The Chant of Savant

Sunday 10 April 2011

Breaking News Makamba nje Mukama ndani


Wilson Mukama katibu mkuu mpya wa CCM


Habari tulizopokea ni kwamba, hatimaye, CCM imeamua kumpiga kibuti katibu wake Mkuu Yusuf Makamba. Nafasi yake imechukuliwa na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa jiji la Dar Es Salaam, Wilson Mukama. Nafasi ya naibu katibu mkuu imekwenda kwa swahiba na meneja kampeni wa Kikwete, Abdulrahaman Kinana. Naye Nape Nnauye amechukua nafasi ya itikadi na uenezi ilikuwa ikishikiliwa na John Chiligati. Inaonekana zamu hii ni ya watoto wa wakongwe wa CCM. Maana Rehema Nchimbi mtoto wa John Nchimbi baba yake Emanuel Nchimbi,kama Nape, amechukua nafasi ya katibu wa organizesheni.

Swahiba mwingine wa Kikwete, Zakhia Meghji aliyetupwa nje kwa kashfa ya EPA benki kuu na anayedaiwa kushiriki ufisadi wa kutisha kwenye wizara ya utalii amerejea kwa kishindo kwa kunyakua nafasi ya katibu wa fedha na uchumi iliyokuwa chini ya Amos Makala.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa CCM imeamua kujivua gamba kwa kuwatimua vinara na watetezi wa ufisadi hasa Makamba. Hatimaye Kikwete amelitupa jini na jinamizi la Makamba ambaye kimsingi alikuwa akimtawala Kikwete pamoja na uenyekiti wake. Bila shaka akina Tambwe Hiza sasa wanajinonihii kwenye suruali kutokana na muungu wao Makamba kupigwa buti. Je imejivua gamba au ni gamba lile lile la kujuana, kulindana, kufisidi, kuganga njaa, usanii na upuuzi mwingine? Time will tell.

7 comments:

malkiory said...

Alichofanya kwa Kinana ni kulipa fadhila, vinginevyo hana jipya zaidi ya makali yake ya propaganda chafu.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Malkiory uko sahihi.Kinana hana tofauti na Rostam na Chenge. Je unasemaje kuhusu hili la ukoo wa vigogo kupewa ulaji wa juu na Meghji ambaye kama si kuwa mshirika wa Kikwete alipaswa kuwa lupango?
Hiyo ndiyo Tanzania yenu ya kila aina ya majaribio.

malkiory said...

Meghji lazima kuna ufisadi alishirikiana na JK wakati alipokuwa waziri wa fedha. Hili la nepotism kwa kweli linanikera sana.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Hili ni obvious. Bila Meghji kuchota pesa wizarani unadhani pesa iliyotumika kwenye kampeni wangeirudisha vipi? Nepotism is currently the order of the day. Kuondoka kwa Makamba kwa wapenda mageuzi ni pigo. Maana tulipenda aendelee kuivuruga CCM ili upinzani upate soft-landing spot. Hivyo basi, kwa wapenda mageuzi kuondoka kwa Makamba ni pigo kubwa. Maana Mukama kama atarudia alichofanya kwenye tume ya jiji basi CCM wanaweza ku-gain.

Anonymous said...

CCM hawawezi kugain hata kama wangemweka Dr Slaa kuwa katibu wao mkuu!
They are already beyond repair.

But Makamba ni muhimu akapewa nishani ya kujenga upinzani.

malkiory said...

Umenene anonymous. Ni jana tu tulikuwa tukiongelea kuhusu utawala wa kurithishana kifamilia na kiukoo au pengine tuseme utawala wa kifalme au kisultani na zaidi utawala wa kulipana fadhila. Leo hii ameongezeka January Makamba, mwanae katibu mkuu mstaafu. Ama kweli sikio la kufa halina dawa.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Anonymous hapo juu na Malkiory nawashukuruni kwa kuiona hali halisi ya CCM ambayo tunaomba kila siku idondoke kwa aibu kama Laurent Gbagbo.
Ni kweli Makamba alijenga upinzani ingawa hakuwa na nia wala kujua kuwa alikuwa akifanya hivyo.