How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

How the Berlin Conference Clung on Africa: What Africa Must Do

Wednesday, 20 April 2011

Kumbe fisadi mtoto, Ridhiwan, ni bilionea!



Kila uchao orodha ya mafisadi inazidi kuumka. Tangu ilipotangazwa ile ya 2007 pale Mwembe Yanga wengi tulidhani ulikuwa mwisho. Juzi akihutubia wananchi wa Ikungi mkoani Singida, Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk Willibrod Slaa alimtaja Ridhiwan Kikwete kama bilionea ambaye anapaswa kuchukuliwa hatua na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kupata uhalali wa utajiri wake.

Richa ya Ridhiwan kutuhumiwa kuwa bilionea, yeye na mamake wa kambo Salma wamekuwa wakitumia madaraka ya baba yake yaani Rais Jakaya Kikwete kwa namna inayotia mashaka. Wengi wanajiuliza Kikwete anapopata mshipa wa kuwatuhumu hata kuwafukuza mafisadi wenzake wakati yeye na ukoo wake na mafisadi. Kwa habari zaidi, SOMA HAPA

7 comments:

Anonymous said...

Naamini viongozi wa Afrika hawajifunzi na hawana aja ya kusoma alama za nyakati.Yaliyowafika Mbarak na Gbagbo na familia zao kumbe bado si funzo kwao...yetu macho,tuombe Mwenyezi atupe uhai mkubwa naamini uko mbele kuna miujiza ya kushuhudia hapa Tanganyika.

Simon Kitururu said...

Mtakatifu ,...
..kuachia yote ulisha nidaka hapa:


``Kujivua gamba kusiishie kuwa kuvuana nguo .´´


Halafu hapa :
``Ukijua kudanganya ujue na kukumbuka!´´

kuna jamaa wa mwisho kukritiki kitabu chako akaingilia kati kwa kuhisi KISWALI:``Unajua labda MTAKATIFU anahisi wewe muongo?´´


Mkuu kile kitu kinakuja na kiuhakika ! Nimatumaini yangu unakumbuka nakumbuka! n ni stori ndefu kwa nini imechelewa ndude na nikianza kuelezea niliyempa flash diski ili aongezee mwenyewe ni miaka mingapi kachukua hasa kutokana na mikosano ya ratiba zetu za kukutana....

Ndio naongelea Kitabu :

SAA YA UKOMBOZI
by Nkwazi Nkuzi Mhango

ISBN 978 9987 07039 8

katika yaliyojimiksi kwenye hii komenti kwa wasiostukia!:-(
Pamoja sana MTAKATIFU!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Mtakatifu mwenzangu,
Nimekusikia na kukuelewa. Kazi kwenu mie nshaweka mambo hadharani.
Kula la heri na Pasaka njema.

Simon Kitururu said...

Asante Mtakatifu !

Ingawa hii kitu PASAKA na mchezo wa kupitiwa nayo pembeni!:-(

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Nimekupata ni suala la mtu binafsi.

Simon Kitururu said...

Halafiu MTAKATIFU kiimani umestukia KIMTU binafsi KIIIMANI kibinafsi siku hizi TANZANIA swala zima hili limekaa ki BABU WA LOLIONDO KWELI yani!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Loliondo si suala la imani bali kukata tamaa na ombwe la uongozi. Hujui Mwasapile ametumika kuua kashfa ya Dowans. Hii imefanya hata niwastukia akina Slaa. Anyway, they are Tanzanians or Bongolalalanders.