Monday, 27 April 2009

Majibu ya mafisadi kwa Mengi tosha kujua ukweli


Haitakuwa haki kuanza makala haya bila kumpongeza kwa dhati Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwa ujasiri na uzalendo wake. Ameonyesha hili kwa maneno na matendo siku zote.

Katika watu walioweka historia safi na ya pekee katika kupambana na ufisadi nchini hivi karibuni, Mengi amevunja rekodi. Amejitenga na unafiki na woga wa kuogopa kuwakabili mafisadi ambao wamekuwa wakiliibia taifa kwa miongo.

Aliwataja Rostam Aziz, Yusuf Manji, Jeetu Patel wa EPA, Tanil Somaiya na Subash Patel kuwa mapapa wa ufisadi nchini ambao kimsingi ni kikwazo cha maendeleo ya walio wengi.

Tofauti na wanasiasa tena wenye nafasi na majina, Mengi ameepuka unafiki kujifanya mambo ni safi wakati hali ni tete. Amekwenda mbele hatua mia na kutaja majina. Waingereza huita hii to call a spade spade. Licha ya kutaka uzalendo na mapenzi makubwa kwa taifa, hakika alichofanya Mengi, licha ya kuhitaji ujasiri na kujitoa mhanga, kimetoa somo kuwa kumbe tukiamua inawezekana.

Kati ya wote waliotajwa, hakuna aliyekuwa akisumbua vichwa vya watanzania kama Rostam Aziz ambaye anasemekana kuwa nyuma ya Kagoda na Richmond . Vita aliyoanzisha Mengi huenda inaweza kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye makucha ya wezi wa kigeni wanaomilki na kuchezea uchumi wetu watakavyo kutokana na kuwa na mawakala wao serikalini.

Kitu kilichomvutia mwandishi ni majibu mepesi yaliyo karibu na kukiri ya watuhumiwa watatu. Ukiangalia majibu yao , licha ya kukwepa, yanaonyesha wazi wasivyo na la kujibu bali kujibaraguza wakidhani watanzania ni mataahira. Na hakika hii licha ya kumpandisha Mengi chati, ni ushahidi kuwa madai yake ni ya kweli na hivyo kama watapanga kumhujumu kwa njia yoyote, umma basi usimame nyuma yake. Kwani vita hii si kwa faida yake tu bali taifa.

Alipohojiwa na vymbo vya habari nini majibu yake kwa tuhuma za Mengi, Rostam Aziz alitoa majibu ya ajabu kama ifuatavyo: “Mengi amejaa chuki, wivu na fitina. Sina cha kumsaidia isipokuwa kumuombea Mungu ili amsaidie kwa kumpuuzia hayo maana ni adhabu kwa nafsi yake mwenyewe. Kwa malezi niliyopata, siwezi kubishana na mzee.”

Hivi kweli kuna uzee au malezi kwenye jinai? Mengi awe na fitina na chuki kwa Rostam kwa lipi? Kama ni hivyo basi kila mtu ana chuki naye tena bila sababu. Hata alipotuhumiwa na Dr. Harrison Mwakyembe kuwa ameanzisha vyombo vyake vya habari kwa pesa za EPA alizoiba kutumia Kagoda, Rostam aliishia kujikanyaga kanyaga kama alivyofanya kwa Mengi! Umefika wakati wa serikali kumshughulikia na kuacha kumlinda. Kwani mazingira yanaonyesha Rostam ni nani katika wizi wa Kagoda na Richmond .

Hata alipotuhumiwa na mwanasheria Bhyidinka Michael Sanze kuwa yuko nyuma ya EPA hakukanusha. Hata alipotuhumiwa na Ibrahim Msabaha (Bangusilo) waziri wa zamani aliyetimuliwa sambamba na waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na wengine kutokana na kashfa ya Richmond . Msabaha alimueleza kama ‘mwarabu’ wa waziri mkuu.

Hata alivyotajwa na baadhi ya vyombo vya habari aliishia kunywea na kutafuta waandishi uchwara kumtetea kwa kuwaandama anaowaona maadui zake. Kimsingi Rostam anapaswa kubanwa aseme ukweli ukiachia mbali kuchunguzwa na waliomzunguka hata waliomo serikalini au chamani.

Ukija kwa Manji aliyetuhumiwa kuibia umma kupitia NSSF alipokopa pesa na kujenga majengo na kuyauza kwa bei ya kulangua kwa NSSF ile ile. Yeye, kama Rostam naye alitoa majibu ya kukata tama. Alikaririwa akisema, “Mengi... (si mstaarabu), biashara zake zimemshinda ndio maana anazungumza ovyo.”

Hapa issue si ustaarabu wa Mengi bali anayosema ni kweli au la? Swali rahisi tu. Lakini angejibu nini wakati kila kitu kiko wazi?

Naye Jeetu Patel gwiji wa wizi wa EPA alikuwa na haya ya kusema, “Hayo ni matatizo yake, amewaita waandishi kuzungumza nao... sikumsikia lakini ninachoweza kusema ni kwamba anatumia uhuru wake wa kujieleza.”

Huyu angesema nini wakati anajulikana alivyosaidiana na wenzake kutengeneza makampuni feki na kuliibia taifa?

Kimsingi watuhumiwa wote hawana la kusema. Na kama siyo mamlaka kuwafumbia macho, walipaswa kuchunguzwa zaidi. Na mengi yangefumka yasiyojulikana hata idadi kuongezeka. Maana ufisadi wao unafanyika kimduara. Umefika wakati wa kulikomboa taifa.

Cha muhimu sasa ni kwa watanzania kuanza kuchukua hatma ya uchumi na nchi yao . Kwanini nchi yetu imegeuzwa No man’s land ambapo wageni hasa wahindi wanaweza kuja na kujichotea watakavyo? Inatisha kuona wanamiliki karibu uchumi wetu wote, nyumba za msajili, wanapewa tenda karibu zote za maana, wana uraia wa nchi nyingi wakati sisi tunakatazwa, na sasa wameingia kwenye siasa ili kulinda uchafu wao.

Kila wakiguswa wanasema wanchukiwa na kubaguliwa. Kuna watu wabaguzi kama wao? Mbona wanapopendelewa na kuruhusiwa kuibia taifa hawasemi wanabaguliwa? Mtu kwao. Nani anaweza kwenda India au Iran akamilki uchumi wao?

Tangu waletwe na mkoloni kutudhoofisha, wemekuwa wakiwatumia wakoloni weusi kuendelea kufanya kazi hii.

Wengi watajiuliza kwanini mafisadi wetu wanapenda kuwatumia wahindi. Kwanza ni rahisi kuwafukuza mambo yakichacha kama ilivyotokea kwa Chavda. Pili, wanasifika kwa fitina na kujikomba. Yao ni divide and rule.

Hatuchukii wageni katika nchi. Lakini mgeni anapofikia kumwambia mwenye nyumba toka kitandani nilale tena na mkeo. This is but too much.

Hivyo basi, kuna haya ya kuanza kuishinikiza serikali iwashughulikie mafisadi hawa ukiachia mbali umma kuanza kudai uzawa kama alivyowahi kusema Idd Simba wakamfanyia mizengwe.

Pia kuna haja ya kuangalia uhamiaji wa holela na rushwa ambapo wahindi wamekuwa wakiingia na kutenda jinai watakavyo na kuondoka. Rejea kutoroka kwa yule mhindi wa rada na hata Chavda.

Tulipigania uhuru ili kuwa huru siyo kuwa wanyonywaji.

Mwisho, kama Mengi atadhurika, sina shaka wakati wa Mtikila wa magabacholi utarejewa kwa uzito unaostahili. Huu ndiyo wakati wa kupambana na ufisadi kwa vitendo na siyo maneno.
Chanzo: Kulikoni Aprili 27, 2009.

No comments: