The Chant of Savant

Sunday 24 April 2011

Zawadi yangu ya pasaka toka kwa Salma Kikwete



Hizo hapo chini ni salamu zangu na wengine wenye kutilia shaka wizi wa NGO za wake za wakubwa toka kwa Mama Salma Kikwete first lady wa Tanzania kama ilivyotumwa na mpambe wake kwa maagizo yake.
Maana haiingii akilini mtu awe na taarifa muhimu za ndani kama kabila la mtu na asiwe anafanya kazi chini ya maagizo ya WAMA yenyewe ambayo ni Salma.Tumemstukia atafute mbinu nyingine ya kujivua gamba.

Hapa chini wameorodheshwa wafanyakazi wa WAMA. Hawa wanaojiona wajanja wakati siyo wamesahau kuwa tunachopigia kelele si hawa wafanyakazi bali Bodi nzima ambayo ndiyo mmilki na mnufaika wa WAMA.

Tuwakumbushe. Tunapoongelea WAMA hatumaanishi hawa wafanyakazi wadogo wanaochapa kazi ili kupata mkate wao. Tunamaanisha mapapa wake za wakubwa au wakubwa wenyewe hapa chini:

Mama. Salma Kikwete Chairaperson mke wa rais Jakaya Kikwete
Mama. Sophia Simba Chairperson of the Board waziri katika utawala wa Kikwete
Mama. Zakia Zamdan Meghji Board Member waziri wa zamani wa fedha aliyeondolewa kwa ufisadi
Amb. Mwanaidi Majaar Sinare Board Member balozi wa serikali ya Kikwete nchini Marekani anayedaiwa kusaini mikataba mingi ya kifisadi na asikanushe
Mama. Regina Lowassa Board Member mke wa waziri mkuu wa zamani aliyetimuliwa kwa ufisadi
Mama. Blandina Nyoni Board Member
Mama Hulda S. Kibacha Board Member
Kama kweli nia ya WAMA ni njema na si kutafuta kuchuma kwa kutumia matatizo ya akina mama, kwanini kwenye bodi ambayo ndiyo roho ya WAMA hakuna wanawake wa mashambani ambao ndiyo walengwa na waathirika? Bila kutoa jibu linaloingia akilini kuhusiana na NGO hii ya mke wa rais na mashoga zake bado umma utaendelea kuamini ni ya kiulaji kama ilivyokuwa EOTF ya Anna Mkapa.Mbona siku hizi imedoda? Simple. Mkapa si rais tena. Naandaa makala iitwayo WAMA ni wizara ya mambo yote. Je wizara husika zitafanya kazi gani? WAMA bado itaendelea kuwa kitendawili cha utawala wa kujuana na kuibiana hadi itakapotokomea baada ya Kikwete kuondoka madarakani hapa 2015. Tusiruhusu rais ajaye kuwa na NGO ya mkewe. Ni ufisadi wa kimfumo huu.






Namfagilia mhe mama salma kikwete

Wana jf salaam,

leo najitokeza rasmi kumfagilia kwa sana f/lady wa tanzania mhe mama salma kikwete kwa utendaji wake wa kazi tangu ameingia madarakani mumewe mhe rais jakaya mrisho kikwete .

Wana jf nimekuwa nikosoma mara hapa jamvini. Kadhaa mada mbalimbali juu ya huyu mama nyingi zikionyesha kumshambulia pengine kwa kutojua kazi alizozifanya mpaka sasa. Pia baadhi ya magazeti hasa mwanahalisi na raia mwema zimekuwa zikiandika makala yenye mtizamo hasi juu ya f/lady na taasisi ya wama . Mwandishi mmoja nkwazi anaeishi kanada ktk makala zake nyingi juu ya f/l na wama ameonyesha waziwazi chuki binafsi juu ya wama na f/l

wana jf taasisi ya wama inafanya kazi kubwa ya kusaidia makundi maalum ya kijamii husasani wanawake na watoto wa kike walio katika mazingira hatarishi yaani yatima na familia duni kwa kuwapatia elimu itakayoweza kuwakuomboa .

Taasisi ya wama inayo bodi ya wakurugezi, timu ya menejimenti iliyopatikana kwa njia ya usaili wenye ushindani . Na katika timu ile mama salma hana ndugu hata mmoja aliemweka . Kuna wakati alituhumiwa kwa ukabila na udini katika taasisi yake ufuatao ni ukweli wa timu ya menejimenti ya wama ;

1. Daudi nasib- katibu mtendaji mpare muilslam
2. Neema mhada-afisa afya msukuma - mkiristo
3 gloria minja - afisa tathimini -mchaga-mkiristo
4 philomena marijani -afisa uraghibishi-mpare-mkiristo
5 john mataka -afisa elimu ya mtoto wa kike-mmakonde-mkiristo
6 tabu likoko- afisa uwezeshaji wanawake-mzigua -muislam
7 christina ngonyani(cpa)- mhasibu -mngoni -mkristo
8 subira mgalu(cpa) -mhasibu -mzaramo-muislam
9. Anande munuo -secretary f/l-mchaga-mkristo
10. Veronica -ngulupa -mhudumu-mnyasa-mkiristo

haya hoja ya ukabila na ukiristo ina mshiko ? Watanzania tumuogope molla wetu

hoja nyingine kwamba wama inapata fedha toka ikulu hii sio kweli tangu wama ianzishwe haijawahi kuchangiwa pesa yoyote toka ikulu wala mfuko mkuu wa hazina . Vyanzo vya mapato ni kutoka kwa wasamalia wema wenye kuguswa na shughuli zinazofanywa na f/l kupitia taasisi yake ya wama . Fedha zote zinazochangwa zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa .

Kila mwaka taarifa hesabu za taasisi zinaandaliwa kwa viwango vya kimataifa na kuwasilishwa kwa mkaguzi wa nje kampuni ya kimataifa pkf iliyopo jengo la amani house floor ya tisa na zinapewa hati . Miaka mitatu mfululizo wama imepata hati safi .

Mafanikio ya wama inayoongozwa na mhe mama salma kikwete ni mengi sana na



yameelezwa katika ripoti ya mwaka ya taasisi hasa 2006/2007 , 2007/2008 , 2008/2009.

Lakini jambo kubwa ni kwa mama salma kikwete kujenga shule ya kisasa ya mfano wa kuigwa wilayani rufiji mkoa wa pwani kwa mchango wa mfadhili hayao nakayama wa japan na wadau wa ndani ya nchi .shule hii mpaka sasa imegharimu zaidi ya billion 1.9 za kitanzania na inasomesha bure watoto yatima na wanaotoka kwenye familia duni toka mikoa yote ya tanzania bara na visiwani. Shule hii ina wanafunzi mpaka kidatio cha pili wapatao 272 na kati ya hao hakuna hata ndugu mmoja wa mama salma au mjumbe yoyote wa bodi au ndugu wa mfanyakazi wa wama

watoto hawa wanachaghuliwa na wizara ya tamisemi bila ya kujali dini,kabila , itikadi za wazazi wao,rangi n.k . Tunaomba wadau waendelee kumuunga mkono mhe mama salma kikwete kwa moyo wake huu wa kizalendo .kupitia shule hiyo taifa la tanzania litapata wataalamu wa kutosha katika maeneo mbalimbali . Shime wananchi/wadau/wahisani tuache kusikiliza maneneo ya mitaani , mhe mama salma ni mfano wa kluigwa .

5 comments:

Jaribu said...

Hao wapambe wanaotetea ndio wanafaidika na ufisadi huo. Hao ndio walikuwa wanawauza ndugu zao utumwani kwa shanga na gololi za kun'gara. Kama huyo Sophia Simba, wakati wa "kujivua gamba" Dodoma alikuwa anamtetea Chenge kuwa kasafishwa na Serious Fraud Office ya Uingereza, wakati kila mtu anajua kua Ubalozi wa Uingereza Dar ulishakanusha hiyo. Naona jamaa wanatufanya kama wanavyosema Wanigeria, "Mugu, I go take your dollar!", I mean shilling.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu usihangaike na Sophia Simba. Mara nyingi manung'aembe kama yeye na wengine walio na utukufu kwenye nchi yetu hujikomba kwa wanaume ili lau wapate vimada wa kujivinjari nao.

Ogopa viumbe kama hawa ambao wameshindwa kuheshimu utupu wao. Hawawezi kuheshima maslahi ya umma. Wameharibikiwa na wanataka wote tuharibikiwe.

MloMmoja said...

Eti Mama Salma ni mfano wa kuigwa,wewe pumbahead coacroach kibaraka uliejitoa fahamu aka mchumia tumbo,ebu funga bakuli lako.
Salma angekuwa mfano wa kuigwa kama angeazisha WAMA kabla JK hajaingizwa ikulu na Magamba aka x-wanamntandao wenzie. Hamuwezi kutuhadaa,Fulsa sawa kwa wote ya Anna Mkapa ipo wapi leo?hakuna asiejua huo ni mtandao wenu wa wizi wa waziwazi kutumia mgongo wa ikulu na wame zenu mazezeta.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

MloMmoja umeniacha hoi. Una usongo ile mbaya. Ndivyo inavyotakiwa maana hawa viumbe wanaharibu maisha ya mamilioni ya watu wetu na bado wanatuona kama hatuna akili wala kumbukumbu kama wao. Hakika Salma ni gamba jingine la CCM sawa na Jakaya. Je CCM iko tayari kuyavua haya magamba ambayo kimsingi waweza kuyaita vichwa vyenye kutunza sumu ya maangamizi yetu?
Bado kuna vinyoka kama Nape na Januari bila kusahau mengine mapya kama Kinana ambaye anajulikana alivyomaliza nyara za taifa letu.

Anonymous said...

Mhango, sio ufisadi wa kimfumo bali ndio ufisadi wenyewe - ufisadi ni mfumo (kleptocracy ndani ya the so called democracy and good governance). Wanasahau kitu kimoja kuwa siku nguvu ya umma itakapofanya vitu vyake hao wote watafikishwa mbele ya pilato kujibu mashtaka. Wamuulize Hosni Mubarak!!!!!