haoooo!
Mkuu wa nchi, wizara hii inatakiwa uisafishe kwa ufagio wa chuma, toka juu hadi chini, weka watu wenye uchungu na taifa...bila hivyo hapa panaweza pakawa sehemu ya kuanzia machafuko..hatuombeii hili, lakini watu wamevumilia mapka imefika basi.....

malkiory matiya said...

Ama kweli hii ni picha ya mwaka!

Rik Kilasi said...

Hii ni aibu sana kwa taifa kama Tanzania umeme wenyewe unawaka maeneo machache tu ya nchi and yet mgao mkali sasa ungekua unawaka nchi nzima mgao si ungekua kwa wiki 2 unawaka mara moja.Serikali naona haiangalii long term future as in athali ya kutokua na umeme wa uhakika na hao wanafunzi wanaoitwa taifa la kesho sijui wanasomaje? Hapo hapo watasema wanataka foreign investors kwenye nchi yenye giza sijui nani chizi aje kuwekeza gizani.Nadhani huu ni mfano mmoja katika mambo mengi ambayo yanaendeshwa kiholela.JK asafishe wizara husika kama anataka kurudisha imani kwa wananchi maana hii ni aibu na inaashiria how unserious our government is. Ni hayo tu :((

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Rik Kilasi usemayo ni kweli. Wanafunzi wanaathirika sana na upuuzi na utoto huu. Hapa hujaongelea wachapakazi wengine wanaokwaza na balaa hili la mgao kwenye karne ya 21. Je tumlaumu Kikwete peke yake wakati tukishuhudia nchi za wenzetu wanawashupalia watawala wao?

Rik Kilasi said...

Tunajua kuna collective responsibility lakini mkuu wa kitengo mwisho wa siku ndiye ambaye hubeba lawama kwa asilimia kubwa kwani watendaji wabovu anawaona na ana uwezo wa kuwaondoa na kutofanya hivyo kuna ashilia kulindana kusiko na maslahi zaidi ya kuboronga tu kazi thinking wanadanganyika hawaoni!!