Saturday, 19 July 2014

Adhimisho la Ndoa


Jana ilikuwa siku yetu ya maadhimisho ya ndoa yetu. Tulisherehekea japo kimya kimya na watoto wetu kuendelea kula chumvi na sukari ya ndoa. Tunazidi kumshukuru Mungu kwa hili kwani miaka inazidi kwenda huku matunda nayo yakizidi kukua. Tunashukuru kwa kupata kila tulichotarajia na zaidi kwenye ndoa yetu. Kwani tumepanda mabonde na milima yote pamoja kwa furaha na amani na kila uchao tunaona ni kama siku tuliyofunga ndoa miaka mingi iliyopita.

7 comments:

Mbele said...

Hongera sana. Kila la heri.

NN Mhango said...

Kaka Mbele kwanza shikamoo. Habari za siku nyingi? Nisamehe ni miaka mingi sijapita kwenye uga wako kutokana na kuwa na madude mengi ya kuandika. Tunashukuru kwa pongezi zako.
Kila la heri nawe pia.

Anonymous said...

Hongera sana Mwalimua, maana sisi kijiwe chetu cha walevi tupo tunapanga jinsi kuwaweka kiti moto wale wote wachumia tumboni, baada kupata haya mapesa makampuni feki ya kufua umeme hapa nchini kwetu na jinsi yanavyoendelea kuharibu kila kona na mikakati yao kuongeza michepuo.

Anonymous said...

Hongera

NN Mhango said...

Anon hapo juu nawashukuruni kwa pongezi na dua zenu. Inshallah Mwenyezi Mungu atawalipeni hasa wale wanaowaibia walevi wakidhani hakuna siku ya malipo.

Anonymous said...

Mwalimu kumbe una mke bomba! Hongera sana.

NN Mhango said...

Anon hapo juu,
Kwangu kila mwanandoa ni bomba kwa mwenzake. Hatuwezi kufanana wote. Hivyo, wewe ni bomba na mwenzio ni bomba. Je kama mwili wote ungekuwa mguu, huo mkono ungekuwa wapi? Shukrani wa salamu zako na hongera zako.