The Chant of Savant

Wednesday 23 July 2014

Kutupwa viungo vya waswahili ingekuwa India waswahili wakafanya hivyo ingekuwaje?

Makamu Mkuu wa Chuo cha International Medical and Technological University (IMTU), Profesa PV Prabhak Rao (mwenye koti la blue)  na viongozi wengine wakisindikizwa na polisi kuingia kwenye Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na upatikanaji wa viungo vya binadamu eneo la Mpigi Bunju. Picha na Rafael Lubava
Tukio la chuo chenye kutia shaka cha International Medical and Technological University IMTU cha Dar es salaam kuhusika na kashfa ya kutupa miili na viungo vya binadamu kwenye bonde la Mpiji  limeniachia maswali mengi mojawapo yakiwa: Je miili hiyo ingekuwa imetupwa nchini India na Chuo Kikuu cha Kiafrika hali ingekuwaje? Bila shaka moto ungewaka na wahusika huenda wangekuwa marehemu. Je kwanini chuo cha kihindi kitupe miili ya waswahili kama ya mbwa na hali iendelee kuwa shwari? Je nini mantiki ya kuwa na serikali ambayo inaonekana kuwa mfukoni mwa watu hawa ambao Idd Simba waziri wa zamani wa Biashara na Viwanda alisema wahindi kumi tu wanamilki uchumi wa Tanzania?
Hawa jamaa pamoja na ubaguzi na ufisadi wao wa wazi wazi wameendelea kututendea ukaburu huku tukichekelea kana kwamba sisi ni jamii ya nyani? Je akitokea kiongozi mwingine kama Mtikila akakumbushia yote haya kuanzia ujambazi wa Chavda, EPA, Rada, Ndege ya rais, ESCROW, ubaguzi majumbani na sasa kutupa maiti zetu kama mbwa hali itakuwaje? TAFAKARINI KWA KINA. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

2 comments:

Anonymous said...

Hii dhihaka!

Lakini Je kuna-utaratibu wowote uliopo jinsi ya utupaji sahihi wa viungo vya binadamu kutoka serikalini na jiji kwa kuanzia?

Anonymous said...

Chamsingi hapa ni kuwachukulia hatua waliofanya makosa haya
Nimesoma kwenye gazeti moja eti chuo kifungwe
Kwanini wanafunzi na baadhi ya walimu wawana makosa
Ok ulaya kuna baadhi ya Watu huacha wosia wakifa miili Yao itumike kwa mafunzo kwenye vyuo vya udakitali
Hili la bongo jipya tujifunze japokuwa kutupa miili ya binadamu si ungwana. Pls wote waliohusuka sheria ifate mkondo
Nawasilisha hoja mwenyekiti