The Chant of Savant

Thursday 21 April 2011

Rais Salma, Rahma na Kikwete na walamba viatu wao


Kwa wanaojua urais barani Afrika ulivyo mtaji mkubwa kwa familia na waramba viatu wa kwenye kuwa nao, watakubaliana nasi kitu kimoja. Chunguza picha hiyo hapo juu ambapo Rais wa WAMA, Salma Kikwete yuko ziarani nchini Marekani.
Je Salma amekuwa rais lini zaidi ya baada ya mumewe kuwa rais? Kabla hapo rais wa kutumia NGO hakuwa mwingine bali Anna Mkapa ambaye alitimka baada ya mumewe kuutema ulaji.

Je rais Salma ameandamana na nani? Kwenye picha anaonekana Zakhia Meghji aliyekuwa waziri wa fedha wa mumewe kabla ya kuondolewa kwa kashfa mbali mbali za wizi wa mabilioni ya fedha za umma.

Anayefuata nani? Mwanaidi Maajar ambaye ni balozi wa mumewe nchini Marekani anayetuhumiwa kusaini nyaraka za baadhi ufisadi wa kutisha na mwisho wa yote kuzawadiwa ubalozi. Je aliteuliwa kuwa balozi kutokana na merit au kuwa karibu na bwana au bi mkubwa kama anavyooneka? Je ni wangapi wamo kwenye ofisi za umma kupitia mgongoni mwa ufisadi huu wa kunuka unaoendelea kuvumiliwa? Tuliwahi kuandika makala ya Hidden Presidents of Africa.

Wanaoikumbuka wanaweza kujua ni marais wangapi Afrika inao nyuma ya pazia. Wa mwisho mkumbuke Simone Gbagbo na alivyoisha kabla ya Suzana Mubarak na Leila Trebelsi wa Tunisia. Wakumbuke marais hawa waliopata urais kutokana na kulala kitanda kimoja na rais wako wakati ukiangalia picha ya rais huyo wa WAMA.

Bado rais Rahma al Kharoos Kasiga wa RBP Group ambayo imeota baada ya Kikwete kuingia madarakani.

2 comments:

Anonymous said...

Bravo Mhango kwa kutoogopa. Kikwete na familia yake ni vibaka tu na mafisadi hata wafanyeje.

Tonyacfcq said...

Bravo Mhango kwa kutoogopa. Kikwete na familia yake ni vibaka tu na mafisadi hata wafanyeje.