The Chant of Savant

Monday 11 April 2011

At last Gbagbo kwishinei!




Hatimaye,Laurent Gbagbo na mkewe Simone amekamatwa kama Saddam Hussein akiwa amejificha shimoni huku jasho likimchuruzika. Ameondoka kwa aibu, pingu mikononi huku akipewa taulo ajifute jasho. Aliloa kuanzia kichwani hadi unyao. Alionekana kuchanganyikiwa na kunywea akijifuta jasho hata kwenye makwapa bila aibu. Ile jeuri na mbwembewe na midenguo tuliyozoea toka kwake na mkewe aliyewahi kuwatukana viongozi wote maarufu duniani vilikuwa vimetoweka.
Ni furaha iliyoje imla mwingine kuangukwa kwa kila aina ya aibu!Kwa habari zaidi, Bonyeza hapa.

No comments: