Obama awamaliza wanaodai hakuzaliwa Marekani
Rais Barack Obama amewakata ngebe wabaguzi wote wanaodai hakuzaliwa nchini Marekani hivyo hafai kuwa rais. Wachambuzi wanaamini kuwa sasa Obama amekata mzizi wa fitina.
Obama amewambia waandishi wa habari kuwa alijua kuwa wabaya wake wasingeacha suala hili lijifie zaidi ya kutapatapa nalo. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
2 comments:
Wabaguzi hawa hawataacha siasa zao hizi. Hata baada ya miaka miwili sasa bado hawajaamini kwamba kweli wako chini ya uongozi wa mtu mweusi.
Tayari Donald Trump anajisifu eti kwa kufanikiwa kumlazimisha Obama kukitoa cheti hicho na amedokeza kwamba hatashangaa kama hicho cheti kitakuwa ni cha kugushi.
Wachambuzi wote makini wanakiri kwamba hii ni aibu kwa Donald Trump mwenyewe na vigogo wote wa hii inayoitwa "birther" movement.
Mtazame huyu Bilionea mwenye majivuno na makeke hapa:
http://abcnews.go.com/Politics/donald-trump-claims-credit-obamas-releasing-birth-certificate/story?id=13465438
Kwa wanaomfahamu Donald Trump hawasiti kutoa hukumu kuwa akili yake ina walakini. Wachambuzi wengi makini wanamdharau. Huyu kimsingi hana tofauti na Ze Comedy kule kwetu. Hata Ze Comedy wana nafuu kwani huwachekesha watu na si kuwafedhehesha kama Trump. Amekuwa akisikika akisema eti atagombea urais jambo ambalo wengi wanaona ni kama kushusha hadhi ya ofisi hii.
Obama ni intellectual wakati Trump ni just a mere opportunist.
Obama kaishakuweka historia ya kuwa rais wa Marekani hata kama hawataki. Ajabu hawa hawa wahafidhina ni wale wale walioiingiza Marekani kwenye balaa linalotishia kufanya ipitwe na Uchina muda si mrefu. Maana inakopa karibu kila ndururu toka Uchina. Tungoje tuone.
Post a Comment