The Chant of Savant

Friday 15 April 2011

Nani ana haki ya kumchoka mwingine? Muungano au Mgongano?


Pamoja na kuwapa gesi,uwaziri, umakamu wa rais, ukuu wa idara na mikoa ubunge, umeme na vinono vingine bure bure, wenzetu wa visiwa vya Zanzibar na Pemba wametuchoka. Je wanaona kama tunawahonga ili waendelee kuishi kwenye ndoa ya kulazimisha? Je ni wachumia tumbo wasio na shukrani? Je bara ni mabwege tusema akina chumaulete? Je tatizo ni nini na tunapata nini cha mno kiasi cha kung'ang'ania ndoa hii?

Tuliingilia na kuitwaa Zanzibar kukwepa adha ya ubepari kusumbua taifa la kijamaa wakati ule. Je bado tuna tishio hili kiasi cha kujitoa kafara kiasi hiki? Je kila mtu ashike hamsini zake tuone nani atamhitaji nani au tuendelee kunyonywa na kudhalilishwa? Kwanini tusiende zetu tuka-export mchele na nishati kwa bei ya haja? Je wenzetu hili wanalijua? Kwanini tusichukue kila mtu hamsini zake tukawarejeshea mzigo wa watu wao waliokuja kuzaliana na kupata neema bara? Let's try it and see who will become the first person to weep and gnash teeth.
Je huu ni mgongano au muungano wa Tanzia?
Kila mwenye akili atie maanani na aamue.

4 comments:

Jaribu said...

Ni wachumia tumbo. Mimi sielewi kwa nini unalazimisha watu kuwa kwenye muungano ambao hauna faida kwa upande mmoja. Mambo yote hayo uliyoyataja, pamoja na kuwa uwakilishi wao kwenye serikali ya muungano ambao hauko proportionate to size na mchango wao kwa taifa hili.

Lakini tusishangae sana, wanatufanyie mambo yale yale tunayofanyia mataifa mengine. Kulalamika kwingi kuwa hawa mabeberu wanataka kututawala, halafu mkono tumenyoosha tunataka fadhila.

Napenda ule mfano wa Czechoslovakia. Slovakia walikuwa wanalalamika mpaka wakatengana na Czech Republic. Wao wamebakia kuwa wakulima tu wakati wenzao wanasonga mbele na uchumi wa viwanda. Mimi naona tujitue mzigo na kuwaacha waondoke, tuone kama ujanja wa kuuza genge utawafikisha mbali.

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Jaribu asante sana kwa kunena vyema. Tuwabebea hadi lini na kwanini?
Hili ndilo swali linalonisumbua.

Ungujaukuu said...

Mpayukaji:
Wananchi wa Zanzibar wanaponzwa na wanasiasa,wanasiasa wanajinufaisha wao wenyewe na wameshindwa kuwapa huduma za msingi wananchi waliowaweka madarakani,leo hii wamepandikiza 'muungano' kama chanzo cha matatizo ya Zanzibar.Ebu jiulize,serikali ya umoja wa kitaifa inamsaidia vipi mwananchi wa kawaida zaidi ya kumuongezea mzigo wa kuindesha?Leo hii serikali badala ya kuimalisha kilimo inagombana na wafanyabiashara kuhusu mchele 'mapembe' yatokayo nje ambayo mkemia mkuu amethibitisha haufai kwa matumizi ya binaadam.Viongozi hawa ni majuha???Zanzibar ilikaa gizani kwa miezi 3,SMZ ilifanya nini zaidi ya kusubiri kudra za Mwenyezi??ivi wanajua Shirika la umeme Zanzibar wanadaiwa bilioni ngapi na Tanesco,na watu wamekaa kimyaa??ivi kukiwa na mkuu wa majeshi au mkuu wa polisi mzanzibar,mwananchi wa kawaida itamsaidiaje???umefika wakati wanasiasa waache kuwaongopea wapiga kura wao, watu wanalipa kodi,jukumu lenu ni kuwapa maisha bora na si kupandikiza chuki. Scholarship zote za nje wanaenda watoto wa wakubwa,mafukara wanaambiwa tatizo ni muungano. Wenyewe wanenda tibiwa nje,Mnazi Mmoja kina mama wafa kwa uzazi,ilo nalo tatizo ni muungano??Waambieni watoto wenu waache kushinda MASKANI,Zanzibar ina bandari,Mustafa Jumbe (DG) anajinufaisha yeye na familia yake tu,Zanzibar wameanzisha ZRB wanakushanya kodi wenyewe,bara wamekaa kimya tu,mgeni akitoka nje analipa kodi JK airport na akifika Zenj analipa tena,ilo nalo tatizo ni muungano...nyie mwataka jamani????

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Asante sana Ungujaukuu kwa mchango wako wenye mashiko. Kweli umetufungua macho. Uwepo muungano au usiwepo si jambo la maana zaidi ya huduma safi kwa wananchi wetu. Kama huduma ni mbovu ndani au nje ya muungano bado tatizo ni utawala mbovu wa mafisi na mafisadi walielemewa kufikiri wakaabudia ubinafsi na uroho na roho mbaya.