Sunday, 1 May 2011

Eheee! Gadaffi kumekucha mwanae auawa!


Habari ni kwamba mtoto wa mwisho wa imla wa Libya aitwaye Saif al Arabi Gadaffi aliuawa nyumba yao iliposhambuliwa na majeshi ya NATO usiku wa kuamkia jumapili ya tarehe mosi Mei.

Habari zinatonya kuwa katisha shambulizi hili makini, Muamar Gadaffi na mkewe walikoswakoswa kimiujiza. Saif al Arabi ameuawa sambamba na wajukuu watatu wa kiume wa Gadaffi.

Hakikia hii ni hatua muhimu kwa wapinzani na NATO. Kwani anaanza kudhoofishwa kisaikolojia kama ilivyotokea kwa mwenzake wa Iraq Saddam Hussein walipouawa watoto wake wawili katili.
Je Saif al Arabi alikuwa nani na alifanya nini? BONYEZA HAPA

No comments: